Uchaguzi 2020 Nilishawaambia muengueni Tundu Lissu, hamkusikia. Oneni!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
LISSU UMENISIKITISHA SANA, NILIKUWA SAHIHI KUSEMA UENGULIWE NA NEC. ONA SASA!

Na, Robert Heriel

Kipindi cha mchakato wa NEC kuteua wagombea watakaopeperusha bendera za Urais kupitisha vyama vya siasa hapa nchini, nilipendekeza kuwa Tundu Lissu aenguliwe kwa maslahi ya Muungano. Nilisema, Tundu Lissu sio tishio huku bara, hawezi kushinda huku bara, lakini hofu yangu ipo Zanzibar. Macho yangu yaliona kitakachotokea. Sijajua kwa nini NEC ilimpa nafasi, je mlimpuuza, au mlijua ananguvu ndogo bara hivyo mkasahau ya Zanzibar?

Tundu Lissu ni Rafiki yangu, ndugu na jamaa wangu wa karibu wanajua jinsi ninavyomfagilia. Lakini haiondoi ukweli kuwa Kupita kwake NEC kutaleta athari zaidi huko Zanzibar.

Tundu Lissu umeniudhi sana, hatuwezi kumchagua mtu anayetaka kuvunja umoja wetu. Hatuwezi kuiondoa hiyo CCM kwa kuligawa taifa hili. Hatuwezi kupata madaraka kwa kuleta uzanzibar na Utanganyika. Lisu leo umeniudhi mno.

Hotuba yako huko Zanzibar haijanivutia kwa sehemu kubwa. Imenifanya nikuone hauna nia njema na taifa hili.

Nilitegemea ungeongea kwa namna nyingine kabisa. Hasa kuhamasisha umoja, ikiwezekana useme kuwa; ingefaa taifa hili lisiwe na marais wawili. Rais awe mmoja ili kuondoa ile dhana ya upande mmoja kuonewa. Hii ni kusema kuwa, kuwe na serikali moja badala ya serikali mbili. Rais awe mmoja tu badala ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kung'ang'ania Zanzibar ni nchi hakuna la maana zaidi ya uchu wa madaraka kwa baadhi ya viongozi wetu. Zanzibar ni ndugu zetu, ni sehemu ya nchi yetu. Hata kama historia inaweza kutugawa lakini haizuii sisi kuwa nchi moja. Nafikiri Tundu Lisu hukupaswa kutoa maneno yanayoleta utengano baina ya nchi yetu kwa kuwafanya Watu waishio Zanzibar kujiona wanaonewa, ilhali hawaonewi.

Kugusa Muungano na kuuvunja, ni kuifisha nguvu Zanzibar. Ni kuwaonea ndugu zetu wa Zanzibar.

Ifike mahala tuijadili Zanzibar kama sehemu ya nchi yetu na wala sio nchi huru. Zanzibar ichukuliwe kama sehemu ya Mkoa wa Tanzania na kufuta serikali mbili ili iwe serikali moja. Najua itakuwa ngumu lakini itasaidia kupunguza migogoro ndani ya nchi.

Nafasi pekee niliyoiona ya Zanzibar kubaki salama ni kipindi kile cha mchakato wa kuchukua Fomu ya kuwania Urais NEC ambapo nilishauri Tundu Lisu aenguliwe, kwa makusudi ya kutokumpa nguvu Maalimu Seif. Nilisema pia kuwa, najua haitakuwa halali na sio haki lakini yote ni kulinda umoja wa nchi hii.

Tundu Lissu Leo umezingua mno. Huku najua hautashinda lakini macho yangu yanauona mchango wako katika ushindi wa Maalimu Seif kuichukua Zanzibar.

Zingatia; Taikon atazingatia zaidi maslahi ya nchi siku zote, kwa maana ndipo anapopata chakula, mke, watoto, na kila kitu. Taikon hata nyamaza pale anapoona maslahi ya nchi yanaathiriwa kwani kwa kunyamaza kwake ni kuruhusu Athari hizo zimfikie.

Acha Nipumzike sasa. Leo sitaki maswali, kama hujaelewa pumzika kama mimi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Kugusa Muungano na kuuvunja, ni kuifisha nguvu Zanzibar. Ni kuwaonea ndugu zetu wa Zanzibar.
Mwambie Robert ashike adabu zake na arudi kunyonya maziwa ya aliemzaa yamtoshe.

Waliikuta Zanzibar kabla ya Muungano ikiwa na maendeleo kuliko Tanganyika. Ilipoingia kwenye Muungano imefishwa yote. Miaka 50+ Zanzibar leo tunahangaika na vitu vya kipuuzi. Kisiwa kidogo tu kinakosa barabara nzuri, kisiwa kidogo tu maji hata mjini shida. Mataifa ya nje yakitaka kuisaidia Zanzibar JMT inaweka pingamizi.

Sina chama ila mwaka huu, nataka Maalim Seif asimamie kauli yake ya liwalo na liwe ili watu waheshimiane!
 
Ukweli huwa una athari hizi kwa wanafiki kama mleta mada. Usipende kufurahishwa na uongo wa muda!! Chagua ukweli unaoumiza lakini ukadumu.

Zanzibar ni nchi huru yenye katiba yake, mahakama yake, bendera yake, chombo chake cha maamuzi!! Kama vitu hivo si alama za uhuru - hakutakuwa na kielelezo kingine cha uhuru!

Tatizo haliondoka kwa kulikana bali kulikiri na kisha kulishughulikia.
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€

Mkuu mbona wanitisha asee!
Nyie ndio mnao tidhurumu haki zetu za msingi lazima tue wakali yaan nyie ambao mnanufaika ni wachache kuliko sie tusio nufaika naikumbukwe nchi ni yetu sote kama mema ya nchi yaliwe na watz wote na sio kikundi tu mpaka ajira mna ajili wenye kadi za uchama wa kijani hatutaki saizi tumekataa
 

Mimi sijawahi kumdhulumu Mtu Mkuu.

Kuhusu Ajira, nimeshamwambia Magufuli sitamchagua hata alie, kama hanipi kula kwa nini nimpe kura. Aniombe nimuajiri alafu yeye hata kuniajiri. Nilishamuandikia.

Mimi sina ufuasi wa kipuuzi.
 
Mimi sijawahi kumdhulumu Mtu Mkuu.

Kuhusu Ajira, nimeshamwambia Magufuli sitamchagua hata alie, kama hanipi kula kwa nini nimpe kura. Aniombe nimuajiri alafu yeye hata kuniajiri. Nilishamuandikia.

Mimi sina ufuasi wa kipuuzi
Kura yangu nilimpa 2015 hiyo imenitesa mpaka saizi nirudie tena kosa ? Noooooo bora nife nitoweke kwenye sura ya dunia Ila siwezi rudia kosa wanao neemeka ni ccm peke yao wananchi wa kawaida sisi tumesahaulika nooo kura yangu bora iende upinzani tu hakuna namna
 
Tunataka zanzbar yetu tuimiliki kwa imaan yetu maana munazidi kujenga makanisa tu mutuachie unguja yetu tumechoka.
We nawe kiazi mbatata kweli so we umeona makanisa tu eBu jaribu kujenga hoja zenye mashiko ila udini na ukabira hazikuzuii wewe kwenye angle yoyote, kama makanisa yanajengwa hadi UAE ijekuwa Zanzibar shame on u.
 


Shida ya Lissu unaijua Mkuu?
 
CCM ndio chanzo cha makanisa znzbar hatutaki tumechoka tunataka quraan ndo iwe katiba yetu mara tu baada ya kushinda na kukabidiwa nchi jambo la mwanzo ni kuvunja muungano fake baina ya Tanganyika na sisi. kwa kwel tumechoka
so we umeona makanisa tu eBu jaribu kujenga hoja zenye mashiko ila udini na ukabira hazikuzuii wewe kwenye angle yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…