Mleta mada unapaswa kutambua haya kuhusu Zanzibar.
-Muungano ni jambo la hiari, hivyo wazanzibar hatupaswi kulazimishwa kuwepo kwenye muungano huu.
-Zanzibar ilikuwa ni taifa huru kabla ya muungano, hivyo muungano hauna haki ya kupora uhuru wa Zanzibar.
-Malengo ya muungano yalikuwa ni kushirikiana na sio nchi moja kuitawala nchi nyingine na wala sio muungano kuimeza Zanzibar.
-Muungano ni jambo la ziada tu kwa mzanzibar, maisha ya mzanzibar hayategemei uwepo wa huu muungano.
-Muungano kwa mzanzibar ni kama koti tu, ambalo ukilichoka unaweza kulivua mara moja. Zanzibar kwanza muungano baadaye.