Nilishawahi kusema, Yanga SC hamjawahi kujaribiwa

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Poleni Wanayanga, hakika huko Sudan kuchomoa ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Hii ni michezo ya kimataifa, hatuchezi mpira kama tunacheza na Singida Big Stars. Kuna nidhamu zake, tahadhari na hekima.

Hutetemi temi tu kama mgonjwa wa akili. Ni nidhamu sana, mbinu na uzoefu. Inawapasa kuendelea kuiheshimu Simba Sc daima kwenye hizi anga za kimataifa.

Kwa michezo ya kimataifa, ni lazima ushinde nyumbani ili ufike makundi na robo fainali, na ndiyo huwa mnaona SSC nayo ikifika kwenye mtoano, hali inakuwa ni mbaya na ndiyo huko inapata maujanja.

Nilishawahi kusema Yanga hamjawahi kujaribiwa na hizi kutoshindwa shindwa siyo kipimo cha ubora wake. Kipimo cha ubora hakipo kwenye kutokushindwa na Singida Big Stars, Geita Gold. Sasa mnaenda kujaribiwa kwa mara ya kwanza tangu 1998.

Na itahitaji kama miaka mitano ijayo mjaribiwe kwa mtindo huu mfululizo ndiyo angalau mpate ka ubora mnako katamani. Siyo rahisi kama mnavyofikiria.

Tusipeane moyo, kuitoa Al Hilal pale Khartoum sio rahisi hivo. Mtapumua pumzi ya moto kama Injinia Hersi alipotoa pumzi nzito pale kwa Mkapa. Maisha siyo rahisi rahisi kihivyo. Mambo makubwa kamwe siyo rahisi, nayo pia yanahitaji muda.

Mara ya mwisho nyie kucheza nje ya nchi ugenini ni lini? Mechi za hatua ya kwanza mlichezea hapo hapo Tanzania, mkachukulia maisha poa. Mlitakiwa kustuka na hizo goli 9 za mchongo!

Kazi mnayo kweli kweli. Halafu kumbukeni mwaka ni mrefu sana, mkitolewa sasa hivi ni hadi mwakani ni parefu sana.

Nipo hapa Angola nasubiria mchezo wa wabishi.
 
Ujue hii michezo sometimes unaweza kujikita kusheherekea shughuli ya mwingine baada ya kufanya vibaya wakati mechi yako ya kesho hujui outcome yake ikoje mwisho wake unakuwa sio mzuri.

Wanasema the one who laugh later laughs better, Simba haijazungumziwa sana kwenye mechi yake inayocheza kesho kwa watu wengi kuamini upinzani anaoenda kukutana nao ni dhaifu.

Lakini vipi kama tukaenda kukutana na kitu tofauti?

Hii kumbuka iliwahi kutukuta kwa Kaizer Chiefs, wakati tupo kwao mpira tulicheza kuliko wao lakini tulipasuka goli 4

Sijui kama makosa kama yale wataweza kuyarudia tena ila nilichojifunza ni haijalishi mpinzani wako ana rekodi gani mbaya hupaswi kum underestimate at any angle.
 
Sisi tunanafasi ya kuja kusahihisha makosa kwa mkapa so hata tukibondwa kesho sio case ila hawa uto lazima tuwaseme
 
Sisi tunanafasi ya kuja kusahihisha makosa kwa mkapa so hata tukibondwa kesho sio case ila hawa uto lazima tuwaseme
Kumbuka tulikuwa na nafasi ya kusahihisha makosa tuliyofanya kwa Kaizer chiefs kule kwao lakini bado haikutufanya tusonge mbele

Saizi ukiwa na upimzani na timu ambayo sio kubwa ni bora uomae ushinde nje ndani
 
Kumbuka tulikuwa na nafasi ya kusahihisha makosa tuliyofanya kwa Kaizer chiefs kule kwao lakini bado haikutufanya tusonge mbele

Saizi ukiwa na upimzani na timu ambayo sio kubwa ni bora uomae ushinde nje ndani

Hapana Simba tunaimani nayo. Yanga wamekosa Technical Experience, na kule kartoum sio rahisi kama unavyodhani. Ni katika mazingira magumu snaa watacohomoa. Kibaya zaidi Yanga haijawahi kucheza mechi za ugenini nje ya nchi . Kuna shurba nyingi ugenini. Ngoja mpigwe COVID kwanza ndio mtaelewa ugumu wa ugenini unaanzia pale Airport.
Si unasikiaga wale wengine wakilalamika kuwa wanapuliziwa dawa
 
Kumbuka tulikuwa na nafasi ya kusahihisha makosa tuliyofanya kwa Kaizer chiefs kule kwao lakini bado haikutufanya tusonge mbele

Saizi ukiwa na upimzani na timu ambayo sio kubwa ni bora uomae ushinde nje ndani

Ni kweli. Mechi ya kesho ni ngumu zaidi ya hii ya Utopolo vs Al Hilal. Na tukumbuke kwamba Angola iko juu ya Sudan kwenye FIFA rankings.
 
Timu yetu nzuri iko full kuanzia kipa mpaka fundi mayele. Bahati mbaya tu leo ila tuna bangala, aziz ki, morrison leg 2 hao wasudan watakoma we subiri tu.
 
Mtawalaumu bure lakini kila timu ina malengo yake imejiwekea yaani.

Yanga wamejitengenezea Kijiji chao kwenye Ligi Kuu.

Simba SC wao wamejikita kutengeneza Kijiji chao kwenye CAF
 
MAKOLO mliowahi kutusua mlichukua kombe gani haswa huko CAF?
 
Na mashabiki wa wabishi FC tupo hapa tumejaaa tele kusapoti chama kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…