Megalodon
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 3,534
- 7,866
Poleni Wanayanga, hakika huko Sudan kuchomoa ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Hii ni michezo ya kimataifa, hatuchezi mpira kama tunacheza na Singida Big Stars. Kuna nidhamu zake, tahadhari na hekima.
Hutetemi temi tu kama mgonjwa wa akili. Ni nidhamu sana, mbinu na uzoefu. Inawapasa kuendelea kuiheshimu Simba Sc daima kwenye hizi anga za kimataifa.
Kwa michezo ya kimataifa, ni lazima ushinde nyumbani ili ufike makundi na robo fainali, na ndiyo huwa mnaona SSC nayo ikifika kwenye mtoano, hali inakuwa ni mbaya na ndiyo huko inapata maujanja.
Nilishawahi kusema Yanga hamjawahi kujaribiwa na hizi kutoshindwa shindwa siyo kipimo cha ubora wake. Kipimo cha ubora hakipo kwenye kutokushindwa na Singida Big Stars, Geita Gold. Sasa mnaenda kujaribiwa kwa mara ya kwanza tangu 1998.
Na itahitaji kama miaka mitano ijayo mjaribiwe kwa mtindo huu mfululizo ndiyo angalau mpate ka ubora mnako katamani. Siyo rahisi kama mnavyofikiria.
Tusipeane moyo, kuitoa Al Hilal pale Khartoum sio rahisi hivo. Mtapumua pumzi ya moto kama Injinia Hersi alipotoa pumzi nzito pale kwa Mkapa. Maisha siyo rahisi rahisi kihivyo. Mambo makubwa kamwe siyo rahisi, nayo pia yanahitaji muda.
Mara ya mwisho nyie kucheza nje ya nchi ugenini ni lini? Mechi za hatua ya kwanza mlichezea hapo hapo Tanzania, mkachukulia maisha poa. Mlitakiwa kustuka na hizo goli 9 za mchongo!
Kazi mnayo kweli kweli. Halafu kumbukeni mwaka ni mrefu sana, mkitolewa sasa hivi ni hadi mwakani ni parefu sana.
Nipo hapa Angola nasubiria mchezo wa wabishi.