Nilisomesha Mchumba aje kuwa Mke, Wazazi wakanivuruga na Mchumba akadanganyika

Nilisomesha Mchumba aje kuwa Mke, Wazazi wakanivuruga na Mchumba akadanganyika

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
PART 1

Huyu dada ndiye ambaye ilikuwa nimuoe. Nlimpenda sana kwa kweli na ku risk kumsomesha. Baada ya kuwa alikuwa na ufaulu ambao ungeweza msaidia kuendelea na masomo. Hakuwa na wazazi. Na ndugu zake hawakuwa tayari kumsomesha.

Nikamwambia aombe kusoma IFM. akaomba akapata nikamlipia ada na kumpangia chumba. Asilimia 100 kila kitu nlikuwa namlipia. Nlimpenda sababu pia alikuwa na akili Darasani.

Mkoani nlikuwa na mwanamke ambaye nlikuwa nimezaa naye. Huyu dada mapenzi yalipungua kwake sababu alikuwa na Ujeuri flani kwangu. Alipopata ujauzito nlimwambia tutoe ikiwa na miezi 2. Akakataa nikamwambia its ok. Then asubiri nifanye mchakato wa kuwajulisha wazazi wangu suala hilo na nimtafutie sehemu ya kukaa.

Hakusubiri hata siku mbili. Mimi nipo Dar napigiwa simu na mama kuwa kuna binti kaenda pale home anasema ana ujauzito wangu. Kuuliza jina natajiwa lake. Nlikwazika sana. Nliona ni mwanamke ambaye ameshindwa nisikiliza, mkaidi na mbabe. Mapenzi kwake yalianza pungua. Yaliingia dosari kubwa sana toka siku ile.

Ndo chanzo cha kuanza mahusiano na huyu ambaye ninamsomesha. Maana siku nampigia namuuliza kwa nini umenitendea hivi alinijibu

"We unadhani mimi utanitelekeza nikuache tu unaniambia ukanipangie uniletee na dada wa kazi then sijui nikasome....sitaki hii mimba yako utalea mwenyewe" akakata na simu

Huyu binti alikuwa amemaliza form 6 ana ufaulu mzuri tu kwenda Chuo. Na ndo maana sikutaka azae coz nlitaka kwanza aende Chuo. Ila nilikuja gundua hakutaka kuendelea kusoma.

Alikuwa anaona mimi nipo vizuri kiuchumi na wazazi wangu wana uwezo basi akaridhika sana. Hapo ndo nlipoanza pia kuchoka naye.


Basi katika pita pita ndo nikaja kutana na huyu dada Irene. Irene alikuwa mzuri na anapenda kusoma. Nikaona nimsaidie kielimu. Baadaye tukawa tunapendana sana.

Akaanza mwaka wa kwanza, wa pili changamoto zikaanza. Kule yule mwingine Latipher alikuwa ameshajifungua. Anaishi home na wazazi. Namhudumia vizuri na anahudumiwa vizuri pia. Hakukuwa na changamoto yoyote kwa suala la huduma. Ila sasa yameibuka mengine...
 
PART 2

wazazi sasa wanaanza niuliza nina mpango gani endelevu na yule binti. Mimi sikutaka tena kumwoa yule binti. Latipher. Nliaona kama hatutasikilizana na upendo umeisha. Hanitii,. Mkaidi na Mbabe.

Wakaniita niende Mkoani. Nikaenda. Kikafanyika kikao na wakaniambia wao wanamtambua Latipher kama mke wangu sababu nimeshamzalisha na hawatamtambua mwingine yeyote. Nilipata wakati mgumu sana sababu nliona kabisa mapenzi yamepungua sana kwa Latipher.

Baadaye nikarudi Dar. Nikawa napata wakati mgumu kumwambia Irene suala hilo.maana kule walichoniambia sasa ni kufanya mchakato wa Ndoa. Nikakubali kwa shingo upande. Nakumbuka nlikaa week nzima pale home. Nalala naye lakini hamu ya kufanya naye sina kabisa.

Basi nikaona nimwambie Irene jambo hili. Nikamueleza. Alilia sana. Karibia week nzima aligoma kwenda chuo nami nikawa siwezi toka kwenda kazini. Maana alikuwa anatishia kujiua. Nlijitahidi sana kumwelekeza issue ilivyo hakutaka nielewa. Maisha yetu yakawa yamejaa huzuni. Anashinda analia. Hataki kula.

Nami naumia kwa hali hiyo. Nlimwambia nitaendelea msomesha, nitalipia kila kitu kama kawaida ila itakuwa ngumu kuoana naye. Hakunielewa. Mwishoni akaniambia niondoke nimpe muda afikiri. Kwa shingo upande nikarudi nikawa nakaa kwangu kwake aliniambia nisiende kwanza mpaka atakapotulia.

Ikapita week, weeks, mwezi, miezi. Nikimpigia hatuongei sana. But namtumia pesa za matumizi n.k sikuwahi acha mhudumia. Nlijua nami nimemuumiza kwa kile kitendo ila sikuwa na namna. Basi tukawa baadaye tunaona juu juu. Muda wote huo namsihi arudishe moyo nyuma. Akumbuke tumetoka wapi na tunaenda wapi.
 
PART 3
Ukafika wakati nikaenda Mkoani kufunga ndoa. Ikafanyika na harusi kubwa tu. Hayo yote sikuwa namficha Irene. Kumbe naye huku Dar akapata mwanaume mmoja toka Kinondoni. Jamaa akamdanganya danganya sana. Na Irene akaona aniumize na mimi akashika Mimba.

Mwaka watatu mwanzoni akawa anapost picha zake na jamaa yake na akionesha ana mimba. Nliumia sana. Nliumia sababu toka nimemuambia ile issue yangu sikuacha mpenda. Na nlimwambia hakuna ambacho kingebadilika. But naye alikuwa amerudisha moyo nyuma.

Alianza mahusiano na mtu mwingine. Jamaa alimuahidi mambo mengi sana. But kiuhalisia jamaa hakuwa mkweli ni hawa vijana wanaoruka ruka wa mjini. Alikuwa akienda kwake anaazima magari watu anaonekana ana uwezo. Irene akaona huyu ni mtu muafaka. So akawa sasa anafanya kuniumiza.

Nikaacha mhudumia ule mwaka wa tatu. jamaa akamchukua akampeleka kwao. Ndo Irene kuufahamu ukweli. Jamaa alikuwa tu anabebwa bebwa na ujanja janja wa mjini. Hakuwa na kazi ya kueleweka. Alikuwa anatembea na mijimama imtoe pesa na bado alikuwa anategemea kwao ndo wamsaidie.

Chuo akashindwa endelea. Akashindwa kulipa kodi kile chumba so akawa anakaa kwa wakwe. Pale home kero zikawa nyingi. Jamaa hatake care of her. Irene akaanza kupoteza nuru. Maisha yakawa magumu. Chuo ndo basi ameacha, haelewi afanye nini. Mtoto analea mwenyewe.

Mtoto alipoanza kukua kua kidogo Ikabidi Irene akaanze kutafuta kazi. akaja pata kazi ya kusafiri na kuhudumia abiria na kukatisha tiketi. Hapo akaamua akapange aishi yeye na mtoto wake. Kipindi chote hicho alishakata mawasiliano nami. Maana kipindi kile ana post picha zake na jamaa. Nlimtafuta tuongee. Akanijibu niachane naye. Anafanya maisha yake.

Nlijaribu sana kumbembeleza akumbuke tumetoka wapi. Akumbuke nlimwahidi nini.alikataa na kuniambia amepata mtu ambaye wanapendana na wataoana.basi kwa maumivu makubwa sana nliamua kuachana naye. Nakumbuka nliteseka karibia miezi 3 nikiumia sana.

Sikuweza enda pale anapoishi. Sikutaka enda na kumkuta yupo na yule kijana. Kwenye nyumba ambayo nlimpangia mimi na vitu ambavyo nlimnunulia mimi. Irene alikuwa amebadilika. Akipost picha zake kuwa anakula maisha n.k

Lakini sasa Irene si yule tena. Rafiki zake wakaanza kunitafuta na kutaka nimrudie Irene. Wakitaka nimsamehe... But sikuwa na jibu lolote tena kwao. Nlikuwa na maumivu makubwa sana moyoni. Irene aliharibiwa. Nlijaribu kumlinda hakutaka.sasa amekuwa konda wa mabasi ya mkoani.

Miaka ikapita mpaka jana natoka Mkoa flani nikiwa kwenye Bus. Naamshwa ili wakague ticket. Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa ticket.nikamkabidhi akaniita Chizi....nikageuka kumwangalia. Ni Irene.
 
PART 4.

IRENE alikuwa amebadilika usoni. Uzuri wake umeisha, alionesha kuwa alikuwa akitumia sana pombe. Nlimsalimia nikitabasamu. Aliinama chini. Akajibu akiwa hana furaha.
Mimi: Habari za miaka?
Irene : nzuri
Mimi: upo?
Irene : yes nipo... Tutaongea
Mimi : its ok hamna shida.

Akaendelea kwa abiria wengine. Nilimtizama. Lile umbo lake namba 8 halikuwepo tena. Alikuwa amepungua mvuto. Kasuka rasta na amevaa suruali ya jeans na tshirt yenye nembo ya bus husika.

Bado alikuwa ana uzuri kiasi flani hakuwa wa kumbeza hata kidogo. Akafungua mlango kuelekea nyuma maana mimi nlikuwa nimepanda upande huu ambao ni VIP/LUXURY. akaelekea kukagua tickets upande ule wa kawaida.

Nimefika safari haraka nikashuka kuulizia yule dada aliyekuwa anakagua tickets yu wapi. Wakaniambia alishuka sehemu flani then akarudi na Bus jingine Dar. Irene hakutaka hata kuniaga. Hakutaka tuongee. Nlimkosea ndiyo lakini si kwa kiwango hiki. Alisahau tulifanya mengi pamoja. Nilimtafuta rafikiye jana. Akaniambia Irena alimpigia simu na kumwambia ameniona kwenye gari.. akamwambia hawezi endelea na safari coz anajisikia aibu na maumivu kwa yale ambayo alitenda kwangu. So akaamua kubadilishana na mtu mwingine na yeye kurudi Dar.


Nikirudi Dar.... Nitamtafuta Irene.... Angalau niongee naye. Nilishamsamehe maisha hayana budi kuendelea....


NITAELEZEA NINI KINAENDELEA. NAANDIKA NIKIWA NA MAUMIVU MAKUBWA MOYONI.
 
Ulitaka awe nke mdogo?au kama unamsaidia mtaji mpe mwache na maisha yake we ushaoa
 
PART 4.

IRENE alikuwa amebadilika usoni. Uzuri wake umeisha, alionesha kuwa alikuwa akitumia sana pombe. Nlimsalimia nikitabasamu. Aliinama chini. Akajibu akiwa hana furaha.
Mimi: Habari za miaka?
Irene : nzuri
Mimi: upo?
Irene : yes nipo... Tutaongea
Mimi : its ok hamna shida.

Akaendelea kwa abiria wengine. Nilimtizama. Lile umbo lake namba 8 halikuwepo tena. Alikuwa amepungua mvuto. Kasuka rasta na amevaa suruali ya jeans na tshirt yenye nembo ya bus husika.

Bado alikuwa ana uzuri kiasi flani hakuwa wa kumbeza hata kidogo. Akafungua mlango kuelekea nyuma maana mimi nlikuwa nimepanda upande huu ambao ni VIP/LUXURY. akaelekea kukagua tickets upande ule wa kawaida.

Nimefika safari haraka nikashuka kuulizia yule dada aliyekuwa anakagua tickets yu wapi. Wakaniambia alishuka sehemu flani then akarudi na Bus jingine Dar. Irene hakutaka hata kuniaga. Hakutaka tuongee. Nlimkosea ndiyo lakini si kwa kiwango hiki. Alisahau tulifanya mengi pamoja. Nilimtafuta rafikiye jana. Akaniambia Irena alimpigia simu na kumwambia ameniona kwenye gari.. akamwambia hawezi endelea na safari coz anajisikia aibu na maumivu kwa yale ambayo alitenda kwangu. So akaamua kubadilishana na mtu mwingine na yeye kurudi Dar.


Nikirudi Dar.... Nitamtafuta Irene.... Angalau niongee naye. Nilishamsamehe maisha hayana budi kuendelea....


NITAELEZEA NINI KINAENDELEA. NAANDIKA NIKIWA NA MAUMIVU MAKUBWA MOYONI.
Mtunze mke wako , usiendekeze hsia
 
Bora wewe ulisomesha mimi nilikuwa na hudumia mtoto kidawa kaja kunipiga chini kisa sina hadhi ya chuo na dini yake.
nyie ZnZ na hasira na nyie shwaini
 
Umesoma, una maisha yako, unalazimishwa kuoa usiyempenda.
Wataalamu wa afya ya akili Wana kusubiri pale Milembe.
 
Back
Top Bottom