Nilisomesha Mchumba aje kuwa Mke, Wazazi wakanivuruga na Mchumba akadanganyika

Nilisomesha Mchumba aje kuwa Mke, Wazazi wakanivuruga na Mchumba akadanganyika

Bora wewe ulisomesha mimi nilikuwa na hudumia mtoto kidawa kaja kunipiga chini kisa sina hadhi ya chuo na dini yake.
nyie ZnZ na hasira na nyie shwaini
Siyo wapemba wote tupo hivyo....😂
 
PART 3
Ukafika wakati nikaenda Mkoani kufunga ndoa. Ikafanyika na harusi kubwa tu. Hayo yote sikuwa namficha Irene. Kumbe naye huku Dar akapata mwanaume mmoja toka Kinondoni. Jamaa akamdanganya danganya sana. Na Irene akaona aniumize na mimi akashika Mimba.

Mwaka watatu mwanzoni akawa anapost picha zake na jamaa yake na akionesha ana mimba. Nliumia sana. Nliumia sababu toka nimemuambia ile issue yangu sikuacha mpenda. Na nlimwambia hakuna ambacho kingebadilika. But naye alikuwa amerudisha moyo nyuma.

Alianza mahusiano na mtu mwingine. Jamaa alimuahidi mambo mengi sana. But kiuhalisia jamaa hakuwa mkweli ni hawa vijana wanaoruka ruka wa mjini. Alikuwa akienda kwake anaazima magari watu anaonekana ana uwezo. Irene akaona huyu ni mtu muafaka. So akawa sasa anafanya kuniumiza.

Nikaacha mhudumia ule mwaka wa tatu. jamaa akamchukua akampeleka kwao. Ndo Irene kuufahamu ukweli. Jamaa alikuwa tu anabebwa bebwa na ujanja janja wa mjini. Hakuwa na kazi ya kueleweka. Alikuwa anatembea na mijimama imtoe pesa na bado alikuwa anategemea kwao ndo wamsaidie.

Chuo akashindwa endelea. Akashindwa kulipa kodi kile chumba so akawa anakaa kwa wakwe. Pale home kero zikawa nyingi. Jamaa hatake care of her. Irene akaanza kupoteza nuru. Maisha yakawa magumu. Chuo ndo basi ameacha, haelewi afanye nini. Mtoto analea mwenyewe.

Mtoto alipoanza kukua kua kidogo Ikabidi Irene akaanze kutafuta kazi. akaja pata kazi ya kusafiri na kuhudumia abiria na kukatisha tiketi. Hapo akaamua akapange aishi yeye na mtoto wake. Kipindi chote hicho alishakata mawasiliano nami. Maana kipindi kile ana post picha zake na jamaa. Nlimtafuta tuongee. Akanijibu niachane naye. Anafanya maisha yake.

Nlijaribu sana kumbembeleza akumbuke tumetoka wapi. Akumbuke nlimwahidi nini.alikataa na kuniambia amepata mtu ambaye wanapendana na wataoana.basi kwa maumivu makubwa sana nliamua kuachana naye. Nakumbuka nliteseka karibia miezi 3 nikiumia sana.

Sikuweza enda pale anapoishi. Sikutaka enda na kumkuta yupo na yule kijana. Kwenye nyumba ambayo nlimpangia mimi na vitu ambavyo nlimnunulia mimi. Irene alikuwa amebadilika. Akipost picha zake kuwa anakula maisha n.k

Lakini sasa Irene si yule tena. Rafiki zake wakaanza kunitafuta na kutaka nimrudie Irene. Wakitaka nimsamehe... But sikuwa na jibu lolote tena kwao. Nlikuwa na maumivu makubwa sana moyoni. Irene aliharibiwa. Nlijaribu kumlinda hakutaka.sasa amekuwa konda wa mabasi ya mkoani.

Miaka ikapita mpaka jana natoka Mkoa flani nikiwa kwenye Bus. Naamshwa ili wakague ticket. Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa ticket.nikamkabidhi akaniita Chizi....nikageuka kumwangalia. Ni Irene.
Mbna hyo Kazi nzuri sana etiee. Hakosi 30000 au 40000 Kwa siku
 
Ulitaka awe nke mdogo?au kama unamsaidia mtaji mpe mwache na maisha yake we ushaoa
Sawa. Haina shida dada. Sasa amekuwa Mke mkubwa
1. Hakumaliza Chuo
2. Ameteswa Ukweni
3. Mzazi mwenzie hajui mtoto wake anaishi na anakula nini.
4. Irene ananionea aibu jinsi alivyo.

So ni kweli nliamua kumwacha aishi maisha ya mke Mkubwa.
 
Mbna hyo Kazi nzuri sana etiee. Hakosi 30000 au 40000 Kwa siku
Ha ha ha.... Asikudanganye mtu. Tena asikudanganye kabisa. Siku hizi kuna mabasi yana Cctv camera. Kuna mabasi hayaruhusu kusimamisha abiria. Tickets zinakatwa za umeme. Wizi kama upo ni mdogo sana. Hakuna hilo jambo unalosema. Na bado wanaanza kazi saa 11 asubuhi na kumaliza saa 4 usiku. Habari nimepewa na rafikiye ambaye ni wa karibu sana.
 
Hivi huu ushujaa huwa mnapata wapi wa kusomesha mpenzi eti utakuja kumuoa!!!
 
B
Ha ha ha.... Asikudanganye mtu. Tena asikudanganye kabisa. Siku hizi kuna mabasi yana Cctv camera. Kuna mabasi hayaruhusu kusimamisha abiria. Tickets zinakatwa za umeme. Wizi kama upo ni mdogo sana. Hakuna hilo jambo unalosema. Na bado wanaanza kazi saa 11 asubuhi na kumaliza saa 4 usiku. Habari nimepewa na rafikiye ambaye ni wa karibu sana.
Basi Lake likoje??uhuni upo tu ndg.. haukosekan hawez kukosa pesa za Kula hyo.. ukiacha abiria kuna mizigo ya hapa na pale.. hafii njaa uyooo...
 
Sawa. Haina shida dada. Sasa amekuwa Mke mkubwa
1. Hakumaliza Chuo
2. Ameteswa Ukweni
3. Mzazi mwenzie hajui mtoto wake anaishi na anakula nini.
4. Irene ananionea aibu jinsi alivyo.

So ni kweli nliamua kumwacha aishi maisha ya mke Mkubwa.
Msaidie mtaji afanye biashara
 
Hata
PART 4.

IRENE alikuwa amebadilika usoni. Uzuri wake umeisha, alionesha kuwa alikuwa akitumia sana pombe. Nlimsalimia nikitabasamu. Aliinama chini. Akajibu akiwa hana furaha.
Mimi: Habari za miaka?
Irene : nzuri
Mimi: upo?
Irene : yes nipo... Tutaongea
Mimi : its ok hamna shida.

Akaendelea kwa abiria wengine. Nilimtizama. Lile umbo lake namba 8 halikuwepo tena. Alikuwa amepungua mvuto. Kasuka rasta na amevaa suruali ya jeans na tshirt yenye nembo ya bus husika.

Bado alikuwa ana uzuri kiasi flani hakuwa wa kumbeza hata kidogo. Akafungua mlango kuelekea nyuma maana mimi nlikuwa nimepanda upande huu ambao ni VIP/LUXURY. akaelekea kukagua tickets upande ule wa kawaida.

Nimefika safari haraka nikashuka kuulizia yule dada aliyekuwa anakagua tickets yu wapi. Wakaniambia alishuka sehemu flani then akarudi na Bus jingine Dar. Irene hakutaka hata kuniaga. Hakutaka tuongee. Nlimkosea ndiyo lakini si kwa kiwango hiki. Alisahau tulifanya mengi pamoja. Nilimtafuta rafikiye jana. Akaniambia Irena alimpigia simu na kumwambia ameniona kwenye gari.. akamwambia hawezi endelea na safari coz anajisikia aibu na maumivu kwa yale ambayo alitenda kwangu. So akaamua kubadilishana na mtu mwingine na yeye kurudi Dar.


Nikirudi Dar.... Nitamtafuta Irene.... Angalau niongee naye. Nilishamsamehe maisha hayana budi kuendelea....


NITAELEZEA NINI KINAENDELEA. NAANDIKA NIKIWA NA MAUMIVU MAKUBWA MOYONI.
Yakiwa maumivu makubwa mataqoni we malizia story yote kwanza ndio uende.
 
Hata
Yakiwa maumivu makubwa mataqoni we malizia story yote kwanza ndio uende.
Aiseee nimesikitika tu kwa ulichoandika.... Kuna sehemu huwa unatoa mchango wa maana sana. Sikutegemea unaweza kuja andika kitu kama hiki. Anyway yote heri ndugu yangu. Tunajifunza zaidi kuhusu watu kupitia vitu kama hivi. Shukrani.
 
Mchumba hasomeshwi, sina hata haja ya kusoma....ilikuwa lazima neno litimie🐒
 
Aiseee nimesikitika tu kwa ulichoandika.... Kuna sehemu huwa unatoa mchango wa maana sana. Sikutegemea unaweza kuja andika kitu kama hiki. Anyway yote heri ndugu yangu. Tunajifunza zaidi kuhusu watu kupitia vitu kama hivi. Shukrani.
Mzee usiwaze sana, leo nina hasira sana yani. Sitaki kuona jambo lolote la tofauti. We malizia story
 
☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️☹️hii emoji inani chekesha sana🤣🤣☹️☹️
 
Back
Top Bottom