uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 17,060
- 32,400
PART 4.
IRENE alikuwa amebadilika usoni. Uzuri wake umeisha, alionesha kuwa alikuwa akitumia sana pombe. Nlimsalimia nikitabasamu. Aliinama chini. Akajibu akiwa hana furaha.
Mimi: Habari za miaka?
Irene : nzuri
Mimi: upo?
Irene : yes nipo... Tutaongea
Mimi : its ok hamna shida.
Akaendelea kwa abiria wengine. Nilimtizama. Lile umbo lake namba 8 halikuwepo tena. Alikuwa amepungua mvuto. Kasuka rasta na amevaa suruali ya jeans na tshirt yenye nembo ya bus husika.
Bado alikuwa ana uzuri kiasi flani hakuwa wa kumbeza hata kidogo. Akafungua mlango kuelekea nyuma maana mimi nlikuwa nimepanda upande huu ambao ni VIP/LUXURY. akaelekea kukagua tickets upande ule wa kawaida.
Nimefika safari haraka nikashuka kuulizia yule dada aliyekuwa anakagua tickets yu wapi. Wakaniambia alishuka sehemu flani then akarudi na Bus jingine Dar. Irene hakutaka hata kuniaga. Hakutaka tuongee. Nlimkosea ndiyo lakini si kwa kiwango hiki. Alisahau tulifanya mengi pamoja. Nilimtafuta rafikiye jana. Akaniambia Irena alimpigia simu na kumwambia ameniona kwenye gari.. akamwambia hawezi endelea na safari coz anajisikia aibu na maumivu kwa yale ambayo alitenda kwangu. So akaamua kubadilishana na mtu mwingine na yeye kurudi Dar.
Nikirudi Dar.... Nitamtafuta Irene.... Angalau niongee naye. Nilishamsamehe maisha hayana budi kuendelea....
NITAELEZEA NINI KINAENDELEA. NAANDIKA NIKIWA NA MAUMIVU MAKUBWA MOYONI.
Jitu lishaoa, miaka imeenda, lianaume, eti lina maumivu makali moyoni, rubbish