Nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Heri ya mwezi mpya wa Novemba, 2017 wanajf.

Jana muda wa saa mbili usiku nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

Nyoka wa kimo cha kati, mweusi.

Nimeshangaa amepitia wapi na hali milango imefungwa, amewezaje kupita kwenye vigae na hali vigae vinateleza.

Niliogopa na hata kuchanganyikiwa!

Mungu mkubwa, ninaishi vizuri na majirani zangu waliweza kunisaidia kumuua!!!
Nimelala nastuka nastuka namuona kama vile ananipandia kitandani.

Naomba mnisaidie ushauri na kinga ya kuzuia huyo "ndudu" asiingie tena ndani na hali sioni sehemu ya kumuwezesha kupenya hadi ndani.
 
Haya, wahuja chwi? Kama ni hivyo, tulia tu. Haji mwingine ila huyo mwenye hiyo nyumba mkono wa kulia unapotoka home, ukimwona msalimie kwa sauti kuubwa kila siku asubuhi.
 
Huyo nyoka alivyokuingia ulijisikiaje? Mbona mlango wenyewe hukuufunga yaani sitaki nataka, nyoka mzuri mweusi saizi ya kati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…