Nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

Nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

Heri ya mwezi mpya wa Novemba, 2017 wanajf.

Jana muda wa saa mbili usiku nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

Nyoka wa kimo cha kati, mweusi.

Nimeshangaa amepitia wapi na hali milango imefungwa, amewezaje kupita kwenye vigae na hali vigae vinateleza.

Niliogopa na hata kuchanganyikiwa!

Mungu mkubwa, ninaishi vizuri na majirani zangu waliweza kunisaidia kumuua!!!
Nimelala nastuka nastuka namuona kama vile ananipandia kitandani.

Naomba mnisaidie ushauri na kinga ya kuzuia huyo "ndudu" asiingie tena ndani na hali sioni sehemu ya kumuwezesha kupenya hadi ndani.
Unakaa Dar?
 
Kuna mambo mawili ya kufanya nyoka anapoingia ndani.

1. Muue

2. Muue haraka sana.

Kama ukishindwa yote hayo basi hakikisha unamkata kichwa.
Mie ni mwoga sana, yaani kukosa majirani nadhani ningehama kabisa nikalale hotelini hahahahahahahhahh
 
Back
Top Bottom