Nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

Heri ya mwezi mpya wa Novemba, 2017 wanajf.

Jana muda wa saa mbili usiku nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

Nyoka wa kimo cha kati, mweusi.

Nimeshangaa amepitia wapi na hali milango imefungwa, amewezaje kupita kwenye vigae na hali vigae vinateleza.

Niliogopa na hata kuchanganyikiwa!

Mungu mkubwa, ninaishi vizuri na majirani zangu waliweza kunisaidia kumuua!!!
Nimelala nastuka nastuka namuona kama vile ananipandia kitandani.

Naomba mnisaidie ushauri na kinga ya kuzuia huyo "ndudu" asiingie tena ndani na hali sioni sehemu ya kumuwezesha kupenya hadi ndani.
Pole sana mkuu! Naskia kuna baadhi ya binadamu wanawatetea hawa wadudu kibaya wanawafuga kabisa sijui wana maana gani..!!!!
 
Ni kweli wengine wanawafuga tena watafutia chakula, hapa Mwanza kuna sehemu ina Bujora kuna makumbusho watalii wa nje na ndani wanatembelea humo, huwa wanafuga chatu, wanawalisha kuku na sungura, tena hao chatu hawali mzoga, inabidi kuku au sungura anaachiwa akianza kukimbia wao ndio wanamfukuza hadi wanamkamata
 
Hii hatari!! Badala ya kuku kuliwa na binadamu, anapewa kiumbe ambaye ni adui hatari wa maisha ya binadamu...
 
Wanatunzwa kwa gharama kubwa sana!
Nakumbuka kuna siku kulikuwa na kongamano Fulani, basi waandaji wakaona tuwaalike hao wacheza ngoma wa Bujora ambao wanacheza na nyoka, mgeni rasmi alikuwa Dr. Mary Nagu, saalaaale!!! kumbe wambulu wanaogopa nyoka, yaani ile tunaingia getini alivyoona wale nyoka aliruka mama wa watu akaniuliza"........ ndio mmeandaa nini hiki?"
Nyoka sio kabisa
 
Heri ya mwezi mpya wa Novemba, 2017 wanajf.

Jana muda wa saa mbili usiku nilistuka kumuona nyoka yuko ndani kwangu, pembeni ya mlango wa kutokea nje!

Nyoka wa kimo cha kati, mweusi.

Nimeshangaa amepitia wapi na hali milango imefungwa, amewezaje kupita kwenye vigae na hali vigae vinateleza.

Niliogopa na hata kuchanganyikiwa!

Mungu mkubwa, ninaishi vizuri na majirani zangu waliweza kunisaidia kumuua!!!
Nimelala nastuka nastuka namuona kama vile ananipandia kitandani.

Naomba mnisaidie ushauri na kinga ya kuzuia huyo "ndudu" asiingie tena ndani na hali sioni sehemu ya kumuwezesha kupenya hadi ndani.
Pole mkuu, mwagia mafuta ya taa nyoka, na mafuta ya taa vitu viwili tofauti.
 
aggyjay chini hakuna upenyo! ila mie kwa imani yangu ya kanisa katoliki nilichofanya nilinyunyizia maji ya Baraka nyumba nzima
Pole Mkuu
Ni hivi upepo mkali hupeperusha vingi kama una miti karibu na nyumba inawezekana alipeperushwa na upepo karibu na mlango sometimes wanaangukia kwenye madirisha akajisogeza palipo na joto mfano kwenye kingo za milango vitanda makabati etc.
Maji ya baraka ni vyema kulingana na imani yako. Maombi na kukemea pepo wabaya ni jambo jema pia.
Kuwa mzoefu wa kuchoma chumvi ya mawe na hata kunyunyiza kwenye vichaka au miti karibu na nyumba utawafukuza nyoka. Chumvi ni adui wa nyoka.
 
Naomba nije kukusaidia kulala humo ili nyoka akija nipambane nae Effectively
 
Back
Top Bottom