Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Dah! Upo kama me nina binti wa kislamu me ni mkristo huyu mwanamke ni mzuri ile mbaya ananipa mahaba haswa ukirudi home anivua shati, viatu sometimes nalishwa sema sasa hiv kasafiri kikazi nimemmiss ila alinipa tahadhari kuwa Wazazi wake hawapendi yeye aje aolewe na mkristo ingawa bado sijajitambulisha kwao kujulikana.Mzee baba niliwahi kuleta mada hapa "Wanawake wa waislamu wengi Wana mahaba ukilinganisha na wakristo wakristo wanakwama wapi"? kuna baadhi wakanipinga especially wanawake wa kikristo lakini uhalisia tunauona sisi Wanaume kiukweli wanawake wakislamu wanajua mahaba na wajua kumtreat mwanaume vizuri kwenye Hili lazima tuwape sifa yao na mademu wakikristo wasione wivu kuna jambo la kujifunza kwao
Weeehhh!! Sasa si ubadili dini tu kaka, Wote tunamwabudu Mwenyezi Mungu na kikubwa amani ya moyo
 
yeye akiwa ni Muislam na mie Mkristo;

Alikua pisi haswa, mtoto mkaree kila angle na anayajua mapenzi haswa, nikasema tabu za nini hasa ukizingatia bint mwenyewe ananitii kila nnalomwambia, sikua na upinzani wowote kwake, najipigia mwenyewe tu ki uhakika.

Sasa nilivyotangaza tu kumuoa na kuwaambia ndugu na jamaa kwamba kuna sehemu nimenasa na sasa nabeba jiko jumla hapo sasa ndio vita vikazuka, mwanzo nikaona ni mambo ya kawaida "jamaa wanaingilia maisha ya watu tena, hawa hawanijui hawa?" Lakin nikashangaa wazazi wote pande mbili wanapinga, wajomba wameshika mabango kwamba watu wa dini ile nyingine hakuna kabisa hawafai, nikasema eeh maji mazito kuliko damu ya mtume?

Binti alikua so so down, hana mzuka kabisa, mie na fosi bibie tulia wala usiwe na hofu dini tumeletewa na mabeberu tu, lakin ikamshinda nguvu maskini binti wa watu analia, maza ake nae kaja juu anasema kijana mkristow hakanyagi hapa kwangu, huba likakosa connection kabisa kimzaa mzaa tu, tukawa tunakulana tu na binti akawa anasema haoni future sa itakuaje? Nikamwambia basi tuzae tu wataelewa, akasisitiza mtume alishapinga kuzaa nje ya ndoa, basi ikaishia ivyo tu na sasa binti yupo na shekhe wake msoma visomo.

Hivi hua kuna bifu la chini chini kati ya hizi dini mbili? na raia hua hawasemi au ni nini? why wakule ni wakule na wa huku ni wa huku hakuna kuingiliana?
Kama unampenda badili wewe dini.
 
Ukitaka kuharibu jamii basi ruhusu mahusiano ya kimapenzi baina ya imani mbili tofauti.

Ukiona mtu ana uhusiano wa kimapenzi na mtu wa imani nyingine huyo hajitambui au anajiendekeza. Huu ukweli mchungu.
 
Mimi nilibadili dini kitambo kidogo nikiwa na miaka 17 Ukristo kwenda Uislamu. Lakini nilichokiona huko ni tofauti kabisa na nilichokuwa naamini. Hizi dini zipo tu tuzifuate lakini siyo kila unachoambiwa ukichukulie kuwa ni kweli.
 
Dah umenikumbusha kaka yangu alipomfata ex wangu eti niachane nae kisa ni dini tofauti tena alimfata na panga hiki kisa natamani niazishie uzi yale mahusiano nilipigwa mikanda sana home😬
Sasa bibie ilikuwaje ukawa na mahusiano na mtu wa imani tofauti na yako ? Au ndiyo huwa mnasema Mapenzi ni upofu ?
 
Lakini zote zinatambulika kama Ibrahimism, zina vinasaba vya pamoja na ndio maana mitume karibu wote wanatajwa na vitabu vya dini hizi mbili kwa pamoja na matendo yale yale.
Hiyo siyo kweli hili jina wanalitumia kimakosa. Nabii Ibrahimu alikuwa Muislamu, Uyahudi na Ukristo ni Dini zilizo kuja kuzuliwa, ukiziangalia zote zimewakana mitume walio fata baadae.
 
Hapa ndipo vijana wengi tunapokwama.

Unajua fika wewe ni dini tofauti na mpenzi wako. Unajua fika ukifosi kuna sehem pande zote mbili kwa wazazi na ndugu mtatengwa. Tena hata mkifosi mkaoana kuna uwezekano watoto wakakosa direction na kujua wafate mafundisho ya dini gani maana wazazi mpo dini tofauti. Mmoja anasali msikitini mwngne kanisani. Wapo mtakaosema ikitokea tumezaa mtoto akikua ataamua afate dini ipi! Jamani mafunzo mazuri ya dini siku zote huanzia utotoni, hapo ndipo mtoto anapopata good narration to see the right and wrong.

Hali hii itazidi kuwatafuna kadri vizazi vyenu vitakavyoendelea na hakutakua na amani ndani. Trust me hakutakua na amani. Najua wapo watakaonipinga na kusema mapenzi hayaangalii dini. Ni kweli mapenzi hayaangalii dini, lakini kuishi na mtu kama mke na mume dini lazima ipewe kipaumbele chake. Tena ni kigezo muhimu sana hiko wala tusidanganyane.

Tusitake kuishi kizungu wakati bado tamaduni zetu hazijafika huko. Na sidhani kama tutafika huko maana kila dini ina mafundisho yake na tunarithishana vizazi na vizazi. Kuepuka usumbufu wowote ule na mpasuko ktk familia ni bora uwe na mahusiano na mtu wa dini yako. Itakuweka huru sana.

Ifike hatua tusiishi kwa kuendeshwa na hisia bali akili. I REST MY CASE.
Umeandika vya maana sana, ndiyo maana nasema watu wanajiendekeza na kuzembea.

Watu waende na watu wa imani zao, mbona wako wengi sana.
 
Ni hatari mimi marehemu baba alisema nikioa mwanamke wa kiislamu hatakaa aingie kwenye kizingiti cha mlango wake hata akiwa kaburini naogopa kweli kweli. ingawa nilipataga toto moja inajua kunidekeza hatari nikaona simfanyii poa nikamuacha nisimpotezee mda.Hizi dini bana.
 
Watoto zetu wa kike mna ujinga mwingi sana huwa mnaona hakuna maisha baada ya huba . Allah awasitiri na awape msimamo thabiti, kuna sehemu ulikosea bibie.
kila kitu ni mipango ya Mungu upendo sioni na siwezi kuushika ila nahisi upo kama imetokea nimependa sehemu nawezaje kujizuia maana kwa hakika hakitokei kitu bila Allah kubariki basi asingenipa upendo kwa Mwanaume dini tofauti hata hivyo tuliachana
 
Back
Top Bottom