Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Nilitaka kumuoa binti wa Dini tofauti na yangu vita kubwa ikaibuka. Kuna kitu gani kati ya hizi dini mbili?

Umenikumbusha mbali 😄
Sijui yuko wapi huyu ustadh feki wangu
 
Kosa langu ni lipi mkuu ulishawahi zuia upendo

IMG_20220502_145722.jpg
 
Ideally zote ni Abrahamic religions lakini uchunguzi wa kina unaonyesha Islam wanamuabudu Allah ambaye siyo Yehova ambaye ni Mungu wa Abraham. Unaweza ukasema ni majina tu, Mungu ni yuleyule lakini siyo kweli
Ulivopakazania hapo pakusema Allah sio Mungu sasa,
Mi mnyakyusa yesu namwita Kyala.......!!! napo utakataa utasema huyo Yesu na kyala ni watu wawili tofauti.


Yani wakristo na waislamu imefika point nawaonaga wapuuzi tu,.....wana haribu image ya Mungu, wameharibu na kuvuruga ovyo maandiko ya Mungu kwenye vitabu vyake, mfano wew mleta mada hapa......umejawa chuki uliolishwa na wachungaji zako....
Atakuja muislamu nae atashusha chuki juu ya ukristo aliolishwa na mashekhe wake na maustadh.

Kwa kifupi kuna wakati nawaona nyie wote mafala tu.

Mmejitoa kabisa katika ibada na misingi sahihi ya Mungu.

Utafiti uliofanyika mwaka 2013 unaonesha utofauti wa dini na mafundisho yake unachangia 30% ya chuki baina ya binadamu na binadamu duniani.

Ndo zinafata tofauti kama "Rangi za ngozi, Mali, Ukabila, etc
 
Hapa ndipo vijana wengi tunapokwama.

Unajua fika wewe ni dini tofauti na mpenzi wako. Unajua fika ukifosi kuna sehem pande zote mbili kwa wazazi na ndugu mtatengwa. Tena hata mkifosi mkaoana kuna uwezekano watoto wakakosa direction na kujua wafate mafundisho ya dini g
Hahahahaa naona mkuu umeshasahau kwamba hata maisha ya udini ( ukristo, uislamu, ubuda, uyahudi etc) ni maisha ya wazungu na wa asia sio maisha ya kiafrika.

Yalizolewa tu huko yakaletwa huku afu sa hv wenyewe kule wameyatupa na kutusia. (maajabu ni kwamba unaweza ukaja ukapinga hili, nawajua nyie)

Waafrica bhana[emoji38][emoji38].
 
by the way,,,,,wazazi wangu ni dini mbili tofauti ( ukristo na uislamu) dada angu akapata wito moyoni akaenda sabato, mdogo wangu mmoja ni Assemblies mwingine Mroman,

Na wengine wawili wamepata kuona kama wanaitwa zaid kwenye uislamu basi wapo huko.

Na ukitukuta wote kipindi cha likizo tupo nyumbani huwezi hata kidogo kudhani sisi wote ni dini tofauti.

Yote ni kwa sababu wazazi hawakuamua hata kidogo kutuchagulia njia ya Kumfikia Mungu au kutufanya tufate njia zao, ( vipi tufike huko tukute baba hakua njia sahihi na tulimfata yeye). Na hyo sio excuse kabisa kwa Mungu, anakukoka live live. ( au vip tusali dhehebu la mama afu tufike huko tukute kumbe hakua sahihi) Kutokuijua sheria hakuipunguzi makali, Mungu ataturoast.

Mwisho wa siku ni kwamba tu, unachokiabudu, make sure ndicho hicho ulikichagua tena kwa upembuzi yakinifu na ukiwa na akili zako timamu za utambuzi, ( then weka imani hapo na uamini kwa imani thabiti haswa)

Mungu hana excuse ya (ooooohh Mungu hii dini alinifundisha baba au ni mama alianza kunipeleka tangu mdogo)

Atakuchoma mchana kweupeeeee!!!! usiamini na macho yako
 
yeye akiwa ni Muislam na mie Mkristo;

Alikua pisi haswa, mtoto mkaree kila angle na anayajua mapenzi haswa, nikasema tabu za nini hasa ukizingatia bint mwenyewe ananitii kila nnalomwambia, sikua na upinzani wowote kwake, najipigia mwenyewe tu ki uhakika.
Sina hata hamu na haya mambo ya dini

Kijana wa watu aliforce akaleta barua Ivo Ivo licha ya kua alijua dini ni tofauti

Walichomjibu home kwenye io barua sina hamu na mama wala hao kaka zake wanaojiita wajomba (mana mzee yupo mbali)

[emoji1][emoji1][emoji2] Kuanzia pale kijana wa watu akabadilika ,uku mwenzie bado nampenda yani niliteseka na ninateseka mpka kesho mana ni ngumu kuachia penzi lake na yeye kuniacha hataki kutamka ila ni matukio tu kimya kimya napigwa

Nilimwambia mama hayo majibu yenu mliomjibu uyo mtoto wa watu na kaka zako mimi yananitesa sasa

Kijana mkristo( licha ya kua mama ake alikua muislam akabadili dini kua mkristo)

Mimi muislam
 
kila kitu ni mipango ya Mungu upendo sioni na siwezi kuushika ila nahisi upo kama imetokea nimependa sehemu nawezaje kujizuia maana kwa hakika hakitokei kitu bila Allah kubariki basi asingenipa upendo kwa Mwanaume dini tofauti hata hivyo tuliachana
Ukielekea sehemu fulani Allah anakuacha uelekee huko huko na Allah anabariki mambo ya kheri tu. Jiulize kwanini kuna maovu na ukifanya uovu unalipwa adhabu, almuhimu hilo tuliache.
 
Hapo ndipo inatokea unakuja kuoa Dini yako.
Unakuwa kama umeoa Pepo..unateseka vibaya mno mpaka unajuta kuzaliwa.
Halafu kwenye familia anatokea mjinga mmoja anakwambia aisee Bro bora angeoa yule Dada yule wa Kiislamu.

Yanatokea kila siku kwenye maisha yetu hayo.
 
yeye akiwa ni Muislam na mie Mkristo;

Alikua pisi haswa, mtoto mkaree kila angle na anayajua mapenzi haswa, nikasema tabu za nini hasa ukizingatia bint mwenyewe ananitii kila nnalomwambia, sikua na upinzani wowote kwake, najipigia mwenyewe tu ki uhakika.

Sasa nilivyotangaza tu kumuoa na kuwaambia ndugu na jamaa kwamba kuna sehemu nimenasa na sasa nabeba jiko jumla hapo sasa ndio vita vikazuka, mwanzo nikaona ni mambo ya kawaida "jamaa wanaingilia maisha ya watu tena, hawa hawanijui hawa?" Lakin nikashangaa wazazi wote pande mbili wanapinga, wajomba wameshika mabango kwamba watu wa dini ile nyingine hakuna kabisa hawafai, nikasema eeh maji mazito kuliko damu ya mtume?

Binti alikua so so down, hana mzuka kabisa, mie na fosi bibie tulia wala usiwe na hofu dini tumeletewa na mabeberu tu, lakin ikamshinda nguvu maskini binti wa watu analia, maza ake nae kaja juu anasema kijana mkristow hakanyagi hapa kwangu, huba likakosa connection kabisa kimzaa mzaa tu, tukawa tunakulana tu na binti akawa anasema haoni future sa itakuaje? Nikamwambia basi tuzae tu wataelewa, akasisitiza mtume alishapinga kuzaa nje ya ndoa, basi ikaishia ivyo tu na sasa binti yupo na shekhe wake msoma visomo.

Hivi hua kuna bifu la chini chini kati ya hizi dini mbili? na raia hua hawasemi au ni nini? why wakule ni wakule na wa huku ni wa huku hakuna kuingiliana?

Wewe kafiri hebu muache Binti wa ki-islamu huyo, unataka kumlisha nguruwe ama??
 
Ideally zote ni Abrahamic religions lakini uchunguzi wa kina unaonyesha Islam wanamuabudu Allah ambaye siyo Yehova ambaye ni Mungu wa Abraham. Unaweza ukasema ni majina tu, Mungu ni yuleyule lakini siyo kweli
hujui kitu unaropoka kama umekunywa maji ya chooni we mfuasi wa paulo
 
Dah! Upo kama me nina binti wa kislamu me ni mkristo huyu mwanamke ni mzuri ile mbaya ananipa mahaba haswa ukirudi home anivua shati, viatu sometimes nalishwa sema sasa hiv kasafiri kikazi nimemmiss ila alinipa tahadhari kuwa Wazazi wake hawapendi yeye aje aolewe na mkristo ingawa bado sijajitambulisha kwao kujulikana.Mzee baba niliwahi kuleta mada hapa "Wanawake wa waislamu wengi Wana mahaba ukilinganisha na wakristo wakristo wanakwama wapi"? kuna baadhi wakanipinga especially wanawake wa kikristo lakini uhalisia tunauona sisi Wanaume kiukweli wanawake wakislamu wanajua mahaba na wajua kumtreat mwanaume vizuri kwenye Hili lazima tuwape sifa yao na mademu wakikristo wasione wivu kuna jambo la kujifunza kwao
Mmmmmh [emoji849][emoji849][emoji849] hao wakristo umedate nao wangapi mkuu??
 
Lakini zote zinatambulika kama Ibrahimism, zina vinasaba vya pamoja na ndio maana mitume karibu wote wanatajwa na vitabu vya dini hizi mbili kwa pamoja na matendo yale yale.
Tulikuja kugawanyika baada ya Yesu.
Soma biblia vzr kwann Mungu alikuwa anawakataza wana waisrel kuoa,kuolewa kila mahali?
Ngoja nitafute zile verse
 
Ukielekea sehemu fulani Allah anakuacha uelekee huko huko na Allah anabariki mambo ya kheri tu. Jiulize kwanini kuna maovu na ukifanya uovu unalipwa adhabu, almuhimu hilo tuliache.
وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

“Atakayempinga Mtume baada ya kumbainikia uongofu na akafuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamwacha aelekee huko alikoelekea na [baadaye] Tutamwingiza Motoni – na uovu ulioje mahali pa kuishia.” (04:115)

Allah atuongoze na atuhifadhi.
 
Ideally zote ni Abrahamic religions lakini uchunguzi wa kina unaonyesha Islam wanamuabudu Allah ambaye siyo Yehova ambaye ni Mungu wa Abraham. Unaweza ukasema ni majina tu, Mungu ni yuleyule lakini siyo kweli
Fact
Hatuabudu Mungu mmoja kabisa ,huu ni ukweli mchungu ambao wengi hawaujui
 
Back
Top Bottom