Mtu mzima akilia hakika ujue kuna jambo. Majuzi nililia njia nzima mpaka kufikia kushindwa ku drive vizuri. Roho inaniuma mpaka muda huu ninaoandika hapa.
Dada zetu wamechoka, dada zetu wana hali mbaya. Ni mabinti wa miaka 15 mpaka 25 wengi wao, ila sura zinakataa, sura zimechoka, sura za kizee[emoji24][emoji24][emoji24]
Nilifikiria mengi. Wamekata tamaa ya maisha na je, miongoni mwao angekuwepo dada au ndugu yangu yeyote?
Nilikuwa naingia vyumbani(kwa Wahaya) as if nataka huduma, nauliza bei then namlipa mara mbili yake na kutoka nje. Nilifanya hivi kwa wale malaya walioonekana kuwa na umri mkubwa mno[emoji24] naumia sana.
Na hata kwa vibinti nilifanya vivyo hivyo, Kimboka nilitoa machozi, Lubumbashi, River Side, Kitambaa cheupe n.k japo kwa siku tofauti tofauti.
Naumia sana[emoji24][emoji24][emoji24] daaaah
Kumbe kuna watu wanateseka hivi?
Roho inaniuma mno.
Naomba nisiendelee tafadhali[emoji24]