Rais Samia alipoingia madarakani mwaka 2021 katika hotuba zake za mwanzoni kabisa aliwahi kusema kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Nakumbuka siku ile niliposikia matamshi hayo nilipatwa na hofu ndani yangu kwani kwanza sikutegemea angesema hayo na pili mimi nilielewa maneno hayo yalimaanisha nini katika utendaji wa kawaida wa serkali, masuala ya haki, demokrasia na uchumi wa Taifa.
Pia nilielewa nini maana ya matamshi hayo katika roho ya kujiweka sambamba na hayati Magufuli na kufikia kusema kuwa yeye (Samia) ni kitu kimoja na Magufuli.
Pamoja na kuwa wawili hawa ni tofauti sana kimaumbile, haiba na katika mambo mengi mengine, yawezekana kweli wao ni kitu kimoja katika masuala ya weledi wa utunzaji na matumizi ya rasilimali za taifa, demokrasia, haki ya kujieleza na mtindo wa kisiasa unaozingatia waimba sifa wengi na matumizi makubwa ya rasilimali za wananchi maskini kushindana na wapinzani au wakosoaji ili kuendelea kubaki madarakani.
Wanachotofautiana viongozi hawa wawili ni ile namna yao ya kufanya jambo lile lile.
Tumwombee rais Samia aepukane na matumizi ya nguvu na ubabe dhidi ya wakosoaji au wapinzani wake kisiasa, na asiwe kitu kimoja na mtangulizi wake katika mambo haya.