Kijakazi Chizi
Member
- Dec 9, 2025
- 89
- 213
Pole kwa kuumizwa na mtu uliyemuamini kama rafiki.hayo yamepita.songa mbeleWanasema urafiki wa kweli hujengwa kwenye misingi ya kuaminiana, kusaidiana kwenye shida na kulindana dhidi ya jambo lolote linaloumiza. Lakini maisha yangu kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni yalikuja kunivuruga kabisa, na kunifanya nianze kujihoji:
Hivi kweli nahitaji watu maishani mwangu kama rafiki, au ni bora tu nisonge mbele peke yangu?
Katika muhula wa kwanza, nilikuwa na bahati ya kupata chumba kwenye hosteli za chuo. Siku niliyofika kwenda kukiangalia chumba hicho kabla ya kuhamia rasmi, nilikuta roommate wangu tayari kaingia. Alikuwa mchangamfu sana, mwenye upendo, na muongeaji kweli kweli.
Kuna msemo unasema, "Kabla ya kuzoea watu au mahali kwa haraka, soma kwanza mazingira." Kawaida yangu, pindi ninapokutana na watu wapya au mazingira mapya, huwa nachagua kukaa kimya kama introvert, japo kiuhalisia mimi ni mtu mchangamfu sana na wa watu. Hata hivyo, ukaribu wetu kama roomates ulizaa urafiki mkubwa sana, na baada ya muda, tukajikuta tunatengeneza kundi kubwa zaidi la marafiki.
Mwaka wa pili chuoni roomate wangu aliamua kugombea nafasi ya Katibu wa chuo. Sisi kama marafiki zake wa damu, tulijitoa kwa hali na mali kumuunga mkono kwenye kampeni zake zote, na kwa baraka za Mungu, alishinda nafasi ile. Kwenye lile kundi letu la marafiki, mimi ndiye niliyekuwa mtu wa kimya zaidi kuliko wote hadi kuna watu wengine walikuwa wananambia nimekosea njia.
Siku zikaenda, basi kukatangazwa programu moja maalum iliyokuwa ikileta fursa kwa wasichana chuoni. Kwa sababu rafiki yangu sasa alikuwa kiongozi, alizipata habari hizo mapema kabisa kabla hazijawa wazi kwa umma. Kwa wema kabisa, alikuja kutushirikisha sisi marafiki zake na kutusaidia majina yetu yawe miongoni mwa wanafunzi wachache waliofanikiwa kuingia kwenye fursa hiyo.
Programu ilianza vizuri sana. Siku moja, mkufunzi wetu alimualika mtu maarufu sana mtandaoni ambaye sote tulikuwa na shauku kubwa ya kukutana naye. Baada ya somo kuisha, tuliruhusiwa kwenda kupiga naye picha. Hapo ndipo palikuwa mwanzo wa donda langu la moyo, tukio lililonifanya nijione sifai na sina thamani yoyote.
Wakati kila mtu akikimbilia mbele kupata picha na yule staa, mimi pia nilisogea karibu kwa upole ili nipate kumbukumbu yangu. Ghafla, nilisikia sauti ya yule rafiki yangu niliyemwamini na kumthamini ikipaza sauti:
"Wewe Diana, toka apo na sura yako mbaya, waachie wengine wapige picha!"
Moyo wangu uliumia. Nilijihisi kufedheheshwa, na niliyeaibishwa mbele ya watu wote. Nilishindwa hata kupiga ile picha.
Mimi si mtu wa kugombana au kurudisha maneno kumface mtu kumchana siwezi kabisa. Huwa nachagua kukaa kimya na kufanya maaamuzi sahihi kwangu.
Tangu siku ile, ilinichukua muda nikibishana na nafsi yangu kama kweli nilikuwa kwenye kundi sahihi la marafiki. Mwishowe, nilichukua uamuzi wa kujitenga, kukaa na kusimama peke yangu na mambo yangu.
Niliuvunja ule urafiki kwa sababu haukuwa salama tena kwa afya ya akili yangu. Maneno ya kashfa na dharau kutoka kwa mtu niliyemwita rafiki yaligeuka kuwa sumu na maumivu kwenye moyo wangu.
Utani kama huu akitaniwa mtu ambaye ni mzuri hauna shida ila kwa sie tunaoambiwaga 'Beauty is in the eye of the beholder' unachoma kama pasiLabda ni utani tu!
Duh! Sijawahi experience lakini mtu akiniambia hivi atakuwa na chuki na dharau sana! Lazima utajisikia vibaya tu!Utani kama huu akitaniwa mtu ambaye ni mzuri hauna shida ila kwa sie tunaoambiwaga 'Beauty is in the eyes of the beholder' unachoma kama pasi
Issue ni kauli inatoka kwa mtu ambaye unamuaminia ambaye hukutegemea kabisa kukudhalilisha mbele za watuKwani hadi unafika chuo hukuwahi kuambiwa una sura personal?
kuna kitu kinaitwa tone na pitch kwenye matamshi, ukivijua ni rahisi sana kutambua hii imetumika kwa dhamira ganiLabda ni utani tu!
Asante sana, nimemove on muda sana na leo nimeshare kama uelewa tu kwamba tuwe makini katika kuchagua watu wa kuwa nao karibu na pia unapoona red-flag jitathmini kama inafaa kwako kuimuduPole kwa kuumizwa na mtu uliyemuamini kama rafiki.hayo yamepita.songa mbele
Kwa sasa nime-glow π π πWeka picha yako hapa tuichambue kama kuna kasoro
Anayejua thamani yako halisi ni Mungu muumba wako, hivyo msikilize yeye anachokunenea kisha kishike kama kilivyo pasipo kuyumbishwa na misemo ya mitaani ya walimwengu.Wanasema urafiki wa kweli hujengwa kwenye misingi ya kuaminiana, kusaidiana kwenye shida na kulindana dhidi ya jambo lolote linaloumiza. Lakini maisha yangu kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni yalikuja kunivuruga kabisa, na kunifanya nianze kujihoji:
Hivi kweli nahitaji watu maishani mwangu kama rafiki, au ni bora tu nisonge mbele peke yangu?
Katika muhula wa kwanza, nilikuwa na bahati ya kupata chumba kwenye hosteli za chuo. Siku niliyofika kwenda kukiangalia chumba hicho kabla ya kuhamia rasmi, nilikuta roommate wangu tayari kaingia. Alikuwa mchangamfu sana, mwenye upendo, na muongeaji kweli kweli.
Kuna msemo unasema, "Kabla ya kuzoea watu au mahali kwa haraka, soma kwanza mazingira." Kawaida yangu, pindi ninapokutana na watu wapya au mazingira mapya, huwa nachagua kukaa kimya kama introvert, japo kiuhalisia mimi ni mtu mchangamfu sana na wa watu. Hata hivyo, ukaribu wetu kama roomates ulizaa urafiki mkubwa sana, na baada ya muda, tukajikuta tunatengeneza kundi kubwa zaidi la marafiki.
Mwaka wa pili chuoni roomate wangu aliamua kugombea nafasi ya Katibu wa chuo. Sisi kama marafiki zake wa damu, tulijitoa kwa hali na mali kumuunga mkono kwenye kampeni zake zote, na kwa baraka za Mungu, alishinda nafasi ile. Kwenye lile kundi letu la marafiki, mimi ndiye niliyekuwa mtu wa kimya zaidi kuliko wote hadi kuna watu wengine walikuwa wananambia nimekosea njia.
Siku zikaenda, basi kukatangazwa programu moja maalum iliyokuwa ikileta fursa kwa wasichana chuoni. Kwa sababu rafiki yangu sasa alikuwa kiongozi, alizipata habari hizo mapema kabisa kabla hazijawa wazi kwa umma. Kwa wema kabisa, alikuja kutushirikisha sisi marafiki zake na kutusaidia majina yetu yawe miongoni mwa wanafunzi wachache waliofanikiwa kuingia kwenye fursa hiyo.
Programu ilianza vizuri sana. Siku moja, mkufunzi wetu alimualika mtu maarufu sana mtandaoni ambaye sote tulikuwa na shauku kubwa ya kukutana naye. Baada ya somo kuisha, tuliruhusiwa kwenda kupiga naye picha. Hapo ndipo palikuwa mwanzo wa donda langu la moyo, tukio lililonifanya nijione sifai na sina thamani yoyote.
Wakati kila mtu akikimbilia mbele kupata picha na yule staa, mimi pia nilisogea karibu kwa upole ili nipate kumbukumbu yangu. Ghafla, nilisikia sauti ya yule rafiki yangu niliyemwamini na kumthamini ikipaza sauti:
"Wewe Diana, toka apo na sura yako mbaya, waachie wengine wapige picha!"
Moyo wangu uliumia. Nilijihisi kufedheheshwa, na niliyeaibishwa mbele ya watu wote. Nilishindwa hata kupiga ile picha.
Mimi si mtu wa kugombana au kurudisha maneno kumface mtu kumchana siwezi kabisa. Huwa nachagua kukaa kimya na kufanya maaamuzi sahihi kwangu.
Tangu siku ile, ilinichukua muda nikibishana na nafsi yangu kama kweli nilikuwa kwenye kundi sahihi la marafiki. Mwishowe, nilichukua uamuzi wa kujitenga, kukaa na kusimama peke yangu na mambo yangu.
Niliuvunja ule urafiki kwa sababu haukuwa salama tena kwa afya ya akili yangu. Maneno ya kashfa na dharau kutoka kwa mtu niliyemwita rafiki yaligeuka kuwa sumu na maumivu kwenye moyo wangu.
Asante sana, nimeichukua hiiChukua hii ka
Anayejua thamani yako halisi ni Mungu muumba wako, hivyo msikilize yeye anachokunenea kisha kishike kama kilivyo pasipo kuyumbishwa na misemo ya mitaani ya walimwengu.
Miluzi mingi humpoteza.......!
sema utan kutokana na mazingira, fikilia utaniwe mbele ya watu afu waangue vicheko na kibaya zaid huyu ni introvert ni ngumu kutafsiri halaka neo kwa mda huo.Labda ni utani tu!
kwakweli mimi hata nisingefikiria mara mbili! πsema utan kutokana na mazingira, fikilia utaniwe mbele ya watu afu waangue vicheko na kibaya zaid huyu ni introvert ni ngumu kutafsiri halaka neo kwa mda huo.
Angekua Extrovert angemjibu kwa haraka palepale kama utan