Nilivunja urafiki wetu baada ya kauli iliyonidhalilisha na kunikejeli nina sura mbaya

Nilivunja urafiki wetu baada ya kauli iliyonidhalilisha na kunikejeli nina sura mbaya

Kwa vile bado ni kijana na bado uko chuo, naona bora nikusanue mapema. Achana na habari za marafiki ni delusion tu. Hakuna marafiki ni watu unaofahamiana nao tu, kaa ukijua no body care for you. Anza kupunguza watu mapema hii itakufanya watu wasikutumie kwenye maisha yako kwasababu hapa Duniani everyone wants to use you. Jaribu kuwa na privacy na kama hawakujui sana, then it'll be difficult to hurt your feelings
 
Kwa vile bado ni kijana na bado uko chuo, naona bora nikusanue mapema. Achana na habari za marafiki ni delusion tu. Hakuna marafiki ni watu unaofahamiana nao tu, kaa ukijua no body care for you. Anza kupunguza watu mapema hii itakufanya watu wasikutumie kwenye maisha yako kwasababu hapa Duniani everyone wants to use you. Jaribu kuwa na privacy na kama hawakujui sana, then it'll be difficult to hurt your feelings
Asante sana kwa ushauri, tayari nimeshahitimu chuo miaka mingi sana ila nime-share as an experience ambayo pia inawezekana wengine wameipitia au ndo wanaipitia bila kujua ni red-flag na and pia kujifunza kujiweka kipaumbele
 
Pole kipenzi 😢
Mie huambiwa nina sauti ya madeko na hua nakwazika utasikia we nae kaza sauti hii hua inanikwaza sana but napotezea tu

Jipende jikubari 🫂
Asante sana dear,
Najipa moyo sana maana kuna siku niliwahi kuandika pia mahusiano yangu yaliyodumu miaka 3 na baadaye akaniacha, baadaye kuna bestie yake alinambia kumbe alikuwa anaona aibu kuwa na mimi kisa muonekano wangu wa sura
 
Wanasema urafiki wa kweli hujengwa kwenye misingi ya kuaminiana, kusaidiana kwenye shida na kulindana dhidi ya jambo lolote linaloumiza. Lakini maisha yangu kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni yalikuja kunivuruga kabisa, na kunifanya nianze kujihoji:

Hivi kweli nahitaji watu maishani mwangu kama rafiki, au ni bora tu nisonge mbele peke yangu?

Katika muhula wa kwanza, nilikuwa na bahati ya kupata chumba kwenye hosteli za chuo. Siku niliyofika kwenda kukiangalia chumba hicho kabla ya kuhamia rasmi, nilikuta roommate wangu tayari kaingia. Alikuwa mchangamfu sana, mwenye upendo, na muongeaji kweli kweli.

Kuna msemo unasema, "Kabla ya kuzoea watu au mahali kwa haraka, soma kwanza mazingira." Kawaida yangu, pindi ninapokutana na watu wapya au mazingira mapya, huwa nachagua kukaa kimya kama introvert, japo kiuhalisia mimi ni mtu mchangamfu sana na wa watu. Hata hivyo, ukaribu wetu kama roomates ulizaa urafiki mkubwa sana, na baada ya muda, tukajikuta tunatengeneza kundi kubwa zaidi la marafiki.

Mwaka wa pili chuoni roomate wangu aliamua kugombea nafasi ya Katibu wa chuo. Sisi kama marafiki zake wa damu, tulijitoa kwa hali na mali kumuunga mkono kwenye kampeni zake zote, na kwa baraka za Mungu, alishinda nafasi ile. Kwenye lile kundi letu la marafiki, mimi ndiye niliyekuwa mtu wa kimya zaidi kuliko wote hadi kuna watu wengine walikuwa wananambia nimekosea njia.

Siku zikaenda, basi kukatangazwa programu moja maalum iliyokuwa ikileta fursa kwa wasichana chuoni. Kwa sababu rafiki yangu sasa alikuwa kiongozi, alizipata habari hizo mapema kabisa kabla hazijawa wazi kwa umma. Kwa wema kabisa, alikuja kutushirikisha sisi marafiki zake na kutusaidia majina yetu yawe miongoni mwa wanafunzi wachache waliofanikiwa kuingia kwenye fursa hiyo.

Programu ilianza vizuri sana. Siku moja, mkufunzi wetu alimualika mtu maarufu sana mtandaoni ambaye sote tulikuwa na shauku kubwa ya kukutana naye. Baada ya somo kuisha, tuliruhusiwa kwenda kupiga naye picha. Hapo ndipo palikuwa mwanzo wa donda langu la moyo, tukio lililonifanya nijione sifai na sina thamani yoyote.

Wakati kila mtu akikimbilia mbele kupata picha na yule staa, mimi pia nilisogea karibu kwa upole ili nipate kumbukumbu yangu. Ghafla, nilisikia sauti ya yule rafiki yangu niliyemwamini na kumthamini ikipaza sauti:

"Wewe Diana, toka apo na sura yako mbaya, waachie wengine wapige picha!"

Moyo wangu uliumia. Nilijihisi kufedheheshwa, na niliyeaibishwa mbele ya watu wote. Nilishindwa hata kupiga ile picha.

Mimi si mtu wa kugombana au kurudisha maneno kumface mtu kumchana siwezi kabisa. Huwa nachagua kukaa kimya na kufanya maaamuzi sahihi kwangu.

Tangu siku ile, ilinichukua muda nikibishana na nafsi yangu kama kweli nilikuwa kwenye kundi sahihi la marafiki. Mwishowe, nilichukua uamuzi wa kujitenga, kukaa na kusimama peke yangu na mambo yangu.

Niliuvunja ule urafiki kwa sababu haukuwa salama tena kwa afya ya akili yangu. Maneno ya kashfa na dharau kutoka kwa mtu niliyemwita rafiki yaligeuka kuwa sumu na maumivu kwenye moyo wangu.
Njoo dm nikupe ushauri
 
Asante sana dear,
Najipa moyo sana maana kuna siku niliwahi kuandika pia mahusiano yangu yaliyodumu miaka 3 na baadaye akaniacha, baadaye kuna bestie yake alinambia kumbe alikuwa anaona aibu kuwa na mimi kisa muonekano wangu wa sura
Kwanni unajiita kijakazi chizi?
 
Asante sana dear,
Najipa moyo sana maana kuna siku niliwahi kuandika pia mahusiano yangu yaliyodumu miaka 3 na baadaye akaniacha, baadaye kuna bestie yake alinambia kumbe alikuwa anaona aibu kuwa na mimi kisa muonekano wangu wa sura
Nimegundua huyo hajawahi kua rafiki yako usikute huna sura mbaya ni chuki zake pole kipenzi we jifunze kupokea positive tu hizo negative zi ignore japo zinaumiza
 
Pole Sana,kuna ubaya mdogo unaweza kufanyiwa vikakuumiza Sana!
Mfano: Mimi Nikicheka yanatokea mashimo kwenye mashavu(dimpos)
Sasa kitu siwezi kujizuia ni kutabasamu,Yaani Mimi muda wote uso wangu Una bashasha,Kumbe kuna wanafunzi wenzangu hawapendi,Sasa kuna huyo mmoja alikua bausa alikua ananisemea maneno mabovu Sana,mara najichekesha ili kuonesha wanaume ma dimpos☹️☹️☹️
Kiukweli Yule dada sijawahi kumsamehe kutoka moyoni hata nikutane nae Leo!
 
Hiyo lugha ni misumari ya moto kwa mwanamke yyt kuambiwa hivo
hatari sana na mtu akiambia huwa haimtoki kichwani

mimi niliwahi muita mdada masudi (kwa maana ya masudi sura mbaya ) muda sana

kundi la shule la wasap likatukutanisha pamoja tena akiwa amesha pata kazi kampuni moja ya uanasheria n kawa mzuri sana

katika stori 2-3, kwenye kundi tukazama inbox na kutumiana picha aseeh nikachombeza vile amekuwa mrembo

akanambia najua unataman kuwa na mm ila huwez toboa maana kuna siku shuleni uliniita masudi hadi leo nakumbuka ko kaa mbali mita 100

ko haya maneno ukweli yanawaumiza sana wadada
 
Back
Top Bottom