Ray J Enterprise
Member
- Jul 18, 2022
- 49
- 57
Baada ya kuhitimu chuo kwa ngazi ya shahada nilipata sehemu ya kujishikiza kufundisha chuo ambacho kimsingi hakikuwa na kipato kikubwa sana kwa hivyo nilikuwa kama najitolea kwa muda wa miaka mitano.
Lakini badae tulianzisha programu ya kuwanufaisha wakufunzi kupitia kuleta wanafunzi kwa maana ya kwamba kila mtumishi wa chuo atanufaika kulingana na idadi ya wanafunzi aliowaleta. Kwa watumishi wote mimi ndiye niliibuka kinara kuleta wanafunzi wengi kuja kujiunga na chuo chetu. Nilipata uzoefu mkubwa ktk suala zima la marketing ya kutafuta wanafunzi.
Lakini pia nilipewa kazi kubwa kama mratibu wa mafunzo (mtaaluma na msajili na wakati mwingine nikikaimu Ukuu wa Chuo) hivyo nilijifunza mambo mengi ya uendeshaji na usimamizi wa chuo.
Katika kipindi ambacho nilileta wanafunzi wengi nilikidai chuo fedha nyingi sana kiasi ambacho wivu na ubinafsi ulianza kuibuka wakaanza kuleta uswahili na uhuni kwenye malipo kufikia hatua ya kushtakiana ili kushinikiza kulipa malipo yangu. Hali hii ilinivunja sana moyo na kunikatisha tamaa.
Nilianza kujiuliza kwa sasa naweza kuendesha chuo na pia naweza kuleta wanafunzi wengi hivi siwezi kufungua chuo changu? Wakati nawaza hivyo nikajiuliza mtaji nitautoa wapi? Kumbuka hapo fedha zote za kuleta wanafunzi sijalipwa.
Niliwashirikisha rafiki zangu wawili ambao tulikuwa na mchango mkubwa pale chuoni ambao nao walikuwa wahanga wa kutolipwa stahiki zao. Tulichambua uwezo wa kila mmoja na eneo ambalo anaweza kusaidia.
Kuna mmoja alikuwa ni fundi wa kuandika business proposal na mwingine alikuwa ni mtaalamu wa TEHAMA ambaye alitusaidia kuandaa logo na mambo ya kitehama.
Tulifanya research ya kuanzisha chuo tukaona sekta ya afya kwa ukanda wetu ilikuwa ndio kila kitu. Baada ya kufanya consultation ya mahitaji ya chuo cha afya tulianza kuainisha mahitaji yote kwenye business proposal.
Nilimshirikisha rafiki yangu ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya afya wilayani ambaye aliunga sana mkono wazo letu. Akaniambia angalia kwenye simu yako utakutana na majina ya watu wengi wenye uwezo wa kufanikisha wazo lenu kwa maana ya connection.
Tukaanza mchakato wa kusajili kampuni ambayo tutaitumia kuanzisha chuo na kutafuta wadau (wadhamini) kwa kufanya presentation ya wazo letu tukaanza kuuza hisa ili kupata fedha tunazohitaji. Katika ile presentation niliwaalika vigogo wengi wakubwa ambao nilikuwa na ukaribu na mazoea nao kama special appearance ili kuwafanya watu waongeze imani na sisi.
Tukaanza kama utani, tukapata eneo la kanisa ambalo lilikuwa na madarasa mengi ambayo yalikuwa hayatumiki tukaingia nao mkataba wa miaka mitano ambao ni renewable.
Tukaingia mtaani kusaka vijana waliomaliza kozi za afya waungane na sisi kufundisha (kumbuka kwa sasa kuna supply kubwa ya wahitimu hivyo haikuwa kazi ngumu). Mahitaji yote kwa ajili ya kusajili chuo tumetimiza sasa imebakia sehemu ndogo ili tukamilishe usajili wa chuo. Baadhi ya shughuli tutafanya wenyewe kwa kuwa tuna uzoefu mkubwa mfano kutafuta wanafunzi nk.
Nilichojifunza ni kwamba kila changamoto au tatizo ni muhimu sana kwani linakufanya upate akili ya kufanya makubwa. Pia ukiwa na wazo zuri ukaliweka katika maandishi pesa ni kitu kidogo sana.

Upvote
7