Nilivyofanikiwa kubadili majina yangu yaliyokosewa NIDA

Nilivyofanikiwa kubadili majina yangu yaliyokosewa NIDA

Mimi changu kilikuwa na makosa jina mwisho lipo kati, na lineongezwa herufi moja, la kati lipo mwisho...sasa sababu nilikuwa na haraka nacho nilikuwa nataka kusafiri nikakitumia kutafutia passport, na kufungulia account, sasa nitaka niweke taarifa zangu sawa, passport tayari bado Nida hizo process jau kinoma.
 
Inakuaje hadi jina lako linakosewa?
Kama uliwapa documents sahihi na wao wakakosea kosa ni lako au lao? Lakini kabla ya kuweka alama za vidole si wanakuonesha kuthibitisha majina yako?
Ule usajiri wa fasta fasta 2020 ulitengeneza tatizo kubwa sana watu wengi majina yao yamekosewa herufi.
Unaitwa Idd wanakuandikia Idi au Adolf wanaandika Adofu
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamii forum, Watu (Wananchi ) wamekuwa wakilalamika juu ya hadha (usumbufu) wakati wakifuatilia juu ya kubadili majina Yao yalikosewa NIDA .
Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ombi lako la kubadili majina linaweza kukubaliwa Au kukataliwa inategemeana Na afisa wa NIDA kujiridhisha Na document zako ulizopeleka ..

HATUA NILIZOCHUKUA KUBADILI MAJINA YANGU MAWILI YALIYOKOSEWA..

1. Hatua Ya Kwanza Kiapo cha mwanasheria Au Mahakama kinachoomba kubadili jina kutoka A Kwenda B Kwa lugha ya kingereza wanaita DeedPol , Gharama Kwa mwanasheria ni 30,000/= maana zinakuwa jumla Karatasi 3 Ila ukienda mahakamani ukilia lia wataku charge 15,000/=
2.Hatua Ya Pili kupeleka kwa msajiri Wa Ardhi hizo Karatasi tatu ulizotoka nazo kwa mwanasheria au Mahakama . Kwa wakazi wa Dar es salaam unapeleka pale Ardhi kivukoni , unatakiwa kuambatanisha Vyeti Au Vitambulisho vinavyoonyesha hayo majina yaliyotofautiana , Kipindi kile walikuwa Wana charge 32,500Tsh/= Unakata Baada Ya Wiki (Siku 7) unafuata majibu Yako.
3. Hatua ya tatu kupeleka tangazo kwa mhariri wa gazeti la serikali , Gharama yake ni Elfu 20,000Tsh/= Kwa watu Wa Dar es salaam Ofisi ya mhariri wa gazeti la serikali wapo pale darajani Karibu na Fly Over ya Veta Mataa , Ukishalipia malipo yao Unaenda kutuma posta Kwa mhariri wa gazeti la serikali Dodoma , Unatumia njia ya EMS Gharama yake 15000/= Unakaa ndani ya siku 21unafuata majibu yako ., Ukiwa Unatuma kwa mhariri hakikisha unahambanisha copy vyeti Au Vinavyotambulisha taharifa zako.
4. Hatua Ya Nne Unapeleka NIDA , utajaza Ile form ya nida upya ya Kuomba namba ya nida , utaenda serikali ya mtaa barua ya utambulisho na kugonga mhuri wa mtendaji mtaa Au kata , Baada ya hapo unarudi NIDA Uhamiaji wagonge mhuri Wao Baada ya Hapo utaenda Kwa afisa wa NIDA mapokezi kwa ajili ya kukutolea control number ILA UTARATIBU WA NIDA KWA MTU ANAYEBADIRI MAJINA KUANZIA MAWILI UNATAKIWA KUANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI WA NIDA
5. Hatua Ya Tano Ikabidi Niandike barua ya Kuomba kubadili majina kutoka A Kwenda B Kwa mkurugenzi mkuu Wa NIDA , nikamhuliza Afisa Nida barua inakaa Muda Gani kujibiwa akasema ajui Ila Inaweza kukaa Hata miezi 3 Hata 7 majibu yakawa Bado , Nikasema Duuuh Hii Hatari
6. Hatua Ya Sita Baada Kukaa Mwezi Bila majibu nikaenda Ofisi Ya Nida ,wakaniambia majibu ya barua Yangu Bado , Ikabidi Niende Makao Makao Makuu Ya Nida Karibu Na Ubalozi Wa Ufaransa nikafanikiwa Kupata Barua Iliyojibiwa Kuwa ombi Langu Limekubalika La Kubadili Majina Kutoka A Kwenda B . Nilivyorudi Ofisi Za Nida Wakanibadilishia Majina Kwa Gharama ya 20,000/=
Japokuwa Watu Wanalalamika Kuhusu Nida Ila Nida Wanafanya Kazi Safi Na Wanakuelekeza Hatua Hadi Hatua Ya Kufanya , Nimehamua Kutoa Elimu Hii Maana Watu Wengi wanachangamoto Hii

View attachment 2767597

Lilipaswa kuwa zoezi jepesi sana simply kwa ku produce birth certificate au vyeti vya chuo.
 
Ule usajiri wa fasta fasta 2020 ulitengeneza tatizo kubwa sana watu wengi majina yao yamekosewa herufi.
Unaitwa Idd wanakuandikia Idi au Adolf wanaandika Adofu
Duuh kuumbe, sikulijua hili ni kama kipindi kile cha Kitambulisho cha Mpiga Kura, mambo yalikua hovyo hovyo
 
Habari za muda huu ndugu zangu wa jamii forum, Watu (Wananchi ) wamekuwa wakilalamika juu ya hadha (usumbufu) wakati wakifuatilia juu ya kubadili majina Yao yalikosewa NIDA .
Kitu cha kwanza unachotakiwa kujua ombi lako la kubadili majina linaweza kukubaliwa Au kukataliwa inategemeana Na afisa wa NIDA kujiridhisha Na document zako ulizopeleka ..

HATUA NILIZOCHUKUA KUBADILI MAJINA YANGU MAWILI YALIYOKOSEWA..
1. Hatua Ya Kwanza Kiapo cha mwanasheria Au Mahakama kinachoomba kubadili jina kutoka A Kwenda B Kwa lugha ya kingereza wanaita DeedPol , Gharama Kwa mwanasheria ni 30,000/= maana zinakuwa jumla Karatasi 3 Ila ukienda mahakamani ukilia lia wataku charge 15,000/=

2.Hatua Ya Pili kupeleka kwa msajiri Wa Ardhi hizo Karatasi tatu ulizotoka nazo kwa mwanasheria au Mahakama . Kwa wakazi wa Dar es salaam unapeleka pale Ardhi kivukoni , unatakiwa kuambatanisha Vyeti Au Vitambulisho vinavyoonyesha hayo majina yaliyotofautiana , Kipindi kile walikuwa Wana charge 32,500Tsh/= Unakata Baada Ya Wiki (Siku 7) unafuata majibu Yako.

3. Hatua ya tatu kupeleka tangazo kwa mhariri wa gazeti la serikali , Gharama yake ni Elfu 20,000Tsh/= Kwa watu Wa Dar es salaam Ofisi ya mhariri wa gazeti la serikali wapo pale darajani Karibu na Fly Over ya Veta Mataa , Ukishalipia malipo yao Unaenda kutuma posta Kwa mhariri wa gazeti la serikali Dodoma , Unatumia njia ya EMS Gharama yake 15000/= Unakaa ndani ya siku 21unafuata majibu yako ., Ukiwa Unatuma kwa mhariri hakikisha unahambanisha copy vyeti Au Vinavyotambulisha taharifa zako.

4. Hatua Ya Nne Unapeleka NIDA , utajaza Ile form ya nida upya ya Kuomba namba ya nida , utaenda serikali ya mtaa barua ya utambulisho na kugonga mhuri wa mtendaji mtaa Au kata , Baada ya hapo unarudi NIDA Uhamiaji wagonge mhuri Wao Baada ya Hapo utaenda Kwa afisa wa NIDA mapokezi kwa ajili ya kukutolea control number ILA UTARATIBU WA NIDA KWA MTU ANAYEBADIRI MAJINA KUANZIA MAWILI UNATAKIWA KUANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI WA NIDA.

5. Hatua Ya Tano Ikabidi Niandike barua ya Kuomba kubadili majina kutoka A Kwenda B Kwa mkurugenzi mkuu Wa NIDA , nikamhuliza Afisa Nida barua inakaa Muda Gani kujibiwa akasema ajui Ila Inaweza kukaa Hata miezi 3 Hata 7 majibu yakawa Bado , Nikasema Duuuh Hii Hatari.

6. Hatua Ya Sita Baada Kukaa Mwezi Bila majibu nikaenda Ofisi Ya Nida ,wakaniambia majibu ya barua Yangu Bado , Ikabidi Niende Makao Makao Makuu Ya Nida Karibu Na Ubalozi Wa Ufaransa nikafanikiwa Kupata Barua Iliyojibiwa Kuwa ombi Langu Limekubalika La Kubadili Majina Kutoka A Kwenda B . Nilivyorudi Ofisi Za Nida Wakanibadilishia Majina Kwa Gharama ya 20,000/=

Japokuwa Watu Wanalalamika Kuhusu Nida Ila Nida Wanafanya Kazi Safi Na Wanakuelekeza Hatua Hadi Hatua Ya Kufanya , Nimehamua Kutoa Elimu Hii Maana Watu Wengi wanachangamoto Hii

View attachment 2767597
Hongera
 
Hii nchi iko complicated sana

Me kipindi nafatilia passport yangu ..walikosea tarehe ya kuzaliwa kutokana na cheti cha kuzaliwa kilikua na makosa kwenye tarehe ya kuzaliwa
yule afisa uhamiaji tutakubaliana nkashughulikie cheti cha kuzaliwa then nlete copy sahihi ya cheti kipya ,nkafanya hvyo cha ajabu passport ikatoka na tarehe ya zamani ya cheti chenye makosa...nlimind sana

Ikabidi nifanye mchakato upya wa ku apply passport nyingine ...kwenye hichi kipengele nlikutana na vikwazo mpaka ikabidi nikubali kutoa hela ili wanisaidie chap...ila bila hvyo ningehangaika sana
 
Binti yangu kafanikiwa kubadilisha, lkn huko ardhi hatukwenda. Shida ni kwamba wafanyakazi wa nida wao wenyewe hawana taarifa sahihi ya nini cha kufanya, ukienda leo unaambiwa kalete moja, mbili, tatu, kesho yake ukienda unakutana na mwingine nae anakwambia kafanye moja mbili tatu.....nenda rudi ni nyingi but tulifanikiwa
Kumbe una mtoto over 18
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom