kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nilikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na wasiwasi kuhusu kuchanja chanjo ya covid 19. Hofu yangu kubwa kuliko zote ilikuwa kuganda kwa damu yangu baada ya kuchanja. Lakini Mimi ni miongoni mwa watu waliochanjwa chanjo ya COVID-19 Johnson And Johnson siku ya pili tu baada ya zoezi la kuchanja kuzinduliwa na Rais
Nilijisikia yafuatayo:
1. Nilichanjwa kwenye bega la kushoto, sehemu niliyochanjwa nijisikia maumivu ya sindano kwa siku kama 3 hivi
2. Baada ya kuchanjwa nilijisikia kama kichwa kizito kidogo kwa siku kama 3 hivi
3. Nilijisikia kutaka kupumzika nyumbani nisifanye kazi kwa siku kama tatu hivi
4. Sikutamani kufanya tendo la ndoa kwa siku kama 5 hivi
5. Baada ya wiki moja kupita nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida na zaidi
6. Nilijisikia hamu zaidi ya kutaka kujamiiana baada ya wiki hivi
7. Nguvu za kiume ziliongezeka mara tatu zaidi
8. Nilitoa mbegu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujamiiana
9. Nikajisikia mtu mwenye nguvu kuliko kabla ya chanjo.
10. Tangu nichanjwe sijawahi kupata kikohozi, mafua
11. Kama Koo likinikereketa ilikuwa lazima nimung'unye lozenges au nimeze antibiotics ili nipone lakini juzi koo linikereketa likatulia lenyewe bila kutumia dawa yoyote.
12. Umakini (concentration yangu na busara zangu nahisi kama vimeongezeka kuliko awali.
Nadhani chanjo Iko poa, unaweza kuja kujutia kama chanjo zitaisha bila wewe kuchanjwa. Maana kwenye foleni tulikuwa na watu raia wa Ulaya na Asia wanahitaji kuchanjwa.