#COVID19 Nilivyojisikia baada ya kuchanjwa chanjo ya COVID-19

#COVID19 Nilivyojisikia baada ya kuchanjwa chanjo ya COVID-19

Hakuna maswali yeyote,kinachosumbuwa watu kwa sasa ni utandawazi.

Hivi zile chanjo za surua,ndui,nk Nini walijadiliana na nani zikaletwa huku Africa? Au zikakubalika na wengine?
Si tumeletewa tu? Au kulikuwa na.mjadala kama huu wa chanjo ya uvico?
Kuna yeyote aliyehoji usalama wa chanjo zile?
Majibu yenu ya kubeza haya maswali ya wengine ndio yanazidisha wasiwasi.
 
Mkuu usitumie nguvu nyingi sana kuwaaminisha watu kuhusu usalama Wa chanjo.
Kumbuka hata mababu zetu walipoletewa ustaarabu wa kujenga vyoo na kujisaidia chooni, vita vya kupinga kujisaidia chooni ilikuwa kubwa kuliko hili la wapinga chanjo.
Maana walishazowea kujisaidia vichakani.

Mimi nimechoma faizer ,,Nina muda sasa nipo okay.
Na hakuna tatizo lolote.,

Waache waendelee kupinga ,,huku wakiumwa wanakimbilia hospital kwenye dawa za kizungu ,,
badala ya kwenda kwa mganga wa kienyeji kutibiwa.
Ni kweli waligoma kunyea kwenye vyoo kwa visingizio vya kijinga kama vile siwezi kutumia choo kimoja na mkwe wangu, mtoto wangu lakini wakienda hospitali wanatumia vyoo wote. Siwezi kujenga nyumba ya mavi wakati ng'ombe wangu wanalala nje, sio vizuri watoto wajue kama na baba anaenda chooni, nk.

Ndugu zangu tunatia aibu kutoa sababu za kijinga na zakufikiria TU kuhusu chanjo. Utake usitake Mimi nimechanja na hivyo ndivyo ninavyosikia. Kalabaho
 
Hakuna maswali yeyote,kinachosumbuwa watu kwa sasa ni utandawazi.

Hivi zile chanjo za surua,ndui,nk Nini walijadiliana na nani zikaletwa huku Africa? Au zikakubalika na wengine?
Si tumeletewa tu? Au kulikuwa na.mjadala kama huu wa chanjo ya uvico?
Kuna yeyote aliyehoji usalama wa chanjo zile?
Kaka wapo wanaojifunza kutokana na makosa ya wengine na wapo wanaojifunza kutokana na makosa Yao wenyewe. Waafrika wanatabia ya kusubiri kujifunza kutokana na makosa Yao wenyewe. Wanasubiri mpaka Rais, makamu wa Rais, Waziri, mbunge, baba yake, mkwewe, na jirani yake augue au kufa kwa covid-19 ndiyo wachukue hatua.
 
Mlinganisho huo na wa polio surua haviendani mkuu sababu ilichukua muda mrefu kupatikana chanjo yake ila hii imekuja very soon yaani testing yake inafanyika directly ndio maana hata uchanjwe bado uko hatarini na zinapingwa kwa sehemu kubwa sana
Wewe ndiyo uko gizani kabisa totoro, kwahiyo unapenda kusafiri na Yale mabasi ya abiria ambayo zamani yalikuwa yakichukua siku nzima kutoka dar es Salaam kwenda Morogoro? Yaani unataka bado utumie dawa Kali kutibu minyoo?

Kaka technology imekuwa sana, kutoka simu za waya hadi internet kiganjani. Kama mzungu anataka kukudhuru sasa unamwambia kuwa aanze kutudhuru kwa kutumia chanjo za magonjwa mengine na dawa za Panadol, mseto, ampicillin, na dawa za vikohozi ambazo tunazikubali?

Msiwatukanishe Waafrika
 
Mimi ni miongoni watu waliochanjwa chanjo ya covid-19 Jonson Johnson siku ya pili TU baada ya zoezi la kuchanja kuzinduliwa na Rais.
Nilijisikia yafuatayo:

1. Nilichanjwa kwenye bega la Lushoto, sehemu niliyochanjwa nijisikia maumivu ya sindano kwa siku kama 3 hivi.

2. Baada ya kuchanjwa nilijisikia kama kichwa kizito kidogo kwa siku kama 3 hivi.

3. Nilijisikia kutaka kupunzika nyumbani nisifanye kazi kwa siku kama tatu hivi.

4. Sikutamani kufanya tendo LA ndoa kwa siku kama 5 hivi.

5. Baada ya wiki moja kupita nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida na zaidi.

6. Nilijisikia hamu zaidi ya kutaka kujamiana.

7. Nguvu za kiume ziliongezeka mara tatu zaidi.

8. Nilitoa megu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujamiana.

9. Nikajisikia mtu mwenye nguvu kuliko kabla ya chanjo.

10. Tangu nichanjwe sijawahi kupata kikohozi, mafua
11. Kama Koo likinikereketa ilikuwa lazima nimung'unye lozenges au nimeze antibiotics ili nipone lakini juzi Koo linikereketa likatulia lenyewe bila kutumia dawa yoyote.

12 umakini (concentration yangu na busara zangu nahisi kama vimeongezeka kuliko awali.

Nadhani chanjo Iko pia, unaweza kuja kujutia kama chanjo zitaisha bila wewe kuchanjwa. Maana mwenye foleni tulikuwa na WAtu raia wa Ulaya na Asia wanahitaji kuchanjwa.
Wewe ni mtu wa pili kumsikia akisema km wewe mzee moja baada ya chanjo km siku Tano hivi akasema na baadhi ya magonjwa alikuwa nayo yamepona pia baada ya chanjo mie nilikuwa fix tu.
 
Mimi ni miongoni watu waliochanjwa chanjo ya covid-19 Jonson Johnson siku ya pili TU baada ya zoezi la kuchanja kuzinduliwa na Rais.
Nilijisikia yafuatayo:

1. Nilichanjwa kwenye bega la Lushoto, sehemu niliyochanjwa nijisikia maumivu ya sindano kwa siku kama 3 hivi.

2. Baada ya kuchanjwa nilijisikia kama kichwa kizito kidogo kwa siku kama 3 hivi.

3. Nilijisikia kutaka kupunzika nyumbani nisifanye kazi kwa siku kama tatu hivi.

4. Sikutamani kufanya tendo LA ndoa kwa siku kama 5 hivi.

5. Baada ya wiki moja kupita nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida na zaidi.

6. Nilijisikia hamu zaidi ya kutaka kujamiana.

7. Nguvu za kiume ziliongezeka mara tatu zaidi.

8. Nilitoa megu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujamiana.

9. Nikajisikia mtu mwenye nguvu kuliko kabla ya chanjo.

10. Tangu nichanjwe sijawahi kupata kikohozi, mafua
11. Kama Koo likinikereketa ilikuwa lazima nimung'unye lozenges au nimeze antibiotics ili nipone lakini juzi Koo linikereketa likatulia lenyewe bila kutumia dawa yoyote.

12 umakini (concentration yangu na busara zangu nahisi kama vimeongezeka kuliko awali.

Nadhani chanjo Iko pia, unaweza kuja kujutia kama chanjo zitaisha bila wewe kuchanjwa. Maana mwenye foleni tulikuwa na WAtu raia wa Ulaya na Asia wanahitaji kuchanjwa.
atuchanji ata kama zilikusaidia ku...........[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mimi nilisafiri kwenda vijijini kuhakikisha mimi na wapendwa wangu wa huko uswekeni tunachanjwa (bila mtu kupotoshwa) kama sehemu ya utalii wa ndani.

Tulijiandikisha kama ilivyohitajika siku kama ilivyotangazwa. Tukasubiri maelekezo hadi walipokuwa tayari nasi tukachanjwa.

Ilikuwa siku ya uzinduzi kwenye eneo husika. Wachanjwa tulikuwa wengi (kwenye 300).

Haya ndiyo yaliyonisibu:

Nilichanjwa bega la kushoto. Yafuatayo ni niliyoyaona au kuyahisi kwa siku 3 tokea nilipochanjwa.

1. Muda mfupi baada ya kuchanjwa nilianza kusikia kiu, kilichoendelea bila kukoma, pamoja na kuongeza kiwango cha maji ambacho hunywa kwa kawaida.
3. Sense ya balance ilikuwa compromised kwa kiasi cha kutosha kwa kipindi chote.
4. Nilipata maumivu makali ya kichwa yasiyopungua mfululizo tokea muda kidogo baada ya kuchanjwa.
5. Mwili ulikuwa si wangu. Viungo viliniuma na mwili kulegea.
6. Nilibakia ndani mgonjwa kitandani kwa muda wote.
7. Mwili ulikuwa ukihisi baridi zaidi.
8. Palikuwa na hali ya kichefu chefu.

Ningali ninajifanyia tathmini kuhusiana na hali yangu yote leo kujilinganisha na ile ya mapema.

Sina majuto yoyote kwa kupokea chanjo hii. Ninayo furaha kuwa hatimaye nilipata. Ninamini kuwa faida za chanjo ni kubwa kuliko madhara.

Niko tayari kuendelea kuleta mrejesho wa wazi kuhusiana na muendelezo wote, kulingana na hali yangu yote.

Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

#COVID19 - Chanjo - Mrejesho: Wizara tambueni changamoto hizi

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe
Nilichokifanya mimi na wenzangu baada ya kuchanjwa tulipunzika palepale kama dakika 20 hivi tukipiga stori kabla ya kuondoka. Tukapitia duka la dawa kununua junior Aspirin na kumeza moja palepale dukani na nyingine tukaondoka nazo ili kila siku tumeze kidonge kimoja, lakini mmoja wetu alikuwa na vidonda vya tumbo akashairiwa ameze Panadol TU.

Siku hivyohivyo nilikuwa najifanyia mazoezi mepesi ya kurukaruka, kutembea na deep breathing. Aaaaa! Alhamdulilah, gari limewaka tena bila shida yoyote. Na wenzangu wote 4 (cohort) wako barabarani.

Miili yetu inapotea dawa, vinywaji na vyakula kwa njia tofauti. Mwingine akinywa kahawa TU kichwa kitamuuma, mwingine akinywa maziwa anaharisha, mwingine akila nyama ya ng'ombe anavimba mwili, mwingine akimeza SP anawashwa, mwingine akichomwa PPF anazirai. Hivyo hata chanjo ziko hivyohivyo.
 
Mimi ni miongoni watu waliochanjwa chanjo ya covid-19 Jonson Johnson siku ya pili TU baada ya zoezi la kuchanja kuzinduliwa na Rais.
Nilijisikia yafuatayo:

1. Nilichanjwa kwenye bega la Lushoto, sehemu niliyochanjwa nijisikia maumivu ya sindano kwa siku kama 3 hivi.

2. Baada ya kuchanjwa nilijisikia kama kichwa kizito kidogo kwa siku kama 3 hivi.

3. Nilijisikia kutaka kupunzika nyumbani nisifanye kazi kwa siku kama tatu hivi.

4. Sikutamani kufanya tendo LA ndoa kwa siku kama 5 hivi.

5. Baada ya wiki moja kupita nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida na zaidi.

6. Nilijisikia hamu zaidi ya kutaka kujamiana.

7. Nguvu za kiume ziliongezeka mara tatu zaidi.

8. Nilitoa megu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujamiana.

9. Nikajisikia mtu mwenye nguvu kuliko kabla ya chanjo.

10. Tangu nichanjwe sijawahi kupata kikohozi, mafua
11. Kama Koo likinikereketa ilikuwa lazima nimung'unye lozenges au nimeze antibiotics ili nipone lakini juzi Koo linikereketa likatulia lenyewe bila kutumia dawa yoyote.

12 umakini (concentration yangu na busara zangu nahisi kama vimeongezeka kuliko awali.

Nadhani chanjo Iko pia, unaweza kuja kujutia kama chanjo zitaisha bila wewe kuchanjwa. Maana mwenye foleni tulikuwa na WAtu raia wa Ulaya na Asia wanahitaji kuchanjwa.
Johnson Johnson ndiyo nini?
 
Namba 11 unatujaza upepo. Watengenezaji wamethibitisha kua hata ukichanjwa unaambukiza/zwa. Hii promo yako jipange upya.
Sijasema siambukizi Corona, Ila mimi nilikuwa na tabia kila Koo likiniwasha lazima nitumie dawa ili nipone, lakini nilishangaa baada ya kuchanjwa sihitaji dawa kuponya Koo. Nikahisi kuwa LABDA pia chanjo hii inaweza kuimarisha kinga yangu hata kwa magonjwa mengine.
 
Mkuu usitumie nguvu nyingi sana kuwaaminisha watu kuhusu usalama Wa chanjo.
Kumbuka hata mababu zetu walipoletewa ustaarabu wa kujenga vyoo na kujisaidia chooni, vita vya kupinga kujisaidia chooni ilikuwa kubwa kuliko hili la wapinga chanjo.
Maana walishazowea kujisaidia vichakani.

Mimi nimechoma faizer ,,Nina muda sasa nipo okay.
Na hakuna tatizo lolote.,

Waache waendelee kupinga ,,huku wakiumwa wanakimbilia hospital kwenye dawa za kizungu ,,
badala ya kwenda kwa mganga wa kienyeji kutibiwa.
Mhe; tatizo unaweza usilipate wewe akaja kupata mtoto wako inscase Bado kama unazaa au unazalisha tena may be baada ya miaka hata 10+ hukoo, au hata wewe baada ya miaka kadhaa l, so usitoe conclusion Kwa Muda wa hata miezi 6 haujafika unasema upo okay!, Itafika Muda watu tutakuwa tunaumwa lakini hatujui shida Nini? Lakini huwez jua pengine ni kitu ambacho tunakitengeneza saizi.
So be extra Carefully
 
6. Nilijisikia hamu zaidi ya kutaka kujamiana.

7. Nguvu za kiume ziliongezeka mara tatu zaidi.

8. Nilitoa megu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujamiana.

9. Nikajisikia mtu mwenye nguvu kuliko kabla ya chanjo
😆😆Umekazana sana na eneo hilo,ukijua utapata vijana wengi... hongera
 
Mimi baada ya kuchanja J&J nilipata homa kali siku hiyo. Lakini baada ya siku mbili nikawa freshi. Nisingekuwa nimesoma kuhusu side effects mapema ningehisi ni malaria. Kwa sasa niko vizuri na ninaishi kwa amani.
 
Nilichokifanya mimi na wenzangu baada ya kuchanjwa tulipunzika palepale kama dakika 20 hivi tukipiga stori kabla ya kuondoka. Tukapitia duka la dawa kununua junior Aspirin na kumeza moja palepale dukani na nyingine tukaondoka nazo ili kila siku tumeze kidonge kimoja, lakini mmoja wetu alikuwa na vidonda vya tumbo akashairiwa ameze Panadol TU...

Mkuu tuna wenzetu waluotupia panadol kabla ya chanjo, kuna waliotupia panadol baada ya chanjo.

Kama mhamasishaji nguli kutokea mjini, mfuatiliaji na mchambuzi, wote hao wapo kwenye kanzidata yangu tangia tulipochanjwa.

Ila miye niliubeba msalaba wote bila panadol bila cha zaidi katika ushauri uliopo ili kuweza kuhakiki vilivyo, kulikoni.

Yaliyonisikitisha ambayo ni muhimu yakarekebishwa:

1. Badala ya kuendelea na chanjo kulifanywa uzinduzi wenye mlengo zaidi wa kisiasa.
2. Chanjo hii inajulikana kuletwa na beberu bure. Siyo mheshimiwa Rais, CCM wala serikali yake.
3. Kutuhamasisha sisi kwa hotuba mbalimbali ili kuchanjwa kwenye eneo la chanjo ilikuwa sawa na kupanga mikakati ya kuwavua samaki waliokwisha kuvuliwa.
4. Kutokuzingatia vigezo wala masharti ya mtengeneza chanjo kwenye zoezi la utoaji chanjo kwa hakika si sahihi.

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

Muhimu: kuweka ukweli mbele na kuweka siasa nje ya ugonjwa huu, zaweza kuwa njia pekee za kutuvusha.
 
Back
Top Bottom