Mimi baada ya chanjo asubuhi na mapema kwenye saa 4 hivi nilikuwa poa tu nilikuja kusikia dalili kama za homa jioni kabisa,
Mwili nikawa naiusikia kama ninavyoaanza kuumwa Maleria, kichwa kizito na kuuma. Lakini nikuwa nimeshaambiwa tayari na Wataalamu wa afya kuhusu hizo side effects kwamba unaweza kupata uchovu, kuumwa na kichwa, kichefuchefu na maumivu ya viungo hiyo ni kwa sababu chanjo inakuwa unazunguka kwenye mwili kuamsha kinga zote za Mwili na kwamba unaweza jisikia hivyo ndani ya siku mbili.
Sikuwa na shaka baada siku moja tu nikawa vema sana kwakweli hata mimi niliona mabadiliko makubwa na mazuri mno. Mwanzo nilikuwa nafanya kazi kila siku jioni narudi nimechoka mno now hakuna. Naona mwili wangu una nguvu zaidi ya mwanzo. Kwakweli nendeni mkachanje msiwasikilize watu wa mitandaoni humu maana hata chakushangaza nilichokiona vijana kama mimi ni wengi sana vituoni ila ukija huku nako comment za wabishi wasiotaka chanjo nazo nyingi huwenda wanabisha huku nyuma ya pazia wanaenda kuchanja.
Kwenye ukoo wetu wote mimi ndio nilkuwa wakwaza kuchanja, ndugu zangu wakaanza kuniita Zombie. Sasa hivi nao wote wanataka chanjo.