Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Ilikuwa mwaka 2004 nikiwa darasa la 6. Alikuja ndugu yangu toka mjini na kuja na kuber. Ilikuwa jioni flan kijijini wakatii huo kumetulia watu tunasubiri ugali wa usiku, kipindi hicho hakuna milo miwili wala mitatu, asubuhi uji,mchana matunda shambani usiku ndio chakula.
Nimekaa njaa inanisokota kweli, ndugu yangu akaja na mjomba wake ambaye nae alizimwa mchana kwa zaga hilo hilo. Kwa ushamba nikaomba nionje,nilivyonusa tu, nikahisi harufu kaali sana,yan zaidi ya ugoro,nikauliza hii si kama ugoro(sababu ugoro naujua na siupendi)wajamaa huu tofauti onja uone utakayokuwa kama huyu jamaa kwenye picha hapa.
Nikapewa nikaweka mdomoni, akaniambia usimeze, nikajichanganya nikachuka mate nikameza. Niliambaa na ukuta mpaka chumbani, nilikuja kushtuka asubuhi saa 12 asubuhi pamoja na njaa yangu sikuweza kula chakula tena. Sitosahau tukio hili la kuber.
Je unakumbuka nini?