Nilivyokutana na Msukuma kwenye msitu wa Malangamilo

wana makusudi hawa jamaa wa nyuzi za "itaendelea", mpaka sasa najiuliza yeye yupo mkoa gani na huko Malangimilo ni wapi japokuwa nimeona sehemu moja tu inaitwa Samora, nikajiuliza Samora ya Iringa ama wapi...ngoja tusubiri mwendelezo
Yupo Mbeya, Iyo Malangamilo Ni Chunya Huko Kwa Wachimba Dhahabu.
 
NILIVYO KUTANA NA MSUKUMA KWENYE MSITU WA MALANGAMILO

SEHEMU YA PILI

ALLY KATALAMBULA.

NAVUTA moto, chopa inapepea, ndani ya dakika sufuri tayari nimetokea upande wa pili wa Ile barabara ya vumbi.

Nimefanikiwa kulikwepa geti la polisi...sasa nakatisha kwenye uwanja wa gulio la kila mwezi (mnadani) kisha naachana na barabara ya vumbi ya Lupa tayari nipo kwenye barabara ya kuelekea Gepu.

Naendelea kuendesha kwa mwendo wa kukimbia, kama nilivyo sema huko nyuma, tayari nilikuwa nyuma ya muda.

Hii barabara ya Gepu inatia karaha kwani ni mbovu. Ni njia fulani yenye mashimo na madimbwi ya maji.

Halafu kitu Cha kushangaza ni kwamba, hii njia bwana inatumiwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mbunge wa Jimbo hili la Lupa.

Huko 'site' nasikia Kuna miradi yao mbalimbali, sasa huwa najiuliza inamaana hawa vigogo wa serikali huwa wahaioni hii shida ya barabara au ndio kusema nao wamaeridhika na hili tatizo!!!!!!!

Any way, tuaachane na hilo, nisije onekana nimeanza harakati za siasa mwisho nikapewa kesi ya uchochezi na uhujumu uchumi..... Tangu mwaka 2015 mambo ya Siasa huwa yananiogopesha sana sijui kwa nini tu.

Basi bwana.... mbilinge za huku na kule, dakika 20 zikanikuta Gepu makalashani, nikaendelea kunyoosha na barabara chopa ikiacha vumbi la kutosha huko nyuma.

Hatimaye nikaaunza msitu wa MALANGAMILO msitu wenye miti mikubwa yenye matawi ambayo yameacha kivuli barabarani sambamba na hewa nzuri ya oxygen.

Ni msitu ambao kama unakwenda MALANGAMILO, upande wa kushoto Kuna mlima na ni eneo la hifadhi ya taifa... hii nchi ni kubwa halafu nzuri asikwambie mtu tembea uone sio unakaa tu Tandale kama Nyemo Chilongani 🤣🤣🤣

Basi bwana......safari na muziki,, inaendelea.., Njiani napishana na washkaji Wana appolo mbalimbali wanao pambana kuitengeneza kesho yao na familia zao,

Tunaepeana 'hi' tabasamu na ukarimu, si unajua tena Watanzania desturi zetu, wakati naumaliza msitu wa MALANGAMILO mara ghafla mbele yangu, naliona kundi la ng'ombe Lenye pembe ndefu..... mang'ombe kibao yamejaaa barabarani.

Napunguza mwendo, haya Madudu yakiwa na pembe ndefu huwa yananiogopesha sana🤣

Napishana na mag'ombe hayo yenye afya nzuri yameshiba kama nyati, halafu nyuma yao namuona Jamaa mmoja pichani kavaa kama kimasaai lakini sio mmsai.

Yeye alivaa bangili mikononi na miguuni halafu kiunoni kavaa zake kanga, hana habari na mtu anafurahia maisha yake...

Jamaa huyu bila shaka ni Mchungaji wa zile ng'ombe kwani mkononi alikuwa ameshika bakora.

"Keneh ngoy...., Mwangaruka." Jamaa akanisalimu kwa Lugha ya kisukuma.

"Mwangaruka dela gawiza ngoy," namjibu.

Mimi pia kisukuma kimo kidogo, bwana weee.😆🤣

Anatabasamu, nadhani Kuna mahali nimekosea, potelea mbali, atajijua mwenyewe. kwani aliponipa 'hi' ya kisukuma yeye anadhani kila mtu msukuma.

Japokuwa huwa nakutana na hawa viumbe mara kibao. Lakini hata hivyo leo ni huyu Jamaa aliyenivutia sana., huwa nawaona hawa watu mara kibao lakini sijui kwa nini huyu Leo amefanya niwaze mambo kadhaaa.

Kwanza Jamaa ni Mtanzania, Msukuma, ambaye anaonekana anatunza na kuenzi Mila na destuli zake.

Mavazi yake ni kielelezo tosha Kwamba Jamaa ni mwafrika ambaye haja athiriwa na utamaduni wa wazungu na warabu.

Kwa Tanzania Inasemekana kabila la Kimasai ndilo lilofanikiwa kutunza Mila na Desturi zake,,,, nakubaliana na huu uchunguzi hata hivyo kwa utafiti wangu mdogo, wasukuma ni wa pili katika kutunza utamaduni wao, nyuma ya wamasai.

fuatilia kuanzia

Mavazi Yao
Chakula Chao
Makazi yao
Shughuli zao za kiuchumi
Mahusiano na jamii nyingine wasukuma ni watu fulani poa sana wacheshi na wakarimu hasa.

Mwisho msukuma akaniuliza kama ninayo simu, Nikamjibu ndio akaniomba nimuazime eti ambipu sijui shangazi yake gani wa huko Bariadi🤣🤣🤣 Ila wasukuma bhana.

Nikamwambia hapa tulipo hakuna network labda kitu naweza msaidia nimfotoe picha.

Msukuma Anafurahia akanimbia sawa haina shida Maana mara ya mwisho alifotolewa picha mwaka Jana wakati wa sikukuu za wakulima 🤣

Basi tunatafuta location nzuri nikamfotoa picha ndugu yangu mtanzania huyu pichani, nikawa nimeongeza rafiki mwingine aitwaye WA IMWENE.

Kwa kuhitimiaha hivi ndivyo NILIVYO KUTANA NA MSUKUMA KWENYE MSITU WA MALANGAMILO....

Baada ya hapo, nilivuta moto chopa ikatoa mlio kama dege la jeshi, safari yangu ya 'site' kwa George Mlewa a.k.a Mkandawile. ikaendelea....

Mwisho.
FB_IMG_1656875233288.jpg
 
NILIVYO KUTANA NA MSUKUMA KWENYE MSITU WA MALANGAMILO

SEHEMU YA PILI

ALLY KATALAMBULA.

NAVUTA moto, chopa inapepea, ndani ya dakika sufuri tayari nimetokea upande wa pili wa Ile barabara ya vumbi.

Nimefanikiwa kulikwepa geti la polisi...sasa nakatisha kwenye uwanja wa gulio la kila mwezi (mnadani) kisha naachana na barabara ya vumbi ya Lupa tayari nipo kwenye barabara ya kuelekea Gepu.

Naendelea kuendesha kwa mwendo wa kukimbia, kama nilivyo sema huko nyuma, tayari nilikuwa nyuma ya muda.

Hii barabara ya Gepu inatia karaha kwani ni mbovu. Ni njia fulani yenye mashimo na madimbwi ya maji.

Halafu kitu Cha kushangaza ni kwamba, hii njia bwana inatumiwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo mbunge wa Jimbo hili la Lupa.

Huko 'site' nasikia Kuna miradi yao mbalimbali, sasa huwa najiuliza inamaana hawa vigogo wa serikali huwa wahaioni hii shida ya barabara au ndio kusema nao wamaeridhika na hili tatizo!!!!!!!

Any way, tuaachane na hilo, nisije onekana nimeanza harakati za siasa mwisho nikapewa kesi ya uchochezi na uhujumu uchumi..... Tangu mwaka 2015 mambo ya Siasa huwa yananiogopesha sana sijui kwa nini tu.

Basi bwana.... mbilinge za huku na kule, dakika 20 zikanikuta Gepu makalashani, nikaendelea kunyoosha na barabara chopa ikiacha vumbi la kutosha huko nyuma.

Hatimaye nikaaunza msitu wa MALANGAMILO msitu wenye miti mikubwa yenye matawi ambayo yameacha kivuli barabarani sambamba na hewa nzuri ya oxygen.

Ni msitu ambao kama unakwenda MALANGAMILO, upande wa kushoto Kuna mlima na ni eneo la hifadhi ya taifa... hii nchi ni kubwa halafu nzuri asikwambie mtu tembea uone sio unakaa tu Tandale kama Nyemo Chilongani [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Basi bwana......safari na muziki,, inaendelea.., Njiani napishana na washkaji Wana appolo mbalimbali wanao pambana kuitengeneza kesho yao na familia zao,

Tunaepeana 'hi' tabasamu na ukarimu, si unajua tena Watanzania desturi zetu, wakati naumaliza msitu wa MALANGAMILO mara ghafla mbele yangu, naliona kundi la ng'ombe Lenye pembe ndefu..... mang'ombe kibao yamejaaa barabarani.

Napunguza mwendo, haya Madudu yakiwa na pembe ndefu huwa yananiogopesha sana[emoji1787]

Napishana na mag'ombe hayo yenye afya nzuri yameshiba kama nyati, halafu nyuma yao namuona Jamaa mmoja pichani kavaa kama kimasaai lakini sio mmsai.

Yeye alivaa bangili mikononi na miguuni halafu kiunoni kavaa zake kanga, hana habari na mtu anafurahia maisha yake...

Jamaa huyu bila shaka ni Mchungaji wa zile ng'ombe kwani mkononi alikuwa ameshika bakora.

"Keneh ngoy...., Mwangaruka." Jamaa akanisalimu kwa Lugha ya kisukuma.

"Mwangaruka dela gawiza ngoy," namjibu.

Mimi pia kisukuma kimo kidogo, bwana weee.[emoji38][emoji1787]

Anatabasamu, nadhani Kuna mahali nimekosea, potelea mbali, atajijua mwenyewe. kwani aliponipa 'hi' ya kisukuma yeye anadhani kila mtu msukuma.

Japokuwa huwa nakutana na hawa viumbe mara kibao. Lakini hata hivyo leo ni huyu Jamaa aliyenivutia sana., huwa nawaona hawa watu mara kibao lakini sijui kwa nini huyu Leo amefanya niwaze mambo kadhaaa.

Kwanza Jamaa ni Mtanzania, Msukuma, ambaye anaonekana anatunza na kuenzi Mila na destuli zake.

Mavazi yake ni kielelezo tosha Kwamba Jamaa ni mwafrika ambaye haja athiriwa na utamaduni wa wazungu na warabu.

Kwa Tanzania Inasemekana kabila la Kimasai ndilo lilofanikiwa kutunza Mila na Desturi zake,,,, nakubaliana na huu uchunguzi hata hivyo kwa utafiti wangu mdogo, wasukuma ni wa pili katika kutunza utamaduni wao, nyuma ya wamasai.

fuatilia kuanzia

Mavazi Yao
Chakula Chao
Makazi yao
Shughuli zao za kiuchumi
Mahusiano na jamii nyingine wasukuma ni watu fulani poa sana wacheshi na wakarimu hasa.

Mwisho msukuma akaniuliza kama ninayo simu, Nikamjibu ndio akaniomba nimuazime eti ambipu sijui shangazi yake gani wa huko Bariadi[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ila wasukuma bhana.

Nikamwambia hapa tulipo hakuna network labda kitu naweza msaidia nimfotoe picha.

Msukuma Anafurahia akanimbia sawa haina shida Maana mara ya mwisho alifotolewa picha mwaka Jana wakati wa sikukuu za wakulima [emoji1787]

Basi tunatafuta location nzuri nikamfotoa picha ndugu yangu mtanzania huyu pichani, nikawa nimeongeza rafiki mwingine aitwaye WA IMWENE.

Kwa kuhitimiaha hivi ndivyo NILIVYO KUTANA NA MSUKUMA KWENYE MSITU WA MALANGAMILO....

Baada ya hapo, nilivuta moto chopa ikatoa mlio kama dege la jeshi, safari yangu ya 'site' kwa George Mlewa a.k.a Mkandawile. ikaendelea....

Mwisho.
View attachment 2281871
Acha utopolo hii ndo nini
 
Nimejikuta natabasamu 🤣🤣
 
Hata mim nilitabasam kwa sabab ameimaliza kwa namna ambayo sikutarajia[emoji41][emoji41][emoji41]
Huyu jamaa ana uandishi mzuri sana lkn umakiziaji wake unaweza kumtukana😂

Kuna stori nyungine aoikutana demu mkali porini lkn chopa ikagoma kuwaka....alimalizia kidezi sana lkn mwandiko hauchoshi kusoma
 
Hapo kwa Mkandawile umenikumbusha ticha wangu kichwa wa kemia wa kuitwa Mkandawile aka mkanda boy!
 
Aiseee, sijajua mleta thread alikuwa analenga nini?🤓🤓🤓🤓🤓
 
Umenikumbusha mbali sana…
Enzi hizo nipo chunya.
 
Back
Top Bottom