Nilivyokutana na Mzee Sued Kagasheki katika mazungumzo na Dossa Aziz 1980s

Nilivyokutana na Mzee Sued Kagasheki katika mazungumzo na Dossa Aziz 1980s

Kwani Quran haina mafundisho ya Udaktari? Maana Quran ndiyo kila kitu. Leo hii wangejaa madaktari wa afya dunia nzima waliosomea Udaktari kupitia Quran. Allah kaweka wazi kila kitu kwenye Quran kulingana na Waumini. Isitoshe ma Engineer wa kila nyanja wangesomea fani zao kupitia Quran, maana Quran kwa Waumini ndiyo mpango mzima wa maisha ya binaadamu.
 
Mkuu Maalim Mohamed Said, vitu vingine ni just using the common sense, colonialism imeanzia South Africa mwaka 1652. Siera Leone was colonized mwaka 1787. Liberia imeanza mwaka 1822. ukoloni wa German East Africa ulianza baada ya ile mkutano wa Berlin 1884, Mkoloni Mungereza kaingia Tanganyika 1920.
Kwa akili ya kawaida tuu, dakitari wa Kwanza Africa atoke vipi Tanzania ya ukoloni wa 18c?!. Ungesema Daktari wa kwanza Tanganyika, sawa not Africa. And by the way, Bara la Africa, Misri ilikuwa civilized miaka mingi kabla ya wazungu na wana madakitari bingwa wazungu cha mtoto, hata huku kwetu bongo, dakitari bingwa wa kwanza kabisa ni babu yangu Ng'wana Malundi, alikuwa anatibu kila kitu. Mkama Rumanyika wa Karagwe pia ni bingwa wa tiba. All and all acha tuendelee kula nondo, chakula ukikiongezea chumvi chumvi kinanoga zaidi.
Asante kwa chakula hiki na chumvi yake, kiukweli nakifurahia.
P

Pascal,
Nilitegemea haya yote yaliyohitimishwa na hilo neno, ''chumvi.''

Hii inaitwa, ''bashing,'' ni kawaida sana katika hali kama yangu.

Sichukizwi na hayo zaidi na sana sana ni kipimo changu.

Katika makala iliyo na mengi ya kufikirisha mfano wa mkutano wa Jomo Kenyatta na Abdul Sykes Niarobi 1950 na mkutano wa pili Arusha ulioitishwa na Kenyatta 1951 ambao haukufanyika haya yote yamekupita ulichokiona wewe ni mimi kusahau kuweka ''coma,'' kwenye sentensi.

Juu ya haya yote nimekujibu kistaarabu.

Jibu halikukuridhisha umerudi na mengine na suala la ''chumvi.''

Hili ni tusi kwangu.

Ikiwa unataka ushahidi wa mkutano huu ninao kutoka Nyaraka za Special Branch kutoka Rhodes House, Oxford.

Nifahamishe ikiwa unataka kuona ushahidi nitauweka hapa.

Mimi nimesomeshwa ilm ya ''mnakasha,'' yaaani mjadala na mwalimu wangu marehemu Sheikh Haruna.

Yeye somo la kwanza alilonifunza ni adabu ya elimu.

Ukiwa na elimu alikuwa akisema ionekane kwa watu katika lugha na hoja zako.

Akisema, ''Usiende ukanitukanisha kwani wakusikiao ukiropoka watauliza nani alikusomesha?

Hapo nitatukanwa mie mwalimu wako.''

''It takes two to Tango.''
 
Pascal,
Nilitegemea haya yote yaliyohitimishwa na hilo neno, ''chumvi.''
Hii inaitwa, ''bashing,'' ni kawaida sana katika hali kama yangu.

Sichukizwi na hayo zaidi na sana sana ni kipimo changu.

Katika makala iliyo na mengi ya kufikirisha mfano wa mkutano wa Jomo Kenyatta na Abdul Sykes Niarobi 1950 na mkutano wa pili Arusha ulioitishwa na Kenyatta 1951 ambao haukufanyika haya yote yamekupita ulichokiona wewe ni mimi kusahau kuweka ''coma,'' kwenye sentensi.
Wewe mzee unaishi kwenye historical "bubble". Pamoja na kwamba una tabia ya kupotosha ukweli, lakini ukubali tu Tanzania siyo nchi ya Udini. Unahangaika sana kupotosha ukweli kwa kuipaka Historia ya Tanzania kwa kutumia udini, na ni dhahiri umeshindwa kwenye juhudi zako, na sasa unakuja na mbinu mbadala kueneza udini wako kupitia nyuzi za Wasifu wa Wazee au Wafu waumini wa Uislamu.
 
Kwani Quran haina mafundisho ya Udaktari? Maana Quran ndiyo kila kitu. Leo hii wangejaa madaktari wa afya dunia nzima waliosomea Udaktari kupitia Quran. Allah kaweka wazi kila kitu kwenye Quran kulingana na Waumini. Isitoshe ma Engineer wa kila nyanja wangesomea fani zao kupitia Quran, maana Quran kwa Waumini ndiyo mpango mzima wa maisha ya binaadamu.
Flori...
Nakusihi usiende huko inawezekana sana unafanya haya kwa kutokujua nami nakuchukulia hivyo.

Kwa ajili hiyo basi nitabaki kimya ili uelewe na urudi nyuma sote tusalimike.
 
Hata huko msikitini kwako sidhani kuna mtu atakuelewa ukianza kuhubiri harakati za TANU na mchango wa Waislamu kwenye kudai uhuru. Hao audience wako Waumini wa Uislamu na Watanzania wenzetu tumesoma nao pamoja shuleni kuanzia Nursery School. Mzee hawatakuelewa.
 
Wewe mzee unaishi kwenye historical "bubble". Pamoja na kwamba una tabia ya kupotosha ukweli, lakini ukubali tu Tanzania siyo nchi ya Udini. Unahangaika sana kupotosha ukweli kwa kuipaka Historia ya Tanzania kwa kutumia udini, na ni dhahiri umeshindwa kwenye juhudi zako, na sasa unakuja na mbinu mbadala kueneza udini wako kupitia nyuzi za Wasifu wa Wazee au Wafu waumini wa Uislamu.
Flori...
Umeghadhibika.

Kawaida mtu anapoanza na kejeli kama kunitambulisha kwa, "Wewe Mzee," ni wazi hasira zimepanda.

Mimi nimeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Si kuwa nimetafiti kuhusu dini peke yake nimeingia kwenye mengi yaliyokuwapo katika historia hii mfano wa nyimbo za lelemama, taarab, mpira wa Sunderland na Yanga nk.

Kwa kawaida khasa kijana anapozungumza na mzee ikiwa ana malezi mema atachunga mipaka ya adabu.

Historia ya TANU imeandikwa mwaka wa 1981 na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini haikuwa historia niijuayo mimi.

Nimeandika historia hii kama ilivyostahili kuandikwa.

Kitabu kimependwa sana na kimechapwa sasa mara nne kwa Kiingereza na Kiswahili.

Kimepata review katika Cambridge Journal of African History.

Waulize wajuzi wakueleze nini maana ya kitabu kufanyiwa review katika journal hii.

Hao unaowatukana kwa kuwaita "wafu," mimi wengine ni baba na babu zangu na ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana.

Ikiwa unaghadhibishwa na mimi kuandika historia yao hii ni bahati mbaya sana kwako kwani wengi wamenipongeza kwa kazi hii ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na nimepokea medali na mialiko kadhaa kutoka vyuo mbalimbali duniani.

Hizi si dalili ya mtu aliyeshindwa.

Screenshot_20210903-215034_WhatsApp.jpg
 
Hata huko msikitini kwako sidhani kuna mtu atakuelewa ukianza kuhubiri harakati za TANU na mchango wa Waislamu kwenye kudai uhuru. Hao audience wako Waumini wa Uislamu na Watanzania wenzetu tumesoma nao pamoja shuleni kuanzia Nursery School. Mzee hawatakuelewa.
Flori...
Naeleweka sana.

FM stations na TV achilia mbali wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wanapishana mlangoni kwangu kutaka mahojiano na mimi.

Nadhani wewe ndiye usiyeeleweka kwa kuogopa historia ya kweli na kuja katika mjadala na hamaki na kejeli.

Hao uliosomanao ndiyo waliofanya kitabu cha Abdul Sykes kichapwe mara nne katika miaka 23 toka kichapwe kwa mara ya kwanza kwa Kiingereza.

Picha hiyo ni mazungumzo yangu na Mtangazaji Maureen wa TBC 2020.

Screenshot_20210903-223146_WhatsApp.jpg

Sikiliza majadiliano hapo chini:

NILIVYOKUTANA NA MZEE SUED KAGASHEKI KATIKA MAZUNGUMZO NA DOSSA AZIZ 1980s

Mmoja katika marafiki zangu ameniletea picha kadhaa za wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika Kanda ya Ziwa, Bukoba.

Moja ya picha hizi ni picha ya Sued Kagasheki mmoja wa viongozi wa TAA na muasisi wa TANU Kanda ya Ziwa, Bukoba.

Namkumbuka Mzee Sued Kagasheki siku alipokuja Msikiti wa Shadhly hapa Dar es Salaam.

Sikumbuki siku ile kulikuwa na hafla gani lakini ninachokumbuka ni kuwa alipofariki palifanyika kisomo chake pale msikitini na Sheikh Aboud

Maalim alimzungumza Mzee Kagasheki baada ya dua.

Sheikh Aboud Maalim akaeleza ile hadhira kuwa Mzee Kagasheki alikuja kusali Msikiti wa Manyema wakati ule unajengwa.

Kwa kuona kuwa pale pana ujenzi Mzee Kagasheki alitoa fedha kumpa Sheikh Aboud zisaidie ujenzi.

Baada ya utangulizi huu nataka nieleze jinsi nilivyokuja kukutana na mzalendo huyu wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.

Tulikuwa tumekaa barazani kwa Dossa Aziz nyumbani kwake Mlandizi nyakati za asubuhi kama saa nne mimi, Ally Sykes na mama mmoja Mmarekani Mweusi mwandishi wa Washington Post.

Pembeni ya mabaki ya landrover mbele ya nyumba wa Dossa Aziz, Ally Sykes alikuwa ameegesha Mercedes Benz yake rangi ya bluu iliyokoza, yaani ‘’dark blue.’’

Dossa Aziz akanyoosha kidole chake cha shahada akaniambia, "Nimetembea Tanganyika nzima na Nyerere kwenye Land-rover hii."

Miaka mingi sana Ally Sykes na Dossa Aziz walikuwa hawajaonana.

Walikumbatiana kwa mapenzi makubwa mimi nikiwaangalia na kuvuta hisia watu hawa walikuwaje katika ujana wao wakati wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Tofauti baina yao ilikuwa kubwa sana.

Wote walikuwa watoto kutoka familia kubwa mashuhuri na tajiri katika Dar es Salaam ya miaka ile na wote walikuwa wafadhili wakubwa wa TANU na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Dossa alikuwa amepigwa na ufukara.

Hayo hapo chini ndiyo niliyoelezwa na Dossa Aziz siku ile na akanifisha na kunikutanisha ndani ya mazungumzo na Sued Kagasheki kama alivyokuwa miaka ya 1950:

‘’Mwaka wa 1951 Kenyatta kwa mara nyingine aliitisha mkutano mwingine baina ya KAU na TAA mjini Arusha (mwaka wa 1950 Abdul Sykes alifanya mkutano wa siri na Kenyatta Nairobi).

Katika ujumbe alioutuma kwa TAA, Kenyatta alisisitiza kuwa uongozi wa chama cha TAA uende mkutanoni na silaha.

TAA iliwateua Abdulwahid, Dossa Aziz na Stephen Mhando kuhudhuria mkutano huo.

Abdulwahid alikuwa na bastola aliyopewa wakati wa vita na ofisa mmoja mzungu kama zawadi.

Ilitokea kuwa siku ya kuzaliwa ya Mzungu yule ilikuwa sawa na yake na kwa sababu yule mzungu akampa bastola yake kwa ukumbusho.

Dossa Aziz alikuwa na bunduki iliyokuwa ikipiga risasi tano kwa mfululizo.

Haijulikani kama Mhando alikuwa na silaha.
Wajumbe wa TAA walisafiri kila mtu peke yake kupoteza lengo.

Dossa Aziz alikuwa wa kwanza kuondoka kuelekea Arusha kupitia Dodoma.

Siku zile kulikuwa hakuna barabara ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha.

Wasafiri waliotaka kwenda Arusha ilibidi wasafiri wapitie Dodoma.
Dossa Aziz alifungasha ile bunduki yake ya risasi tano.

Mjini Dodoma, Dossa Aziz alipokelewa na Mwalimu Ali Juma Ponda, katibu wa TAA Central Province.

Baada ya kuelezwa na Dossa kuhusu ule mkutano wa TAA na KAU uliopangwa kufanyika Arusha, Ponda aliwaarifu Dossa Aziz kuwa kulikuwa na mapigano makali kati ya Mau Mau na vikosi vya Waingereza yaliyosababisha viongozi wa KAU kusakwa na kukamatwa.

Ponda alimfahamisha Dossa kuwa ingelikuwa vigumu katika hali kama hiyo kwa Kenyatta na ujumbe wake kuja Arusha.

Dossa Aziz aliamua kuvunja safari ya Arusha na kuelekea Mwanza kwa gari la moshi kukagua matawi ya TAA.

Mwanza, Dossa Aziz alipokewa na Dr Joseph Mutahangarwa, makamu wa rais wa TAA katika kanda ya ziwa.

Dr Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kufuzu udaktari.

Baada ya kuelezwa kuhusu ule mkutano wa Arusha, Dr Mutahangarwa alimwonya Dossa kuhusu hatari ya mwenendo aliokuwa akichukua Abdulwahid kama katibu na kaimu rais wa TAA.

Dr Mutahangarwa alimweleza Dossa hatari ambazo TAA na uongozi wake ungezikabili pindi serikali ikigundua kwamba TAA ilikuwa ikijaribu kuunganisha mapambano ya TAA na yale ya KAU.

Hofu hii aliyoonyesha Dr Mutahangarwa ilikuwa bila wasiwasi wowote hofu ya kweli kabisa kwa sababu KAU ilikuwa inaunga mkono harakati za Mau Mau na Waingereza waliamini kuwa uongozi wa mapambano yale ulikuwa ukitoka KAU na Kenyatta wakiwa na Kaggia walishukiwa kuwa kati ya viongozi hao.

Kutoka Mwanza Dossa alipanda meli hadi Bukoba ambako alipokewa na Chifu Rutinwa pamoja na mwanasiasa mkongwe, Ally Migeyo na Suedi Kagasheki na wanachama wengine wa TAA katika tawi la Bukoba.

Aliporudi Dar es Salaam, Dossa alikamatwa katika stesheni ya gari moshi na kupelekwa Central Police.

Kituo hiki kilikuwa mkabala la lango kuu la steshini ya treni.
Dossa alipelekwa pale na kuhojiwa.

Ofisa wa Polisi Mzungu alitaka kujua kwa nini Dossa alikuwa akisafiri na bunduki.

Baba yake Dossa, Aziz Ally aliingilia kati na Dossa akaachiliwa huru
bila ya kufunguliwa shtaka lolote.

May be an image of 1 person
View attachment 1921439
Bwana Mohamed historia safi sema sina uhakika kama huyo Daktari Muta ni mswahili wa kwanza kuwa daktari. Kwa upande wa kusini mwa jangwa la Sahara nadhani mmojawapo wa madaktari wa mwanzo ni Dr William Anderson Soga wa Afrika Kusini aliyepata shahada yake ya utabibu mwaka q1883 ukiachia wengine waliofuatia toka Ghana, Nigeria na Siera Leone kama sikosei.
 
Mkuu Maalim, Mohamed Said, naomba tuambizane ukweli bayana, sio mara moja wala mbili katika hoja zako ama unadanganywa na hao sources wako na kutuletea urongo humu, ama ni wewe ndio huongeza chumvi ili kunogesha hoja zako.

Kazi yangu mimi ni moja tuu, being critical kwenye urongo na chumvi chumvi.

Ameandika huyu Daktari ndiye Daktari wa kwanza Africa, nikakuomba substiate, umeshindwa!.

Jee unaukumbuka ule urongo wako wa kusema ndani ya Bunge letu, Waislamu ni asilimia 6%?, na uliwekwa hadi YouTube ?. Baada ya mimi kukukosoa kuwa huo ni urongo, ndipo kule YouTube ukaondolewa?. What was your motive kwa uongo kama ule ?.
Amini usiamini, angalizo hili
lilisaidia ulitulia kidogo, sasa naona unaanza tena mdogo mdogo, kwa vichumvi chumvi vidogo vidogo, tukinyamaza utazidi kukoleza!.

Kama unaamini dakitari wa kwanza Bara zima lote la Africa alitoka Tanzania, thibitisha !. Kama mimi kukuambia hiyo ni chumvi na umeona neno hilo ni tusi, naomba radhi, naomba msamaha, nisamehe bure, mimi ni Mkristo wa type ya Tomaso, kazi yangu ni kuhoji tuu na sio kwako tuu, nimemuhoji hadi Magufuli !.

Samahani tena, endelea na mnakasha huu bila bughudha ya kuhojiwa hojiwa na sisi akina Tomaso wa humu JF.
P
Pascal,
Unaandika kifua chako kikiwa kina joto na sababu ya moto huo kifuani ni "disappointments."

Kwa muda mrefu ukisomeshwa historia ambayo kwa uhakika haikuwa historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nakusoma na kuona hizo dharau na kejeli kama ilivyo kawaida ambayo umeathirika vibaya mno.

Lugha zisizo na adabu nk.

Ungeweza ukasema kuwa niliyoandika yana makosa lakini ghadhabu zimetawala fikra zako na lugha inayokupendeza ni kujaribu kunifedhehesha kwa kuniita mimi muongo.

Ningekuwa na sifa ya uongo nisingealikwa kuzungumza kwenye vyuo vikuu ndani na nje ya Tanzania.

Ningekuwa muongo nisingèchapwa na wachapaji vitabu wa kutajika ulimwenguni kama Oxford University Press.

Ningekuwa muongo nisingeshirikishwa katika uandishi wa historia kwa shule za msingi Afrika ya Mashariki.

Ningekuwa muongo nisingejumuishwa na Harvard na Oxford University Press, New York kuandika Dictionary of African Biography (DAB).

Hilo la Dr. Joseph Mutahangarwa nimekujibu lakini wewe si mtu wa kufanya mjadala wa kistaarabu wewe umekuja kwangu kutaka kuniumbua.

Hawa walikuwa madaktari watano waliofuzu Makerere College, Uganda- Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Michael Lugazia na Dr. Wilbard Mwanjisi.

Umekuja na vichekesho.
Ama kuhusu vyanzo.

Chanzo kimoja katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni babu yangu Salum Abdallah.

Yuko hapa JF mtafute.

Chanzo kingine ni Nyaraka za Sykes.

Nimeandika kitabu kizima kuhusu Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968).

Sifa zake zinafahamika.

Baba yake ni muasisi wa Tanganyika African Association 1929.

Abdul mtoto sihitaji kumueleza.
Mtafute JF yuko mwingi sana.

Mengine uliyoleta hapa nimeona bora kukaa kimya.
 
yaani wewe Pascal Mayalla nilikua nakuona mstaarabu kumbe kiazi kabisa, ndio maana mwenda zake alikupa za uso kipindi kile. Huna hoja zaidi ya kutafutia umaarufu kwenye thread za wenzio, hata hivyo jaribu kua mstaarabu/ kua na adabu kwa wazee wako. Kumradhi sheikh Mohamed Said .
Planet,
Kinachomchoma ni hizi "facts."

1950 Abdulwahid Sykes anafanya mkutano wa siri na Jomo Kenyatta. Nairobi.

Pamoja na Kenyatta walikuwa Peter Mbiu Koinange, Kun'gu Karumba, Bildad Kaggia, Paul Ngei kwa kuwataja wachache.

Abdul wakati huo alikuwa na miaka 26.

Mwaka wa 1954 Abdul atakapokuja kuwa mmoja wa wazalendo 17 walioasisi TANU kadi yake no.3.

Haya ndiyo yanayomchoma moyo kwani historia hii haikutakiwa ifahamike.

Ndiyo sababu hagusi huko yeye muhimu kwake ni kuwa ningesema Dr. Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kuhitimu uganga Tanganyika.

Kwa kutoitaja Tanganyika mimi nimefanya kosa kubwa sana la kusema chembelecho, "urongo."
 
Flori...
Nakusihi usiende huko inawezekana sana unafanya haya kwa kutokujua nami nakuchukulia hivyo.

Kwa ajili hiyo basi nitabaki kimya ili uelewe na urudi nyuma sote tusalimike.
Asante kwa majibu ya kistaarabu, maana wengine hata hawajui wanachozungumza alimradi tu waonyeshe chuki zao.
 
Flori...
Umeghadhibika.

Kawaida mtu anapoanza na kejeli kama kunitambulisha kwa, "Wewe Mzee," ni wazi hasira zimepanda.

Mimi nimeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Si kuwa nimetafiti kuhusu dini peke yake nimeingia kwenye mengi yaliyokuwapo katika historia hii mfano wa nyimbo za lelemama, taarab, mpira wa Sunderland na Yanga nk.

Kwa kawaida khasa kijana anapozungumza na mzee ikiwa ana malezi mema atachunga mipaka ya adabu.

Historia ya TANU imeandikwa mwaka wa 1981 na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini haikuwa historia niijuayo mimi.

Nimeandika historia hii kama ilivyostahili kuandikwa.

Kitabu kimependwa sana na kimechapwa sasa mara nne kwa Kiingereza na Kiswahili.

Kimepata review katika Cambridge Journal of African History.

Waulize wajuzi wakueleze nini maana ya kitabu kufanyiwa review katika journal hii.

Hao unaowatukana kwa kuwaita "wafu," mimi wengine ni baba na babu zangu na ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana.

Ikiwa unaghadhibishwa na mimi kuandika historia yao hii ni bahati mbaya sana kwako kwani wengi wamenipongeza kwa kazi hii ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na nimepokea medali na mialiko kadhaa kutoka vyuo mbalimbali duniani.

Hizi si dalili ya mtu aliyeshindwa.
Sheikh Mohammed naamini unaelewa maana ya 'summun, bukmun, umyun' (deaf, dumb, blind) - kwa hivyo hata ukijitahidi vipi ni kazi bure tu.
 
Samahani mzee Said.
Ilikuchukua miaka mingapi kufanya utafiti wa kuandika kitabu Cha Abdulwahid Sykes,na je ulifanya utafiti mfululizo?
Na fedha ya kugharamia utafiti ulipata wapi?

Nisamehe Kama maswali yangu hutayapenda.

Mimi mwandishi chipukizi.
 
Nyati...
Swali lako halina tatizo.

Ni tabu kwangu kusema lini nilianza utafiti.

Lakini moto wa mimi kuzungumza na kusahihisha yale niliyoona yanakosewa ulipamba mwaka wa 1984 nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.

Hapo ndiyo nikaingia Maktaba ya chuo na kuanza kusoma kila kitabu juu ya Julius Nyerere.

Nikatumia muda mwingi East Africana kusoma magazeti ya zamani hasa Kwetu la Erika Fiah, Zuhra la Ramadhani Mashado Plantanl, Mwafrika na Sauti ya TANU.

Utafiti ulikuwa mfululizo na haukunigharimu fedha za kusema kuwa zilikuwa fedha nyingi.

Nilipokuja kufungua Nyaraka za Sykes hapo ndipo nilipopigwa na butwaa na kupata mshtuko mkubwa.

Mswada ulikamilika mwaka wa 1991 lakini kila publisher niliyempa mswada aliogopa kuchapa kitabu changu.

Niliwaonyesha Oxford University Press wao waliniambia kazi ni nzuri sana lakini wao hawawezi kuichapa na wakanieleza sababu zao lakini wakanielekeza kwa publisher mwingine ambae angechapa.
 
Shukran
 
Hivyo wazee wakiongopa, wakisema uongo au urongo wasiambiwe ?. Kama JK ameambiwa ukweli humu, JPM ameambiwa ukweli humu na Samia pia ataambiwa, who is he compared hata aje adanganye humu asiambiwe. Dawa pekee ya kutunza heshima kwa wakubwa zetu hawa, ni kwa wao kusema ukweli daima, uongo kwao mwiko!. Ni bahati mbaya sana, sisi wengine wenu sio watu wa kukopesha, ukisema uongo tunakurekebisha.
P
Pascal,
Ajabu ya Rahman.
Nimeishiwa maneno.

Imekuwa, "who is he?"
Unanishambulia mimi binafsi.

Mimi si lolote si chochote.

Mjukuu wa Salum Abdallah mmoja katika wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika toka enzi za African Association.

Kwa ajili hii nimeijua historia ya TANU kuliko watu wengi sana.

Historia hii ndiyo hii naisomesha hapa.

Salum Abdallah babu yangu mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa mwisho wa Railways dhidi ya Waingereza uliodumu siku 82.
 
Back
Top Bottom