Nilivyokutana na Mzee Sued Kagasheki katika mazungumzo na Dossa Aziz 1980s

Kuna mzee mmoja huko Bukoba anaitwa Mzee King, anayo hazina kubwa ya Historia ya wapigania Uhuru kule BuKoba na West Lake Region kwa ujumla kama ilivyojulikana hapo zamani.
Bullet,
Picha ya Mzee Sued Kagasheki nimepata kwake Bwana Ramadhani Kingi.
 
Kwani Quran haina mafundisho ya Udaktari? Maana Quran ndiyo kila kitu. Leo hii wangejaa madaktari wa afya dunia nzima waliosomea Udaktari kupitia Quran. Allah kaweka wazi kila kitu kwenye Quran kulingana na Waumini. Isitoshe ma Engineer wa kila nyanja wangesomea fani zao kupitia Quran, maana Quran kwa Waumini ndiyo mpango mzima wa maisha ya binaadamu.
 

Pascal,
Nilitegemea haya yote yaliyohitimishwa na hilo neno, ''chumvi.''

Hii inaitwa, ''bashing,'' ni kawaida sana katika hali kama yangu.

Sichukizwi na hayo zaidi na sana sana ni kipimo changu.

Katika makala iliyo na mengi ya kufikirisha mfano wa mkutano wa Jomo Kenyatta na Abdul Sykes Niarobi 1950 na mkutano wa pili Arusha ulioitishwa na Kenyatta 1951 ambao haukufanyika haya yote yamekupita ulichokiona wewe ni mimi kusahau kuweka ''coma,'' kwenye sentensi.

Juu ya haya yote nimekujibu kistaarabu.

Jibu halikukuridhisha umerudi na mengine na suala la ''chumvi.''

Hili ni tusi kwangu.

Ikiwa unataka ushahidi wa mkutano huu ninao kutoka Nyaraka za Special Branch kutoka Rhodes House, Oxford.

Nifahamishe ikiwa unataka kuona ushahidi nitauweka hapa.

Mimi nimesomeshwa ilm ya ''mnakasha,'' yaaani mjadala na mwalimu wangu marehemu Sheikh Haruna.

Yeye somo la kwanza alilonifunza ni adabu ya elimu.

Ukiwa na elimu alikuwa akisema ionekane kwa watu katika lugha na hoja zako.

Akisema, ''Usiende ukanitukanisha kwani wakusikiao ukiropoka watauliza nani alikusomesha?

Hapo nitatukanwa mie mwalimu wako.''

''It takes two to Tango.''
 
Wewe mzee unaishi kwenye historical "bubble". Pamoja na kwamba una tabia ya kupotosha ukweli, lakini ukubali tu Tanzania siyo nchi ya Udini. Unahangaika sana kupotosha ukweli kwa kuipaka Historia ya Tanzania kwa kutumia udini, na ni dhahiri umeshindwa kwenye juhudi zako, na sasa unakuja na mbinu mbadala kueneza udini wako kupitia nyuzi za Wasifu wa Wazee au Wafu waumini wa Uislamu.
 
Flori...
Nakusihi usiende huko inawezekana sana unafanya haya kwa kutokujua nami nakuchukulia hivyo.

Kwa ajili hiyo basi nitabaki kimya ili uelewe na urudi nyuma sote tusalimike.
 
Hata huko msikitini kwako sidhani kuna mtu atakuelewa ukianza kuhubiri harakati za TANU na mchango wa Waislamu kwenye kudai uhuru. Hao audience wako Waumini wa Uislamu na Watanzania wenzetu tumesoma nao pamoja shuleni kuanzia Nursery School. Mzee hawatakuelewa.
 
Flori...
Umeghadhibika.

Kawaida mtu anapoanza na kejeli kama kunitambulisha kwa, "Wewe Mzee," ni wazi hasira zimepanda.

Mimi nimeandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Si kuwa nimetafiti kuhusu dini peke yake nimeingia kwenye mengi yaliyokuwapo katika historia hii mfano wa nyimbo za lelemama, taarab, mpira wa Sunderland na Yanga nk.

Kwa kawaida khasa kijana anapozungumza na mzee ikiwa ana malezi mema atachunga mipaka ya adabu.

Historia ya TANU imeandikwa mwaka wa 1981 na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini haikuwa historia niijuayo mimi.

Nimeandika historia hii kama ilivyostahili kuandikwa.

Kitabu kimependwa sana na kimechapwa sasa mara nne kwa Kiingereza na Kiswahili.

Kimepata review katika Cambridge Journal of African History.

Waulize wajuzi wakueleze nini maana ya kitabu kufanyiwa review katika journal hii.

Hao unaowatukana kwa kuwaita "wafu," mimi wengine ni baba na babu zangu na ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana.

Ikiwa unaghadhibishwa na mimi kuandika historia yao hii ni bahati mbaya sana kwako kwani wengi wamenipongeza kwa kazi hii ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na nimepokea medali na mialiko kadhaa kutoka vyuo mbalimbali duniani.

Hizi si dalili ya mtu aliyeshindwa.

 
Flori...
Naeleweka sana.

FM stations na TV achilia mbali wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wanapishana mlangoni kwangu kutaka mahojiano na mimi.

Nadhani wewe ndiye usiyeeleweka kwa kuogopa historia ya kweli na kuja katika mjadala na hamaki na kejeli.

Hao uliosomanao ndiyo waliofanya kitabu cha Abdul Sykes kichapwe mara nne katika miaka 23 toka kichapwe kwa mara ya kwanza kwa Kiingereza.

Picha hiyo ni mazungumzo yangu na Mtangazaji Maureen wa TBC 2020.


Sikiliza majadiliano hapo chini:

https://www.facebook.com/
 
Bwana Mohamed historia safi sema sina uhakika kama huyo Daktari Muta ni mswahili wa kwanza kuwa daktari. Kwa upande wa kusini mwa jangwa la Sahara nadhani mmojawapo wa madaktari wa mwanzo ni Dr William Anderson Soga wa Afrika Kusini aliyepata shahada yake ya utabibu mwaka q1883 ukiachia wengine waliofuatia toka Ghana, Nigeria na Siera Leone kama sikosei.
 
Pascal,
Unaandika kifua chako kikiwa kina joto na sababu ya moto huo kifuani ni "disappointments."

Kwa muda mrefu ukisomeshwa historia ambayo kwa uhakika haikuwa historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nakusoma na kuona hizo dharau na kejeli kama ilivyo kawaida ambayo umeathirika vibaya mno.

Lugha zisizo na adabu nk.

Ungeweza ukasema kuwa niliyoandika yana makosa lakini ghadhabu zimetawala fikra zako na lugha inayokupendeza ni kujaribu kunifedhehesha kwa kuniita mimi muongo.

Ningekuwa na sifa ya uongo nisingealikwa kuzungumza kwenye vyuo vikuu ndani na nje ya Tanzania.

Ningekuwa muongo nisingèchapwa na wachapaji vitabu wa kutajika ulimwenguni kama Oxford University Press.

Ningekuwa muongo nisingeshirikishwa katika uandishi wa historia kwa shule za msingi Afrika ya Mashariki.

Ningekuwa muongo nisingejumuishwa na Harvard na Oxford University Press, New York kuandika Dictionary of African Biography (DAB).

Hilo la Dr. Joseph Mutahangarwa nimekujibu lakini wewe si mtu wa kufanya mjadala wa kistaarabu wewe umekuja kwangu kutaka kuniumbua.

Hawa walikuwa madaktari watano waliofuzu Makerere College, Uganda- Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Michael Lugazia na Dr. Wilbard Mwanjisi.

Umekuja na vichekesho.
Ama kuhusu vyanzo.

Chanzo kimoja katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni babu yangu Salum Abdallah.

Yuko hapa JF mtafute.

Chanzo kingine ni Nyaraka za Sykes.

Nimeandika kitabu kizima kuhusu Abdulwahid Kleist Sykes (1924 - 1968).

Sifa zake zinafahamika.

Baba yake ni muasisi wa Tanganyika African Association 1929.

Abdul mtoto sihitaji kumueleza.
Mtafute JF yuko mwingi sana.

Mengine uliyoleta hapa nimeona bora kukaa kimya.
 
Planet,
Kinachomchoma ni hizi "facts."

1950 Abdulwahid Sykes anafanya mkutano wa siri na Jomo Kenyatta. Nairobi.

Pamoja na Kenyatta walikuwa Peter Mbiu Koinange, Kun'gu Karumba, Bildad Kaggia, Paul Ngei kwa kuwataja wachache.

Abdul wakati huo alikuwa na miaka 26.

Mwaka wa 1954 Abdul atakapokuja kuwa mmoja wa wazalendo 17 walioasisi TANU kadi yake no.3.

Haya ndiyo yanayomchoma moyo kwani historia hii haikutakiwa ifahamike.

Ndiyo sababu hagusi huko yeye muhimu kwake ni kuwa ningesema Dr. Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kuhitimu uganga Tanganyika.

Kwa kutoitaja Tanganyika mimi nimefanya kosa kubwa sana la kusema chembelecho, "urongo."
 
Flori...
Nakusihi usiende huko inawezekana sana unafanya haya kwa kutokujua nami nakuchukulia hivyo.

Kwa ajili hiyo basi nitabaki kimya ili uelewe na urudi nyuma sote tusalimike.
Asante kwa majibu ya kistaarabu, maana wengine hata hawajui wanachozungumza alimradi tu waonyeshe chuki zao.
 
Sheikh Mohammed naamini unaelewa maana ya 'summun, bukmun, umyun' (deaf, dumb, blind) - kwa hivyo hata ukijitahidi vipi ni kazi bure tu.
 
Samahani mzee Said.
Ilikuchukua miaka mingapi kufanya utafiti wa kuandika kitabu Cha Abdulwahid Sykes,na je ulifanya utafiti mfululizo?
Na fedha ya kugharamia utafiti ulipata wapi?

Nisamehe Kama maswali yangu hutayapenda.

Mimi mwandishi chipukizi.
 
Samahani mzee Said.
Ilikuchukua miaka mingapi kufanya utafiti wa kuandika kitabu Cha Abdulwahid Sykes,na je ulifanya utafiti mfululizo?
Na fedha ya kugharamia utafiti ulipata wapi?

Nisamehe Kama maswali yangu hutayapenda.

Mimi mwandishi chipukizi.
Nyati...
Swali lako halina tatizo.

Ni tabu kwangu kusema lini nilianza utafiti.

Lakini moto wa mimi kuzungumza na kusahihisha yale niliyoona yanakosewa ulipamba mwaka wa 1984 nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.

Hapo ndiyo nikaingia Maktaba ya chuo na kuanza kusoma kila kitabu juu ya Julius Nyerere.

Nikatumia muda mwingi East Africana kusoma magazeti ya zamani hasa Kwetu la Erika Fiah, Zuhra la Ramadhani Mashado Plantanl, Mwafrika na Sauti ya TANU.

Utafiti ulikuwa mfululizo na haukunigharimu fedha za kusema kuwa zilikuwa fedha nyingi.

Nilipokuja kufungua Nyaraka za Sykes hapo ndipo nilipopigwa na butwaa na kupata mshtuko mkubwa.

Mswada ulikamilika mwaka wa 1991 lakini kila publisher niliyempa mswada aliogopa kuchapa kitabu changu.

Niliwaonyesha Oxford University Press wao waliniambia kazi ni nzuri sana lakini wao hawawezi kuichapa na wakanieleza sababu zao lakini wakanielekeza kwa publisher mwingine ambae angechapa.
 
Shukran
 
Pascal,
Ajabu ya Rahman.
Nimeishiwa maneno.

Imekuwa, "who is he?"
Unanishambulia mimi binafsi.

Mimi si lolote si chochote.

Mjukuu wa Salum Abdallah mmoja katika wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika toka enzi za African Association.

Kwa ajili hii nimeijua historia ya TANU kuliko watu wengi sana.

Historia hii ndiyo hii naisomesha hapa.

Salum Abdallah babu yangu mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa mwisho wa Railways dhidi ya Waingereza uliodumu siku 82.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…