Nilivyokutana na Mzee Sued Kagasheki katika mazungumzo na Dossa Aziz 1980s

ukweli utabaki palepale kua paskali wewe unapenda zaidi umaarufu kwa kudhalilisha wengine kwa kujiona mjuaji.
PERIOD.
 
Leo hii wangejaa madaktari wa afya dunia nzima waliosomea Udaktari kupitia Quran. Allah kaweka wazi kila kitu kwenye Quran kulingana na Waumini. Isitoshe ma Engineer wa kila nyanja wangesomea fani zao kupitia Quran

CHUO GANI DUNIANI kinatoa mafunzo ya Udaktari kupitia Quran ??!!
 
Jina la mwandishi wa Washington post tafadhali
 
Alipata hadhi, amewahi kukalia kiti cha ubalozi Tanzania nchini Uswissi baada ya idara.
 


Why Una overreacting?
 
Hujawahi kuwa Na rafiki aliye wa Imani tofauti nayako?

Hujui historian yeyote ya nchi Yetu inayomuhusu mtanzania aliye Mkiristo?
 
Hujawahi kuwa Na rafiki aliye wa Imani tofauti nayako?

Hujui historian yeyote ya nchi Yetu inayomuhusu mtanzania aliye Mkiristo?
Uzalendo...
Ninao marafiki wengi wa imani tofauti nami.

Najua historia inayomuhusu Mtanzania aliye Mkristo.
 
Bwana Mohamed historia safi sema sina uhakika kama huyo Daktari Muta ni mswahili wa kwanza kuwa daktari. Kwa upande wa kusini mwa jangwa la Sahara nadhani mmojawapo wa madaktari wa mwanzo ni Dr William Anderson Soga wa Afrika Kusini aliyepata shahada yake ya utabibu mwaka q1883 ukiachia wengine waliofuatia toka Ghana, Nigeria na Siera Leone kama sikosei.
 
Why Una overreacting?
The Boss,
Kichekesho ni kuwa hakuna popote niliposema, "Daktari wa kwanza Afrika."

Kilichomchoma ni ule msisimko katika historia ya Abdul Sykes alivyokuja kuunda TANU 1954.

Kijana wa mjini Dar es Salaam 1950 akiwa na umri wa miaka 26 na akiwa kiongozi wa TAA anafanya mkutano wa siri na viongozi wa KAU ambao baadae walikuja kujulikana kama The Kapenguria Six, hili kwake ni zito sana.

Kijana huyu, Abdul Sykes si tu alikuwa kiongozi wa TAA baba yake ndiyo muasisi wa harakati hizi 1929.

Abdul Sykes atampokea Julius Nyerere 1952 na 1953 atafanya mkutano mwingine wa siri na Hamza Mwapachu nyumbani kwake Nansio Ukerewe kujadili ikiwa Julius Nyerere aingizwe kwenye uongozi wa juu wa TAA awe President na mwaka wa 1954 waunde TANU.

Katika mkutano huu mwingine aliyekuwapo alikuwa Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama kilichotokana na African Association na kiliundwa 1933 na baba yake Abdul Syke Kleist Sykes na Mzee bin Sudi aliyekuwa President wa African Association.

Historia hii inamchoma Pascal kiasi inamvuruga akili.

Kalamu yangu katika historia hii ya TANU na uhuru wa Tanganyika na katika kumueleza Julius Nyerere hapo ndipo ilipobeba kikombe.

Hakuna aliyekuwa anayajua haya.

Vipi Pascal historia hii haimshughulishi anahangaishwa na jambo dogo lisilo na uhusiano wowote na historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika?
 
Father,
Mimi katika historia hii nazungumza historia ya Tanganyika African Association na wanaharakati wake watano madaktari.

Kati ya hao watano Dr. Joseph Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kuhitimu.

Ghana, Nigeria na Afrika Kusini wanaingiaje katika historia hii?
 

Mzee kwa bahati mbaya sana hauelezei historia ya Tanganyika kwa ufasaha ila unajaribu kupotosha kwa makusudi kwa kuingiza udini
 
Ukiandika maelezo yako uwe unayapitia pia kuyakumbuka. Ngoja nikunukuu kujibu swali lako "Dr Mutahangarwa alikuwa Mwafrika wa kwanza kufuzu udaktari." Wapi hayo unayosema kuwa hao niliotaja wanaingiaje. Kimsingi, linaweza kuwa kosa la kawaida katika uandishi. Hata hivyo, umefanya general assertion ambayo, kiuandishi wa kisomi, kama ningekuwa nakusahihisha, nisingekosa kuuliza swali, MWAFRIKA WA KWANZA KUFUZU UDAKTARI?!!!!! Seriously? Kwa vile wewe ni mwandishi na msomi, hapa utaelewa na kukubali kuwa ulikosea jambo ambalo ni la kawaida na kama binadamu lazima utakosea hata pale ambapo hukutegemea kwa msomi wa kiwango chako.
 
Kuna watu humu, they are always right, wakileta hoja hata kama zina uongo na chumvi ndani yake, hawataki kukosolewa!. Mtu analeta uongo, anaambiwa huo ni uongo, anasema ametukanwa!.
P
 
Ustaarabu ni ukikosea, kwanza kubali kosa, kisha sema sorry, rekebisha mnakasha uendelee kwa amani bila kuongeza chumvi chumvi !.
P
 
Mzee kwa bahati mbaya sana hauelezei historia ya Tanganyika kwa ufasaha ila unajaribu kupotosha kwa makusudi kwa kuingiza udini
Uzalendo...
Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa ukweli wake ingawa bahati mbaya wewe unaona ni historia inayokuza Uislam kwa hiyo ni udini.

Angalia picha za nyakati zile zilivyo.

Hatuwezi kuukataa ukweli huu vinginevyo itakuwa si historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.
 
Ustaarabu ni ukikosea, kwanza kubali kosa, kisha sema sorry, rekebisha mnakasha uendelee kwa amani bila kuongeza chumvi chumvi !.
P
Pascal,
Mimi sijaona kosa wala wahariri wanne wa kitabu hicho hawakuliona hilo kosa.

Sijapata kuandika chembelecho "chumvi" kama unavyoshikilia lau nimekutahadharisha kuwa hilo ni tusi.

Ungekuwa muungwana ungeacha lakini ajabu ni kuwa hushughulishwi na akhlak njema.

Unaendelea kunitukana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…