Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Jinsi nilivyokuwa napika kitimoto na ndizi. Kwanza mfahamu kuwa nilikuwa napika chakula kingi, siyo kama kile cha kwenye video.
Mahitaji.
Kitimoto kilo moja.
Ndizi mzuzu kumi, napendelea zile zinakaribia kuiva(zisiive sana).
Kitunguu kimoja kikubwa.
Nyanya kubwa nne.
Hoho moja kubwa
Pilipili ya tunda(Optional).
Namenya na kukatakata ndizi kwa saizi ya kati, ila zisiwe ndogo sana. Nazichemsha hadi zinaiva kidogo. Ndizi zikiiva natenga nyama ya kitimoto niliyokatakata motoni kuichemsha kwa maji. Naweza kuweka pilipili ya tunda ila siipasui. Kitimoto kikishaiva bado kinakuwa na supu ya kutosha. Hapo natoa ndizi na kuziweka ndani ya sufuria ya kitimoto.
Juu yake naweka Nyanya, hoho na vitunguu nilivyokatakata. Nakoroga, nafunika na kupunguza moto. Baada kama ya robo saa mambo yanakuwa tayari.
Siweki mafuta sababu supu ya ktmt tayari ina mafuta mengi. Halafu nafikiri vitunguu vya kushemshia vinafanya chakula kuwa na ladha kuliko vya kukaanga.
Hapo napakua msosi mwingi sana kwenye sahani. Nikimaliza naongeza kidogo. Moja ya chakula bora kabisa kwangu, mchuzi mzito kabisa.