Nakumbuka mwaka 2007 nilikua na ndoto za kwenda dzonga ila sikua na mpunga, kuna jamaa yangu alikua amerudi toka lebanon huko alikua deployed kwenye peace keeping alikua amerudi bongo na fedha za kigeni nikaona kupitia huyu mwamba nitapata nauli nitambae zangu ng'ambo.
Nikawa chawa wa mwamba full kumsaidia kusolve harakati za hapa na pale kutokana na uzoefu wangu wa mtaa
Sasa bhana mwamba alikua na binti mmoja wa kitanga ndio alikua anataka amfanye mkewe ili dingi yake ni mnoko kikuda mchumba ndio alituambia kipindi mwamba anampa idea ya kwenda bumbuli kujitambulisha ,mimi kama chawa nisie na maadili nikamshauri mwamba ampe binti ujauzito ndio tuende ili zoezi liwe rahisi mwana apate jiko na mimi niende zangu ng'ambo.
Mwamba akafanikiwa kurutubisha yai binti kitumbo kikaota ikapangwa safari ya kwenda usambaani kuonana na wazee.
Kufika Tanga tukapokelewa fresh na bimkubwa, na mashemeji kumbe kamanda walikua wanamjua wote kasoro mshua boy tu, na bahati mbaya au nzuri hakuwepo siku hio ikabidi mzee apigiwe simu alikua shambani kwake huko anakaaga hata mwezi bila kurudi home. Alitaarifiwa uwepo wetu akaombwa arudi fasta mzee akaomba aongee na muoaji, mshkaji akatoka nje kuongea na mkwewe, mzee akamwambia jamaa anarudi kesho jioni lakini asitukute nyumbani kwake na hataki kabisa kutusikia, mshkaji kwa tabia zake za kijeshi akamkazia mzee na mikwara ya hapa na pale kwamba hatuondoki tutakaa hata mwezi mpaka arudi tuondoke na mke wetu. Mshua akasema kesho jioni anarudi lakini hatotukuta maana tutaondoka bila kuaga kamanda akasema sawa ngoja tuoneshane umwamba.
Ilifika usiku tukapewa room ya wageni kuna bed mbili kila mtu na lake, tukaangusha na mwanangu ,tulienda na begi moja tu , mchumba aliliweka chumbani kwake kwa usalama zaidi maana chumba chetu kilikua nje,
Kufika mishale ya saa nane usiku niliota ndoto kwamba yule mzee kaihamishia mimba kwa mjeshi halafu tuko leba kamanda anajifungua, mimi na manesi tunamwambia mchizi push! push! Jamaa anapiga kelele kumbe mimi nivyoota hivyo napiga kelele kwanguvu na jamaa naye anaota ndoto hiohio na anapiga kelele za uchungu mara tukashtuka wote mshkaji ananiuliza mtoto wangu yuko wapi nikamjibu kua makini usimlalie kuinuka dah! Mwamba alikua kashusha bonge la kimba mazee halafu hawezi kulikataa yaani kafanana nalo copyright alafu mashuka yote kitanda kizima kilikua makimba tu , nikampa mashuka ya kitandani kwangu ajisafishe tutoroke kabla hakuja kucha maana asingeweza kubadili nguo zilikua chumbani na mama kijacho mjeshi akaniambia kukimbia ni mbinu ya kijesh kabisa wao wanaiita ku retreat.
Tulitoka chumbani mule kwa kucraw mpaka kwenye toyota porte yetu huku mchizi akiwa kajifunga shuka rubega tukatokomea
Tukiwa njiani mwamba ndio akakumbuka conversation yake na mkwe wetu kwamba tutaondoka bila kuaga kama PAUL KEAGAN
Tulifaka town hata mawazo ya kumpiga mzinga wa nauli ya kaisha maana analia tu kama kabinti muda wote