Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Keyboard ya mwandishi imeisha wino,akiupata wino atatuletea mrejesho sehemu ya 17.
 
Jozi, nilikuwa kwenye apartment kama siku ya pili toka nifike, natoka room kwenda kwenye vending machine iliyopo humo humo kwenye apartment kuchukua soda, nikawa niko kwenye simu naongea kiswahili, nikapishana na mdada mzuri hivi wa makamo kama 42 hivi yuko na msichana wa kazi na mtoto wa kike wana vifurushi wanaonekana wametoka shopping. Wakati narudi kwangu yule dada alikuwa bado amesimama ananisubiri nilivyotoka nilikuwa na pajama hivyo alijua kabisa siendi mbali. Akaniambia nimekusikia unaongea kiswahili wewe ni mtz au mkenya? Nikamjibu mTz, tukapiga piga stori hapo akafurahi sana, nikajua nimepata shost, Akanihoji hoji nikamwambia nimekuja tu kutembea, akaniambia yeye anaishi cape town, hapo amepita tu akitokea gaborone kwa mumewe, atakaa siku 4 then ataondoka. Nadhani alifurahi kupata mtu wa kuongea nae kiswahili siku hiyo maana appartment hiyo haikuwa na waswahili zaidi yetu, au kama ilikuwa nao sikupata kuwaona.

Basi, mi nilikaa kama miezi mitatu, nikawa namuona mara kwa mara basement kwenye parking na familia yake mi nikipanda zangu uber. Nikawa najiuliza huyu alisema atakaa siku nne sasa mbona haondoki? Nikajiongeza tu kuwa huyu anaishi hapa hapa, hakutaka tu kuniambia labda alihisi nitamzoea, au labda hakuniamini aliona sina ramani maana kiumri nilikuwa msichana mdogo bado tukawa tukionana tunasalimiana basi mpaka siku naondoka nilimuona jana yake jioni maana tulikuwa tunaishi floor moja, wing moja yeye apartment yake ilikuwa ya familia zile zina 3 bedrooms na vikorombwezi vingine, mimi yangu ilikuwa ndogo, Bedroom+sitting room, kitchen.
Mbona mnanichqnganya nyie?? Hii mbona kama Uzi ndani ya Uzi?
 
Mara nikashangaa yule Askari wa Uhamiaji wa pale Kaunta anamuita Askari mwenzie aje kumkamata yule jamaa etu kwa kosa la kutoa rushwa. Ukweli nilitetemeka kishenzi, fasta sana nilitoa pesa niliyoiweka katikati ya Passport yangu kisha nikasogea pale Kaunta. Yule Mzungu Mkaburu akawa ananiangalia tu.
Hahahaha..
You made my day bro!
 
SEHEMU YA KUMI

Kwa Kifupi ndo nikawa South Africa nimeshaingia ivo bila ya kuwa na Ndugu wala Rafiki wakunipokea. Mambo ya kusubiria kuwa na Ndugu au Rafiki yangenichelewesha sana.

Basi Nilikaa pale nje mpaka saa saba usiku ndo Jamaa akaja kunichukua. Alisema kuna sehemu alikuwepo kuna Harakati alikuwa anafanya. Jamaa akanipokea Begi hao mdogo mdogo mpaka KFC tukapata chakula kisha tukaenda Magetoni kwake. Ilikuwa ni ghorofa. Yeye alikuwa amepanga Ghorofa kama ya tatu hivi. Tulifika na kuingia ndani kwake. Kilikuwa ni chumba kimoja, sebure kubwa, Choo na Jiko. TV Kubwa, Makochi ya Kisasa. Kwa kifupi jamaa alikuwa anaishi vizuri.

Tukawa tunapiga piga story pale, Jamaa alikuwa ananichukua Maelezo ili awe na uhakika kama kweli Mimi ni Mtanzania na Kama kweli natokea Temeke. Wabongo wengi wanafanya hivyo ili kujiridhisha kama kweli wewe ni Mbongo wasije kupokea Mburundi, Mkenya au Mkongoman. Baada ya story kidogo jamaa akaniambia panda kitandani upumzike.

Hapa nitasema kama ilivyokuwa, Juu ya Kile Kitandani jamaa alikuwa ametandaza Dawa za Kulevya Kibao. Ilikuwa ndo Mara yangu ya kwanza kuziona dawa za kulevya vile. Zilikuwa nyingi sana halafu Jamaa haogopi wala nini. Alikuwa anazifunga funga. Nikahisi pengine jamaa alichelewa kuja kunifata labda alikuwa busy kufunga hizi Kete zake. Yan jamaa anafunga bila woga, tena mbele ya Mgeni. Nikajiuliza jamaa anajiamini nini.

Mimi sasa, Usingizi wote wa Safari ulikata. Maana nakumbuka nililala pembeni ya hicho kitanda halafu pembeni yangu ndo kulikuwa na hizo Dawa. Huku tunaendelea kupiga story.

Katika Maisha yangu, Dawa za Kulevya nilikuwa nazisikia tu kwenye Vyombo vya Habari na kuwaona Mateja Mtaani. Lakini ile nafika tu South Afrika ndo kama hivi nilikutana nazo tena ile ile siku ya kwanza. Mara pale ghetto tukasikia Hodi, Kisha Jamaa wawili wakaingia ndani. Nao ni wabongo. Tukasalimiana pale kisha wakaendelea na Mishe zao. Wakafungua mabegi yao na kuanza kutoa Kete zao za Dawa za Kulevya na Pesa, ni kama vile walikuwa wanamkabidhi jamaa mahesabu ya siku hiyo. Kwa haraka haraka nilisikia pale, kila mmoja alimkabidhi jamaa kama Laki Nane za Kitanzania. Moyoni nikasema duh jamaa anatengeneza hela. Laki Nane kila mmoja, Je Jamaa ana vijana wangapi ambao kwa Siku kila mmoja anamletea Laki Nane?

Baada ya mahesabu yao, jamaa aliwapatia tena mzigo mwengine wa kuuza siku inayofuata yaani asubuhi yake. Kisha jamaa akaniambia "Sasa Homeboy utafatana na hawa jamaa utakwenda kuishi wanapoishi wao"

Basi pale nikaamka chap, Nikatoka pale Ghetto na wale jamaa wawili. Hao mtaa kwa Mtaa na Begi langu Mgongoni. Hiyo ni Kama saa Tisa au Kumi hivi usiku. Uchovu wote umekata. Natembea na jamaa ambao najua kabisa kwenye Mabegi yao kuna Dawa za Kulevya kibao.

Yan Mwili wangu ni kama vile ulichanganyikiwa kiasi, kutokana na uchovu wa safari, Mambo ya Dawa za Kulevya na Macho nayo yalikuwa yanashangaa tu uzuri wa ile Mitaa. Mitaa mizuri sana. Basi ilikuwa shida tu. Mchanganyiko wa Hofu na Furaha kwa pamoja.

Hao Hao mpaka kama mtaa wa Saba huko. Tulisimama mbele ya Ghorofa kubwa kama Kama Ghorofa 12 hivi. Pale getini mmoja wao alitoa Kadi ya kufungulia Mlango kisha Mlango ulifunguka wenyewe. Hao mpaka ndani, Tulipanda kwenye Lift mpaka Ghorofa ya 8 au 9 hivi. Walifungua Mlango tukaingia ndani. Kilikuwa chumba kimoja kikubwa, Chini walilaza magodoro kama manne hivi. Kulikuwa na Sebure, Choo na Jiko. Jamaa wakanikaribisha pale, tukapanda kwenye Magodoro tukalala. Kwa jinsi chumba kilivyokuwa nilihisi hawa jamaa humu ndani hawana muda wa kupika, vyombo vilikuwa shagalabagala, Kilikuwa ni chumba cha wao kulala tu.

Basi haikuchukua muda jamaa wengine kama Watatu wakaingia ndani. Ndo walikuwa wametoka kwenye mizunguko yao. Tukasalimiana kidogo kisha wote tukalala.

Baadae nilikuja kuelewa kuwa hawa jamaa wote wanafanya kazi ya kuuza na kusambaza Dawa za Kulevya za yule jamaa wa kwanza niliyekuta ametandaza Dawa Kitandani. Wote ni wabongo. Yule Jamaa Bosi wao, tumpe Jina Y, anawatumia nauli hawa Vijana huku Bongo halafu anakwenda kuwafanyisha hizo Kazi. Wengine ni Rafiki zake, Wengine ni ndugu zake. Wakifika hapo South ndo kama ivo anawapangia jamaa chumba na kuwalipia kodi na mambo mengine. Kwa hiyo hiki nacho ni chumba cha yule jamaa Y. Niliwaza kama hawa jamaa wote humu ndani kila mmoja anapewa mzigo wa Laki nane akauze kwa Siku, Jamaa Y atakuwa na pesa kiasi gani? Kwa hiyo Mimi kujileta mwenyewe kwenye huu mtandao wake jamaa alifurahi sana kuwa amepata mtu wa kumuuzia Dawa zake bila shida. Yaan Mbuzi Kafia kwa Muuza Bucha.
Mkuu,
Mbona uliacha kupangilia kama mwanzo ili iwe rahisi kufuatilia somo linalofuata?
 
SEHEMU YA TISA

Kwa ambao hawajafika South Afrika, Umbali kutoka Pretoria mpaka Joberg ni Kama Dakika 45 tu, Lakini Umbali kutoka Pretoria mpaka Capetown ni Masaa 24. Ni Mbali ndo mana Ahamad na Dada yake walitumia ndege.

Sikukaa sana pale kwa Vailet, Vailet aliniambia twende Mitaa wanayokaa Wabongo nikutafutie sehemu ya kuishi.

Kumbuka mpaka nafika hapo Pretoria nimesafiri siku 4, nimechoka sana. Sijawai kusafiri Umbali mrefu hivyo. Halafu mpaka muda huo nipo barabarani nazurura tu na Begi langu mgongoni.

Wakuu hapa ilipofika story yetu, kutokana na Harakati za Maisha na Biashara ambazo nilikuta watu wanafanya ambazo nitazieleza huko mbele, naomba sitotaja watu majina yao ya ukweli.Tukafika mpaka Mitaa fulani kuna Saloon nyingi, Vailet akamuita jamaa mmoja tumpe jina X, Nakumbuka akamwambia "X huyu jamaa ndo ameshuka hapa muda huu, naomba mtafutie sehemu ya kulala" alisema hivyo, wakapiga story kidogo halafu Vailet akasepa. Nikawa chini ya Mikono ya mtu mwengine.

Basi pale X akaanza wenyewe wanasema "Kunichukua Maelezo". Akaanza kuniuliza Dar natokea sehemu gan na maswali mengine mengi. Nikamjibu yote. Nilivyotaja sehemu niliyotokea hapa Dar kuwa ni Temeke, X akasema kuna watu kutoka Temeke kibao wako hapa. Ngoja nimpigie simu Jamaa mmoja wa Temeke akufate tena ndo utaishi kwake.

Alimpigia simu huyo jamaa, Jamaa akasema atanifuata. Mpaka inafika saa mbili usiku X anafunga Saloon yake huyo Jamaa bado alikuwa hajafika. X akafunga akasepa, akaniambia "Msubiri jamaa usiwe na wasiwasi atakuja tu" Nilipigwa na Baridi kwenye nchi ya watu mpaka Saa Sita usiku jamaa bado hajafika. Kumbuka hapo nimechoka ile mbaya. Inaingia siku ya Tano bila kulala Vizuri. Nina Usingizi Kinoma.
Duuh
 
Sitasahau nilivozamia Palestina pale West Bank halafu nikasema role model wangu ni Benjamin Netanyau.
 
Back
Top Bottom