Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Hapa niko class nakula hii course. Ukimaliza kuhadithia nisha graduate... Mtoa mada wewe ni mkweli nimeunganisha dot sana nimeona ni ukweli mtupu. Kilichobaki ni kutafuta jitu nilitapeli nipate 1.5m na mimi niingie uko.... Mpaka kieleweke. Uzuri mimi nina washkaji wa mtaani wananitambia tu na mapicha yao Facebook. Naenda kule buzaman nakuwa shoeshine muuza ngada.
 
Kiukweli sina ushuhuda wowote wa msingi, zaidi nilivyosoma stori ya mtoto wa Makonda nami nikakumbuka tu. Ni kawaida mtu akizungumzia kitu unachoweza kurelate.

Sina stori maana nilienda kutembea/kupumzika, hivyo kazi ni kula kulala na kuzurura, Sina cha msingi cha kuhadithia mkuu.

Ulivaa pajama y’a rangi gani
 
Interesting [emoji91][emoji91][emoji91][emoji848]
 
Kuna watu wananogewa na road trips. Nina kaka yangu yuko SA hela kwake sio tatizo ila kama mara nne za mwisho anakuja na Hilux flani hivi tangu SA mpaka bongo. Hiyo hela si angepanda ndege, maana kuna services za gari anafanya uhakika na hakai mwaka bila kuja.
Achana na kitu inaitwa road trip kibongo bongo dar to arsha kama mko masela mnaweza kaa hapo barabarani mwezi mnaizunguka hii tz
 
SEHEMU YA SABA

Tulifika pale CHIRUNDU nikiwa makini sana yasije yale ya Tunduma yakajirudia. Nilikuwa naogopa sana kutumia pesa nyingi kwa sababu nilikua sijui niendapo.

Kuna swali kuna mdau ameniuliza naomba nilitolee ufafanuzi, ameniuliza kama Bongo nilikuwa sina ajira nilipata wapi hiyo pesa Milioni Moja ya kuweka Akiba Banki. Ni hivi hapo Kabla kuna Ofisi nilikuwa nafanyia Kazi, kuna wafanyakazi tulipunguzwa ndipo nikaanza kufatilia mafao yangu pale GEPF. Mafao yangu hayakuwa makubwa sana ndo nilitumia kwenye hii Safari.

Sasa tuendelee, Pale Chirundu nilipanga foleni hadi kwa Afisa Uhamiaji, Swali langu kichwani likiwa moja tu, Je niweke hela kidogo katikati ya Passport kama nilivyofanya Tunduma? Uzuri hapa hapakuwa na Vishoka wengi kama Tunduma. Yule Dada Matilda ambae ni Abiria mwenzangu tulishaanza kuzoeana kidogo, kumbuka yeye alikuwa ni mzoefu wa hii njia, alinifuata akaniambia mdogo angu sio kila sehemu unakimbilia kuweka hela, soma kwanza upepo. Ukiwa na mazoea ya kuweka hela kila boda utaishiwa utafika South bila hela. Nikamwambia basi Dada tangulia, Mimi nitapanga foleni nyuma yako. Akasema sawa.

Tulifanikiwa kugongewa Mihuri bila kutoa pesa Ila kwa tabu sana maana maswali yalikuwa mengi, Mara kuna karatasi walinipa nijaze, niandike taarifa zangu, Kama Passport Namba, Mahali ninapokwenda, Namba za Bus nililopanda na maelezo mengine. Utaratibu huu wa kupewa karatasi tulipewa wengi. Lakini mwisho wa siku tulikomaa hatukutoa hela.

Tulifanikiwa kuingia nchi ya Zimbabwe mpaka Harare.Tulifika Harare kwenye kama saa kumi na moja jioni. Pale Harare ilikuwa ni stand ndogo, sio kubwa kama Ubungo lakini ilikuwa na Mabus mazuri sana. Tulikuta kuna wapiga debe kibao wa Mabus hayo ambao ni Wabongo, kwa hiyo tulivyoshuka tu kwenye Bus walitukimbilia na kutupa Msaada wa kupata Bus la South.

Pale tulitawanyika kwenye mabasi mbalimbali, kwenye bus nililopanda Mimi tulikuwa wabongo 4 tu, Nilikuwa Mimi , Ahamad, Matlida na Jamaa mwengine. Ndani ya Bus wengi walikuwa ni abiria wa pale Zimbabwe na Zambia. Ndani ya Bus Kiswahili ndo kilipotea kabisa. Hata Matangazo ya ndani ya Bus yalitolewa kwa lugha zao za pale Zimbabwe.

Nakumbuka tukiwa tumeanza safari, tunatoka pale Stand, niliwaona wale madogo wakiingia mtaani utafikiri ni wenyeji vile. Ukweli nilijifunza kitu kutoka kwa wale madogo, walikuwa majasiri mno.

Hatimae usiku wa saa Tisa, tulifika Boda ya Mwisho ya BeitBridge, Nadhan ndio Boda kubwa ukanda wetu wa chini mwa jangwa la Sahara. Palikuwa busy balaa, watu kibao.

Nilivyoona watu wengi vile, kitu cha kwanza nilichojisemea moyoni ni kwamba "Muda huu Mimi huwa nimelala kumbe kuna sehemu nyengine hapa duniani muda huu watu wapo busy hivi"

Kulikuwa na watu mataifa mbalimbal, Weupe na Weusi. Sasa wabongo tukawa kama ndugu tayari. Ukweli moyoni nilikuwa siwaamini sana hawa jamaa maana nilishawai kusikia South Afrika, Wabongo kwa wabongo ndo hatari kuliko hata wageni. Lakini nikasema No sweti maji nishayavulia nguo. Kama wakitaka kuniibia au kunifanya jambo baya poa tu. Hata Matlida mara nyingi alikuwa ananihimiza dogo usiwaamini sana wabongo watakuliza. Basi muda wote nilikuwa makini.

Tulipanga foleni kwenye Ofisi za Uhamiaji, yule jamaa mwengine alisema tukitaka South Africa tupewe siku nyingi za kuishi humo, hapo ni Lazima katikati ya Passport tuweke hela.

Alisema tusipoweka hela basi tutapewa siku chache sana. Huyo jamaa, Ahamad na Matlida wakawa wanabishana pale, Matlida anasema tusiweke, yule jamaa anasema lazima tuweke la sivyo tutapewa siku chache mno.

Matlida anasema hata tukipewa siku chache sio mbaya maana lengo tufike kwanza, tukishafika hayo mengine tutajua huko ndani namna ya kuongezewa muda.

Mwisho wa mabishano tukakubaliana tuweke pesa, ila kwenye foleni yule jamaa ndo asimame mbele yetu, yaani awe wa kwanza. Mimi nilisimama nyuma yake. Matlida akasimama nyuma yangu, Ahamad akasimama nyuma ya Matlida. Foleni yetu ilivyofika Kaunta. Mara nikashangaa yule Askari wa Uhamiaji wa pale Kaunta anamuita Askari mwenzie aje kumkamata yule jamaa etu kwa kosa la kutoa rushwa. Ukweli nilitetemeka kishenzi, fasta sana nilitoa pesa niliyoiweka katikati ya Passport yangu kisha nikasogea pale Kaunta. Yule Mzungu Mkaburu akawa ananiangalia tu.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Ungedakwa
 
Keagan mbna kimya au ushadakwa na kete!!

Sema ma video queen wengi miaka ya 2007 had 2014
Wamesambaza Sana drug hum duniani;


Hawa wa siku hizi wanauza tu mwili
Wanaishia kuwa addicted na ngono;

Cjui Kati yao Nan Bora???
 
SEHEMU YA KUMI

Kwa Kifupi ndo nikawa South Africa nimeshaingia ivo bila ya kuwa na Ndugu wala Rafiki wakunipokea. Mambo ya kusubiria kuwa na Ndugu au Rafiki yangenichelewesha sana.

Basi Nilikaa pale nje mpaka saa saba usiku ndo Jamaa akaja kunichukua. Alisema kuna sehemu alikuwepo kuna Harakati alikuwa anafanya. Jamaa akanipokea Begi hao mdogo mdogo mpaka KFC tukapata chakula kisha tukaenda Magetoni kwake. Ilikuwa ni ghorofa. Yeye alikuwa amepanga Ghorofa kama ya tatu hivi. Tulifika na kuingia ndani kwake. Kilikuwa ni chumba kimoja, sebure kubwa, Choo na Jiko. TV Kubwa, Makochi ya Kisasa. Kwa kifupi jamaa alikuwa anaishi vizuri.

Tukawa tunapiga piga story pale, Jamaa alikuwa ananichukua Maelezo ili awe na uhakika kama kweli Mimi ni Mtanzania na Kama kweli natokea Temeke. Wabongo wengi wanafanya hivyo ili kujiridhisha kama kweli wewe ni Mbongo wasije kupokea Mburundi, Mkenya au Mkongoman. Baada ya story kidogo jamaa akaniambia panda kitandani upumzike.

Hapa nitasema kama ilivyokuwa, Juu ya Kile Kitandani jamaa alikuwa ametandaza Dawa za Kulevya Kibao. Ilikuwa ndo Mara yangu ya kwanza kuziona dawa za kulevya vile. Zilikuwa nyingi sana halafu Jamaa haogopi wala nini. Alikuwa anazifunga funga. Nikahisi pengine jamaa alichelewa kuja kunifata labda alikuwa busy kufunga hizi Kete zake. Yan jamaa anafunga bila woga, tena mbele ya Mgeni. Nikajiuliza jamaa anajiamini nini.

Mimi sasa, Usingizi wote wa Safari ulikata. Maana nakumbuka nililala pembeni ya hicho kitanda halafu pembeni yangu ndo kulikuwa na hizo Dawa. Huku tunaendelea kupiga story.

Katika Maisha yangu, Dawa za Kulevya nilikuwa nazisikia tu kwenye Vyombo vya Habari na kuwaona Mateja Mtaani. Lakini ile nafika tu South Afrika ndo kama hivi nilikutana nazo tena ile ile siku ya kwanza. Mara pale ghetto tukasikia Hodi, Kisha Jamaa wawili wakaingia ndani. Nao ni wabongo. Tukasalimiana pale kisha wakaendelea na Mishe zao. Wakafungua mabegi yao na kuanza kutoa Kete zao za Dawa za Kulevya na Pesa, ni kama vile walikuwa wanamkabidhi jamaa mahesabu ya siku hiyo. Kwa haraka haraka nilisikia pale, kila mmoja alimkabidhi jamaa kama Laki Nane za Kitanzania. Moyoni nikasema duh jamaa anatengeneza hela. Laki Nane kila mmoja, Je Jamaa ana vijana wangapi ambao kwa Siku kila mmoja anamletea Laki Nane?

Baada ya mahesabu yao, jamaa aliwapatia tena mzigo mwengine wa kuuza siku inayofuata yaani asubuhi yake. Kisha jamaa akaniambia "Sasa Homeboy utafatana na hawa jamaa utakwenda kuishi wanapoishi wao"

Basi pale nikaamka chap, Nikatoka pale Ghetto na wale jamaa wawili. Hao mtaa kwa Mtaa na Begi langu Mgongoni. Hiyo ni Kama saa Tisa au Kumi hivi usiku. Uchovu wote umekata. Natembea na jamaa ambao najua kabisa kwenye Mabegi yao kuna Dawa za Kulevya kibao.

Yan Mwili wangu ni kama vile ulichanganyikiwa kiasi, kutokana na uchovu wa safari, Mambo ya Dawa za Kulevya na Macho nayo yalikuwa yanashangaa tu uzuri wa ile Mitaa. Mitaa mizuri sana. Basi ilikuwa shida tu. Mchanganyiko wa Hofu na Furaha kwa pamoja.

Hao Hao mpaka kama mtaa wa Saba huko. Tulisimama mbele ya Ghorofa kubwa kama Kama Ghorofa 12 hivi. Pale getini mmoja wao alitoa Kadi ya kufungulia Mlango kisha Mlango ulifunguka wenyewe. Hao mpaka ndani, Tulipanda kwenye Lift mpaka Ghorofa ya 8 au 9 hivi. Walifungua Mlango tukaingia ndani. Kilikuwa chumba kimoja kikubwa, Chini walilaza magodoro kama manne hivi. Kulikuwa na Sebure, Choo na Jiko. Jamaa wakanikaribisha pale, tukapanda kwenye Magodoro tukalala. Kwa jinsi chumba kilivyokuwa nilihisi hawa jamaa humu ndani hawana muda wa kupika, vyombo vilikuwa shagalabagala, Kilikuwa ni chumba cha wao kulala tu.

Basi haikuchukua muda jamaa wengine kama Watatu wakaingia ndani. Ndo walikuwa wametoka kwenye mizunguko yao. Tukasalimiana kidogo kisha wote tukalala.

Baadae nilikuja kuelewa kuwa hawa jamaa wote wanafanya kazi ya kuuza na kusambaza Dawa za Kulevya za yule jamaa wa kwanza niliyekuta ametandaza Dawa Kitandani. Wote ni wabongo. Yule Jamaa Bosi wao, tumpe Jina Y, anawatumia nauli hawa Vijana huku Bongo halafu anakwenda kuwafanyisha hizo Kazi. Wengine ni Rafiki zake, Wengine ni ndugu zake. Wakifika hapo South ndo kama ivo anawapangia jamaa chumba na kuwalipia kodi na mambo mengine. Kwa hiyo hiki nacho ni chumba cha yule jamaa Y. Niliwaza kama hawa jamaa wote humu ndani kila mmoja anapewa mzigo wa Laki nane akauze kwa Siku, Jamaa Y atakuwa na pesa kiasi gani? Kwa hiyo Mimi kujileta mwenyewe kwenye huu mtandao wake jamaa alifurahi sana kuwa amepata mtu wa kumuuzia Dawa zake bila shida. Yaan Mbuzi Kafia kwa Muuza Bucha.
[emoji16][emoji16][emoji16] [emoji119]
 
Uzi uko [emoji91][emoji91][emoji91][emoji8]sana
 
SEHEMU YA NANE

Ukweli ndugu zangu moja ya kitu nilichojifunza kwenye Safari hii sio kwamba ukifika kila boda basi unakimbilia kutoa pesa. Unatakiwa kusoma kwanza upepo wa Boda husika.

Kwenye hii boda ya BeitBridge tulikosea kwa sababu pale Kaunta kulikuwa na Mkaburu. Wazoefu wanasema ukikuta pale Kaunta amekaa Mkaburu basi usikimbilie kutoa rushwa. Sababu wanasema Mkaburu hapendi sana watu weusi, hivyo ukianza tu kutoa rushwa ndo anapata sababu ya kutokukuruhusu kuingia nchini mwao.

Basi Mimi namshukuru mungu yule Mkaburu akaniangalia kisha akanigongea mhuri. Nakumbuka alinipa Mwezi mmoja tu wa kukaa South Africa. Wenzangu walipewa Wiki mbilimbili. Jamaa zangu waliniambia Mimi nilipewa Mwezi mmoja sababu yule Mkaburu aliona Passport yangu haijawai kugongwa Mhuri wa Africa Kusini. Wao walipewa siku chache kwa sababu Passport zao zishagongwa sana Mihuri ya Afrika Kusini.

Mpaka tunarudi kwenye Bus yule Jamaa etu walikuwa bado wamemshikiria. Tuliondoka tukamuacha pale, tena hata namba za simu tulikuwa bado hatujapeana. Mpaka kunakucha tulikuwa bado tupo njiani.

Ahamad aliniambia kama sina sehemu ya kufikia basi nishuke nae Pretoria. Kwa sababu Bus kabla ya kufika Joberg linafika kwanza Pretoria. Ahamad akasema tushuke wote hapo atanitafutia sehemu ya kukaa kwa jamaa zake ambae ni wabongo. Matlida yeye alikwenda kushukia Mwisho wa Bus kule Power House Karibu na Park Station Joberg.

Mimi na Ahamad tulishuka pale Pretoria kama saa Nane mchana. Ukweli nchi ya wenzetu ni nzuri sana.

Nilikuwa natembea huku najiuliza "Kama hapa pako hivi huko Ulaya na Marekani patakuwa vipi?" Watu wanajua kujenga nchi zao.

Ahamad alikuwa na miaka kama mitano toka atoke South hivyo tulivyoshuka tu tukawa tunapita mitaa Fulani ya washkaji zake anakwenda kuwasalimia. Mimi nipo nyuma yake tu. Nakumbuka tulikwenda mpaka mitaa Fulani kuna Wazanzibar wengi wana maduka. Tukaacha hapo mabegi yetu. Mimi nilikuwa sina imani kuacha hapo Begi langu lakini kwa kuwa ATM Card yangu ilikuwa mfukoni nikasema sio mbaya, kilichokuwa kinanipa wasiwasi peke yake ni vyeti vyangu vyote vilikuwepo ndani ya Begi. Ukishaamua kujilipua inabidi uwe na roho ngumu.

Tulivyofika hapo Pretoria ndo nikajua kuwa kumbe Ahamad alikuwa anaendelea na Safari ya kwenda Capetown. Hapo alikuja kukutana na Dada yake ambae wangekwenda wote Capetown kwa ndege. Huyo Dada yake alikuwa ameolewa huko Capetown na Tajiri mmoja. Maelezo yote hayo alinipa Ahamad mwenyewe.

Tukaenda mahali kukutana na Huyo Dada yake, naye ni Mtanzania. Nakumbuka alikuja na Range Rover mpyaa, tukaingia ndani, kisha Ahamad akanitambulisha kwa Dada yake. Dada yake akasema kwa kuwa wao walikuwa wanawahi kupanda ndege basi Mimi ataniacha kwa rafiki yake.

Hao mpaka kwa huyo rafiki yake, tulivyofika kwa huyo rafiki ake, Dada yake na Ahamad akaniuliza "Unamjua huyu". Mimi nikamjibu hapana simjui. Nikawa namwangalia vizuri yule Mrembo ambae nimepelekwa kwake. Nikajiridhisha kuwa simjui.

Dada yake na Ahamad akasema "Huyu ni Vailet, yule Video Queen kwenye Wimbo wa Matonya, ule wimbo wa Vailet, huyu ndo Vailet mwenyewe"

Duh nikabaki nimeduwaa tu, demu amekuwa mrembo kinoma noma. Kumbe Alishakimbiliaga South Afrika Kitambo sana. Wakuu ukitaka kumkumbuka vizuri huyu demu unaweza kuingia YouTube, Video ya Matonya wimbo wa Vailet, ndo huyo demu mule ndani. Mimi nikaachwa pale. Ahamad na Dada yake hao wakaondoka kuchukua mabegi wakaniletea Begi langu kisha wenyewe wakasepa Capetown.
Hahahaha usijekutuambia ulijiweka hapo
 
SEHEMU YA TISA

Kwa ambao hawajafika South Afrika, Umbali kutoka Pretoria mpaka Joberg ni Kama Dakika 45 tu, Lakini Umbali kutoka Pretoria mpaka Capetown ni Masaa 24. Ni Mbali ndo mana Ahamad na Dada yake walitumia ndege.

Sikukaa sana pale kwa Vailet, Vailet aliniambia twende Mitaa wanayokaa Wabongo nikutafutie sehemu ya kuishi.

Kumbuka mpaka nafika hapo Pretoria nimesafiri siku 4, nimechoka sana. Sijawai kusafiri Umbali mrefu hivyo. Halafu mpaka muda huo nipo barabarani nazurura tu na Begi langu mgongoni.

Wakuu hapa ilipofika story yetu, kutokana na Harakati za Maisha na Biashara ambazo nilikuta watu wanafanya ambazo nitazieleza huko mbele, naomba sitotaja watu majina yao ya ukweli.Tukafika mpaka Mitaa fulani kuna Saloon nyingi, Vailet akamuita jamaa mmoja tumpe jina X, Nakumbuka akamwambia "X huyu jamaa ndo ameshuka hapa muda huu, naomba mtafutie sehemu ya kulala" alisema hivyo, wakapiga story kidogo halafu Vailet akasepa. Nikawa chini ya Mikono ya mtu mwengine.

Basi pale X akaanza wenyewe wanasema "Kunichukua Maelezo". Akaanza kuniuliza Dar natokea sehemu gan na maswali mengine mengi. Nikamjibu yote. Nilivyotaja sehemu niliyotokea hapa Dar kuwa ni Temeke, X akasema kuna watu kutoka Temeke kibao wako hapa. Ngoja nimpigie simu Jamaa mmoja wa Temeke akufate tena ndo utaishi kwake.

Alimpigia simu huyo jamaa, Jamaa akasema atanifuata. Mpaka inafika saa mbili usiku X anafunga Saloon yake huyo Jamaa bado alikuwa hajafika. X akafunga akasepa, akaniambia "Msubiri jamaa usiwe na wasiwasi atakuja tu" Nilipigwa na Baridi kwenye nchi ya watu mpaka Saa Sita usiku jamaa bado hajafika. Kumbuka hapo nimechoka ile mbaya. Inaingia siku ya Tano bila kulala Vizuri. Nina Usingizi Kinoma.
Duuuh ndo ukubwa huo
 
Back
Top Bottom