Nilienda kwa bus, kupitia njia aliyopita mtoa mada nikarudi kwa mwewe. Njia Dom-Mbeya-tunduma (Nakonde border)-Lusaka-Chirundu one stop border- Beitbridge border moya kwa moya Jozi. Nililala tunduma boda, nikalala na kukaa Lusaka wiki, nikaongoza Jozi.
Kutoka tunduma nilipanda power tools mabasi fulani ya njano, Kutoka Lusaka nilipanda basi inaitwa Joldan kama sijakosea spelling, nalikumbuka tu ni la rangi ya zambarau.
Changamoto ya safari ya barabara, ni kuombwa rushwa uhamiaji, hata mimi niliombwa tunduma na chirundu, tena aliyeniomba chirundu ni mdada, wanasema kuwa ukionekana na passport ya kijani, lazima uombwe mpunga. ( enzi hizo ni zile pass zetu za kijani) Sijui kwa sasa.