Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Ilipoishia.....

Nywele za Tsheispo zilikuwa zimeangukia mgongoni, chuchu saa sita oclock, guu sasa ndio nilichoka asee, guu nilidhani ni paja la mange kimambi, nikasema hapa keagan lazima leo nimueleze hisia zangu, baada ya kufika pale akesema mbona unaniangalia sana, nikamwambia hapana umependeza sana akacheeka huku tukiongozana kwenda restaurant .

Sasa endelea...

Tulipofika restaurant niliagiza viazi vya kukaanga na kuku Tsheispo yeye aliagiza kuku na juisi basi tulikula weee hadi pale muumini mmoja alipotufata kua tunaitwa na pastor! Tuliondoka na kurudi kanisani nilifurahi sana maana Tsheispo ndie alilipa bili hivo akiba yangu ilibaki salama.

Tulirudi kanisani pastor alisema tujiandae twende tour kwenye national park moja inaitwa Sehlabathebe National Park. Basi tujiandaa na kupanda coaster ambayo ilitumia masaa matatu kufika. Tulienjoy hadi jioni na kurudi pale kanisani tulilala mapema ili asubuhi tuanze safari ya kurudi south.

Sasa tulipofika pale boda ya kuingia south ndo kilitokea kizazaa. Askari wa migration walikua wakali kama wamekula pilipili za mto ruvu hawakutaka kucheka na kima kabisa siku hiyo ndo nilijuta kuwajua makaburu. Waligoma kua siwezi kuingia south maana permit yangu ilikua imeshaisha muda dah! Nilipagawa sana sikujua nifanyeje. Wale wenzangu waliruhusiwa kuondoka, waliondoka na kuniacha pale peke yangu tena chini ya ulinzi mkali kama wa mwendazake! aisee nililia sana nilipojua sitamkula Tsheispo baadae wale askari walinipeleka mahabusu.

Kesho yake nilitakiwa kupelekwa mahakamani lakini huwezi amini kolichotokea askari mmoja alikuja na kuniita kwa nguvu KEEGAN PAULO niliitika kwa uoga naam afande! Yule kaburu alinikata kibao akasema we nyani nikikuita itika Sir nipo Sir. Hilo neno Sir lilimaanisha bwana mkubwa. Basi bwana niliitika kama alivoniekeza. Alitabasamu na kusema njo unifuate nilitolewa nje wakati tunatoka nje nilishangaa kusikia mtu ananiita jina langu kabisa la Keegan Bashite nikazuga kama sijasikia. Mara akanigusa bega na kuniita kwa nguvu we Keegan amka.

Nilishituka sana kumbe nilikua naota. Aisee kumbe aliekua akiita ni Dada wa kazi! alimua akiniamsha nikale. Aisee ndoto za mchana mbaya nilikua nshafika south kimasikhara! Kumbe toka episode ya kwanza nilikua naota huku nakoroma kama jenereta bovu!! Lakini tuache utani Kanya alikua na tako balaa. Ngoja ninywe kiroba nilale nimechoka type. Mwe!!!!..

Mwisho
 
Sio Msimbati ni Kilambo..

Kilambo na Msimbati ni sehemu mbili tofauti..
Nimesema njia ya maji,unavuka kwa kupitia baharini.Nisome vizuri.
Hapo pana mashua/vyombo vya kutweka vya wamakua.
Kilambo ni njia ya barabara kupitia Namuiranga, wote watakutana Quionga au Palma.
 
Wakuu hii story pigieni mstari ndio imeishia hapa, alishawahi kuisimulia na haikuwa na wachangiaji lakini hakuimaliza. Kwaiyo fanyeni mambo mengine tu...

 
Aiseee balaa hii mbna stori ishakuwa kama yakutungwa sasa
 
Aiseee balaa hii mbna stori ishakuwa kama yakutungwa sasa

Uzi maalumu wa Harakati za kutafuta maisha nje ya nchi na changamoto ulizokutana nazo
 
Huyu muha kaamua kujitungia story hapa akivhanganya na story yake ya kweli..Yani hapo mengine ya kweli mengine ni urongo nadhani
 

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Nikiwaambia usifunge kama huna stamina mnakua wabishi matokeo yake ndo huu uterereee
 
Nadhani kila mtu anakushangaa kwa hii coment yako mkuu. Hebu soma vizuri jina la mleta hii thread.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Huyu mwalimu wamempa zamu wakati wa mfungo mumsamehe tu๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 

sikujui hunijui ila kila nkisoma ulichoandika naona una uhusiano moja kwa moja na ccm, yan wewe ni ccm damu damu na hujasoma shule mkuu kuwa mpole na urudi shule ukasome AEIOU na zile mamemimomu zitakusaidia mbelen
 
Muulize yeye ameshawahi kuandika story yoyote hapa jukwaani??
 
Mtoto wa muheshimiwa Keagen Paul

Lengo siyo kuona mapungufu wala kukwazana lkn kwa kuwa tunapaswa kujifunza sio mbaya tukaambiana ukweli wote

Ilikuwaje ukapita mpakani kwenda Lethoso wakati passport yako ilionyesha umezidisha muda wa kukaa SA ( sawa uliweka Rand 300) hauoni kwamba hapo ni issue ya mfumo na nafikiri kuna database ya uhamiaji ktk nchi husika kwa wageni wanao ingia na kutoka ( system) pia si inatakiwa kujazwa taarifa ktk hiyo database au ni suala la kugonga muhuri tu ktk passport bila taarifa zako kuwa stored ktk database yao? Hao ma afisa wa uhamiaji wanawezaje ku โ€˜manipulateโ€™ na ku u โ€˜fixโ€™ huo mfumo kwa kiwango hicho

Ingeleta maana ukisema ulitumia labda kama zile karatasi za zamani kama hauna passport (sijui mpaka miaka hii) kwa mtu kuingia kama EA unapata mpakani mfano Namanga unalipa na hauonyeshi passport na kwa kigezo wewe ni Raia wa kutoka ukanda/ nchi hizo na hapo hata sijui ulirudi vipi tena na ukaweza kuingia SA kutoka Lethoso

Sijatembea nchi za bara letu hili pendwa na labda kuna kiwango kikubwa cha rushwa mpaka tuna zi โ€˜fix systemโ€™ ila kwa nchi chache nilizoenda nje ya Afrika hicho kitu hakiwezekani eti umezidisha muda wa kukaa wa nchi husika afu unaenda dirisha la uhamiaji na sijui uweke $ mambo yaishe ni ngumu sana hiyo

Najua hamu ya kusimuliwa kwa wengi wetu ilivyo kubwa lkn hapa tunatakiwa kupata maelezo kidogo ili tujifunze kutoka kwa Muheshimiwa kama ataona inampendeza na ni hiari tu kutoka kwake

All in all hongera sana kwa uzoefu unaotupa ktk simulizi hii
 
Tena SA wako very strict kwenye mambo ya kuoverstay. Kuna siku natoka joburg kuja dar kwa ndege... pale or tambo airport kuna mbongo mwingine na yeye alikua anakuja dar kwenye hiyo ndege... kufika immigration kumbe ameoverstay.. aliingia SA kwa barabara kupitia mpaka wa zimbabwe pale beitbridge..walimpa siku 90 ye kakaa mwaka. Walibaki naye wala hawakumruhusu kusafiri pamoja na kwamba alikua anarudi nyumbani.. sijui alichomokaje kwenye huo msala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ