Behaviourist
JF-Expert Member
- Apr 8, 2016
- 39,926
- 95,626
Huu mziki wao wa kupiga filimbi unaitwaje?😂😂😂Bata za South hizi. Hapa ukiingia lazima stress zote ziishe.View attachment 1756648
Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu mziki wao wa kupiga filimbi unaitwaje?😂😂😂Bata za South hizi. Hapa ukiingia lazima stress zote ziishe.View attachment 1756648
Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
Sasa utatumis vipi na hauondoki JF?Wanajf kwaherini jamani kesho naondoka Tanzania, ntawamiss....
Mkuu usihangaike na huyo haijui barabara mimi nimekuelewa unaweza kwenda hadi Uganda kwa hiyo balabalaMkuu mbona unanishambulia, Bwanga ukiacha kuelekea chato, unaenda katoro Buseresere/ katoro geita, sengerema, mwanza, mwanza unaweza kuamua uende Musoma then upite mbugani serengeti ili utokee geneva of africa, au urudi utokee Bariadi/simiyu uingie Arusha kupitia loriondo. Bado unaswali? Kule juu nimetaja njia ya Runzewe lakini unaweza kukatisha njia ya vumbi ushirombo kutokea katoro ukaendelea na safari zako
Kumekucha 🤣 😵😵😵Wewe ni nguruwe gaidi kizazi cha fisi, ukoo Ngiri, familia ya fungo wala dubu kabare mkubwa wewe
Hahahaha tunajilipua ila ndo kivingine wanawake wengi wamefika huko kwa kutumia (mahusiano), hivyo njia yao huwa rahisi kidogo, tumeumbwa kwa udongo laini Sana kuhimili hiyo mikiki ndugu yangu
Mkuu usihangaike na huyo haijui barabara mimi nimekuelewa unaweza kwenda hadi Uganda kwa hiyo balabala
Hahahaahahaha nice bait, tunasibiri simulizi tukimalizi hili
Mkuu wewe umepita hiyo barabara tena kile kipindi ujenzi wa Lami ulipokuwa ukiendelea achana na huyo anayekuita muongoKabisa Mkuu ukipitia bwanga, unaamua uue kona utokee biharamulo au unyooshe hadi muganza, magarini unakula hadi kibaoni unakatisha kuelekea runazi hadi muleba then Bukoba unaitafuta mutukula, uende ukale lukaay au masaka au utoe kidebe karibu pale kyotera, naona kanishambulia mkongwe nimeanza kupita kilimasera kuja mnazi mmoja enzi hizo ni vumbi pale kilimanj ukikuta imenyesha hakuna cha chepe wala nini unapaki unatoa jiko lako unaanza kupika ukishiba unalala, acha Boss
Msela wa ngada huyu hapa tena!😁😁😂😂SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Kwa hiyo Mimi kujileta mwenyewe kwenye huu mtandao wao, jamaa alifurahi sana kuwa amepata mtu wa kumuuzia Dawa zake bila shida.
Siku ile ni kama hatukulala kabisa, Wale jamaa wameshazoea kuchelewa kulala na kuwahi kuamka. Tulilala Saa Kumi na Kuamka Saa Moja. Yan Saa moja asubuhi tukawa macho. Jamaa wakaanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kuzungusha biashara yao hiyo. Na Mimi wakaniambia nijiandae ili tutoke wote wataniacha kwa yule Bosi wao, Jamaa Y. Nadhan kwa kuwa nilikuwa mgeni walishindwa kuniacha peke angu pale gheto. Walikuwa kama hawaniamini hivi.
Tukajiandaa tukatoka wote, Niliacha pale Gheto Begi langu ambalo lina vyeti vyangu ndani. Ukweli muda wote nilikuwa nawaza vile vyeti tu. Hao Hao mpaka kwa yule jamaa Y, wakaniacha pale, wao hawakuchukua muda wakasepa. Pale ghetto tukabaki Mimi na Jamaa Y. Jamaa Y akatengeneza chai pale tukanywa, tulivyomaliza kunywa tukashuka mpaka chini kuna mtaa Fulani tukaelekea huko.
Wakati tunatembea ndo nilipata muda mzuri wa kuuona mjini wao. Ebana nchi ya wenzetu nzuri jamani. Warembo kama wote, wote wamejazia hatari. Nikajisema moyoni ndo mana wabongo wengi wakija huku hawarudi Bongo mpaka baada ya miaka mingi. Ukweli kwa wenzetu mademu wanajua kuvaa, kila stail yan. Warembo wanavaa na kupendeza haswa. Nilikuwa natoa macho mpaka najishtukia.
Mimi na Jamaa Y tulifika mpaka sehemu Fulani karibu na Barabara tukasimama hapo. Tulikuta majamaa wengine wengi kama Tisa hivi nao wamesimama. Pale nilikuja kugundua kuwa ni Kijiwe chao cha kuuzia dawa za Kulevya. Jamaa wanakuwa na Kete ndogo ndogo wanaficha mdomoni, mteja akifika tu, wanatoa mdomoni wanampatia. Jamaa wamevaa Kibrazameni huwezi kuzania kama wanapiga ishu hizo hapo.
Wateja wao wengi waliofika pale walifika na Magari yao. Unakuta gari inapaki pale halafu hawa jamaa mmoja wao anazama ndani ya hiyo Gari anauza mzigo.
Walikuwa wanaficha Dawa zao ndani ya Mdomo ili kama itatokea wamekamatwa na Askari inakuwa rahisi wao kuzimeza na kupoteza ushahidi. Ukweli Mimi sikuwa Comfortable kabisa kusimama nao pale. Unajua hapa Bongo ishu ya Madawa ni kubwa sana lakini sio kule. Kule wanaona kitu cha kawaida tu. Tena wanakushangaa wewe unayewashangaa.
Hawa jamaa wa Kibongo karibia wote walionekana kuwa na maisha mazuri. Wao pia walikuwa wamepaki magari yao pembeni ya Barabara. Kila mmoja ukimuuliza pale atakwambia ana miaka kibao hajarudi Bongo. Hata wanunuzi wao pale walikuwa wanafika washua kweli kweli kuja kununua mizigo.
Maelezo yote hayo alikuwa ananipa kidogo kidogo jamaa Y, Ni Kama vile alikuwa ananifundisha Kazi kiaina. Ukweli kwa siku ile ya kwanza Wabongo wengi niliokutana nao walikuwa wanapiga hizi ishu, wachache sana walikuwa wanafanya Kazi kwenye Masaloon na maeneo mengine. Hata hawa ambao walikuwa wanafanya kwenye Masaloon, nyuma ya pazia walifanya dili hizi. Hata ambao walikuwa na Maduka makubwa nyuma ya biashara zao, Jamaa Y aliniambia nao wanauza unga.
Jamaa Y taratibu aliendelea kunifundisha Kazi na kunionesha Mitaa mbalimbali. Nilimweleza jamaa kuwa Mimi natamani kufanya michogo ya halali. Nakumbuka jamaa alinikatisha sana moyo. Kwamba Kazi za Halali ni ngumu sana kupata. Jamaa aliniuliza "Una Kibali cha kufanyia Kazi? (Work Permit)" Nikamjibu Hapana sina. Akasema kama ni hivyo itakuwa ngumu sana kupata mchongo wa halali.
Kwa asiyefahamu, kwa mujibu wa sheria mtu inabidi uombe Kibali cha Kazi kabla ya kuanza Safari. Yan unaombea ukiwa Bongo. Unakwenda pale Ubalozi wa South Africa uko pale Posta unaomba kabisa Kibali kabla ya kuanza safari. Ukifika pale utapewa taratibu zote za kuomba Kibali. Changamoto sio kuomba Kibali, Changamoto ni hayo Masharti yao.
Kwa hiyo Jamaa Y aliniambia kama sina Kibali nisahau kupata Mchongo wa Halali. Aisee nilichoka. Mchongo pekee uliopo mbele yangu ni wa Dawa za Kulevya.
Ngoja tuone story itaisha vipi ...Mkuu kuwa nasubira 😂😂😂Oi.Niache kazi nije Southy nini?Niko 30s naona nawaste time tu.
Hii kibongo bongo ingetokea lugalo ungerushwa kichura chura mpaka basiMkeka wa nguvu na baadhi ya sehemu wamejenga airstrips!na salute kwa kambi ile ya jeshi la Botswana,they helped me big time kuna siku usiku nilipata pacha karibu kabisa na geti lao Panamatenga barracks i salute you
Kwa mbaali nakumbuka mabasi ya Scandinavia wao mkikaribia boarder as horohoro, mamanga, tunduma au isibania walikuwa wanatangaza ndani ya basi kabla ya kufika nini ufanye kuepusha dhahama zozote.SEHEMU YA TANO
Nikaondoka pale kurudi kwenye Bus ili nimuulize Dereva au Konda, Wale Vishoka wapo tu nyuma yangu. Dereva na Konda nao walikataa kutoa ushirikiano kwa madai ya kwamba nimalizane kwanza na wale Vishoka.
Baada ya wale Vishoka kushuka ndani ya Bus niliwauliza Dereva na Konda kwa nini walikataa kunisaidia. Wakaniambia kuwa wao ile njia wanapita kila siku na hao Vishoka wapo hapo Boda ya Tunduma miaka na miaka. Kwa hiyo kama wangenisaidia basi Bus lao lingefanya kazi katika Boda hiyo kwa tabu sana pengine wangeweza kutobolewa matairi kila watakapokuwa wanapita hapo. Kwa kweli niliwaelewa.
Mkuu wewe umepita hiyo barabara tena kile kipindi ujenzi wa Lami ulipokuwa ukiendelea achana na mbwiga anayekuita muongo
Stori za hustle ,stori za kujilipua.. stori za kutoa hamasa ya kufikia mafanikio.. huwa zinanoga mkuuStori za South huwa zinanoga sijui kwanini
Wapo huko South africa,Oman,Dubai,Qatar Uk,Hahahaha tunajilipua ila ndo kivingine wanawake wengi wamefika huko kwa kutumia (mahusiano), hivyo njia yao huwa rahisi kidogo, tumeumbwa kwa udongo laini Sana kuhimili hiyo mikiki ndugu yangu
Honestly siwezi kurisk maisha yangu hivyo, (labda maisha hayajanichapa sawasawa, ama mazingira niliyokulia no)
Wewe jilipue ili ututoe kimasomaso🤩🤩