Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Itabidi utoke nje ya tz Sasa, km huko south nk ila nasikia usalama Ni mdogo Sana

Nasubiri corona ipoe nami nikasafishe nyota sio kwa gundu hili, ila yangu siwezi kuiweka Kama kujilipua Ni safari ya kawaida tu japo Ni ya kwenda kuanza maisha mapya kwenye dunia za watu huko
Nenda aise...mie dec lazima kieleweke..niende kutoa gundu .Mungu anisaidie niweze..all the best
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Niliishi pale kwa jamaa kama Wiki mbili hivi, Story zao zote ni kuhusu Dawa tu. Aisee nilichoka. Nikasema hapa lazima nitoke. Sijajilipua kuja South kuja kuuza Dawa, Nikasema hata nyumbani wakisikia nimekamatwa kwa kesi ya dawa watanishangaa sana. Kama nimeweza kutoka Bongo mpaka South, Sasa nishindwe nini kutoka hapa kwa Washkaji kwenda sehemu nyengine.

Basi taratibu nilipanga kutafuta Marafiki wengine ambao sio wabongo. Niliona labda nikibadilisha watu nitasikia story nyengine tofauti na Madawa. Nikawa muda mwingi najichanganya na watu wengine. Ukiwa South halafu ukianza kufanya mambo tofauti na wengine lazima wabongo wenzio watachukia. Lakini nilijilipua tena kwa Mara ya pili. Liwalo na Liwe, wakichukia poa tu.

Niseme ukweli wakati natoka Bongo, Kichwani nilikuwa na Mipango miwili ya namna ya kupata Mchongo kwa urahisi. Mpango wa kwanza lilikuwa endapo nitachelewa kupata Mchongo basi niende nikajisalimishe kwenye Kanisa lolote. Ukweli nilipanga kwamba endapo nitakosa watu sahihi wa kunisaidia kufikia malengo yangu basi niwe mtu wa kwenda sana Kanisani ili kupata watu sahihi huko. Nilipanga kujisogeza kwa washua wale wa Makanisani. Nilijua washua wengi wenye Biashara zao Halali au Taasisi zao nitawapata huko.

Mpango wangu wa Pili ilikuwa kama nitachelewa kupata Mchongo basi nitafute Mrembo mwenye Kazi yake, nimpe mapenzi kama yote mpaka anipende na kunisaidia kupata Mchongo. Mjumbe hauwawi ndo yalikuwa mawazo yangu.

Nikaanza na hili la Kwanza la kutafuta Kanisa la Washua. Kumbuka Safari hii nilifanya Karibia na Sherehe za X-Mass na Mwaka Mpya, Nilifanya Karibia tarehe hizo Makusudi. Nilijua kwenye Mikesha ya Kanisani, Mkesha wa X-Mass na Mwaka Mpya lazima nitapata mtu wa kunisaidia. Basi tarehe zikasogea mpaka X-Mass ikafika. Niliwaaga wale jamaa zangu kuwa naenda kwenye Mkesha. Jamaa walinishangaa sana kwa sababu wao hawanaga mambo hayo. Tena siku niliyowaambia kuwa nakwenda kwenye Mkesha tulikuwa tumetoka wote kutembea Mitaa ya Midrand Gauteng. Midrand ipo Katikati ya Pretoria na Joberg. Ni kama dakika 20 kutoka Pretoria. Kuna Umbali kidogo sema wenzetu kwa kuwa Barabara zao nzuri ndo unatumia dakika hizi 20, Ingekuwa hapa kwetu ni umbali wa Kama kutoka Tegeta mpaka Magomeni.

Tukiwa huko Midrand ndo niliwaambia hivyo, Wakati wakuondoka wenyewe wakaondoka Mimi wakaniacha pale Midrand. Nikaanza kuzurura zangu Mitaani nauliza watu wapi nitapata Kanisa kubwa. Nilikuwa natafuta Kanisa ambalo ukiliona tu kwa nje unajua hili ni Kanisa la Washua. Sikutaka haya Makanisa Madogo Madogo.

Nilifanya yote haya ili kujiepusha na Biashara ya Dawa, ilibidi niangaike sana pale. Unajua Wabongo wengi wanajikuta wakiingia kwenye Biashara za Dawa kwa Mtindo kama huu, Yan ukifika ukakutana na Wabongo wenzio hawakupi nafasi ya kujipambania zaidi. Sasa kama wewe ni kichwa panzi basi unaishia kwenye biashara hiyo.

Mimi nilisema nitapambana mpaka dakika ya mwisho, swala la Kibali cha Kazi nitajua mbele kwa Mbele.

Basi nikafika mpaka pale Kanisani. Kuliona tu kwa nje nikajisemea hili ndo nilikuwa nalitafuta. Parking ilikuwa na Gari za Kifahari Kibao. Nikauliza Muda wa kuanza Ibada ya Mkesha wakaniambia kuwa ni saa moja usiku watu ndo wanaanza kuingia Kanisani. Washua Kibao walikuwa wamewahi pale, wamesimama kwa nje wakipiga story zao. Mimi nikasoma mazingira kisha nikatoka, nikazunguka zunguka pale Mitaani mpaka saa moja jioni ilivyofika nikarudi tena. Nikatimba zangu ndani.

Kama ilivyokawaida ya Makanisa mengi, mtu ukifika kwa Mara ya kwanza inabidi ujitambulishe. Tulisimama pale Kanisani kama wageni 50 hivi ndo ilikuwa Mara etu ya kwanza kufika pale. Baada ya kusimama na kujitambulisha kisha tulikaa. Wahudumu wa Kanisa wakawa wanapita kwenye kila Mstari kuchukua maelezo yetu. Nakumbuka kwangu alipita Msichana Mrembo hivi. Nilipomwambia kuwa Mimi ni Mtanzania na ndo nimefika south kwa Mara ya kwanza, alifurahi. Kwenye ile form yao nilijaza namba yangu ya simu. Wakuu kwa upande wa Lugha ya Kizungu siko vibaya sana. Naweza kujitetea kiasi chake.

Utaratibu mwengine wa lile Kanisa kwa mtu aliyefika Mara ya kwanza, wakati unajaza ile form yao wanakuuliza "Je kwenye hili Kanisa letu wewe utatusaidia upande upi?" Wakiwa na Maana Kama utaweza kujitolea mfano kufanya upande wa Media, Yan walikuwa wana Camera za kutosha mle ndani, Kanisa lilikuwa linaruka LIVE kwenye Mitandao ya Kijamii. Pia walikuwa wanataka kujua kama utajitolea kwenye upande wa Muziki sababu walikuwa na Kwaya yao na vyombo vyote vya Mziki. Kama wewe ulikuwa mtaalamu wa Maswala hayo ya Mziki basi utapangiwa huko.

Kwa hiyo ndani ya Kanisa Idara zilikuwa nyingi. Nikaona hapa nitumie fursa vizuri, Kwa kuwa Mimi nina taaluma Fulani ya Mambo ya Camera nikasema Mimi nitajitolea kwenye eneo hili. Yule Mrembo alifurahi kusikia hivyo. Akaniandikisha pale kisha akaondoka.

Ukweli Kanisa lilikuwa la Kishua na limechangamka sana. Kanisa lilikuwa na Gari la kwenda kuwachukua na kuwarudisha waumini wake.
Hili uliingia kanisa gani mkuu? Kanisa la kiroho la wakina gwajima au haya makongwe RC, Anglican
 
Kuna watu wananogewa na road trips. Nina kaka yangu yuko SA hela kwake sio tatizo ila kama mara nne za mwisho anakuja na Hilux flani hivi tangu SA mpaka bongo. Hiyo hela si angepanda ndege, maana kuna services za gari anafanya uhakika na hakai mwaka bila kuja.
Atakuwa Anataka kutalii.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Jozi, nilikuwa kwenye apartment kama siku ya pili toka nifike, natoka room kwenda kwenye vending machine iliyopo humo humo kwenye apartment kuchukua soda, nikawa niko kwenye simu naongea kiswahili, nikapishana na mdada mzuri hivi wa makamo kama 42 hivi yuko na msichana wa kazi na mtoto wa kike wana vifurushi wanaonekana wametoka shopping. Wakati narudi kwangu yule dada alikuwa bado amesimama ananisubiri nilivyotoka nilikuwa na pajama hivyo alijua kabisa siendi mbali. Akaniambia nimekusikia unaongea kiswahili wewe ni mtz au mkenya? Nikamjibu mTz, tukapiga piga stori hapo akafurahi sana, nikajua nimepata shost, Akanihoji hoji nikamwambia nimekuja tu kutembea, akaniambia yeye anaishi cape town, hapo amepita tu akitokea gaborone kwa mumewe, atakaa siku 4 then ataondoka. Nadhani alifurahi kupata mtu wa kuongea nae kiswahili siku hiyo maana appartment hiyo haikuwa na waswahili zaidi yetu, au kama ilikuwa nao sikupata kuwaona.

Basi, mi nilikaa kama miezi mitatu, nikawa namuona mara kwa mara basement kwenye parking na familia yake mi nikipanda zangu uber. Nikawa najiuliza huyu alisema atakaa siku nne sasa mbona haondoki? Nikajiongeza tu kuwa huyu anaishi hapa hapa, hakutaka tu kuniambia labda alihisi nitamzoea, au labda hakuniamini aliona sina ramani maana kiumri nilikuwa msichana mdogo bado tukawa tukionana tunasalimiana basi mpaka siku naondoka nilimuona jana yake jioni maana tulikuwa tunaishi floor moja, wing moja yeye apartment yake ilikuwa ya familia zile zina 3 bedrooms na vikorombwezi vingine, mimi yangu ilikuwa ndogo, Bedroom+sitting room, kitchen.
itaendelea au
 
Lete na wewe YAKO .tujifunze.
Alafu ukae na watu waliojaribu vitu vigumu ndo AKILI itatanuka
Aiseeh!!
Watu wanachizika sana na stories za South,one day (sijui lini) nitaleta story yangu kutoka Bongo kupitia Mozambique (Msumbiji) kwenda South,niliyokutana nayo Mozambique,kukamatwa na wajeda boda,kuruka 'nyenge',maisha yangu eManguzi Mbazanwa then harakati zangu ndani ya Johannesburg hasa hasa Jozi!!! South sio poa!!!

Samahani kama nitakuwa nimeingilia thread ya mwana kwa namna yoyote ile, mizuka tu yaani!!
 
Afu Roadtrip inakua tamu kama hamjazidi watatu hivi, huku mko kwenye hata defender ina tent lenu juu, ndani mna soft drinks plus maboksi ya ceres kibao, unagonga huku unachungulia grants zako kwa jicho la mafanikio, maji katoni kadhaa, ngoma inaanzia songea inapumua kidogo makambako unachoma kuku kizushi then inajaza mafuta, gari inawekwa kwa mexisons inapigwa povu kiaina, ikikamata highway inakuja kusimama Dom kidogo, inanunua wine za bei ya jumla, inaamsha kwenye nyama bahi kidogo unakula mbuzi na whisky funda mbili tatu, ngoma inaenda kulala manyoni kuna lodge za maana, hapo asubuhi inakamta supu ya kuku wa kienyeji then inatembea vumbi vumbi inakuja kula Tinde hapo unapumzika gari unafungua milango yote ipate hewa vizuri, baadae. Ikitoka tinde ngoma inasound hadi kahama unashangaa phantom kidogo unapita masumbwe, Ushirombo, Runzewe ngoma inapandisha Bwanga, inakula geita unaenda kulala hapo kwanza unasoma upepo haya mbele utaendelea mwenyewe
Mwamba una penda raha kama paka sofa[emoji38]yaani unavyo zipangilia hatare nanusu
 
Back
Top Bottom