Wangari Maathai
JF-Expert Member
- Aug 13, 2018
- 34,962
- 70,576
Afu Roadtrip inakua tamu kama hamjazidi watatu hivi, huku mko kwenye hata defender ina tent lenu juu, ndani mna soft drinks plus maboksi ya ceres kibao, unagonga huku unachungulia grants zako kwa jicho la mafanikio, maji katoni kadhaa, ngoma inaanzia songea inapumua kidogo makambako unachoma kuku kizushi then inajaza mafuta, gari inawekwa kwa mexisons inapigwa povu kiaina, ikikamata highway inakuja kusimama Dom kidogo, inanunua wine za bei ya jumla, inaamsha kwenye nyama bahi kidogo unakula mbuzi na whisky funda mbili tatu, ngoma inaenda kulala manyoni kuna lodge za maana, hapo asubuhi inakamta supu ya kuku wa kienyeji then inatembea vumbi vumbi inakuja kula Tinde hapo unapumzika gari unafungua milango yote ipate hewa vizuri, baadae. Ikitoka tinde ngoma inasound hadi kahama unashangaa phantom kidogo unapita masumbwe, Ushirombo, Runzewe ngoma inapandisha Bwanga, inakula geita unaenda kulala hapo kwanza unasoma upepo haya mbele utaendelea mwenyewe
Hahahaa umetaja machaka yangu yooote hahahaha dah😊😊