Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Unazaliwa Tabora unaenda kufia Nzega

Hivi mkuu unapajua mpyagula , unaweza kupitia igunga au nzega, haya sio maisha kule mama ntilie wanauza 500 unapata ugali na kambale mkubwa, kuna mabasi wa waraabu koko yanaenda kule basi mtu kule anakuhadithia huku ukituliza hela unatoboa unamchek kiaina unasema ni kweli Boss, funguo za chumba chako lodge anakaa nazo mwenye nyuma, ukitakA kutoka anaitwa kufunga mlango ukirudi kijana anaenda kumwita akufungulie Bongo nyoso acha tu
 
Umenikumbusha jinsi wazanzibar walivopiga pesa dubai, ilikua inaenda kununuliwa gari used dubai, mule ndani siti zinatolewa zote kama ni corola inajazwa mzigo unapangwa vizuri laptops, tv flat screen, na makorokoromengine vioo vinapigwa tinted milango inakua locked kabisa, ngoma ikifika bandarini kinacholipiwa ushuru ni ile gari bidhaa nyingine zote zile zinapita free soko la unguja likawa na vitu vya electronic kibao wapemba wakakuza mitaji then wakaona wahamie kariakoo jamaa walipiga bingo enzi zile basi tu,
Enzi hizo hawakua na scanners????
 
Tupate wadhamini kidogo ....

Ama stori/hustle za jamaa angu mnaija Dubai ,day one anaingia,ubaguzi wa Philippines ,Polisi wa Dubai,maisha ya Sharjah na fujairah, kuwekwa kizuizini Qatar airport jijini doha...kupata pesa kuanza biashara ya kuuza spare parts used from Dubai to Zanzibar then mpaka kufungua maduka mawili Dar es salaam ..
Kukutana na Recho msanii ,Prof Jay...na wengineo ...kutapeliwa 250 million na wabongo ...
Kuanza from scratch ...
Mpaka kuja kutoboa kupitia vifaa vya simu from China...
The guy is real struggle...

Sasa nakuwa mkuda likes kumi tuu Tuwasikilize wadhamini [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Recho ulimla????
 
Haya mambo ya kufikiria sana ndo yanatuponza wengi. Unakaa unapanga wee mipango mipango mpaka unazeeka

Ukiwaona wanaijeria au wakenya walivyojaa diaspora huwezi kuwa na akili kama hizi za kukaa mpaka uwe na mpango. Kujilipua ni kujilipua tu

Sasa hivi kuna vizazi vya pili na vya tatu vya watoto wa kinaijeria marekani,UK na Scandinavia huko wanafanya kazi za maana ila wazazi waliingia kwa mitikasi hivi hivi(bila kupanga)

Matajiri wa kihindi UK(Wanaendesha uchumi wa bibi saiv) waliingia kwa mitikasi

Warusi UK woote wameanzia kwenye magenge ya uhalifu

Waitaliano wote USA na waIreland wameanzia kwenye magenge ya uhalifu

Sometimes uoga wetu ndo umetufikisha hapa...Mambo yakishakua magumu the end justifies the means mkuu
Watanzania huko nje tunajulikana kwa uoga nadhani nchi kutopitia migogoro inatufanya turidhike na amani tunayohubiriwa na kina ndugai, wanigeria wanaongoza kwa Afrika kuwa huko ulimwengu wa kwanza
 
Hao uhamiaji wanapenda uwape story za huko ili wakuagize kambale hapo mtaongea, passport ni document ya kawaida ambayo ilitakiwa kila Raia anayeitaka awe nayo tu ndani
Hiyo Ni rushwa sasa
 
Achana na kitu inaitwa road trip kibongo bongo dar to arsha kama mko masela mnaweza kaa hapo barabarani mwezi mnaizunguka hii tz
Hahahaha acha tu kuna utalii mwingine raha sana. Haswa kama ni mtu mpenda magari

Wiki kadhaa zilizopita mdogo wangu kafanya utalii wa kuzunguka mikoa 22 ndani ya siku 13 kwa gari na mie nataka nimlipe

Kaanzia Mbeya-Tdm-Swanga-Mpanda-Kigoma-Bukoba-Chato-Geita-Mwanza-Shy-Nzega-Tabora..Then Tabora-Sgd-Babati-Arusha-Moshi-Tanga-Bagamoyo-Dar-Lindi-Mtr-Songea-Njombe-Makambako-Mbeya.

Mwisho wake mwaka huu nataka nilipe nipige mikoa yote ya bara na Mbuga zote za Tanzania kwa mwezi mmoja
 
Hahahaha acha tu kuna utalii mwingine raha sana. Haswa kama ni mtu mpenda magari

Wiki kadhaa zilizopita mdogo wangu kafanya utalii wa kuzunguka mikoa 22 ndani ya siku 13 kwa gari na mie nataka nimlipe

Kaanzia Mbeya-Tdm-Swanga-Mpanda-Kigoma-Bukoba-Chato-Geita-Mwanza-Shy-Nzega-Tabora..Then Tabora-Sgd-Babati-Arusha-Moshi-Tanga-Bagamoyo-Dar-Lindi-Mtr-Songea-Njombe-Makambako-Mbeya.

Mwisho wake mwaka huu nataka nilipe nipige mikoa yote ya bara na Mbuga zote za Tanzania kwa mwezi mmoja
Kuna watu mnajua kula maisha bhana hongereni sana
 
Watanzania huko nje tunajulikana kwa uoga nadhani nchi kutopitia migogoro inatufanya turidhike na amani tunayohubiriwa na kina ndugai, wanigeria wanaongoza kwa Afrika kuwa huko ulimwengu wa kwanza
Yaaani tumetengenezwa kizazi cha uoga sana na kuwaza mipango mipango mipango mpaka mtu anazeeka alikua anapanga tu

Huko serikalini sasa ndo kila siku mchakato,Tuko mbioni,upembuzi yakinifu,tunaandaa mpango mkakati mpaka kitu kije kufanyika mshachelewa sana

Kwa hili aisee ndo nilimkubali Msee Marehemu. Mipango hakuna unajilipua kila kitu kitajulikana mbele kwa mbele. Ukishakua na hii spirit lazima utapata njia tu ya kutatua ya huko mbele

Wanaijeria nawafahamu vizuri sana wale jamaa yaani wahalifu,wanafanya kazi halali,majinias,waliosoma,kina kalume kenge wale ni kujilipua tu hawaogopi kitu na inawasaidia sana kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na kwa familia pia

Wakenya nao hawako nyuma na wanajua kushikana mikono sana....yaan US mbongo ukiongea Lafudhi tu wanadhani Mnaija😂😂

Sie tumejifungia huku nyumbani Madibila tunakula Pitiku na ugali tunaridhika tunaogopa
 
SEHEMU YA KUMI

Kwa Kifupi ndo nikawa South Africa nimeshaingia ivo bila ya kuwa na Ndugu wala Rafiki wakunipokea. Mambo ya kusubiria kuwa na Ndugu au Rafiki yangenichelewesha sana.

Basi Nilikaa pale nje mpaka saa saba usiku ndo Jamaa akaja kunichukua. Alisema kuna sehemu alikuwepo kuna Harakati alikuwa anafanya. Jamaa akanipokea Begi hao mdogo mdogo mpaka KFC tukapata chakula kisha tukaenda Magetoni kwake. Ilikuwa ni ghorofa. Yeye alikuwa amepanga Ghorofa kama ya tatu hivi. Tulifika na kuingia ndani kwake. Kilikuwa ni chumba kimoja, sebure kubwa, Choo na Jiko. TV Kubwa, Makochi ya Kisasa. Kwa kifupi jamaa alikuwa anaishi vizuri.

Tukawa tunapiga piga story pale, Jamaa alikuwa ananichukua Maelezo ili awe na uhakika kama kweli Mimi ni Mtanzania na Kama kweli natokea Temeke. Wabongo wengi wanafanya hivyo ili kujiridhisha kama kweli wewe ni Mbongo wasije kupokea Mburundi, Mkenya au Mkongoman. Baada ya story kidogo jamaa akaniambia panda kitandani upumzike.

Hapa nitasema kama ilivyokuwa, Juu ya Kile Kitandani jamaa alikuwa ametandaza Dawa za Kulevya Kibao. Ilikuwa ndo Mara yangu ya kwanza kuziona dawa za kulevya vile. Zilikuwa nyingi sana halafu Jamaa haogopi wala nini. Alikuwa anazifunga funga. Nikahisi pengine jamaa alichelewa kuja kunifata labda alikuwa busy kufunga hizi Kete zake. Yan jamaa anafunga bila woga, tena mbele ya Mgeni. Nikajiuliza jamaa anajiamini nini.

Mimi sasa, Usingizi wote wa Safari ulikata. Maana nakumbuka nililala pembeni ya hicho kitanda halafu pembeni yangu ndo kulikuwa na hizo Dawa. Huku tunaendelea kupiga story.

Katika Maisha yangu, Dawa za Kulevya nilikuwa nazisikia tu kwenye Vyombo vya Habari na kuwaona Mateja Mtaani. Lakini ile nafika tu South Afrika ndo kama hivi nilikutana nazo tena ile ile siku ya kwanza. Mara pale ghetto tukasikia Hodi, Kisha Jamaa wawili wakaingia ndani. Nao ni wabongo. Tukasalimiana pale kisha wakaendelea na Mishe zao. Wakafungua mabegi yao na kuanza kutoa Kete zao za Dawa za Kulevya na Pesa, ni kama vile walikuwa wanamkabidhi jamaa mahesabu ya siku hiyo. Kwa haraka haraka nilisikia pale, kila mmoja alimkabidhi jamaa kama Laki Nane za Kitanzania. Moyoni nikasema duh jamaa anatengeneza hela. Laki Nane kila mmoja, Je Jamaa ana vijana wangapi ambao kwa Siku kila mmoja anamletea Laki Nane?

Baada ya mahesabu yao, jamaa aliwapatia tena mzigo mwengine wa kuuza siku inayofuata yaani asubuhi yake. Kisha jamaa akaniambia "Sasa Homeboy utafatana na hawa jamaa utakwenda kuishi wanapoishi wao"

Basi pale nikaamka chap, Nikatoka pale Ghetto na wale jamaa wawili. Hao mtaa kwa Mtaa na Begi langu Mgongoni. Hiyo ni Kama saa Tisa au Kumi hivi usiku. Uchovu wote umekata. Natembea na jamaa ambao najua kabisa kwenye Mabegi yao kuna Dawa za Kulevya kibao.

Yan Mwili wangu ni kama vile ulichanganyikiwa kiasi, kutokana na uchovu wa safari, Mambo ya Dawa za Kulevya na Macho nayo yalikuwa yanashangaa tu uzuri wa ile Mitaa. Mitaa mizuri sana. Basi ilikuwa shida tu. Mchanganyiko wa Hofu na Furaha kwa pamoja.

Hao Hao mpaka kama mtaa wa Saba huko. Tulisimama mbele ya Ghorofa kubwa kama Kama Ghorofa 12 hivi. Pale getini mmoja wao alitoa Kadi ya kufungulia Mlango kisha Mlango ulifunguka wenyewe. Hao mpaka ndani, Tulipanda kwenye Lift mpaka Ghorofa ya 8 au 9 hivi. Walifungua Mlango tukaingia ndani. Kilikuwa chumba kimoja kikubwa, Chini walilaza magodoro kama manne hivi. Kulikuwa na Sebure, Choo na Jiko. Jamaa wakanikaribisha pale, tukapanda kwenye Magodoro tukalala. Kwa jinsi chumba kilivyokuwa nilihisi hawa jamaa humu ndani hawana muda wa kupika, vyombo vilikuwa shagalabagala, Kilikuwa ni chumba cha wao kulala tu.

Basi haikuchukua muda jamaa wengine kama Watatu wakaingia ndani. Ndo walikuwa wametoka kwenye mizunguko yao. Tukasalimiana kidogo kisha wote tukalala.

Baadae nilikuja kuelewa kuwa hawa jamaa wote wanafanya kazi ya kuuza na kusambaza Dawa za Kulevya za yule jamaa wa kwanza niliyekuta ametandaza Dawa Kitandani. Wote ni wabongo. Yule Jamaa Bosi wao, tumpe Jina Y, anawatumia nauli hawa Vijana huku Bongo halafu anakwenda kuwafanyisha hizo Kazi. Wengine ni Rafiki zake, Wengine ni ndugu zake. Wakifika hapo South ndo kama ivo anawapangia jamaa chumba na kuwalipia kodi na mambo mengine. Kwa hiyo hiki nacho ni chumba cha yule jamaa Y. Niliwaza kama hawa jamaa wote humu ndani kila mmoja anapewa mzigo wa Laki nane akauze kwa Siku, Jamaa Y atakuwa na pesa kiasi gani? Kwa hiyo Mimi kujileta mwenyewe kwenye huu mtandao wake jamaa alifurahi sana kuwa amepata mtu wa kumuuzia Dawa zake bila shida. Yaan Mbuzi Kafia kwa Muuza Bucha.
Had nimesisimka maisha makali sana [emoji856][emoji856][emoji22]
 
Kuna watu mnajua kula maisha bhana hongereni sana
Hahahaaa ni passion tu ya road trip

Yaaani 22 regions kuanzia Mbeya-Songwe-Rukwa-Katavi-Kigoma-Kagera-Geita-Mwanza-Shinyanga-Tabora-Singida-Dodoma-Manyara-Arusha-Kilimanjaro-Tanga-Pwani-Dar-Lindi-Mtwara-Ruvuma-Njombe halafu Mby ndani ya two weeks. Ni kudrive tu na kuenjoy mandhari kula vyakula mbalimbali kila sehemu na kujifunza
 
Afu Roadtrip inakua tamu kama hamjazidi watatu hivi, huku mko kwenye hata defender ina tent lenu juu, ndani mna soft drinks plus maboksi ya ceres kibao, unagonga huku unachungulia grants zako kwa jicho la mafanikio, maji katoni kadhaa, ngoma inaanzia songea inapumua kidogo makambako unachoma kuku kizushi then inajaza mafuta, gari inawekwa kwa mexisons inapigwa povu kiaina, ikikamata highway inakuja kusimama Dom kidogo, inanunua wine za bei ya jumla, inaamsha kwenye nyama bahi kidogo unakula mbuzi na whisky funda mbili tatu, ngoma inaenda kulala manyoni kuna lodge za maana, hapo asubuhi inakamta supu ya kuku wa kienyeji then inatembea vumbi vumbi inakuja kula Tinde hapo unapumzika gari unafungua milango yote ipate hewa vizuri, baadae. Ikitoka tinde ngoma inasound hadi kahama unashangaa phantom kidogo unapita masumbwe, Ushirombo, Runzewe ngoma inapandisha Bwanga, inakula geita unaenda kulala hapo kwanza unasoma upepo haya mbele utaendelea mwenyewe
Nimecomment kitu hapo juu mkuu angalia tuandae yakwetu Mwisho wa mwaka. Nataka nimlipe dogo
 
Yaaani tumetengenezwa kizazi cha uoga sana na kuwaza mipango mipango mipango mpaka mtu anazeeka alikua anapanga tu

Huko serikalini sasa ndo kila siku mchakato,Tuko mbioni,upembuzi yakinifu,tunaandaa mpango mkakati mpaka kitu kije kufanyika mshachelewa sana

Kwa hili aisee ndo nilimkubali Msee Marehemu. Mipango hakuna unajilipua kila kitu kitajulikana mbele kwa mbele. Ukishakua na hii spirit lazima utapata njia tu ya kutatua ya huko mbele

Wanaijeria nawafahamu vizuri sana wale jamaa yaani wahalifu,wanafanya kazi halali,majinias,waliosoma,kina kalume kenge wale ni kujilipua tu hawaogopi kitu na inawasaidia sana kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na kwa familia pia

Wakenya nao hawako nyuma na wanajua kushikana mikono sana....yaan US mbongo ukiongea Lafudhi tu wanadhani Mnaija😂😂

Sie tumejifungia huku nyumbani Madibila tunakula Pitiku na ugali tunaridhika tunaogopa
Wabongo nyoso sana tuko vizuri kwenye kupigana majungu na kurogana kwingineko tuko nyuma mno hasa sehemu hizo ukiwa unatulinganisha na nchi nyingine za barani Afrika, Yani sie labda tunawazidi Burundi tu ila nchi nyingine zote za East Africa wanatuzidi mbali mno
 
Back
Top Bottom