Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Yaaani tumetengenezwa kizazi cha uoga sana na kuwaza mipango mipango mipango mpaka mtu anazeeka alikua anapanga tu

Huko serikalini sasa ndo kila siku mchakato,Tuko mbioni,upembuzi yakinifu,tunaandaa mpango mkakati mpaka kitu kije kufanyika mshachelewa sana

Kwa hili aisee ndo nilimkubali Msee Marehemu. Mipango hakuna unajilipua kila kitu kitajulikana mbele kwa mbele. Ukishakua na hii spirit lazima utapata njia tu ya kutatua ya huko mbele

Wanaijeria nawafahamu vizuri sana wale jamaa yaani wahalifu,wanafanya kazi halali,majinias,waliosoma,kina kalume kenge wale ni kujilipua tu hawaogopi kitu na inawasaidia sana kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na kwa familia pia

Wakenya nao hawako nyuma na wanajua kushikana mikono sana....yaan US mbongo ukiongea Lafudhi tu wanadhani Mnaija😂😂

Sie tumejifungia huku nyumbani Madibila tunakula Pitiku na ugali tunaridhika tunaogopa
Mkuu umeongea ukweli sana , uoga unajenga hofu sana, na hofu isiyo na msingi inakwamisha ndoto nyingi...

the fear of uncertainty

Hahahah ila hapo kwenye kula pitiku na ugali umenikumbusha songea sehemu moja inaitwa Ruhuwiko ....

Baada ya kushinda njaa siku nzima na kulala na njaa, usiku ulikuwa mrefu lakini nilivumilia hadi kukapambazuka....

asubuhi wakati tunajiandaa kwenda shule kuna msichana alikuwa mwanafunzi mwenzetu alikuwa anapasha kiporo cha ugali na hiyo mboga ya pitiku ili apate kifungua kinywa ..

Na me nikaomba nile maana niliamka na njaa sana,

Kufika darasani kipindi cha kwanza kikaisha , kuingia cha pili , tumbo liliniuma sana, nilihisi kutapika na kuharisha kwa wakati mmoja .

kwenda kujisaidia hakuna kitu kinatoka nikarudi class ...kuendelea kusikiliza kipindi.

Nikaenda kuomba ruhusa nikakatiliwa .

Wakati narudi class kukaaa kidogo kama dk 10
Hali yakutapika ilizidi hadi kunyanyuka mbio kwenda kutapika nje ya darassa lakin sikufika nilitapikia njiani karibu na ubao huku mwalimu wa chemistry akiwa anaendelea na pindi.

Dah mwailmu alishtuka na kutaka kuikimbia nje... maaana alikuwa anaandika ubaoni so wakati anageuka ndio nakutana na mimi natoka mbio kwenye desk kueleka nje, alihisi kama naenda kumvamia hivi. Wanafunzi walicheka sana wengine walicheka zaidi walipoona mzee nimetapika igali na pitiku yani ule mchanganyiko nilioula asubuhi nimeutoa kama ulivyo.

Kuna siku baada ya njaa ya siku nzima nakukosa uhakika wa kula tena usiku hata asubuhi ili tubidi tuanze kutembea kwenye mashamba ya watu na kula mahindi mabichi kama manyani au sokwe ..tukabamia kwenye shamba lilovunwa mihogo... dah

nilikaa kwa muda kama wa miezi mitatu kwangu ilikuwa kama mwaka mzima sitasahu tabu tulizopitia kule na wenzangu...

Ama kweli kusafiri na kuishi ugenini kunafungua akili
 
Hizo ni story za zamani watz wako kibao nje ya nchi kwa sasa na wanafanya vizuri,usikariri zunguka dogo acha kusikia story za vijiweni

Mdogo wangu rate ya watanzania waliopo nje ni ndogo sana kulinganisha na mataifa jirani kama Kenya, Uganda kwa hapa east africa, ukija west africa watu wa kule wanajilipua kiukwelikweli na wanajua kusaidiana na sio waoga, wabongo wengi mfumo wa kijamaa uliwapoteza na ndio maana hata kupigania haki zao za msingi wanaogopa, fuatilia zaidi utagundua dogo
 
Yaaani tumetengenezwa kizazi cha uoga sana na kuwaza mipango mipango mipango mpaka mtu anazeeka alikua anapanga tu

Huko serikalini sasa ndo kila siku mchakato,Tuko mbioni,upembuzi yakinifu,tunaandaa mpango mkakati mpaka kitu kije kufanyika mshachelewa sana

Kwa hili aisee ndo nilimkubali Msee Marehemu. Mipango hakuna unajilipua kila kitu kitajulikana mbele kwa mbele. Ukishakua na hii spirit lazima utapata njia tu ya kutatua ya huko mbele

Wanaijeria nawafahamu vizuri sana wale jamaa yaani wahalifu,wanafanya kazi halali,majinias,waliosoma,kina kalume kenge wale ni kujilipua tu hawaogopi kitu na inawasaidia sana kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na kwa familia pia

Wakenya nao hawako nyuma na wanajua kushikana mikono sana....yaan US mbongo ukiongea Lafudhi tu wanadhani Mnaija[emoji23][emoji23]

Sie tumejifungia huku nyumbani Madibila tunakula Pitiku na ugali tunaridhika tunaogopa
Umeongea point kubwa sana. mimi nilijilipua kwenda ughaibuni ikiwa na watoto wangu nikasema mambo yatajulikana mbele ya safari. Alhamdulilahi Mungu wa wote njia zilifunguka. Cha msingi ni kujilipua leo na si kusubiri kesho maana kesho haipo na mipango unapanga huku unaendelea kuhassle
 
Sent from my moto g power using JamiiForums mobile app

Sorry ww ni ke? Sasa mambo ndo haya..ehe watoto walikua na umri gan mkuu?
 
Sorry ww ni ke? Sasa mambo ndo haya..ehe watoto walikua na umri gan mkuu?
Mimi ke. Nilikuwa na watoto watatu wawili twins na mwingine mmoja. Miaka 12 twins na 10 mdogo. Watu walinishangaa sana kuja na watoto ughaibuni wakanicheka kuwa siwezi kusurvive na watoto ( kitu ambacho ni kweli lakini Mungu ni mkuu sana aisee
 
Duh hongera...hongera mno! Kila kitu kinawezekana aise
Yani mtu lazima kujilipua. Kitendo cha kupata visa na watoto ulikuwa ni muujiza kwangu. Nikajisemea kama tumepata visa basi Mungu ana mpango mwema nami. Ila haikuwa rahisi mwanzoni. Mtu aliyenipokea alinipa wakati mgumu sana. Manyanyaso kama yote na kumbuka hapo nina watoto. Dah sitasahau. Nilikuja kukutana na mwanaume mwenye pesa yake ndefu akanipenda kufa maana nami ni mzuri si haba, akachanganyikiwa na penzi la mtoto wa kitanga
 
Nilikuja kukutana na mwanaume mwenye pesa yake ndefu akanipenda kufa maana nami ni mzuri si haba, akachanganyikiwa na penzi la mtoto wa kitanga

Nilijua tu lazima mtoto wa kike ulikutana na bwana ukaolewa....ninyi wanawake mnaojilipua mna hii sijui niite advantage!

Hii ni mbinu nimeona wamama/wadada wengi wanaitumia, si Wabongo hata mataifa mengine na mkishaolewa hata makaratasi mnapata haraka tu...
 
Nilijua tu lazima mtoto wa kike ulikutana na bwana ukaolewa....ninyi wanawake mnaojilipua mna hii sijui niite advantage!

Hii ni mbinu nimeona wamamam wengi wanaitumia, si Wabongo hata mataifa mengine na mkishaolewa hata makaratasi mnapata haraka tu...
Ni kweli hii mbinu inasaidia na imewatoa wengi wanaume kwa wanawake. Maana kutoka hivi hivi shughuli pevu. Jamaa ni kama alishushwa na Mungu. Alinikubali na kunipenda na unyonge wangu wote. Akawakubali na watoto wangu. Mtu sina mbele wala nyuma naishi kwa watu na ni muhamiaji sina kitu. Jamaa bosi yuko vizuri financially bado akanichagua. Niliamini mwanaume akimpenda mwanamke hakuna kinachoweza kumzuia
 
Kwahiyo mkuu kilichokuokoa ni maliasili za kimataifa unazomiliki?
 
Back
Top Bottom