Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

Niliishi pale kwa jamaa kama Wiki mbili hivi, Story zao zote ni kuhusu Dawa tu. Aisee nilichoka. Nikasema hapa lazima nitoke. Sijajilipua kuja South kuja kuuza Dawa, Nikasema hata nyumbani wakisikia nimekamatwa kwa kesi ya dawa watanishangaa sana. Kama nimeweza kutoka Bongo mpaka South, Sasa nishindwe nini kutoka hapa kwa Washkaji kwenda sehemu nyengine.

Basi taratibu nilipanga kutafuta Marafiki wengine ambao sio wabongo. Niliona labda nikibadilisha watu nitasikia story nyengine tofauti na Madawa. Nikawa muda mwingi najichanganya na watu wengine. Ukiwa South halafu ukianza kufanya mambo tofauti na wengine lazima wabongo wenzio watachukia. Lakini nilijilipua tena kwa Mara ya pili. Liwalo na Liwe, wakichukia poa tu.

Niseme ukweli wakati natoka Bongo, Kichwani nilikuwa na Mipango miwili ya namna ya kupata Mchongo kwa urahisi. Mpango wa kwanza lilikuwa endapo nitachelewa kupata Mchongo basi niende nikajisalimishe kwenye Kanisa lolote. Ukweli nilipanga kwamba endapo nitakosa watu sahihi wa kunisaidia kufikia malengo yangu basi niwe mtu wa kwenda sana Kanisani ili kupata watu sahihi huko. Nilipanga kujisogeza kwa washua wale wa Makanisani. Nilijua washua wengi wenye Biashara zao Halali au Taasisi zao nitawapata huko.

Mpango wangu wa Pili ilikuwa kama nitachelewa kupata Mchongo basi nitafute Mrembo mwenye Kazi yake, nimpe mapenzi kama yote mpaka anipende na kunisaidia kupata Mchongo. Mjumbe hauwawi ndo yalikuwa mawazo yangu.

Nikaanza na hili la Kwanza la kutafuta Kanisa la Washua. Kumbuka Safari hii nilifanya Karibia na Sherehe za X-Mass na Mwaka Mpya, Nilifanya Karibia tarehe hizo Makusudi. Nilijua kwenye Mikesha ya Kanisani, Mkesha wa X-Mass na Mwaka Mpya lazima nitapata mtu wa kunisaidia. Basi tarehe zikasogea mpaka X-Mass ikafika. Niliwaaga wale jamaa zangu kuwa naenda kwenye Mkesha. Jamaa walinishangaa sana kwa sababu wao hawanaga mambo hayo. Tena siku niliyowaambia kuwa nakwenda kwenye Mkesha tulikuwa tumetoka wote kutembea Mitaa ya Midrand Gauteng. Midrand ipo Katikati ya Pretoria na Joberg. Ni kama dakika 20 kutoka Pretoria. Kuna Umbali kidogo sema wenzetu kwa kuwa Barabara zao nzuri ndo unatumia dakika hizi 20, Ingekuwa hapa kwetu ni umbali wa Kama kutoka Tegeta mpaka Magomeni.

Tukiwa huko Midrand ndo niliwaambia hivyo, Wakati wakuondoka wenyewe wakaondoka Mimi wakaniacha pale Midrand. Nikaanza kuzurura zangu Mitaani nauliza watu wapi nitapata Kanisa kubwa. Nilikuwa natafuta Kanisa ambalo ukiliona tu kwa nje unajua hili ni Kanisa la Washua. Sikutaka haya Makanisa Madogo Madogo.

Nilifanya yote haya ili kujiepusha na Biashara ya Dawa, ilibidi niangaike sana pale. Unajua Wabongo wengi wanajikuta wakiingia kwenye Biashara za Dawa kwa Mtindo kama huu, Yan ukifika ukakutana na Wabongo wenzio hawakupi nafasi ya kujipambania zaidi. Sasa kama wewe ni kichwa panzi basi unaishia kwenye biashara hiyo.

Mimi nilisema nitapambana mpaka dakika ya mwisho, swala la Kibali cha Kazi nitajua mbele kwa Mbele.

Basi nikafika mpaka pale Kanisani. Kuliona tu kwa nje nikajisemea hili ndo nilikuwa nalitafuta. Parking ilikuwa na Gari za Kifahari Kibao. Nikauliza Muda wa kuanza Ibada ya Mkesha wakaniambia kuwa ni saa moja usiku watu ndo wanaanza kuingia Kanisani. Washua Kibao walikuwa wamewahi pale, wamesimama kwa nje wakipiga story zao. Mimi nikasoma mazingira kisha nikatoka, nikazunguka zunguka pale Mitaani mpaka saa moja jioni ilivyofika nikarudi tena. Nikatimba zangu ndani.

Kama ilivyokawaida ya Makanisa mengi, mtu ukifika kwa Mara ya kwanza inabidi ujitambulishe. Tulisimama pale Kanisani kama wageni 50 hivi ndo ilikuwa Mara etu ya kwanza kufika pale. Baada ya kusimama na kujitambulisha kisha tulikaa. Wahudumu wa Kanisa wakawa wanapita kwenye kila Mstari kuchukua maelezo yetu. Nakumbuka kwangu alipita Msichana Mrembo hivi. Nilipomwambia kuwa Mimi ni Mtanzania na ndo nimefika south kwa Mara ya kwanza, alifurahi. Kwenye ile form yao nilijaza namba yangu ya simu. Wakuu kwa upande wa Lugha ya Kizungu siko vibaya sana. Naweza kujitetea kiasi chake.

Utaratibu mwengine wa lile Kanisa kwa mtu aliyefika Mara ya kwanza, wakati unajaza ile form yao wanakuuliza "Je kwenye hili Kanisa letu wewe utatusaidia upande upi?" Wakiwa na Maana Kama utaweza kujitolea mfano kufanya upande wa Media, Yan walikuwa wana Camera za kutosha mle ndani, Kanisa lilikuwa linaruka LIVE kwenye Mitandao ya Kijamii. Pia walikuwa wanataka kujua kama utajitolea kwenye upande wa Muziki sababu walikuwa na Kwaya yao na vyombo vyote vya Mziki. Kama wewe ulikuwa mtaalamu wa Maswala hayo ya Mziki basi utapangiwa huko.

Kwa hiyo ndani ya Kanisa Idara zilikuwa nyingi. Nikaona hapa nitumie fursa vizuri, Kwa kuwa Mimi nina taaluma Fulani ya Mambo ya Camera nikasema Mimi nitajitolea kwenye eneo hili. Yule Mrembo alifurahi kusikia hivyo. Akaniandikisha pale kisha akaondoka.

Ukweli Kanisa lilikuwa la Kishua na limechangamka sana. Kanisa lilikuwa na Gari la kwenda kuwachukua na kuwarudisha waumini wake.
kanisa RHEMA? mkuu
 
Kuna wakati kujilipua kusiwe kama fasheni kwasababu unaona watu wanajilipua, hapana jitahidi uwe na sababu hasa ya kujilipua..

Jitahidi unapotaka kujilipua uwe tayari umepambana vya kutosha humu humu imeshindikana na njia pekee ni kujaribu kwingine, kuna wimbi la vijana wako nje kwa sababu ni sifa kwake kuwa nje na hakuna juhudi alizojaribu kufanya akiwa hapa na hata huko aliko hana anachokifanya zaidi ya kuishi normal life ambayo hata hapa si ajabu ungeweka nguvu kidogo ungefanikiwa..

Kwenye kusafiri kuna namna nyingi, wapo wanaosafiri kwenda kutembea, wapo wanaosafiri kwa kutumia ramani zilizoanzia hapa na kwenda kupiga michongo mbele na kurudi hapa, wapo wanaosafiri baada ya kushindwa kabisa kutoboa hapa...
 
Mimi (Keagan Paul) nikiwa na akili zangu timamu, naapa kwamba nitasimulia kila kitu kama nilivyoahidi kwa mujibu wa sheria iliyowekwa.

Na kwamba nitasimulia mwanzo hadi mwisho bila kuingiwa na tamaa za kuhamia telegram.

Ee mnyaazi Mungu nisaidie.
Na washarika Tuungane nae Kwa pamoja tuseme ee myaazi Mungu Utusaidie...

Much:Bwana awabariki na kuwalinda.
Awaaangazie Nuru ya uso wake apate kuwafadhili.

Mch: Bwana akae nanyi.
Ush:Akae na roho yako.
Mch:Tummhimidi bwana.
USH:Tumshukuru Mungu....

Mch:Tukienda kulipia matoleo yetu kule telegram Usharika Tuimbe wimbo namba 205 Beti 5..

Baada ya hapo dada Noelia atatuongoza pambio wakati tunamsubir Keagan Paul Aje atupe Uzi wa leo.
 
Wanaijeria nchi yao inaruhusu uraia pacha. Ukiwa na uraia pacha inasaidia kuwekeza nyumbani. Tanzania uraia pacha hawajaruhusu. Tanzania kila kitu kinyume nyuma tu. Nchi nyingi za Africa wameruhusu uraia pacha
Sio sababu... Ndg zangu kibao wapo ughaibuni na wengine sio watanzania tena, wamebadili uraia wakija wanakuja kama wageni wengine japo huku ndio kwao, na wala wekeza huku pia kusaidia wazazi ndg na jamaa...

Dunia imebadilika sana, Pass ni makaratasi tu kama pesa haiwezi kukuondolea hitaji lako kisa kuukwaa umarekani na kuukana ukenya etc...

Una weza baki nao vilevile na haina tatizo... Una zani wewe ukiwa ughaibuni na Tz wako basi na wanao na wajukuu watakuwa watanzania kama wewe? Waache fursa kisa Utanzania?

Jicho lake la fursa haliwezi kuwa jicho lako, ukishindwa wewe sio kuwa wote watashindwa...

Yusuf Polsen baba yake kwao Tanga na mama mdenish, lakini kaamua kuwa mdenish japo huwa anakuja Tanga kusalimia, kaoa mjerumani na wana mtoto... Una hisi huyu mjukuu atakuja kuwa Tz? Kama sio mjerumani ni mdenish au hata hasiwe kt ya hayo mataifa mawili...

Charlie Chapliman mchekeshaji huyu ana watoto wengi na watoto wana mataifa yao tofauti... Kuna waingereza, waswiz, Uk etc... Haya mambo ya Mimi mzigua au mchaga tuna fata kwa baba kisa baba mchaga au mzigua unashindwa tembea na ndoto zako ni umasikini naona
 
wapo wanaosafiri kwa michongo inayoanzia humuhumu tanzania na kwenda moja kwa moja kwenye michongo kwingineko..

tusijifungie sana ndani, tujitahidi kujichanganya na watu tofauti tofauti, tusidharau watu, tuwe na marafiki tofauti tofauti kila mahala..

Wapo wabongo hapa hapa wanamichongo hatari sana inayoweza kukufikisha mpaka USA u Moscow.... inategemea na marafiki au watu wanaokuzunguka, Kwenda Yemeni huendi tu kwasababu unaenda Yemeni au Kabul hapana unakwenda tayari kuna deal limeanzia Iran likaja bongo then likarudi Yemeni.....tujifunze kuwa na marafiki wengi kila mahala, tujichanganye na kila mtu kuanzia masheikh, wapadri, wachungaji, makahaba, wezi, mateja, wauza unga, mapolisi, wanajeshi, nk...
 
Mimi (Keagan Paul) nikiwa na akili zangu timamu, naapa kwamba nitasimulia kila kitu kama nilivyoahidi kwa mujibu wa sheria iliyowekwa.

Na kwamba nitasimulia mwanzo hadi mwisho bila kuingiwa na tamaa za kuhamia telegram.

Ee mnyaazi Mungu nisaidie.
Do you smoke nicca?.
What's the f"ck hommie
 
Back
Top Bottom