Misunderstood
JF-Expert Member
- Aug 4, 2020
- 384
- 884
SEHEMU YA KUMI NA SITA
Ukweli niseme kitendo nilichokifanya cha kupost zile picha hata mimi nilikijutia sana. Unajua wakati mwengine ukimpenda mtu kuna vitu vingine unajikuta umefanya tu, hata ukiulizwa sababu kwa nini ulifanya hivyo huelewi. Malengo yangu yalikuwa yanamhitaji sana Yule demu mwengine kuliko Kanya. Siku iliyofuata nilienda mpaka alipokuwa anaishi Kanya, Nilijaribu kukaa nae kuzungumzia hii ishu, nilimuomba Msamaha mwishoe alinisamahe, maisha mengine yaliendelea.
Tuliyamaliza lakini Kichwani nilibaki na dukuduku Fulani hivi, nilikuwa nawaza sasa nitafanyaje? Maana Kanya kwangu nilimuona kama mzigo wakati mimi nilipanga kutafuta demu ambae atanisaidia kufikia safari yangu. Namtema vipi Kanya? Yule demu mwengine tukawa tukikutana Kanisani tunasalimiana fresh, kwenye simu tunawasiliana. Ukaribu uliongezeka kiasi chake, Alikuwa hajui chochote kilichokuwa kinaendelea, Baadae nilikuja kujua kuwa huyu demu anaitwa Tshepiso na anafanya kazi Capitec Bank.
Sasa kuna wakati Kanisa lilitangaza kuna Safari ya kwenda kutoa Huduma za Kiroho kwenye Tawi lake lililopo Nchini LESOTHO. Kanisa lilikuwa na Matawi mpaka Marekani na Baadhi ya nchi za Ulaya. Walisema anayetaka kwenda na kama una Passport basi ruksa mtu yeyote kwenda, Usafiri, Chakula, Kulala vyote ni gharama za Kanisa. Nikasema hii ni fursa kwangu ya kuwa karibu zaidi na Mchungaji na Washua zaidi. Mpaka hapa kwa kweli nilianza kukubalika pale Kanisani si kama Mwanzo. Nilikuwa sio mgeni tena kwenye macho yao.
Lesotho ni nchi ndogo, Mfano ni kama Mkoa tu wa Morogoro au Morogoro inaweza kuwa Kubwa pia. Ni nchi ambayo ipo ndani ya nchi ya South Africa. Nchi yote imezungukwa na South Africa. Kama mtu hufahamu unaweza ku google ukaona.
Sasa kwa wasiofahamu, Vijana wengi wazawa wa South Africa hawana Passport za kusafiria, Wengi sio sana watu wa kusafiri safiri, kwa hiyo kigezo cha watu kuwa na Passport kilipunguza waumini wengi sana akiwemo Kanya. Alikuwa hana Passport. Kwenye Upande wa watu wa Camera, Mimi na Max tu ndo tulikuwa na Passport. Nilichofurahi Tshepiso alikuwa na Passport kwa hiyo alikuwepo kwenye hii safari.
Utaratibu wa siku ya Safari tulikuwa tunapewa gari Fulani zina muundo kama wa Toyota Alfad, rangi nyeupe, Mnakuwa mnachaguana wenyewe waumini kama sita, kati yenu anapatikana pia dereva, kisha mnaanza safari. Mimi na Tshepiso tulipanda gari tofauti. Siku ya safari ilikuwa ni jumamosi ila Muda wa safari mnapanga wenyewe wana Kikundi, Mchungaji alisema anachotaka watu wote Jumapili tuwe tumefika Lesotho. Kwa hiyo Kanisa lilitoa gari kama 10 hivi. Watu tukaanza safari. Sisi tulianza safari jumamosi jioni.
Kwenye gari yetu mwanaume nilikuwa peke yangu, wengine wote madem. Wote kati yetu hakuna hata mmoja anaijua njia ya kutufikisha Lesotho. Yan wenzetu wana barabara nyingi kiasi kwamba unaweza kuzaliwa palepale na Baadhi ya barabara za kuelekea baadhi ya nchi huzijui. Na ukikosea tu barabara unaweza kutumia muda mwingi sana kurudi kwenye barabara uliyoikusudia kupita. Nakumbuka tulipotea sana. Mpaka ikabidi tutumie Navigator kwenye simu zetu. Wote ndani ya gari tuliwasha Navigator tunamwelekeza dereva wetu wapi pa kupita.
Tulifika Boda kati ya South Africa na Lesotho usiku wa kama saa Saba hivi. Kwa kuwa nilikuwa na mademu wote, mimi ndo niliwaongoza mpaka mle ndani kwenye Ofisi za Uhamiaji. Kwa kuwa kwenye Passport yangu nilikuwa nimezidisha siku za kuishi mle South Africa, Nilisoma mazingira pale kwenye Passport yangu nikaweka Rand 300, nikagongewa bila shida. Japo Lesotho tulikuwa tunakwenda kukaa siku Tatu tu lakini Uhamiaji upande wa Lesotho walinipa siku Thelathini za kukaa Lesotho. Nilikuwa tayari mzoefu wa kupita kwenye Maboda.
Wale mademu walikuwa wanazinguliwa pale, nikawaambia wekeni Rand 100 kwenye Passport zenu halafu nendeni tena, wakafanya hivyo kisha wakagongewa mihuri kasoro mmoja tu kati yetu ndo hakugongewa huyo demu alikuwa ni Mnaijeria, Kwanza Mnaijeria kuingia Lesotho inabidi alipie visa. Sio kama sisi wengine tunaingia free tu. Pili Yule demu kama mimi tu pale South Africa alikuwa amezidisha siku za kuishi (Ame Overstay). Kwa hiyo wale maafisa uhamiaji walikuwa wanataka pesa ndefu.
Nakumbuka alikuwa anasema “Mbona Mtanzania na yeye ametoka mbali lakini amegongewa bila shida”. Basi pale mmoja wetu akafanya mawasiliano na mchungaji, Mchungaji na baadhi ya waumini walikuwa wameshafika Lesotho tayari. Kwa kuwa sio mbali sana, ule ule usiku, mchungaji ikabidi aje mpaka pale boda. Akaongea nao wale Maafisa Uhamiaji, nadhani aliwapa pesa kidogo ila sina uhakika sana. Hatimae wakatuachia tukaendelea na safari yetu mpka Mji Mkuu wa Lesotho unaitwa Masseru. Masseru pa kawaida sana pengine hata Dodoma pazuri. Huwezi hata kulinganisha na Dar, Arusha au Mwanza. Basi tulienda moja kwa moja kwenye Hostel tulizopangiwa kufikia. Tulilala pale.
Asubuhi mapema sana tuliamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kwenda kupanda Mlima kwa ajili ya Ibada, Ibada ya kwanza tulienda kufanyia milimani huko. Ibada ya Jioni ndo tulienda kwenye Kanisa lao. Kwa hiyo Hata kupanda huo Mlima nakumbuka ilikuwa ni tabu, Mlima ulikuwa mrefu kiasi chake. Wakati magari yetu yanakusanyika pale chini ya Mlima ndo nilikutana na Tshepiso.
Ukweli Lesotho tuliinjoi sana, kwanza tulikuwa wachache, kwa hiyo tulikuwa kama ndugu Fulani hivi, tulipiga picha kama zote mpka leo hii ninazo kwenye Email yangu. Nikiziangaliaga huwa zinanikumbusha matukio yote haya ninayoyaeleza. Kule Lesotho Mimi na Yule demu tulikuwa marafiki kinoma yan, ile Camera ya Kanisa niliyokuwa natumia kupiga picha, Picha nyingi nilimpiga Tshepiso. Wakuu zote hizo ni harakati za kutaka kutafuta Mchongo ndani ya nchi ya watu. Naomba nisieleweke kwamba mimi ni Marioo ila mazingira ndo yalikuwa yananilazimisha kufanya nilichokuwa nafanya. Nilijua hapa nikicheza tu Akiba yangu ya Pesa inaisha yote halafu kinachofuta ni maisha magumu na kurudi Bongo, halafu mpango wa Kurudi Bongo nilikuwa sina kabisa. Na huyu mwanamke naona kabisa kwa maisha yake anaweza kunifikisha Mahali.
Hivi hii story ni ya mwaka gani?? Yani ulikwenda huko miaka ipi?