Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nakumbuka mwaka 2007 nilikua na ndoto za kwenda dzonga ila sikua na mpunga, kuna jamaa yangu alikua amerudi toka lebanon huko alikua deployed kwenye peace keeping alikua amerudi bongo na fedha za kigeni nikaona kupitia huyu mwamba nitapata nauli nitambae zangu ng'ambo.
Nikawa chawa wa mwamba full kumsaidia kusolve harakati za hapa na pale kutokana na uzoefu wangu wa mtaa
Sasa bhana mwamba alikua na binti mmoja wa kitanga ndio alikua anataka amfanye mkewe ili dingi yake ni mnoko kikuda mchumba ndio alituambia kipindi mwamba anampa idea ya kwenda bumbuli kujitambulisha ,mimi kama chawa nisie na maadili nikamshauri mwamba ampe binti ujauzito ndio tuende ili zoezi liwe rahisi mwana apate jiko na mimi niende zangu ng'ambo.
Mwamba akafanikiwa kurutubisha yai binti kitumbo kikaota ikapangwa safari ya kwenda usambaani kuonana na wazee.
Kufika Tanga tukapokelewa fresh na bimkubwa, na mashemeji kumbe kamanda walikua wanamjua wote kasoro mshua boy tu, na bahati mbaya au nzuri hakuwepo siku hio ikabidi mzee apigiwe simu alikua shambani kwake huko anakaaga hata mwezi bila kurudi home. Alitaarifiwa uwepo wetu akaombwa arudi fasta mzee akaomba aongee na muoaji, mshkaji akatoka nje kuongea na mkwewe, mzee akamwambia jamaa anarudi kesho jioni lakini asitukute nyumbani kwake na hataki kabisa kutusikia, mshkaji kwa tabia zake za kijeshi akamkazia mzee na mikwara ya hapa na pale kwamba hatuondoki tutakaa hata mwezi mpaka arudi tuondoke na mke wetu. Mshua akasema kesho jioni anarudi lakini hatotukuta maana tutaondoka bila kuaga kamanda akasema sawa ngoja tuoneshane umwamba.
Ilifika usiku tukapewa room ya wageni kuna bed mbili kila mtu na lake, tukaangusha na mwanangu ,tulienda na begi moja tu , mchumba aliliweka chumbani kwake kwa usalama zaidi maana chumba chetu kilikua nje,
Kufika mishale ya saa nane usiku niliota ndoto kwamba yule mzee kaihamishia mimba kwa mjeshi halafu tuko leba kamanda anajifungua, mimi na manesi tunamwambia mchizi push! push! Jamaa anapiga kelele kumbe mimi nivyoota hivyo napiga kelele kwanguvu na jamaa naye anaota ndoto hiohio na anapiga kelele za uchungu mara tukashtuka wote mshkaji ananiuliza mtoto wangu yuko wapi nikamjibu kua makini usimlalie kuinuka dah! Mwamba alikua kashusha bonge la kimba mazee halafu hawezi kulikataa yaani kafanana nalo copyright alafu mashuka yote kitanda kizima kilikua makimba tu , nikampa mashuka ya kitandani kwangu ajisafishe tutoroke kabla hakuja kucha maana asingeweza kubadili nguo zilikua chumbani na mama kijacho mjeshi akaniambia kukimbia ni mbinu ya kijesh kabisa wao wanaiita ku retreat.
Tulitoka chumbani mule kwa kucraw mpaka kwenye toyota porte yetu huku mchizi akiwa kajifunga shuka rubega tukatokomea
Tukiwa njiani mwamba ndio akakumbuka conversation yake na mkwe wetu kwamba tutaondoka bila kuaga kama PAUL KEAGAN
Tulifaka town hata mawazo ya kumpiga mzinga wa nauli ya kaisha maana analia tu kama kabinti muda wote
Aisee ungelea tukajua mengi, vp mwanamke alimtafuta tena,
 
Huu utamaduni uko border nyingi Sana hapa Africa. Makonda wa Mabus wanajuana na watu wa immigration anatangaza mapema Kama huna passport au passport yako inashida we sema mapema, unampa hela na passport yako kila kitu kinaenda sawa.

Ila ukijifanya mjuaji kuongea na immigration mwenyewe unaweza ombwa dau kubwa au wakutie ndani iwe mwisho wa Safari.

Airport tu ndo naona wanakuwaga strict sio Wala rushwa Ile ya kuonekana. Ukiover stay Sheria ziko wazi wanakukazia.
Kweli kabisa mkuu
 
Kwenye kuongeza inategemea unataka kuendelea kuishi huko kwa shughuli gani? Maana unapotaka kuongeza inabidi utoe sababu maana kuna visa za aina tofauti tofauti kama ya kusoma, kufanya kazi, volunteer etc na zote zina gharama yake.

Mkuu Mimi nimekaa sana nchi ambazo wanakupa miezi mitatu ya kuishi kwa hivyo ikiisha unachofanya kuna watu ndio kazi yao unawapa passport inaenda kugongwa tena mpakani kama umetoka kisha inagongwa tena umeingia kwahiyo utakaa hadi hadi uwe mzee kabisa bila kurudi ama aumue mwenyewe tu kurudi kwa hiari yako mwenyewe
 
Sasa hivi njia ya Msumbiji inapitika kweli? maana wale Magaidi wako bize kuchinja Vichwa vya Wananchi utasema msimu wa mavuno ya vichwa

Bila hata uwepo wa magaidi ukipita Mozambique wanaweza kukusachi hadi p*mbu na uwezo wa kufika safari yako ni 20%,Mozambique pasikie tu hivyo police wana roho ngumu kama Jiwe letu pendwa,pitia zambia mkuu utakuja kunishukuru
 
Hiki kitu ndo kinanikwaza sana ...mwanamke ukijipeleka sehemu kama KFC kurefresh kwa hela yako watu wanadhani unadanga...ukinunua kagari kwa saving zako wanahisi umehongwa...ukianda cheo kazini kuna watu wapumbavu wanahisi unatembea na boss...watu wanawaza ngono ngono ngono muda wote
Mimi ni mwanamke sex ni part muhimu sana ya maisha lakini sio first priority katika maisha na sipendi initawale...napenda sana kuwa na marafiki wa kike na kiume ila sipendi kutongozwa...najikuta napata wakati mgumu kwa baadhi ya watu...ukimchekea tu kashawaza kukufunua nguo...come on maisha ni ziadi ya sex...watu hawawazi productive friendship bila ngono...and i hate that...ngono ngono ngono why?!
Madam tuwe marafiki basi au[emoji1][emoji1]
 
Mkuu Mimi nimekaa sana nchi ambazo wanakupa miezi mitatu ya kuishi kwa hivyo ikiisha unachofanya kuna watu ndio kazi yao unawapa passport inaenda kugongwa tena mpakani kama umetoka kisha inagongwa tena umeingia kwahiyo utakaa hadi hadi uwe mzee kabisa bila kurudi ama aumue mwenyewe tu kurudi kwa hiari yako mwenyewe
Mambo ya HongKong enzi hiyo...sijui kama hadi sasa hii michezo ipo...

Maana wabeba ngada wameharibu sana taswira ya Wabongo
 
Mkuu nimekaa Johnannesburg mwaka mzima bila permit wala ni bibi yake na permit hadi nilipoamua kusepa mwenyewe mwaka 2017,pia kuna rafiki yangu anagonga mwaka wa 8 huu tangia zile passport zetu pendwa za buku 50 kuisha muda hadi leo hajatia maguu bongo!,Mozambique nimetulia miaka 3 bila karatasi yeyote,zambia nimetulia miezi 8 ila kidogo ninyee debe!,nimezururua nchi nyingi za shilole country najua namna ya kuishi bila document yeyote
Inawezekana ila ni maisha magumu sana. Huwezi kufanya kazi halali..ukiona tu polisi au immigration wanapita presha inaanza kupanda. Ukipata shida huwezi kwenda polisi maama watajua wewe mhamiaji haramu.. sio kitu rahisi.
 
Achen mfumo dume pimbi nyie,kwahyo hampend kuona wadada wanacomment,nyau nyie.

Afu,ebu jiulize inawezekana vp uzi mzima ziwe post za keagan peke yake,.......anapata nguvu za kuandka anapoona wafuatiliaji n wengi,kama unataka usome story yote kwa wakat mmoja nunua ktabu,pimbi wew
Pumbavu sana, mie napinga Malaya kuvamia Uzi na kuanza kubadilisha taswira ya Uzi nasio huu tuu nyuz nyingi nyie Malaya (Kama auhusiki jitoe) mnaharibu sababu ya kutaka Mambo yenu.

Sijakataa watu kuongezea Nyama hata iwe stori ya kweli au uongo mie napambana na maneno pili uhalisia Ila personality ya mtu hapana.

Pumbavu sana.
 
Ilipoishia.....

Nywele za Tsheispo zilikuwa zimeangukia mgongoni, chuchu saa sita oclock, guu sasa ndio nilichoka asee, guu nilidhani ni paja la mange kimambi, nikasema hapa keagan lazima leo nimueleze hisia zangu, baada ya kufika pale akesema mbona unaniangalia sana, nikamwambia hapana umependeza sana akacheeka huku tukiongozana kwenda restaurant .

Sasa endelea...

Tulipofika restaurant niliagiza viazi vya kukaanga na kuku Tsheispo yeye aliagiza kuku na juisi basi tulikula weee hadi pale muumini mmoja alipotufata kua tunaitwa na pastor! Tuliondoka na kurudi kanisani nilifurahi sana maana Tsheispo ndie alilipa bili hivo akiba yangu ilibaki salama.

Tulirudi kanisani pastor alisema tujiandae twende tour kwenye national park moja inaitwa Sehlabathebe National Park. Basi tujiandaa na kupanda coaster ambayo ilitumia masaa matatu kufika. Tulienjoy hadi jioni na kurudi pale kanisani tulilala mapema ili asubuhi tuanze safari ya kurudi south.

Sasa tulipofika pale boda ya kuingia south ndo kilitokea kizazaa. Askari wa migration walikua wakali kama wamekula pilipili za mto ruvu hawakutaka kucheka na kima kabisa siku hiyo ndo nilijuta kuwajua makaburu. Waligoma kua siwezi kuingia south maana permit yangu ilikua imeshaisha muda dah! Nilipagawa sana sikujua nifanyeje. Wale wenzangu waliruhusiwa kuondoka, waliondoka na kuniacha pale peke yangu tena chini ya ulinzi mkali kama wa mwendazake! aisee nililia sana nilipojua sitamkula Tsheispo baadae wale askari walinipeleka mahabusu.

Kesho yake nilitakiwa kupelekwa mahakamani lakini huwezi amini kolichotokea askari mmoja alikuja na kuniita kwa nguvu KEEGAN PAULO niliitika kwa uoga naam afande! Yule kaburu alinikata kibao akasema we nyani nikikuita itika Sir nipo Sir. Hilo neno Sir lilimaanisha bwana mkubwa. Basi bwana niliitika kama alivoniekeza. Alitabasamu na kusema njo unifuate nilitolewa nje wakati tunatoka nje nilishangaa kusikia mtu ananiita jina langu kabisa la Keegan Bashite nikazuga kama sijasikia. Mara akanigusa bega na kuniita kwa nguvu we Keegan amka.

Nilishituka sana kumbe nilikua naota. Aisee kumbe aliekua akiita ni Dada wa kazi! alimua akiniamsha nikale. Aisee ndoto za mchana mbaya nilikua nshafika south kimasikhara! Kumbe toka episode ya kwanza nilikua naota huku nakoroma kama jenereta bovu!! Lakini tuache utani Kanya alikua na tako balaa. Ngoja ninywe kiroba nilale nimechoka type. Mwe!!!!..

Mwisho
Baharia kamaliza mchezo ,Aya tukale mafenesi ,matikiti maji kimasihara huko kwa mvulana riki[emoji41]
 
Mkuu nilitaka nisikujibu ila nimeona nikikaa kimya watu wanaweza kuamini hiki ulichokiongea. Humu bhana hatujuani, hata wewe hunijui ila umeongea kama unanijua. Kama hatujuani huo wivu unaouongelea wa nini? Pili niwie radhi kukuambia kuwa kuna vitu huvijui na ni bora ukakaa kimya kuliko kujiaibisha. Kuhusu kuoverstay na kugongewa exit nina uhakika kuna kitu umekificha na kama hujakificha basi huyo kondakita alikuficha. Ukiover stay halafu ukawa unarudi kwenu immigration officer hawawezi kukuzuia kurudi kwenu japo wakikufanyia roho mbaya wanaweza kukukamata na kukufungulia mashitaka ila kwa sababu ulitoa rushwa ya rand 300 wanaweza kukuruhusu uondoke nchini mwao ila huwezi kukanyaga nchini kwao ndani ya miaka 5 kama hutalipa hiyo fine ya kuover stay. Ndio maana nimekuambia kuna kitu hujakiongea kuhusu kuoverstay au huyo konda wa basi hakukuambia. Ukioverstay ukiwa unarudi kwenu in most cases watakuruhusu upite ila utapigwa fine ambayo utaambiwa either uilipe hapo hapo au ukailipie ubalozini kwao nchini mwako. Usipoilipa huwezi kurudi tena nchini kwao kwa muda wa miaka 5 labda ubadirishe passport, na sasa hivi hata ukibadirisha passport ni kazi bure maana finger print zako zitasoma kwenye system yao. Kuna mengi ningekueleza ila acha niishie hapa.
Konda Experience za maisha ya nje ya Bongo zipo tofauti sana usi conclude moja kwa Moja utakosea, Kila mtu ana experience yake na namna alivyopambana kuikabiri hiyo changamoto. Unaweza Ku Overstay, Ukatoa kitu kidogo Passport yako ikawa cleared na Maisha mengine yakaendelea. Na SA ukarudi kwa Passport ile ile. Tumeshafanya ivo sana. Kikubwa jipe nafasi ya kujifunza zaidi.
 
Konda Experience za maisha ya nje ya Bongo zipo tofauti sana usi conclude moja kwa Moja utakosea, Kila mtu ana experience yake na namna alivyopambana kuikabiri hiyo changamoto. Unaweza Ku Overstay, Ukatoa kitu kidogo Passport yako ikawa cleared na Maisha mengine yakaendelea. Na SA ukarudi kwa Passport ile ile. Tumeshafanya ivo sana. Kikubwa jipe nafasi ya kujifunza zaidi.

Kaka achana na haya mambo. Malizia Story tufanye shughuli nyingine. Ni zaidi ya masaa 24 umetulostisha
 
Mtoto wa muheshimiwa Keagen Paul

Lengo siyo kuona mapungufu wala kukwazana lkn kwa kuwa tunapaswa kujifunza sio mbaya tukaambiana ukweli wote

Ilikuwaje ukapita mpakani kwenda Lethoso wakati passport yako ilionyesha umezidisha muda wa kukaa SA ( sawa uliweka Rand 300) hauoni kwamba hapo ni issue ya mfumo na nafikiri kuna database ya uhamiaji ktk nchi husika kwa wageni wanao ingia na kutoka ( system) pia si inatakiwa kujazwa taarifa ktk hiyo database au ni suala la kugonga muhuri tu ktk passport bila taarifa zako kuwa stored ktk database yao? Hao ma afisa wa uhamiaji wanawezaje ku ‘manipulate’ na ku u ‘fix’ huo mfumo kwa kiwango hicho

Ingeleta maana ukisema ulitumia labda kama zile karatasi za zamani kama hauna passport (sijui mpaka miaka hii) kwa mtu kuingia kama EA unapata mpakani mfano Namanga unalipa na hauonyeshi passport na kwa kigezo wewe ni Raia wa kutoka ukanda/ nchi hizo na hapo hata sijui ulirudi vipi tena na ukaweza kuingia SA kutoka Lethoso

Sijatembea nchi za bara letu hili pendwa na labda kuna kiwango kikubwa cha rushwa mpaka tuna zi ‘fix system’ ila kwa nchi chache nilizoenda nje ya Afrika hicho kitu hakiwezekani eti umezidisha muda wa kukaa wa nchi husika afu unaenda dirisha la uhamiaji na sijui uweke $ mambo yaishe ni ngumu sana hiyo

Najua hamu ya kusimuliwa kwa wengi wetu ilivyo kubwa lkn hapa tunatakiwa kupata maelezo kidogo ili tujifunze kutoka kwa Muheshimiwa kama ataona inampendeza na ni hiari tu kutoka kwake

All in all hongera sana kwa uzoefu unaotupa ktk simulizi hii
Mkuu usipoteze muda wa ku type hii Ni chai Kama chai zingine
 
Back
Top Bottom