Mkuu mie unafiki huwa siuwezi, wewe unge-clear tu doubts zetu then ukaendelea kuleta stori. Haya mambo ya watu kuogopa kuuliza maswali ndio sababu hata nchi yetu imefikia hapa ilipo. Watanzania tulio wengi hatujiamini ndio maana viongozi wetu wanatuendesha wanavyotaka, yaani tuna taifa la ndio mzee hata kama kunahitajika maelezo. Kitu kama hakijakaa sawa wewe kitolee ufafanuzi. Kuna vitu hatuwezi kukubishia kwa sababu kweli kila mtu ana experience yake ila mkuu kuna vitu very technical huwezi kusema kila mtu ana experience yake pia, kuna baadhi vitu lazima viwe common kwa kila mtu. Mfano ni hili la kuoverstay haliwezi kumalizwa kwa rushwa ya rand 300 na likaisha completely kwa sababu ni issue ya usalama wa nchi na system iko linked nchi nzima kuanzia makao makuu ya immigration hadi idara zote zinazohusika na maswala ya uhamiaji. So wakiscan tu passport yako hapo boarder au sehemu yoyote inayohusika na mfumo wa passport control taarifa zako zinaonekana hadi makao makuu ya immigration kuwa kuna mtu kaoverstay anahitajika kukamatwa au kulipa fine whatever the case may be. Sasa huyo immigration officer atakusaidiaje hapo? Hiyo fine atakulipia? maana hiyo fine ni zaidi ya rand 4,000. Na hiyo fine inakuwa registered kwenye system mpaka uilipe ndio iwe cleared la sivyo unakuwa black listed kukanyaga nchini kwao for the next five years. Kwa hiyo hoja kama hii unatakiwa uitolee maelezo ili twende sawa. Kuna watu humu wanafurahia tu stori na vitu kama hivi wanavioverlook kwa sababu either hawavijui kama vipo au wameamua kufunika kombe mwanaharamu apite. Halafu hata issue ya kupewa hifadhi na kanisa na yenyewe kuna utata kidogo kama hutajali pia itolee maelezo. South africa inajulikana kwa ujambazi na mauaji hivyo kwa mtazamo wangu sio rahisi viongozi wa dini wakupe hifadhi bila kujiridhisha kama wewe ni mtu salama au la. As a reasonable person nilikuwa nategemea wangekuhoji kwa kina kuhusu uhalali wako wa kuwepo nchini kabla ya kukupa hifadhi, lazima wangekuulizia documents zako kama upo nchini kihalali. Kumbuka hilo ni kanisa na linatakiwa kuheshimu sheria za nchi, hivyo hawawezi kurisk kumhifadhi mtu ambaye anavunja sheria maana ungekamatwa wangeonekana wanahifadhi wahalifu hivyo ingepelekea kanisa kuingia mgogoro na mamlaka za kiserikali na ingepelekea hatari ya kufutiwa usajili wa kanisa lao, mind you Mindrands ni makazi ya watu wenye hela kwa hiyo ni watu wenye uelewa mpana. Samahani wasomaji kama nawaharibia stori yenu ila nimeamua kutokuwa mnafiki kwa kuuliza haya maswali critical.