Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Nilivyokwenda Afrika Kusini bila kuwa na Ndugu wala Rafiki kule

Labda Muumbaji mbingu na nchi kampenda zaidi sisi huku tunamsubiri sana!!
 
Sehemu ya kumi ipo wapi?
Wakuu leo naomba kuleta Story yangu ya kweli ya jinsi nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu kule wala mtu wa kunipokea.

Ukweli kuna wakati ilifika nilichoka sana maisha ya hapa nyumbani, ilikuwa Mwaka 2014, nilikuwa napitia changamoto nyingi za maisha hasa katika familia. Ukweli akili ilikuwa imechoka sana ilisababishwa na kutokuwa na ajira muda mrefu.

Hata baadhi ya watu sikuwa napenda kukutana nao sana. Nikajiuliza kwani Maisha ni hapa tu nyumbani? kwani hakuna sehemu nyengine? Nikajisemea labda sikuandikiwa kutoboa hapa nyumbani ngoja nikajaribu bahati yangu sehemu nyengine.

Kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda South Africa, Kwanza niliwaza kujaribu bahati yangu Marekani, nina ndugu kama watatu huko. Nikamcheki ndugu yangu mmoja akanitumia Invitation Letter. Nikaanza kupambana pale Ubalozini. Nilifika kwenye Usahili lakini nilikosa VISA.

 
Ukimaliza itabidi na mimi nitoe yangu ya siku kwenda China kufunga mzigo bila ndugu rafiki wala nini
Hakika tunataka kujua juu ya safari yako ya china
Au ushaiandika kama tayari naomba nitagi
Kama bado tunaomba uandike tupate kujifunza
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE

Basi nikaanza maisha yangu mapya ndani ya south pale Kalfonteen. Ratiba ya kwenda Kanisani ilikuwa ni karibia kila siku. Uzuri wao muda wa kwenda Kanisani ni Jioni kuanzia saa kumi na mbili na kutoka saa nne usiku. Mpaka Jumapili muda ni huo huo. Gari ilikuwa inatufata mpaka getini, tunaingia hao kanisani. Kwenye gari mnakuwa wengi. Nilikuwa nikifika Kanisani najichanganya sana na Vijana wenzangu, wazee, watoto mpaka Mchungaji nilianza kumzoea. Kwenye maisha ukiamua kujilipua, jilipue mazima, usijilipue nusu nusu, lazima uwe na uwezo mkubwa wa kujitoa ufahamu. Mimi sikuwa mwoga kama Wabongo wengi. Hata hapa Bongo nilikuwa sio mtu wa kwenda sana Kanisani, lakini kule ilikuwa kila siku nipo. Tena vile usafiri wa kwenda na kurudi bure, nyumba Bure, Basi kila siku nilihudhuria Ibada.

Kiongozi wetu kwenye upande wa Camera alikuwa anaitwa Max. Nilimfanya Max kuwa rafiki. Ndani ya muda mfupi nilihakikisha watu wengi wananizoea. Kanisa lilikuwa na siku za Michezo, ilikuwa ikifika siku hiyo naingia uwanjani kucheza mpira wa miguu. Nilikuwa najitahidi kucheza kweli kweli. Uwanja mzima nakimbiakimbia tu. Macho yangu yote yalikuwa kwa washua. Nikaanza kujipendekeza kwa watoto wao. Kupitia Kanya niliwazoea watu wengi pale Kanisani mpaka watu wakaanza kuhisi na date na Kanya hata kabla sijaanza hizo harakati.

Kanya alikuwa anapenda sana kupiga story na mimi. Ukweli hapa ndo kidogo nilianza kuinjoi maisha ya South Africa. Nilikuwa nakaa na watu ambao hata nikitembea nao barabarani nina amani.

Nilichokuwa nafanya muda wa mchana ambao nakuwa free, Kwa kutumia ile Akiba yangu nilikuwa natoka mwenyewe nakwenda mpaka Johanesburg kutembea tembea, Nilikuwa nashuka pale MTN Taxi Rank huyo naingia Mitaani. Nilikuwa nasambaza Barua zangu za Maombi ya Kazi. Niliomba kila aina ya Kazi ilmradi tu iwe ya halali. Nakumbuka niliendaga mpaka sehemu inaitwa Auckland Park, Sehemu ambayo kuna Media mbalimbali kubwa kama SABC, BBC na Media 24. Kwa kuwa nilikuwa najua kidogo mambo ya Camera, kote huko niliacha Barua zangu. Pale BBC nilikutana na Jamaa wa BBC Swahili, Nilikutana na Mzee Anaitwa Omary Muktadha. Hapa nitarudi kufafanua zaidi huko mbele. Kwa hiyo nikawa nafanya hivyo kila nikiwa free nakwenda maeneo mbalimbali, nilikuwa siogopi, nakwenda kwenye maviwanda huko.

Nirudi kwa Thomas, Thomas alikuwa ni mpiga Kinanda pale Kanisani, alikuwa hajui kama Kanya aliniambia kila kitu kuhusu Chumba tulichokuwa tunakaa kama kinalipiwa Kodi na Kanisa. Nashangaa siku moja nimeamka zangu Thomas ananiomba hela ya Kodi. Nikamwambia mbona nimeambiwa hapa Kodi inalipwa na Kanisa, alivyojua najua kila kitu, akaanza kuwa ananuna nuna bila sababu. Hakuna tabu kama kuishi na mtu ambae asubuhi anaamka amenuna bila sababu. Mtapiga story pale atakapojisikia yeye kuongea. Alikuwa Mjinga kweli yule jamaa. Kwa kifupi Thomas alitaka kunipiga hela Kupitia hicho chumba, Chakula tu ndo mtu ulikuwa unajitegemea.

Nilikuwa natumia Akiba yangu nanunua chakula cha kutosha naweka ndani nakuwa najipikia tu. South Africa chakula bei rahisi. Kule gharama kubwa ipo kwenye Kodi za Nyumba na Nauli kwenye vyombo vya Usafiri. Kule Umbali wa Makumbusho mpaka Posta, Kwa Taxi zao, Kule ukisema Taxi ndio Daladala, unaweza kulipia hata Elfu 2 mpaka 3 za Kitanzania. Hiyo ni nauli ya kwenda tu.

Sasa Thomas alikuwa hanunui chakula. Yeye alikuwa akirudi akikuta chakula anakula tu. Tena wakati mwengine alikuwa anakuja kula na rafiki zake. Wakiwa na hela hao walikuwa wanaenda kula KFC, Hakikosa hela anarudi kula nyumbani. Mimi nanunua chakula kwa bajeti zangu. Nilikuwa navumilia ivo ivo tu siku ziende nitimize malengo yangu.

Mara nyingi Kanya alikuwa anakuja pale ghetto, ananisaidia kupika, kufua na kufanya mambo mengine. Kanya alikuwa mzuri na halafu alikuwa na Bonge la Tako.Yan bonge la Shape. Ila mimi ni kama vile nilikuwa namkwepa kwepa kwa sababu mle Kanisani kuna demu nilishamuona, huyo demu huwa anakuja na gari yake, halafu anaonekana kama matawi fulani hivi. Nilikuwa namkwepa Kanya ili asije kuniaribia kumpata huyo mtoto, Kanya alikuwa anaishi kama mimi tu kwenye nyumba inayolipiwa Kodi na Kanisa. Niliona nikianzisha nae mahusiano atakuwa mzigo kwangu, wakati mimi nilipanga kuwa mzigo kwa mtu mwengine.
Lakini Kanya aliniganda kinyama.
Hahaha [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Kanya alikuwa ana, anazingua.
 
Hivi Kuna mtu anaeza kutoka nchi mwake akaja hapo bongo kutafuta maisha?
Wapo
Mfano yule jamaa wa samakisamaki
alihojiwa na salama
Ali kuja bongo hata kiswahili hajui alimfuata rafiki tu mbongo aliyeishi kwao spain
Akaishi zanzibar akajua kiswahili a kahamia dar
Pia wapo wa somali wengi tu kariakoo, wakongo warundi
Achana na wachina wengi wa nafanya biashara ya jumla kariakoo
Na siku hizi kuna waturuki
Ila nadhani nchi zinazozungumza kiingereza na zina uzungu mingi kama sauzi zinavutia wageni kuhamia
 
Wapo
Mfano yule jamaa wa samakisamaki
alihojiwa na salama
Ali kuja bongo hata kiswahili hajui alimfuata rafiki tu mbongo aliyeishi kwao spain
Akaishi zanzibar akajua kiswahili a kahamia dar
Pia wapo wa somali wengi tu kariakoo, wakongo warundi
Achana na wachina wengi wa nafanya biashara ya jumla kariakoo
Na siku hizi kuna waturuki
Ila nadhani nchi zinazozungumza kiingereza na zina uzungu mingi kama sauzi zinavutia wageni kuhamia
Aha achana na hawa wahindi hawa wapo tu ila mataifa mengine sijawahi kukutana nao ..kama wapo basi wabongo hatuoni furusa hadi na jamaa wa nakuja labda na mitaji pia inachangia.
 
SEHEMU YA SITA

Ile Asubuhi kabla ya Safari kuanza, Kuna wadogo zetu kama 4 wa umri kama wa Miaka 16/17/18 walipanda ndani ya Bus. Waliomba kwa Konda kuongea na Abiria. Walituambia kuwa na wao wanaelekea South Afrika ila nauli zao ziliishia pale Tunduma. Waliomba tuwachangie Nauli.

Wametokea Dar ila wamekaa pale Tunduma kwa muda wa wiki nzima wakitafuta nauli ya kuendelea na safari. Kwa hiyo walikuwa wanaomba tuwachangie nauli ili waweze kuendelea na safari. Tulianza kuwachangia, Mmoja wao alikuwa na simu akaiuza mle ndani ya Bus. Madogo walikuwa wamechangamka sana. Mpaka wanakwenda South kwa nauli za kuunga unga. Wenyewe kutumia Mwezi mzima njiani ni kawaida tu.

Akiba waliyokuwa nayo, pamoja na Michango yetu waliweza kupata nauli ya kuwafikisha mpaka Harare. Walisema wakifika Harare watakaa tena wiki nzima wakitafuta nauli ya kuendelea na safari. Hivyo tuliendelea nao na safari kwenye bus letu. Kwa kifupi mbele ya safari katika kupiga piga nao story tulikuja kujua kwamba kati ya wale madogo, mmoja wao ndio kiongozi wao, yeye alishawai kuishi sana South Afrika. Ilionekana kila akirudi kwao Manzese Tanzania, wakati wa kuondoka huwa anachukua Vijana wengine anaenda nao South. Yani kwa zile story za Madogo nilijiona kumbe ni mim tu ndo sijafika South Africa, Kwa maelezo yao ni kama vile Vijana wengi wapo huko tayari.

Ni kweli kwa pilikapilika za Vijana niliowaona pale Tunduma niliona ni kama Vijana wengi sana wanaikimbia hii nchi, kila mmoja akilalamika kuwa Bongo Maisha magumu.

Staili ya hawa madogo kusafiri ni ya kuunga unga nauli, hawa madogo walivyofika Tunduma walikaa hapo, sidhani kama Kuna namna nyengine walifanya ili kupata nauli zaidi ya wizi. Na wapo madogo wengine wengi wa staili hii.

Pia pale Tunduma sio Waburundi wote walifanikiwa kupita, kuna baadhi walikosa pesa ya kulipia Visa ya kuingia Zambia. Sisi watanzania tunaingia Zambia bila kulipia Visa. Hivyo waburundi ndani ya Bus walipungua

Kila tulivyokuwa tukiendelea na Safari ndivyo Lugha yetu pendwa ya Kiswahili ilivyokuwa ikipotea. Tulifika Lusaka Mji Mkuu wa Zambia saa tatu usiku. Tulilala hapo. Wengine tulishuka kwenda kupata Huduma za Chooni, Wengine ndo ilikuwa mwisho wa safari yao. Asubuhi kulivyokucha tuliendelea na safari yetu ya kuelekea boda ya Zambia na Zimbabwe inaitwa CHIRUNDU
Patam Apo🤣
 
Back
Top Bottom