Valencia_UPV
JF-Expert Member
- Mar 31, 2016
- 6,974
- 8,750
Watoto wa south Wana nundu balaa. Nilikaaga Pretoria nikawa nashinda zile restaurant za kwenye malls Ni kwikwi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwaio keagan upo wapi saaiv maan ulipewa permit ya mweziWakuu leo naomba kuleta Story yangu ya kweli ya jinsi nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu kule wala mtu wa kunipokea.
Ukweli kuna wakati ilifika nilichoka sana maisha ya hapa nyumbani, ilikuwa Mwaka 2014, nilikuwa napitia changamoto nyingi za maisha hasa katika familia. Ukweli akili ilikuwa imechoka sana ilisababishwa na kutokuwa na ajira muda mrefu.
Hata baadhi ya watu sikuwa napenda kukutana nao sana. Nikajiuliza kwani Maisha ni hapa tu nyumbani? kwani hakuna sehemu nyengine? Nikajisemea labda sikuandikiwa kutoboa hapa nyumbani ngoja nikajaribu bahati yangu sehemu nyengine.
Kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda South Africa, Kwanza niliwaza kujaribu bahati yangu Marekani, nina ndugu kama watatu huko. Nikamcheki ndugu yangu mmoja akanitumia Invitation Letter. Nikaanza kupambana pale Ubalozini. Nilifika kwenye Usahili lakini nilikosa VISA.
huyu jamaa mwongo alikuwa anatafuta kick tu watu wakafukua mafaili, akatoka nduki kujiokoaKwaio keagan upo wapi saaiv maan ulipewa permit ya mwezi
Anampasua Tanya kwa mara nyingine.Jaman huyu jamaa ndio amepotea kbs
Mwanangu wewe ni LegendWatoto wa south Wana nundu balaa. Nilikaaga Pretoria nikawa nashinda zile restaurant za kwenye malls Ni kwikwi
Tanya Kama TanyaJamaa katutelekeza paspo kutegemea
Hapa JF inatulindaje dhidi ya faragha hizi ni ukiukaji wa maadili wa haki ya kuona
PSEHEMU YA NANE
Ukweli ndugu zangu moja ya kitu nilichojifunza kwenye Safari hii sio kwamba ukifika kila boda basi unakimbilia kutoa pesa. Unatakiwa kusoma kwanza upepo wa Boda husika.
Kwenye hii boda ya BeitBridge tulikosea kwa sababu pale Kaunta kulikuwa na Mkaburu. Wazoefu wanasema ukikuta pale Kaunta amekaa Mkaburu basi usikimbilie kutoa rushwa. Sababu wanasema Mkaburu hapendi sana watu weusi, hivyo ukianza tu kutoa rushwa ndo anapata sababu ya kutokukuruhusu kuingia nchini mwao.
Basi Mimi namshukuru mungu yule Mkaburu akaniangalia kisha akanigongea mhuri. Nakumbuka alinipa Mwezi mmoja tu wa kukaa South Africa. Wenzangu walipewa Wiki mbilimbili. Jamaa zangu waliniambia Mimi nilipewa Mwezi mmoja sababu yule Mkaburu aliona Passport yangu haijawai kugongwa Mhuri wa Africa Kusini. Wao walipewa siku chache kwa sababu Passport zao zishagongwa sana Mihuri ya Afrika Kusini.
Mpaka tunarudi kwenye Bus yule Jamaa etu walikuwa bado wamemshikiria. Tuliondoka tukamuacha pale, tena hata namba za simu tulikuwa bado hatujapeana. Mpaka kunakucha tulikuwa bado tupo njiani.
Ahamad aliniambia kama sina sehemu ya kufikia basi nishuke nae Pretoria. Kwa sababu Bus kabla ya kufika Joberg linafika kwanza Pretoria. Ahamad akasema tushuke wote hapo atanitafutia sehemu ya kukaa kwa jamaa zake ambae ni wabongo. Matlida yeye alikwenda kushukia Mwisho wa Bus kule Power House Karibu na Park Station Joberg.
Mimi na Ahamad tulishuka pale Pretoria kama saa Nane mchana. Ukweli nchi ya wenzetu ni nzuri sana.
Nilikuwa natembea huku najiuliza "Kama hapa pako hivi huko Ulaya na Marekani patakuwa vipi?" Watu wanajua kujenga nchi zao.
Ahamad alikuwa na miaka kama mitano toka atoke South hivyo tulivyoshuka tu tukawa tunapita mitaa Fulani ya washkaji zake anakwenda kuwasalimia. Mimi nipo nyuma yake tu. Nakumbuka tulikwenda mpaka mitaa Fulani kuna Wazanzibar wengi wana maduka. Tukaacha hapo mabegi yetu. Mimi nilikuwa sina imani kuacha hapo Begi langu lakini kwa kuwa ATM Card yangu ilikuwa mfukoni nikasema sio mbaya, kilichokuwa kinanipa wasiwasi peke yake ni vyeti vyangu vyote vilikuwepo ndani ya Begi. Ukishaamua kujilipua inabidi uwe na roho ngumu.
Tulivyofika hapo Pretoria ndo nikajua kuwa kumbe Ahamad alikuwa anaendelea na Safari ya kwenda Capetown. Hapo alikuja kukutana na Dada yake ambae wangekwenda wote Capetown kwa ndege. Huyo Dada yake alikuwa ameolewa huko Capetown na Tajiri mmoja. Maelezo yote hayo alinipa Ahamad mwenyewe.
Tukaenda mahali kukutana na Huyo Dada yake, naye ni Mtanzania. Nakumbuka alikuja na Range Rover mpyaa, tukaingia ndani, kisha Ahamad akanitambulisha kwa Dada yake. Dada yake akasema kwa kuwa wao walikuwa wanawahi kupanda ndege basi Mimi ataniacha kwa rafiki yake.
Hao mpaka kwa huyo rafiki yake, tulivyofika kwa huyo rafiki ake, Dada yake na Ahamad akaniuliza "Unamjua huyu". Mimi nikamjibu hapana simjui. Nikawa namwangalia vizuri yule Mrembo ambae nimepelekwa kwake. Nikajiridhisha kuwa simjui.
Dada yake na Ahamad akasema "Huyu ni Vailet, yule Video Queen kwenye Wimbo wa Matonya, ule wimbo wa Vailet, huyu ndo Vailet mwenyewe"
Duh nikabaki nimeduwaa tu, demu amekuwa mrembo kinoma noma. Kumbe Alishakimbiliaga South Afrika Kitambo sana. Wakuu ukitaka kumkumbuka vizuri huyu demu unaweza kuingia YouTube, Video ya Matonya wimbo wa Vailet, ndo huyo demu mule ndani. Mimi nikaachwa pale. Ahamad na Dada yake hao wakaondoka kuchukua mabegi wakaniletea Begi langu kisha wenyewe wakasepa Capetown.
Wakati wa jiwe watz walipata heshima nchi nyingi ukisema mtz tu unaeshimika hata SA maana jpm alikuwa anakubalika sana ,ndiyo maana alipo tua SA uwanja wote ulimshangilia hivyo acha upumbavu ,kipindi cha kikwete ilikuwa ukijitambulisha tu mtz unapigwa sachi hadi matakoni na vadole wanajua unasafirisha ngadaJiwe lingeendelea kuwepo, wengi mgekimbia nchi pamoja na kwamba lilikuwa linawapumbuza muonekane lina wajali kumbe ndio linapiga pini ya ukakika
Hujui unachoandikaWakati wa jiwe watz walipata heshima nchi nyingi ukisema mtz tu unaeshimika hata SA maana jpm alikuwa anakubalika sana ,ndiyo maana alipo tua SA uwanja wote ulimshangilia hivyo acha upumbavu ,kipindi cha kikwete ilikuwa ukijitambulisha tu mtz unapigwa sachi hadi matakoni na vadole wanajua unasafirisha ngada
Wewe ccm usije huku kwenye huu uzi kwani si nyinyi mnaosababisha watu kujilipua kimaishaHaya maisha kila MTU ana taka kuwa mzigo wenye manufaa... Ungewachngamkia wote... Ukiteleza nao unapata nafuu hata ukikosa sehemu ingine fresh utarejea kujibebisha na madevu yako *****... Maisha nyoso sana
Kwani ukumsikia kuwa wanalala masaa machache hao jamaa ,pia unaweza kuwa tajiri na ukafanya kazi kama punda kwani ukumwona jpm alivyokuwa anafanya kaziMkuu mtoto wa mstaafu, Keagan Paul, naomba uniruhusu nicomment kidogo. Kuna vitu kwenye stori yako havipo sawa kidogo, naelewa huenda labda umeamua kuvifanya visiwe sawa kwa maksudi na si kwa bahati mbaya. Kuna sehemu nimekusoma unasema wale jamaa wanaomuuzia "nyaupe" jamaa Y wanafanya kazi kama punda. Hapo mzee umepindisha ukweli, Dizonga hakuna wabongo wanaokula bata kama wauza nyaupe. Kufanya kazi kama punda kwako wewe labda kuna tafsiri gani? Maana hao jamaa kazi yao ni kupokea simu tu na kupeleka mzigo location unapohitajika na akifika pale ni kitendo cha sekunde mbili keshamaliza kazi, haina hata kuhesabu hela, hela itahesabiwa baada ya kuondoka eneo la tukio, na wale wanunuzi ni waamifu sana hawatoi hela pungufu japo hamuhesabiani eneo la tukio. Zaidi ya yote jamaa wana usafiri hawasambazi kwa miguu, hata kama mtu ameanza kuuza leo haiwezi kumchukua zaidi ya mwezi hajapata usafiri, sasa unaposema wanafanya kazi kama punda kidogo kama umepindisha uhalisia. Pia umesema huwa wanaweka hizo kete mdomoni na polisi wakivamia wanazimeza, mzee hii pia sio kaka. huwezi kumeza madawa kizembe hivyo. Donga ndio zinamezwa wakati wa kuzisafirisha intercontinental lakini sio mzigo umeshafika ndani ya nchi bado mtu ameze. Hiyo risk hakuna mtu wa kuitake, kwanza ufungaji wa hizo kete sio imara sana uimeze halafu ubaki salama. Ufungaji wa donga ndio imara unaweza kumeza na ukasurvive lakini sio kete mkuu. Halafu mademu wa Gauteng yaani Joburg na Pretoria wana attitude flani tofauti na uliyoielezea tena kama hapo Midrands ndio kabisa. Nimekaa Randburg kama miaka 6 au 7, 209 Bellairs Drive, Banbury Cross, North Riding. Randburg nadhani kwa Johannesburg ni sehemu wanayokaa matajiri wa South Africa ukitoa Sandton na Fourways. Ninachotaka kusema hapa mademu wa kishua wa Gauteng nazijua attitude zao maana nimeishi nao. Pia umesema permit (viza) yako iliexpire ukiwa bado kwa bwana Y, sasa uliwezaje kutafuta kazi wakati tayari ulikuwa unaishi kinyume cha sheria maana kitu cha kwanza lazima wakuulize ID yako. Mind you Johannesburg na Pretoria ni miji ambayo kama huna permit ni ngumu sana kusurvive. Joburg hata ukiwa unatembea barabarani unaweza kushitukia tu unasimamishwa na police na kuombwa ID tofauti na miji mingine kama Durban, sasa wewe uliwezaje kutafuta kazi wakati hata permit yenyewe huna? sijui kama umenielewa? Na kwa Johannesburg misako ya kutafuta wahamiaji haramu ipo kila uchwao.
Sijui nini wakati hata bungeni wabunge walisha sema hiki kitu na passport yetu ikapanda thamani sana tu ,Hujui unachoandika