Nilivyonasa kwenye lift jengo la Kitega uchumi kwa masaa 2 bila msaada. Ingekuwa Ulaya au Marekani ningefungua kesi ya kudai fidia

Nilivyonasa kwenye lift jengo la Kitega uchumi kwa masaa 2 bila msaada. Ingekuwa Ulaya au Marekani ningefungua kesi ya kudai fidia

1. Ungetoa ushahidi gan usio na Shaka mahakamani? Je ulisaini sehemu wakati unaingia kwenye jengo/lift?
Swali muhimu sana
Nimeona wabongo wengi wakiingia majengo makubwa, hakuna utaratibu wa kuandikisha, kama mgeni, pale reception, watu wanaiingia tu kiholela, hata moto ukitokea ukachomeka humo, hakuna atakaye jua ni nani?
Au chochote kitakacho kutokea hakuna ushahidi ulikuwa ndani ya jengo kufanya nini ?
 
Pole sana Mkurugenzi.... Lift hizi Huwa zinaogopesha sana.... Nikiingiaga Huwa nawaza mara mbilimbili....

Kingine Huwa nawaza, vipi ikiporomoka downward! Yaani ifyatuke kushuka chini.... Lahaulaaa....
Kuna minyororo huwa inazishikilia ni ngumu kukatika na ingekuwa inakatika ovyo ingekuwa balaa
 
Pole sana zile lift ni balaa sanaa....hengo mojawapo kuanza luft jijini dar.....miaka 80 nilipelekwa pale ili kupanda lift tukienda salimia ndugu huko Bima.....!! Pale chini under ground kuna hotel.nzuro ya gharama hivi tulipata lunch na mzee.....maisha safari ndegu sanaaa
 
Kabisa ni jana juzi tu lakini muda umepita aswaa
 
Mimi pumzi ya kupanda ipo ila ya kufungiwa sehemu siwezi kabisa nina claustrophobia
Najichunga sana na sehemu kama daladala, lift, sehemu yeyote isiyokuwa na hewa ya kutosha
Hata crime naogopa nisije kwenda jela 😄
Mungu akulinde jela sio poa kabisa kana unatatizo kama lako
 
Mwaka 2001 nilitoka zangu Temeke studio za Soundcrafters kwa Enrico kuchukua single yangu niipeleke Clouds.

nikapitia IFM kwa mpenzi wangu wa kipindi hicho tukapata dinner,ilikuwa mishale ya saa mbili usiku,marehenu Steve B alinipa maagizo kuwa hiyo CD niiache kwa dada flani nadhani ilikuwa floor ya 7,la haulaaaa,kufika floor ys tatu lift ikazima,niko mwenyewe tu,niliyepanda nae alishuka floor ya pili.

Nilijaribu kuiachanisha kwa mikono wapi, nikajaribu kupiga mlango wapi,simu yangu siemens 25 imeshaisha chaji sina ujanja,nikaanza kupiga kekeke wapi,nikabonyeza kengele ya dharura wapi sipati msaada,nikaamua kukaa chini kusubiri muujiza,hapo Oxygen inazidi kuisha,kijasho kinanitoka,nikavua shati nikajaribu tena kupanua mlango nikafanikiwa kwa kiasi cha kupitisha kiganja tu,nikavua kiatu changu na kukiweka jatikati ya milangi ilihewa iingie huku nikisikilizia kama kuna mtu atapita au kushuka hiyo floor,

Mungu si athumani nikasikia mlango wa lift jirani unafunguka ndio nikapiga kelele ya kuomba msaada,yule mshangazi sijui alifanyaje nikaona wanakuja technician na kufungua mlango.

Ile CD nilisahau mulemule Kwenye lift nikarudi zangu nyumbani hapo ni saa nne usiku.Niko tumbo wazi mpaka maeneo ya Steers ndio nikakumbuka kulivaa

Baadae nikafuatilia kopi ya ile single yangu studio,nikaipeleka tena Clouds safari hii kwa tahadhari zote, ule wimbo ulipigwa mara moja tu nikajua nyota njema huonekana asubuhi.

Ingekuwa nchi za watu OTIS watengenezaji wa lift wangenilipa mamilioni
Is there any Disclaimer Notice that placed at front of the Main Entrance Gate???
 
Wazungu sio wajinga, unachowaza wao walishawaza siku nyingi...hata ikatike hiyo free fall haipo inagota hapo hapo!
Hapana mimi pia nilishakwama kwenye lifti nilikuwa natoka floor ya kumi ilikwama kisha ikashuka kwa speed na kubamiza chini. Pale maeneo ya Morocco karibu na jengo la airtel. Niliimba nyimbo zote za dini.
 
1. Ungetoa ushahidi gan usio na Shaka mahakamani? Je ulisaini sehemu wakati unaingia kwenye jengo/lift?

2.. OTIS wanahusikaje hapo? Ngumu Sana kuishtaki kampuni na ukashinda ukizingatia Kipato chako hoi bin taabani.
Kuna kitu kinaitwa Occupiers liability. Angweza kufungua kesi ya fidia dhidi ya mmiliki wa jengo.

P.s. kwanini unasema ungekua "ulaya"? Siku hizi utamaduni wa kudai fidia umekua sana Tanzania. Na mahakama zimetoa fidia case nyingi mno.
 
1. "Occupiers liability" unataka ushahidi pia ndugu.

2. Angethibitishaje kuwa alikua ndani ya jengo kihalali na sio mwizi? Alikua na appointment (maandishi yaliyotaja siku, tarehe na muda ya mpangaji halali) kwenye hilo jengo au mwenye jengo?
 
Mkuu majengo ya biashara hakuna haja ya kuonesha ulikuwepo kihalali. Cha muhimu alikuwepo, maana kama jengo ni "public" lazima watu watalitumia kwa issue mbali mbali. Ingekua jengo la mtu binafsi sawa.

Ingetosha kuonesha ushahidi alikuwepo humo ndani ya lifti.
 
Mungu akulinde jela sio poa kabisa kana unatatizo kama lako
Amina, namshukuru Mungu sijawahi kufanya kosa hata la traffic offense
Jela mbaya aisee
Ningekuwa badala yako kwenye lift siku hiyo ningekufa maana ina kupa woga sana na kutapatapa
Ila hata home lazima dirisha moja liwe wazi hata kama kuna barafu na ni -5 nje
 
Back
Top Bottom