Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

hii ndio story pekee ilifaonikiwa kufika tamati .umughaka vipi zile bima za afya bado ipo kiunoni?
 
Umeona maeneo yako hayo
Screenshot_2022-11-15-18-17-08-252_com.google.android.apps.maps.jpg
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 20.



Gari ilitembea tukaikamata njia ya Sirari,sasa tukawa kama tunaelekea Musoma.Yule jamaa akamwambia yule demu aliyekua akiendesha gari ya kwamba inapaswa tuweke kituo kwanza Lamadi tukapate msosi kisha ndiyo tuondoke.

Baada ya kufika lamadi na kupata Msosi tuliondoka kuelekea Bariadi,sikuwahi kufika bariadi ni hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika huko,sasa baada ya kuiacha bariadi tulianza kuingia vijijini huko ndani ndani ambako sikuvifahamu kwa haraka maana sikuwa mwenyeji huko.

Kituo chetu cha mwisho kilikuwa kwenye kijiji cha Mwanaungu ambako baada ya kushushwa hapo,yule jamaa alimwambia yule demu kwamba amsubiri kwanza atupeleke halafu waondoke!.

Mtatiro "Mwanangu kwahiyo mnatuacha?"

Jamaa "Tutarudi kuwachukua ondoa shaka!"

Tulitembea kwa umbali mrefu kidogo hatimaye tukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa umezungushiwa minyaa ya kutosha,baada ya kufika hapo tulikuta kuna vijumba vingi vya nyasi huku kukiwa na watu ambao wengine walikuwa wamelala kwenye majamvi huku wengine wakiendelea na shughuli zao!.Kuna mwanamke akaja kutupokea kwa salamu ya kisukuma huku akipiga magoti,sasa mimi kwakuwa nilikaa usukumani kwa kipindi fulani wakati baba yangu mdogo akiwa headmaster,ile salamu haikunipa taabu kabisa!,na siyo salamu tu,naweza kukizungumza kisukuma ingawaje cha kuombea maji!.

Baada ya ile salamu yule mwanamke alituletea viti ambavyo havikuwa na watu kwa wakati huo.Basi baada ya muda mfupi yule mwanamke akaja na daftari akatutaka kila mmoja wetu kutaja jina lake na kuandikwa,sasa tulipoandikwa akatuchania vikaratasi vikiwa na namba,mimi nilipewa namba 16 na Mtatiro akapewa namba 17,yule jamaa yeye akamwambia yule mwanamke kwamba anahitaji kuonana na Mwami(Ng'wana Mwami).Yule mwanamke akamtaka asubiri kwanza.

Baada ya muda yule mwanamke akaja akamuita yule jamaa akampeleka mpaka kwenye kinyumba cha nyasi kilichokuwa kikubwa kati ya vile vinyumba tulivyovikuta pale.Baada ya muda yule jamaa akatoka akaja akatuambia angerudi baada ya siku mbili,hatukujua alipoingia mle ndani alienda kuzungumza kitu gani na huyo aliyekuwa humo ndani!.Jamaa aliondoka akatuacha pale,hiyo ilikuwa mida ya mchana saa 7.

Ilipofika mida ya saa 10,kuna mwanamke alitoka kwenye kile kijumba huku akijinyoosha kana kwamba alikuwa amechoka sana!.Alianza kuwazungukiwa watu kadhaa waliokuwa pale nje huku akiongea nao kisukuma na kiswahili!.Alipofika kwetu alitusalimia kisukuma na kama kawaida nami nilimuitikia kisukuma,sasa Mtatiro halikuwa haelewi kabisa hata salamu ndipo nilimwambia yule mama ya kwamba mwenzangu haelewi kisukuma,aliamua kumsalimu kiswahili kisha akaendelea na watu wengine!.Yule mama ndiye aliyekuwa mwenyeji wetu na alikuwa mganga!.

Mtatiro "Mwanangu kisukuma kumbe unakipiga fresh"

Mimi "Nimekaa nao,dingi yangu mdogo alikuwa headmaster shule moja huko Tabora hivyo nilikinyaka kiasi fulani"

Ilipofika mida ya saa 12 jioni kuna watu takribani 7 ambao walikuwa wanaume 3 na wanawake 4 waliingia pale nyumbani huku wakiwa wamebeba majembe,mimi nilidhani ni ndugu tu wanaoishi hapo kumbe walikuwa wateja wa huyo mama.Sasa utaratibu ulikuwa ni kwamba,unapofika kwa huyo mama unapewa namba kama sisi tulivyopewa,wakati ukiendelea kusubiri ili namba yako iitwe ilipaswa kila kunapokucha ukamate jembe umfuate mwenyeji akakuelekeze shamba la kulima na ulikuwa unapewa kipande chako ili upambane nacho,na kipande chenyewe hakikuwa cha kitoto,yaani kama ukimaliza kile kipande ndipo unaambiwa sasa umekolifai kupatiwa matibabu na yule mama.Sasa wakati unasubiri matibabu ndipo mnaitwa kwa namba ambazo hata sisi tulipewa.(Yule mganga alikuwa mjanja sana,badala ya kulima mashamba yake,sisi wapumbavu ambao tulifahamika kama wateja wake ndio tuliomlimia wakati yeye akiwa ametulia nyumbani,Daaah![emoji23][emoji23],na kila mtu aliyefika hapo kwake ni lazima ilikuwa akamatishwe jembe aingie shambani![emoji23][emoji23]).

Mimi na Matatiro tulikomaa na vipande vyetu ambavyo tulivianza siku iliyofuata kwasababu siku tuliyofika tulikuwa tumechelewa,bahati nzuri ilikuwa ni palizi na hakukuwa na nyasi sana!.Siku hiyo tulipomaliza kupalilia lile shamba ilikuwa mida ya saa 9 alasiri,tuliporudi hapo nyumbani kiukweli tulikuwa tumechafuka miguu na kunuka majasho hatari,sasa nilimfuata yule mama aliyetupokea siku ile nikawa nimemwambia atupatie maji ili tuoge,alituambia inapaswa tuwasubiri wenzetu ambao nao walikuwa hawajamaliza sehemu zao ili tupate chakula kwa pamoja kisha ndio tuoge!.

Wale walipotoka huko shambani,tulitengewa ugali wa udaga kwa na furu wa kuchemsha.Sasa tulipaswa kukaa watu watatu watatu kwa ajili ya chakula,mimi nilikaa na Mtatiro kama kawaida pamoja na jamaa mmoja ambaye alikuwa mteja kama sisi!.Siku hiyo ikapita kapa bila kuitwa namba lakini kuna watu wao waliitwa wakaendelea kupewa huduma kama kawaida!.

Siku iliyofuata tukaitwa majina watu kama wanne,sasa kwakuwa mimi na Mtatiro tulikuwa na shida moja ilibidi tuambiwe tusubiri kwanza amalizane na wale wa wawili.Zamu yetu ilifika na tukaitwa ndani kwa yule mama,hatukujieleza hata kidogo bali tulipoingia ndani alitutaka tuvue shati ili kitendo cha kupigwa chale kuchukue nafasi!.

Yule mama alitupiga chale kwa kutumia kisu kilichokuwa kikali kama wembe,alituchanja kila sehemu aliyoona yeye inafaa,baada ya hapo alituchanja pia kwenye ulimi kila mtu!.Alipomaliza kutuchanja na kutupaka dawa,alichukua kitu kilichokuwa kimefungwa na kukazwa sana na kutakiwa kila mmoja akivae kiunoni,ile alituambia ni irizi na asije akatokea mtu akaivua,alisema endapo ikitokea ukaivua basi usije ukamlaumu!.

Mpaka wakati huo hatukufahamu kwa huyo mganga tulipelekwa kufanya nini,ingawa tuliambiwa tunakwenda kutengenezwa ili hatukujua utengenezwaji ulikuwa na faida gani katika ile kazi yetu mpya ambayo tungeianza siku chache zilizokuwa mbele yetu!.

Yule mama alituambia ya kwamba,ile irizi haikupaswa kabisa kutolewa kiunoni hata iweje. Basi baada ya kumaliza ile shughuli tulitoka nje tukaendelea kumsubiri jamaa aliyetuambia angekuja kutuchukua!.Ile siku jamaa hakutokea kabisa,hivyo ikatubidi tulale tena kwa yule mama.

Yale mazingira yalikuwa ya hovyo sana lakini ilibidi tukubaliane na hali kwasababu tuliitamani pesa!.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi ya siku iliyofuata yule jamaa alirudi kutuchukua na kisha tukaondoka,sasa tulipoingia kwenye ile Noah tulikuta kuna mabegi kadhaa na kulikuwa na jamaa mmoja akiwa amekaa siti za abiria,dereva alikuwa ni yuleyule demu ambaye alikuwaga azungumzi na mtu!.

Jamaa "Wanangu safari ni moja kwa moja Arusha"

Mtatiro "Kaka mngeturudisha kwanza tukachukue nguo"

Jamaa "Nguo sio sehemu ya kuwazia,utazikuta huko"

Hatukuwa na swali,tuliamua kukausha na safari kuanza.Tulitembea sana na hatimaye tukaikamata lami kuelekea Musoma,baada ya kuivuka lamadi kwa mbele,tukaikamata geti la Ndabaka linaloingia Serengeti.
Yaani niliishia hapa duu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko hapa sirari stand ya kwenda tarime na borega natamani kukuulizia Umughaka lakini ndio hivyo
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 22.


Tuliondoka na gari lile eneo kuelekea ambako tuliambiwa tunakwenda kuchukua pesa ya Bosi.Ile gari baada ya kutembea kwa umbali mrefu hatimaye ilisimama kando ya barabara ya vumbi na ndipo yule jamaa(Jipe)akatutaka tuteremke!.

Jipe "Katusubiri pale mbele ya lile karavati"

Jipe alimwambia yule dereva azime taa kisha akatusubiri kwenye karavati lililokuwa mbele!.Jamaa aliongoza na sisi kumfuata nyuma,mtatiro na Jipe ambao walikuwa na silaha,walikuwa wamevaa makoti marefu ambayo yalifanya zile silaha walizokuwa nazo kutokuonekana kwa urahisi!,sasa baada ya kutembea kwa umbali mrefu kidogo hatimae tukafika kwenye nyumba moja ambayo haikuwa na geti wala fensi!,jamaa alisogea hadi mlangoni akaanza kusukuma ule mlango kana kwamba ulikuwa wazi,baada kusukuma ule mlango na kuzunguka ile nyumba,jamaa alitoa simu akampigia Gabi,baada ya mazungumzo jamaa alitwambia tuondoke haraka maana kumbe tuliingia chaka,eneo lililokusudiwa halikuwa hilo!,tulitembea kwa haraka kuifuata ile gari na hatimaye tukaianza safari kuelekea kulipokusudiwa!.Wakati huo wote mimi sikuwa na silaha zaidi ya kuwafuata nyuma Jipe na Mtatiro ambao wao ndio walikuwa na Silaha!.

Baada ya safari ya dakika kadhaa tukawa tumefika kwenye eneo ambalo lilikuwa na nyumba kadhaa ambazo ilionyesha kabisa walioishi eneo hilo walikuwa na vyanzo vizuri vya Mapato.

Jipe "Kila mtu ajifunge vitambaa"

Aliendelea "Nitakachosema ndicho mtakachokifanya"

Sisi "sawa"

Tuliteremka kwenye ile gari tukaanza kutembea kuelekea kwenye nyumba iliyokusudiwa;Lile eneo lilikuwa limetulia sana kwa wakati huo maana ilikuwa yapata mida ya saa 7 usiku.Tulipofika nje ya geti Jipe alipanda ukuta akawa ameruka kwa ndani,sasa wakati jamaa akiwa ndani nikasikia sauti ya mbwa akibweka kwa nguvu sana,jamaa hakutaka kupoteza muda,nilisikia sauti ya risasi ikipigwa na yule mbwa sikumsikia tena!.

Jipe "Ingieni ndan"

Jipe alituambia kwa sauti kubwa iliyoonyesha msisitizo,basi tulipanda ule ukuta tukaruka kwa ndani!.Baada ya kuingia ndani ndipo jamaa akawa anaangalia namna ya kufanya ili tuingie ndani!.Jipe alianza kupiga lile geti la chuma kwa risasi hadi likaachia ukawa sasa umebaki mlango wenyewe!.Kiukweli mara ya kwanza nilitaka kukimbia baada ya zile sauti za ile bunduki zenye kishindo kikubwa,nilibaki kumtazama Jipe muda huo ambao hakuwa na mchezo kabisa!.

Sasa nilianza kusikia kwa ndani sauti za watu wakilia na kuomba msaada,mahali ilipokuwa ile nyumba kulikuwa na nyumba nyingine ambazo hakukuwa na mtu aliyetoka nje hata mmoja.Wakati jamaa akipambana ili ule mlango ufunguke tuzame ndani,kuna sauti ya kiume ilikuwa inasikika kwa ndani ikisema "Atakaye ingia huyo ni halali yangu!".

Jipe "Hebu nipe hiyo silaha,kamata hii"

Alichukua ile silaha ya Mtatiro akaanza kupiga risasi kwenye kitasa cha ule mlango hadi ukaachia!.Baada ya kitasa kuachia aliusukuma ule mlango kulekea ndani kisha na jamaa akawa ameingia ndani!.

Jipe "Ingieni ndani"

Tuliingia ndani ambako tulifika sebuleni na hatukukuta mtu hata mmoja,sasa jamaa akamrudishia Mtatiro silaha yake kisha akachukua ya kwake ambayo Mtatiro alikuwa nayo!.Jamaa alikuwa jasiri sana na ilionekana hata lile tukio halikuwa la mra ya kwanza,inaonekana alishayafanya sana yale matukio na ndiyo maana alikuwa akijiamimi sana!.Tulitembea kuelekea vyumbani ambako jamaa alituambia tufuatane nae!.Ile silaha ndugu zangu ioneni tu askari wamebeba lakini ni hatari sana,sikuwahi kabisa kusikia ikipigwa karibu,siku hiyo ndiyo nilifahamu kwanini silaha ni hatari sana hadi serikali kupambana na wahalifu!.Pia ni kitu ambacho ukiwa nacho kinakupatia kujiamini kupita maelezo,namna ambazo jamaa alikuwa akijiamini tulivyofika pale haikuwa na mfano,wewe fikiria ile sauti iliyosema "Atakaye ingia ndani huyo ni halali yangu" lakini hakujali kitu!.

Jipe "Magige fungua mlango mwenyewe"

Aliendelea "Nikifungua mimi umeumia"

Sasa kuna sauti ya kiume ikasikika ndani ya chumba ikiwa inajitetea!.

Sauti ya kiume "Tafadhali nawaomba mchukue chochote msiniue!"

Jipe "Fungua mlango unanipotezea muda msenge wewe!"

Basi yule jamaa aliyekuwa chumbani alifungua ule mlango.Baada ya kufunguliwa ule mlango Jipe aliusukuma kwa mguu kwa nguvu ukawa umejifungua zaidi!.Sasa nilibaki kushangaa kwasababu wakati tukiwa nje nilisikia huyo jamaa akisema atakaye ingia ndani atakuwa halali yake nikadhani uenda alikuwa na silaha kumbe ilikuwa zuga tu!.Tulipoingia ndani tulimkuta jamaa akiwa na mwanamke pamoja na dada mmoja na watoto watatu,wa kike wawili na wa kiume mmoja,jumla yao kufanya kuwa watu sita!.

Jipe "Pesa ziko wapi?"

Aliendelea "Usinipotezee muda nataka pesa"

Jipe "Lale chini sitaki mniangalie wapumbavu nyie"

Baada ya kusema vile,niliona yule mwanamke anawakusanya wanae na kulala chini huku wakifunika nyuso zao chini!.Sasa yule jamaa akawa kama anategea kujibu lile swali la wapi pesa ilipo,Jipe alikoki ile silaha akamtandika ya mguuni yule jamaa akaendelea kulia kwa maumivu makali pale chini.

Jipe " Nimekwambia nataka pesa usinipotezee muda"

Baada ya kuona hali inaweza kuwa mbaya zaidi ndipo yule mwanamke akapiga kelele huku akilia akisisitiza tusiwaue na akaeleza pesa ilipo!.Alinyanyuka tukaongozana nae kuelekea jikoni ambako pembeni kulikuwa na stoo!".

Yule mwanamke "Pesa hiyo hapo chini ya vigae!"

Jipe "Oya hebu funua vigae hivyo utoe hiyo hela"

Niliingia ndani ya kile chumba ambacho kilikuwa stoo nikaanza kutoa vile vigae ambavyo vilikuwa vimewekwa juu ya mzigo kwenye gunia.Nilifanya haraka sana maana hatukutaka kupoteza muda kabisa lile eneo!.Nilipofurumusha vile vigae chini,ndipo nikafikia gunia lililokuwa limejaa manguo ikabidi nilinyanyue nikalitoa mle stoo!.

Nilianza kuyatoa yale manguo yaliyokuwa kwenye lile gunia hatimae nikazifikia pesa ambazo zilikuwa nyingi zimefungwa kwenye mabunda ya elfu tano tano na elfu kumi kumi!.

Jipe "Beba tuondoke"

Nikabeba lile gunia na kuondoka eneo la tukio kuifuata ile Mark 2 iliyokuwa imepaki mbali kidogo ikitusubiri.Tuliondoka yale maeneo kwa spidi kali kuikamata njia ya Mwanza na safari ikaanza.Tulitembea kwa spidi kali hadi maeneo ya mgodi ule wa Buzwagi kisha kuikamata njia ya kuelekea eneo tulilokuwa tumemuacha Gabi,baada ya kufika pale jamaa aliniambia nikimbie haraka kumuita Gabi ili tuondoke.Gabi alitoka ndani kwa spidi kali baada ya kumshitua kisha tukaingia kwenye gari na kuondoka lile eneo.

Jipe "Mwanangu hakikisha risasi inakuwa chemba,hatujui kilichoko mbele yetu"

Mtatiro "Iko sawa tayari"

Ile gari ilikuwa inatembezwa kwa spidi kali huku ikiwa imezimwa taa,sasa kuna mahali tulifika Jipe akamwambia dereva asimamishe gari kwanza,gari iliposimamishwa akaniambia nikae siti ya mbele yeye arudi nyuma akae na Mtatiro.

Jipe "Washa taa tuondoke"

Dereva aliwasha taa na safari ikaanza,sasa tulipofika karibu na tinde,Jipe akatoa maelekezo ya kwamba,endapo kuna mtu akatokea akasimamisha gari ahakikishe hasimami!.

Namshukuru Mungu pale tinde tulipita salama kabisa,sasa tulipofika mbele kabisa kuikaribia shinyanga jamaa akachukua zile bunduki akanyanyua siti walizokuwa wamekalia akaziweka,kisha tukaondoka kwa spidi kali!.Njiani hatukusumbuliwa kabisa.Tuliingia Mwanza mida ya saa 9 usiku hadi kule kwenye ile nyumba siku ya kwanza tulipoenda na Gabi!

Zaidi: Sehemu ya 23
Duu maisha haya.
 
Mwanamke anaeleza haraka haraka hela zilipo wakati mwenye hela hajaamua kusema,na kesho jamaa akiwa amelazwa mwanamke atamuomba hela ya matumizi

Mwanaume
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Yaani nmekuwa addicted mpaka nmeanza kununua vitabu vya Musiba, though ni stori za kufikirika lakn ni muandishi mzuri sana.

Kuna mnyama mmoja anaitwa "Willy Gamba" ni mpelelezi mmoja hatari sana anatumiwa kama character mkuu wa vitabu vyake (Musiba), kama hicho kitabu Cha "kikosi Cha kisasi" Willy anatumiwa na OAU kushughulika na makampuni pandikizi ya majasusi yaliyokuwa yanawaua wapigania uhuru, duuh ana show Kali sana

Willy anapenda wanawake sana, Kila nchi anayokwenda na Kila mission anayoanza lazima awe na mwanamke mpya, nafkir Musiba angeonyesha athari za wanawake katika moja ya riwaya zake, Kwa sabb wanawake wametumiwa kama chambo ya kuwaangusha wapelelezi mahili aidha kukwamisha mission kubwakubwa, nakumbuka ule mpango wa kuiangamiza Israel ulioratibiwa na falme za kiarabu, mpaka dakika za mwisho wanajiandaa na mashambulizi, ni mwanamke aliyewakwamisha (utafuatilia Kwa wakati wako)

STORI ZA UMUGHAKA ZIMELETA AROSTO AISEE
NA SASA, AJE AMALIZIE KILE CHA "NILIVYOFEL FORM 6 KISA MAPENZI YA WATOTO WA KITANGA"

KARIBU SANA MKUU

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
View attachment 2429505View attachment 2429507View attachment 2429509
 
Yaani nmekuwa addicted mpaka nmeanza kununua vitabu vya Musiba, though ni stori za kufikirika lakn ni muandishi mzuri sana.

Kuna mnyama mmoja anaitwa "Willy Gamba" ni mpelelezi mmoja hatari sana anatumiwa kama character mkuu wa vitabu vyake (Musiba), kama hicho kitabu Cha "kikosi Cha kisasi" Willy anatumiwa na OAU kushughulika na makampuni pandikizi ya majasusi yaliyokuwa yanawaua wapigania uhuru, duuh ana show Kali sana

Willy anapenda wanawake sana, Kila nchi anayokwenda na Kila mission anayoanza lazima awe na mwanamke mpya, nafkir Musiba angeonyesha athari za wanawake katika moja ya riwaya zake, Kwa sabb wanawake wametumiwa kama chambo ya kuwaangusha wapelelezi mahili aidha kukwamisha mission kubwakubwa, nakumbuka ule mpango wa kuiangamiza Israel ulioratibiwa na falme za kiarabu, mpaka dakika za mwisho wanajiandaa na mashambulizi, ni mwanamke aliyewakwamisha (utafuatilia Kwa wakati wako)

STORI ZA UMUGHAKA ZIMELETA AROSTO AISEE
NA SASA, AJE AMALIZIE KILE CHA "NILIVYOFEL FORM 6 KISA MAPENZI YA WATOTO WA KITANGA"

KARIBU SANA MKUU

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
View attachment 2429505View attachment 2429507View attachment 2429509
Hivyo vitabu vya Musiba Mimi Ninavyo vyote havichoshi kusoma mkuu
 
Yaani nmekuwa addicted mpaka nmeanza kununua vitabu vya Musiba, though ni stori za kufikirika lakn ni muandishi mzuri sana.

Kuna mnyama mmoja anaitwa "Willy Gamba" ni mpelelezi mmoja hatari sana anatumiwa kama character mkuu wa vitabu vyake (Musiba), kama hicho kitabu Cha "kikosi Cha kisasi" Willy anatumiwa na OAU kushughulika na makampuni pandikizi ya majasusi yaliyokuwa yanawaua wapigania uhuru, duuh ana show Kali sana

Willy anapenda wanawake sana, Kila nchi anayokwenda na Kila mission anayoanza lazima awe na mwanamke mpya, nafkir Musiba angeonyesha athari za wanawake katika moja ya riwaya zake, Kwa sabb wanawake wametumiwa kama chambo ya kuwaangusha wapelelezi mahili aidha kukwamisha mission kubwakubwa, nakumbuka ule mpango wa kuiangamiza Israel ulioratibiwa na falme za kiarabu, mpaka dakika za mwisho wanajiandaa na mashambulizi, ni mwanamke aliyewakwamisha (utafuatilia Kwa wakati wako)

STORI ZA UMUGHAKA ZIMELETA AROSTO AISEE
NA SASA, AJE AMALIZIE KILE CHA "NILIVYOFEL FORM 6 KISA MAPENZI YA WATOTO WA KITANGA"

KARIBU SANA MKUU

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
View attachment 2429505View attachment 2429507View attachment 2429509

"Nilivyofeli form 6" si ndio hii story ilianzia kule mwanzo alifeli akafukuzwa nyumbani.
 
"Nilivyofeli form 6" si ndio hii story ilianzia kule mwanzo alifeli akafukuzwa nyumbani.
Hapana, nadhani hii ni story baada ya yeye kufeli form 6 , check hiki kipande kidg cha season one[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

"Mkurya mimi kutoka wilayani Tarime kijiji cha Mogabiri nikajikuta nazamia kwenye dimbwi la mapenzi ya mtoto wa kitanga ambaye alifanya hata kusoma nikaacha nikawa namuwaza yeye na utamu wa papuchi yake!.

(Shamima popote ulipo ulaaniwe mbwa wewe kwa kuniharibia maisha[emoji23][emoji23]). All in all ni kwamba napambana na maisha yanasonga japo ni kibishi!. Sasa haya ya kwanini nilifeli nadhani kwa leo si mahala pake,nitawaeleza tu kilichofuata baada ya mimi kufeli shule!"
.................................................................................

SASA TUJUE SHAMIM ALICHOMFANYIA MWAMBA UMUGHAKA MPAKA AKAFELI.....
 
Back
Top Bottom