Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Sawa mkuu kwenye hii kuna sehemu kaelezea kabisa six alitoka na Div 0 kutokana na huyoo duu wa kitanga na peer pressure huko shule na ndipo mzee alipomfurumusha hom!!
Screenshot_20230131-150204~2.jpg

Hii ni post ya UMUGHAKA alikua anabishana na mtu akasema alipata div 2 pcb! Anyway ngoja tuendelee na story tu hizi ni minor issues tu Antonnia Dejane
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 19.

Baada ya muda wa nusu saa yule Bosi alirudi akiwa na jamaa mmoja wa wale jamaa wawili tuliowakuta pale sebuleni kabla hawajaambiwa watupishe kwa ajili ya mazungumzo!.

Alimwambia yule jamaa "Kaa pale"

Bosi "Hawa ni watu wa kazi,ni wakurya wakwenu huko!"

Basi yule jamaa akaanza kutuongelesha lugha ya kikurya huku akituuliza maswali na sisi tukimjibu kwa ufasaha,sasa baada ya kujiridhisha ya kwamba tulikuwa wakurya,akamwambia Bosi kwamba ni kweli sisi ni Wakurya.

Bosi "Sawa naomba utupishe!"

Yule jamaa akanyanyuka akaondoka akatuacha pale sebuleni!.

Bosi "Kazi nitakayowapa itawatoa kwenye umasikini na hizi shida ndogo ndogo mtazisahau!"

Aliendelea "Pesa yetu ipo mikononi mwa watu hivyo inapaswa irudi kwetu!"

Bosi "Mimi nitawalinda wala msijali!"

Aliendelea "Kanuni huwa ni pasu kwa pasu kwa kitakachopatikana!"

Bosi "Endapo kikinuka jisalimishe au tetea uhai wako,Yeyote atakaye kuwa kikwazo huyo ni halali yako!"

Muda wote wa mazungumzo nilikuwa naona Mtatiro akitikisa kichwa kana kwamba yale maneno yalikuwa yakimuingia sana na yeye kuyakubali!.Mimi kiukweli niliingia uoga sana lakini nilikuwa tayari kumfuata Mtatiro atakachokiamua yeye!.

Bosi "Kufa na siri hapa si hiari ni lazima,fanya ufanyavyo usije ukathubutu kumtaja mtu endapo ukiwa mikononi mwa wendawazimu(Mapongo)"

Aliendelea "Kitakachopatikana narudia tena itakuwa pasu kwa pasu!"

Bosi "Sasa tutaondoka wote kuelekea Arusha,lakini kabla ya kwenda huko mtaondoka na jamaa kwanza mkatengenezwe ndipo tuondoke!"

Aliendelea "Nyinyi ni wanaume bhana,haya ni maisha tu,pesa ndiyo kila kitu na hivyo lazima zirudi mikononi mwetu!"

Bosi "Gabriel mwambie Doto Akupatie milioni mbili uniletee"

Gabi ambaye muda wote alikuwa kimya akimsikiliza bosi wake,alinyanyuka akaelekea huko ndani ambako aliagizwa!.

Baada ya dakika 1 alirejea na bunda mbili ambayo kila moja ilikuwa na milioni moja!.

Bosi "Kamata hii"

Mimi nikapewa bunda moja na Mtatiro nae akakabidhiwa bunda lake!.

Bosi "Hizo ni pesa mtakazo tumia kutatua shida ndogo ndogo!"

Aliendelea "Nadhani utaratibu mwingine Gabi atawaeleza,nendeni mjipange ili ikiwezekana kesho au kesho kutwa muondoke mkatengenezwe kabla ya kwenda Arusha"

Kiukweli ile pesa ilikuwa ni kama vile sumaku,maana baada ya kuipokea ile hela niliona kama nilichelewa kwenye utajiri!.Tulinyanyuka tukamuaga yule jamaa na taa ikazimwa sisi tukatoka nje!.Tulipofika nje tulitembea kuitafuta barabara ambapo ilitulazimu kutafuta Taksi ili tuondoke!.

Gabi "Nyie ni wanangu ni lazima niwaambie ukweli,mara zote huu ni mchongo ambao nikiufanya,kule kwenye zile pesa bandia pia natafuta tu maisha lakini kiukweli maisha yako huku!"

Aliendelea "Siwezi kuwashikisha dili mbovu!"

Gabi "Huyo mliyekuwa mnaongea nae ni Askari lakini mpelelezi!"

Aliendelea "Si mko tayari ndugu zangu tupambane huku?"

Mtatiro "Mi nilitaka kumwambia anikabidhi chuma niingie mzigoni hata muda huu,nishachoka kudharauliwa!"

Gabi "Usiwe na haraka Mtatiro,nyie jiandaeni kesho kuna mahali mtapelekwa na jamaa ili mkitoka huko muwe kamili gado"

Sasa kwakuwa Mtatiro alilidhia ile kazi kwa moyo mweupe,kiukweli na mimi nilijikuta nakubali kwasababu nilikuwa namkubali sana jamaa yangu!.

Muhimu:-

(Yule tuliyeambiwa ni mpelelezi kiukweli hakuwa Askari wala mpelelezi,nilikuja kugundua baadae jamaa alikuwa ni mafia wa hatari na alikuwa akisakwa na jeshi la polisi sana,sasa nilichokuwa nikijipa moyo ni kwamba,kwakuwa alikuwa askari sikuhofia chochote maana nilijua endapo kikitokea cha kutokea tungesaidika,kumbe ile ilikuwa ni zuga tu wanaume tuingie mkenge,sitomtaja jina kwasababu maalumu na hata hivyo jamaa kwasasa ni marehemu).

Gabi "Umughaka mbona kama huna amani mwanangu"

Mimi "Mimi niko fiti kaka"

Gabi "Au unahofu?,mbele ya chuma hakunaga hofu kaka ile subiri uishike ndiyo utaniambia!"

Mimi "Kwahiyo chuma tunapewa lini?

Gabi "Msiwe na haraka,chuma zipo tutazikuta Arusha!"

Aliendelea "Hamuwezi kupewa chuma mpaka mkatolewe uoga ndugu zangu!"

Mtatiro "Mimi si muoga kaka labda Umughaka"

Baada ya ile kauli ya Mtatiro tukajikuta wote tunacheka sana!,basi sisi tulifanikiwa kuondoka tukawa tumeagana na Gabi na kukubaliana asubuhi tungeonana ili kuondoka tulikoambiwa tungeenda ili kutengenezwa kutolewa uoga!.

Tulipofika nyumbani kiukweli kila mtu alianza kuhesabu hela zake na kukuta ilikuwa milioni moja moja!.Mazungumzo yalichukua nafasi pale ndani na kiukweli Mtatiro alikuwa akiniambia sisi ni watoto wa kiume hatuna budi kupambana kwenye madili makubwa ya hela ili tufanikiwe katika maisha!.Ndugu yangu Mtatiro alikuwaga ni jasiri sana na asiyekuwa na chembe ya aibu na uoga!,alikuwaga akiamua kitu basi hakuna kurudi nyuma,ile roho ya ujasiri na isiyokuwa na uoga ndiyo Mtatiro aliniambukiza na mimi pia hata leo!.Mtatiro alikuwa ameamua liwalo na liwe,yeye alichokuwa akitaka ni pesa tu,hakutaka kusikia mambo mengine kabisa!.

Asubuhi kulipokucha Mtatiro alinishauri twende kwanza tukanunue nguo na viatu ili tuwe kila wakati tunapendeza!,sasa hakufahamu hayo ndiyo yalikuwaga mambo yangu,kiukweli nilifanya mambo yote hayo ili nipate pesa ya kula vizuri na kuvaa vizuri tu!.Baada ya lile zoezi la kununua viwalo,tukaianza safari ya kuelekea kitangiri ambapo yalikuwa makazi ya muda yule jamaa.

Tulipofika nje ya geti Mtatiro alimpigia simu Gabi akawa amekuja kutufungulia geti na kuzama ndani!.Tulipofika hapo ndani hatukumkuta yule bosi wa Gabi ila tulimkuta jamaa mmoja ambaye hakutaka tupoteze muda bali tuanze safari!.

Jamaa "Si mko Tayari!?"

Sisi " Ndiyo"

Jamaa "Ok tuondoke"

Tuliondoka kuelekea nje ambapo alianza kuwasiliana na mtu kwenye simu akimaambia asogee maeneo tuliyokuwepo ili tuondoke!.Baada ya muda mfupi gari aina ya Noah Ace ikawa imefika pale na aliyekuwa akiendesha alikuwa Demu!.Tulipanda kwenye ile gari sisi tukakaa katikati na yule jamaa akawa amekaa mbele!.Sasa tulimpa hai yule demu lakini hakutoa

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 25.

"Wewe ni mtu muhimu sana kwangu Mtatiro na umekuwa sehemu ya furaha katika maisha yangu,ulinipokea na kunisaidia wakati mzee aliponitimua nyumbani,hukuniacha katika matatizo bali ulinishika mkono kama kijana mwenzio hivyo na mimi sitokuacha rafiki yangu" ni maneno niliyokuwa nikimwambia rafiki yangu wa damu Mtatiro ili aendelee kuwa na amani kabisa.

USHAURI

Kuishi na Virusi vya Ukimwi si mwisho wa maisha na uhai,kama kuna kitu nakichukia katika maisha yangu ni ubaguzi unaofanywa kwa hawa ndugu zangu,haya ni maisha tu na tunapaswa kupendana,unaweza ukawa muaminifu na bado mumeo/mkeo akakuletea ugonjwa,hivyo hatupaswi kuwanyooshea wengine vidole kana kwamba ni wadhambi kuliko sisi,tuache dharau za kijuaji na kebehi zisizo na msingi.

Ndugu zangu pia niwaombe mzingatie dawa kwa wakati ili ziweze kuwafubaza virusi angalau unapokutana na mwenzako usimuambikize ili muendelee kufurahia maisha,jambo la msingi ni wewe mwenyewe kuacha kujibagua,jikubali na songa mbele.Acha starehe za kijinga,panga mipango yako na timiza ndoto zako,usiwe mlevi kupita kiasi na hakuna sababu ya kuwaambukiza wengine kwa makusudi,wapende watu wote.Pia achana na imani za mitume na manabii kwamba wakupatie maji au mafuta utumie kisha uache dawa,achana kabisa na hizo imani mfu,wewe muombe Mungu atakusikia,kama akipenda anaweza kuuondoa huo ugonjwa na kama akiona inafaa wewe kuendelea nao basi Mshukuru na endelea kuishi,hata kama ukimuomba Mungu na ugonjwa usitoke lakini Mungu bado atabaki kuwa mwema hivyo usikate tamaa.

NAWAPENDA SANA

Basi baada ya afya ya rafiki yangu kipenzi Mtatiro kuimalika tuliendelea na kazi yetu ya kuuza mitumba sehemu na vijiji mbalimbali vya kanda ya ziwa.Nakumbuka siku moja Gabi alimpigia simu Mtatiro akawa amemuambia inapaswa tuonane ili tupange mikakati ya kuelekea maeneo kama kawa.Kweli,tuliondoka siku iliyofuata kuelekea kule yalipokuwa makazi ya muda ilipokuwa inasukwa mipango kabla.Tulipofika pale ndani tulimkuta Gabi kama kawaida akiwepo Jipe na jamaa yule dereva tuliyeenda nae kwenye tukio kahama.

Jipe "Wanangu mko poa"

Mtatiro "Tuko fiti kaka"

Jipe "Sasa Kesho safari ni Kagera"

Aliendelea "Si mko vizuri?"

Mtatiro "Sisi tuko tayari hata leo kaka ni nyinyi tu!"

Jipe "Sawa,Gabriel atatangulia leo halafu sisi kesho jioni tutaondoka"

Basi baada ya yale mazungumzo Jipe akatutaka tujitayarishe kwa ajili ya safari kesho yake.Mimi na Mtatiro tuliamua kurudi nyumbani huku Mtatiro akiapa na kusema safari hii wakijidai kutudhurumu basi ama zake ama zao!.

Siku iliyofuata mida ya saa 7 mchana tulikuwa tushafika eneo la tukio na ndipo tukakamata Noah na kuianza safari ya kuelekea mkoa wa Kagera,kwenye gari nilikuwa mimi na Mtatiro wakati huo jipe akiwa amekaa kwa mbele pamoja na yule jamaa dereva!.Tuliingia Kagera mida ya saa 12 asubuhi siku iliyofuata,njia tuliyotumia ni ileile ya kupitia Kahama huku tukiwa makini kupita maelekezo,Jipe alikuwa ametoa maelekezo ya kwamba,yeyote atakaye jiingiza mkenge basi ingekuwa ni halali yetu!.Baada ya kufika Kagera,Jipe aliwasiliana na Gabi ambaye alimuelekeza maeneo ambayo tungemkuta,nakumbuka tuliikamata njia na uelekeo wa Bukoba mjini,nje kidogo ya mji tukamkuta Gabi.

Gabi "wazee kwa huku itabidi tuzunguke kidogo muda uende kwasababu hatuna makazi,na ikifika mida tutaitana tufanye kilichotuleta".

Kwakuwa mimi na Mtatiro ndiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza kufika Kagera ilibidi tukae kwenye ile gari maana hatukutaka kucheza mbali tukajichanganya na ukizangatia hatukuwa na simu!.Dereva alitafuta maeneo ambayo hayakuwa na shughuli nyingi za watu akapaki gari hapo.

Ilipofika mida ya saa 10 jioni mvua ikaanza kunyesha kama masikhara lakini muda ulipozidi ndipo hali ilizidi kuwa mbaya,tangu nizaliwe sijawahi kuona radi zikipiga kama siku hiyo,ile mvua ilikuwa na radi si mchezo hadi uoga ukawa unaniingia!.Kadiri muda ulivyozidi ndivyo mvua nayo ilizidi kuongeza spidi na nilikuwa naona Jipe anaomba iendelee kunyesha vilevile isikatike.Sasa ikafika mida ya saa 12 ikapungua ikawa inanyesha kidogo sana,tulikuwa ndani ya gari wakati huo tukiendelea kuvuta muda.Ilipofika mida ya saa 3 usiku mvua ikaanza tena kunyesha kama mwanzo.

Jipe "Huu ni muda sasa"

Aliendelea "Aisee wewe utaenda kutusubiri mahali nitakapokuelekeza"

Jipe "Wengine wote tutaongozana na mtafanya kila nitakachowaambia"

Basi ile gari ikaanza kuondoka kuelekea uelekeo wa Bukoba Mjini,kuna mahali tulifika ambapo kwa umbali kama wa mita 500 kulikuwa na sheli(sitoitaja),dereva alitakiwa kuzima taa na kugeuza gari atusubiri hapo!.Kila mmoja alikuwa tayari kwa ajili ya makabiliano.Muda huo ilikuwa ni saa 4 usiku lakini kulikuwa na mvua kubwa sana,tulipofika kwenye ile sheli baada ya Jipe kuchomoa SMG kuna mlinzi alimuona akaanza kukimbia kama mwehu huku akiwa na gobole,Jipe hakutaka kumpotezea muda,alipiga risasi ya mgongoni yule mlinzi akawa amedondoka chini.

Jipe "Mtatiro kusanya hao wauza mafuta wote"

Jipe aliingia ndani kwenye vyumba vilivyokuwa kando ya ile sheli huku akiniambia niongozane nae.Pale nje Mtatiro na Gabi waliendelea kuwadhibiti wale wauza mafuta na kuchukua hela huku wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Jipe "Toa pesa wewe la sivyo nitakuua"

Jipe alikuwa akimwambia dada mmoja kibonge ambaye tulimkuta mle ndani wakati huo akimnyooshea mtutu wa bunduki.Yule dada alifungua boksi moja lilikuwa la mbao na kulikuwa na noti za kutosha,sasa kulibeba lile boksi mwenyewe kidogo likawa zito,Jipe akamuamuru yule demu atupatie mfuko,yule demu alitoa mfuko mmoja ambao ulikuwa kama shuka ambao ulikuwa umechakazwa na rangi ya maoili!,niliukamata ule mfuko haraka nikaanza kuchukua zile hela haraka sana,sikutaka kabisa kuhangaika na silva maana jipe alisema nitemane nazo,baada kumaliza zile hela,Jipe alimuamuru yule demu alale chini na asijaribu kuinua kichwa kwani atamuua,tuliondoka chap mle ndani kuelekea nje ambapo tuliwakuta Gabi na Mtatiro wakiwa wanatusubiri!.

Tulikimbilia gari na tulipofika dereva aliondoka kwa spidi kali sana lile eneo,wakati huo bado mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha sana.Wakati tupo njiani,Jipe alimpigia simu yule demu Kamange na kumtaka achukue ile gari Mark 2 atukute Geita.Ile Noah ilitembea vibaya mno usiku huo na tulifanikiwa kufika Geita mida ya saa 8 Usiku,Jipe akawa amemwambia Gabriel na dereva ya kwamba wao watangulie Mwanza halafu sisi tungeisubiri ile Mark 2.

Kweli,Kesho yake mida ya saa 4 asubuhi yule demu akawa amefika pale Geita kutuchukua tukawa tumeondoka,Tuliingia Mwanza mida ya saa 11 jioni.Tuliwakuta kina Gabi wao wameshafika,sasa tulipofika Mtatiro alimwambia Jipe ya kwamba pesa tulizopora ziletwe zihesabiwe ili kila mtu afe na chake,nadhani wao walidhani Mtatiro anatania lakini jamaa alikuwa serious sana,sikuwahi kufahamu kama Mtatiro akikasirika anakuwa vile aisee,mara zote mimi nimekuwa nikimuona akiwa kawaida nikawa namchukulia poa,siku hiyo ndiyo niliiona rangi halisi ya yule mkurya.

Mtatiro "Haiwezekani tupore pesa halafu nyie muwe mnagawana nyingi na sisi mnatupa kidogo,mkitaka damu leo imwagike ficheni hizo hela muone!"

Jipe "Hakuna atakayedhurumiwa hata mmoja"

Mtatiro "Mbona juzi mmetunyenga?"

Jipe "Yale yalikuwa ni maelekezo ya bosi"

Mtatiro "Basi mwambieni leo kila mtu anapata pasu,sitaki ufara!"

Baada ya jamaa kuona Mtatiro yuko serious,Jipe alimwambia Gabi walete zile pesa ili kila mmoja apewe haki yake.Kweli,mimi na Mtatiro kila mmoja alipata mioni 6,na wao pia walipata kama sisi.Tuliamua kuondoka zetu baada ya kupokea mgao wetu.

Mtatiro "Mwanangu kama ni hela ya mtaji tushapata,tuachane na hizi habari wao kama wanaendelea ngoja waendelee"

Aliendelea "Cha kufanya tukafungue duka la jumla tuachane na mitumba"

Mtatiro "Au wewe unaonaje mwanangu?"

Mimi "Kwanini tusifungue duka la vipodozi?"

Mtatiro "Eti eeeh,sawa?"

Baada ya kupata ile hela kweli tuliachana na biashara ya mitumba na tukafungua duka la vipodozi yale yale maeneo ya Usagara tukaanza kupambana,nakumbuka Mtatiro alikuwaga anafuata vipodozi Uganda kwasababu huko ndiko vilikuwa vinapatikana kwa bei ya chini,kiukweli tulipiga sana hela na maisha yetu yalianza kubadilika mdogo mdogo,ilifika sehemu tukahama pale kwa braza ake Mtatiro kila mmoja akaenda kupanga geto lake mwenyewe.

Nakumbuka siku moja Mtatiro akaja kuniambia kwamba Gabi anampigia simi twende kuna mchongo wenye hela kubwa tukapige.

Mimi "Umemwambiaje!"

Mtatiro "Mi nimemwambia kwasasa tunashughuli zetu,wao kama wanaendelea waendelee!"

Aliendelea "Jamaa baada ya kumwambia ananiambia kwamba tunataka kuwachoma,hivyo tujiangalie tutaumia"

Mimi "Sasa itakuwaje?"

Mtatiro "wale hawawezi kututisha we tulia"

Basi baada ya jamaa kuona hatuwapi tena ushirikiano wakaamua kutokutushirikisha kwenye michongo yao tena lakini walikuwa wamechukia sana baada ya sisi kuachana nao.Baada ya miezi kadhaa kupita,kuna siku Mtatiro akaja kuniambia amesikia habari mahali kuna majambazi wamedakwa wengine wameuawa huko Mbeya na mmoja wapo wa waliodakwa ni Gabi,sasa baada ya kuifatilia ile habari ni kweli kabisa ilikuwa Jipe na majambazi kadhaa wenzie waliuawa palepale eneo la tukio.

Kumbe walienda kumpora mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya India ambaye ndani ya gari alikuwa na madini pamoja na pesa alizokuwa akizitoa huko Chunya kuelekea Mbeya,sasa wao hawakujua yule mfanyabiashara alikuwa na eskoti ya askari kadhaa,yawezekana walijua hilo ila wakajifanya wabishi kwakuwa walikuwa na silaha.Walikufa majambazi wawili na mmoja akiwa Jipe huku Gabi na mwingine mmoja wakisalimu amri.

Gabi alifungwa miaka the thelathini gerezani na mwaka juzi nimetoka kumuona pale gereza la Ruanda Mbeya.Jamaa amechoka sana na aliponiona mara ya kwanza alionyesha huzuni lakini hakuwa na namna ndo hivyo ishatokea.Aliniambia yule aliyekuwa bosi wake alikimbilia huko Kenya kuanzisha maisha huko.Huwa namtembelea jamaa nikipata nafasi,na siachi kumtia moyo na kumfariji,namwambia ashukuru akufa,maadam yuko hai basi atatoka tu gerezani na ataendelea na maisha yake ingawaje atakuwa amepoteza muda.

Mimi na Mtatiro lile duka la vipodozi tuliuza na kila mmoja akaendelea na biashara zake,Mtatiro aliondoka kwenda Uganda kwa anko wake hadi leo anaishi huko.Mimi niliamua kurudi Tarime Sirari nikafungua duka nikaanza kukimbiza,kuna mtoto wa dingi mkubwa anaishi Dar es salaam alikuwa anafanya biashara ya vyombo akaniambia nije tuungane tufanye biashara kwa kua inalipa sana,hivyo nikaondoka Tarime kuja Dar,kufika nikampatia jamaa zaidi ya milioni 9 akanidhurumu hadi leo,niliamua kumuachia Mungu nikaanza kupambana upya kutafuta mtaji,nilipopata mtaji nikanunua bodaboda yangu ambayo ndiyo inaniingizia kipato kwa hapa mjini.

Nawapenda sana.

MWISHO.
Stori ndefu sana lakini nzuri
 
Ni sawa kujiajiri ni kuzuri ila hii ya Bodaboda kupiga 90,000 per day mzee ni TATEPA.
Kuna jamaa nilipanda bolt ya boda ya boda kwenye story aliniambia anakaa kibaha, lakini per day anasema anapata hata 60k tena yeye anapiga city city centre na msasani na maeneo ya town sana sana
 
Hiyo 60k ndio Nini? Laki 6 au? Hongera kwa kucomment kama ni laki SITA sio uongo TU Bali alikudharau sana kukuambia hivyo. Alikuona wewe ni mbumbumbu na lofa
 
Unakata kuniambia kwamba unaamini pia umughaka genuine ni bodaboda na bado anapata nafasi ya kuandika makala kama hizi?
 
Tujifunze kuridhika na kuwa na kiasi basi! Jamaa anajitahidi sana kupost. Kesho pia ni siku Nakadori[emoji4]
Nimefurahi sana yaani kuna watu wnaadai episodes kama vile uhai jamanj hivi inawezekana mtu akawa anahitaji mtu akae anaposts tu epsodes yaani hana analolifanya ,hata chooni mtu asiende au asisinzie akalie kupost tu episode loh!!tujitahidi kua nakiasi buana ndio uungwana naustaarabu jamaniii.
 
Umetisha sanaa 🔥🔥🔥✔️
 
Hiyo 60k ndio Nini? Laki 6 au? Hongera kwa kucomment kama ni laki SITA sio uongo TU Bali alikudharau sana kukuambia hivyo. Alikuona wewe ni mbumbumbu na lofa
Sina comment yaani hujui maana ya 60k halafu unasema mimi mbumbumbu na lofa. Lakini mwerevu kashaelewa nani mbumbumbu na lofa
 
Back
Top Bottom