Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 13.
Mimi "Mama nyakuru Mwita"
Mama "Tata sabhoke"
Ilikuwa ni heshima na salamu ambayo nilimpatia mama yangu baada ya kuwa nimefika hapo sokoni kwenye meza aliyokuwa akifanyia biashara!.
Mama "Ulienda wapi baba?"
Mimi "Nilikuwepo tu mama!"
Mama "Mbona umenenepa hivyo,au umepata kibarua huko baba!?"
Mimi "Nabangaiza tu hivyo hivyo!"
Mama "Nilimpigia mama yako mkubwa lakini akaniambia uliondoka na akajua labda ulirudi nyumbani"
Mimi "Mama nilienda kupambana na maisha yangu!".
Mama "Sasa baba utaendelea kuhangaika hivi hadi lini,rudi nyumbani mimi niliongea na baba yako na akasema hayo yameisha"
Mimi "Mama kwa umri huu siwezi kukaa tena pale nyumbani"
Mimi "Nilipita tu kuwasalimia"
Mama "Ulipita nyumbani?"
Mimi "Nimeanzia huko ndiyo nikaja hapa"
Mama "Dada yako alikuja na amemaliza kuondoka wiki iliyopita!"
Aliendelea "Chukua namba yake utawasiliana nae alisema ukirudi nikwambie umtafute"
Basi baada ya mazungumzo na mama nilichukua ile namba ya dada yangu mkubwa(Sarah)kisha nikaondoka zangu!.Mama yangu mara zote alikuwaga rafiki yangu kipenzi,pamoja na lile seke seke la mzee lakini bado alitaka nirudi pale nyumbani kitu ambacho kisingewezekana kwa wakati huo!.Sasa wakati naondoka nilimpigia dada yangu simu ili kumjulia hali maana tangu nilivyokuwa nimemaliza shule sikuwahi kuongea nae kwasababu yeye alikuwa ameolewa huko Mwanza!.
Baada ya kuongea na dada kwa dakika kadhaa alishangaa sana kwa kile kitendo ambacho mzee alinifanyia na alilaumu sana kwanini nilishindwa kumshirikisha kwa muda wote huo nikawa kimya!.
Da'Sarah "Sasa sikuhizi unafanya kazi gani hapo Tarime?"
Sikutaka kabisa kumficha kitu dada nilimwambia niliamua kuwa mpiga debe angalau maisha yaendeleee,alinishangaa sana ya kwamba nawezaje kuwa na elimu halafu niende kupiga debe!.
Da'sarah "Nilimwambia baba ukweli na kama ni kuchukia ngoja achukie,haiwezekani pesa anamalizia kwa mama yake Robina halafu sisi tunahangaika!"
Aliendelea "Kwahiyo sasa ulikuwa unakaa wapi?"
Mimi "Niliamua kupanga hapo Sirari!"
Da'Sarah "Ngoja nimwambie shemeji yako aje akutumie nauli uje huku"
Aliendelea "Na huyo mzee wala usimwambie chochote,muacheni na hela zake,yeye si anaona mama yetu hana maana!"
Mimi "Mimi nishamsahau na wala sihitaji hata kumi yake!"
Mimi " Halafu dada kama huko kuna sehemu ya kufikia hilo suala la nauli kwangu alinisumbui,we hata usimsumbue shem we kama inawezekana hata leo nianze safari"
Da'Sarah " Sasa hivi kweli kuna gari za kutoka hapo kuja Mwanza?"
Mimi "Hilo suala wewe niachie mimi,mimi nikifika nitakwambia"
Da'Sarah " Sawa wewe panda gari uje kama una nauli na ngoja nimpigie shemeji yako simu muda huo!"
Ile kauli ya Dada kunitaka niende Mwanza nikama ilinisaidia maana mpaka wakati huo nilikuwa sielewi hatma yangu!.Basi nilielekea mpaka stendi ambako nilikuwa nikitembea kwa umakini na tahadhari kubwa ili nisije kujikuta naangukia mkoni mwa mapongo,wakati huo begi langu lilikuwa na hela lipo mgongoni sikutaka kabisa kuliachia!.Basi nilipofika pale stendi nilidandia Hiace za Musoma ambako nilipanga nikifika pale Zero zero( Makutano) nisubiri gari zinazoenda Mwanza kutokea Musoma mjini!.Nilifika pale Makutano mida ya saa 9 alasiri na nikatelemka kusubiri gari za Mwanza.
Sikutaka kupandia gari za Mwanza pale Tarime mjini maana kulikuwa na wajuaji wengi hivyo nikawa naogopa kukamatishwa!.Basi haukupita muda nikawa nimepanda gari za Mwanza na nikawasiliana na dada nikawa nimemjulisha nishapanda gari!.,Kiukweli akili yangu mpaka wakati huo ilikuwa inawaza mambo mengi sana,sikujali ya kwamba Sirari nimeacha vitu vyangu wala nini,mimi nilichojali ni usalama wangu na kama ni vitu niliona ningevifata hali ambapo ingetulia!.
Wakati nikiwa kwenye gari nilimtafuta mshikaji wangu Mtatiro ambaye niliamini yupo Mwanza na nilipanga nikifika Mwanza tuonane!.
Mimi "Mwanangu vipi?"
Mtatiro "Mwanangu umekuwa adimu sana kama mate ya nyoka!"
Mimi "Ahahahaa ahahaaa,nambie mwanangu"
Mtatiro "Nimekutafuta juzi kati ulikuwa hupatikani!"
Mimi "Kuna mahali nilikuwepo mtandao ulikuwa haushiki kaka"
Mimi "Nipo njiani mwanangu nakuja M-Z-A"
Mtatiro "Unakuja lini,leo!?"
Mimi "Yeah nipo njiani"
Mtatiro "Umefika wapi?"
Mimi "Tunakaribia Kiabakari"
Mtatiro "Mimi sipo Mwanza mwanangu"
Mimi "Ulirudi Tarime?"
Mtatiro "Hapana,nipo hapa Bunda kuna ki mgodi kimetema ndiyo tupo na brother"
Mimi "Duuu!"
Mtatiro "Mwanza unaenda kwa nani?"
Mimi "Naenda kwa sista Sarah!"
Mtatiro "Mwanangu achana na habari za Mwanza kwanza,we kama vipi telemkia hapo Bunda mimi nitakufata uje tuone kama tutapata chochote"
Mtatiro alinishawishi hadi nikajikuta tena safari ya Mwanza kama imetoweka moyoni mwangu,nilichokuwa namshukuru Mshikaji wangu Mtatiro alikuwaga kila fursa haachi kunishirikisha kama rafiki yake,iwe haramu au iwe halali,kiukweli kwenye hilo sitamsahau jamaa yangu(Kwasasa anaishi Uganda).
Mtatiro "We mwambie Konda akushushe kituo kinaitwa Nyasura"
Aliendelea "Akikushusha hapo Nyasura ndiyo itakuwa jirani na huku nilipo!"
Mimi "Sawa"
Basi safari ikawa inaishia Bunda ingawa nilishalipa nauli ya Mwanza moja kwa moja,sikuona taabu kwasababu bado fungu nilikuwa nalo la kutosha.Ingawaje pesa niliyokuwa nayo ilikuwa haramu lakini ilikuwa inanipa kujiamini kwingi sana!.
Baada ya safari ya dakika kadhaa tukawa tumefika pale Bunda na mimi kushushwa hapo Nyasura kama Mtatiro alivyokuwa amenielekeza!.Basi nilimpigia simu Mtatiro nikamueleza ya kwamba nishafika hapo Nyasura,jamaa akawa amenitaka nipumzike sehemu aje kunifuata maana alipokuwepo yeye kulikuwa na umbali mrefu kidogo!.