UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,753
- 12,932
- Thread starter
- #241
Mkuu Bujibuji Simba Nyamaume tuko pamoja kakaUMUGHAKA heshima kwako mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Bujibuji Simba Nyamaume tuko pamoja kakaUMUGHAKA heshima kwako mkuu
One love. Episodes zote za stories zako ninazo kwenye archive yanguMkuu Bujibuji Simba Nyamaume tuko pamoja kaka
One love. Episodes zote za stories zako ninazo kwenye archive yangu, nadoma kwa kurudiarudia kama unjiliMkuu Bujibuji Simba Nyamaume tuko pamoja kaka
Jamaa anajua hadi kapitilizaUmaghaka kwa mara nyingen tena mwamba huyu hapa tumetoka kwa Monica now kwa Gab basi Raha tuu Asante mzee wa kuzugia .
Next!Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 9.
Nilifunguliwa lile geti nikawa nimetoka mle ndani.Yule askari aliyenifungulia alinichukia mpaka kwenye kile chumba ambacho jana tulifikishiwa baada ya kufika hapo kituoni!.Sasa nilipofika hapo nilimkuta jamaa mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi,pembeni yake alikuwa amekaa Gabriel ila shemeji ambaye ni mke wa Gabi sikumuona!.
Afande "Kaa chini bhana hapa huwa hatusimami!"
Afande aliyeniambia nikae chini ndiye yuleyule aliyekuwa akituhoji ile jana na ndiye niliyemkuta kule nyumbani kwa Gabriel!.Basi mle ndani kulikuwa na ukimya wa muda fulani ambapo yule askari yeye alikuwa akiendelea kuandika huku kila mmoja akiwa kimya akimtazama.
Afande "Mkuu nadhani sasa tutawasiliana"
Jamaa "Sawa,haina tatizo!"
Basi baada ya hapo nikaambiwa na yule afande niende pale mapokezi nikachukue vitu vyangu nilivyokuwa nimekabidhi kabla ya kuingizwa Selo!.Baada ya kukabidhiwa vitu vyangu nakutoka nje,ndipo Gabriel akanitaka nipande gari iliyokuwa imepaki kando ya hilo jengo la kituo cha polisi na ilikuwa ni Toyota Prado nyeupe!.Basi nilipoingia ndani ya ile gari nikamkuta na demu wa Gabriel.
Yule jamaa aliyekuwa amevaa suti yeye alikaa mbele kando ya dereva halafu na sisi watatu tukakaa nyuma!.Gari ile iliondoka na tukaelekea nyumbani kwa Gabriel maeneo ya Buhemba!.Tulipofika tulishuka na kuingia ndani ambapo kila mmoja aliingia bafuni kuoga na kubadili nguo,sasa kwakuwa mimi nguo zangu zilikuwa Sirari,Gabriel aliniazima nguo zake nikavaa ingawa aliniambia nisimrudishie amenipatia kama ndugu yake!.
Baada ya hapo yule Bosi wa Gabriel alisema tutoke tutafute sehemu iliyotulia ili tupumzishe akili,sasa wakati tunatoka Gabriel akasema mkewe abaki pale nyumbani,sasa yule bosi wake akasema inabidi twende wote lakini Gabriel akakataa akasema yeye abaki na kama ni chakula angeletewa!.Basi tukawa tumeondoka kuelekea mjini!.
Basi baada ya kufika hotelini ile gari ikapaki na sisi tukashuka kuingia ndani!,baada ya kupata msosi wa nguvu ndipo kila mmoja akaanza kushushia vitu vyake,baada ya kupiga vitu niliona sasa Gabriel akaanza kuchamngamka!.
Gabi "Unajua yule mwanamke ni mpumbavu sana Bosi!"
Bosi "Nani!,Mkeo?"
Gabi "Aah! yule si mke wangu hata hivyo mi napita tu!"
Bosi "Kwanini unasema hivyo!"
Gabi "Kila siku naongea lakini yanapitia huku yanatokea kule"
Aliendelea "Ukiachana na hii ishu lakini nadhani unakumbuka kipindi kile Babati ilivyokuwa kaka!"
Bosi "Yeah!,sasa inabidi uwe makini maana serikali sasa hivi wako makini sana,sema ndiyo hivyo tunabanana na hawa askari,lakini kama sivyo ni hatari sana!"
Sasa mimi sikutaka kabisa kuingilia yale mazungumzo lakini nilichokuja kugundua ni kwamba,yule demu wa Gabi ndiye yawezekana alisababisha yale majanga kwasababu Gabi alikuwa amechukia sana na sikujua alisababishaje maana mimi hakutaka kabisa kuniambia na inaonekana si mara moja,yeye na huyo bosi wake ndiyo walikuwa wakifahamu,mimi kazi yangu niliifanya kwa uaminifu kabisa na sikuwa na longo longo!.
Sasa mpaka tunatoka pale polisi aliyesababisha sisi kutoka ni huyo jamaa ambaye Gabi alikuwa akimuita bosi,sikujua amefanya fanyaje hadi sisi kutoka lakini niliamini ilikuwa ni fedha inaongea maana jamaa alionekana alikuwa na hela hatari,na kitu kingine nilichokuja kukigundua baadae ni kwamba yule jamaa ndiye alikuwa akimpatia Gabi zile fedha!.Hii nchi kuna dili haramu nyingi sana lakini huwezi kukuta watu wanaohusika wanawekwa ndani,siye vinyangarakata tusio na mbele wala nyuma ukizingua kidogo tu,utafia gerezani!.
Bosi "Hivi uliniambia huyu jamaa anaitwa nani!?"
Gabi "Huyu anaitwa umughaka"
Bosi "Ooh sawa!"
Aliendelea "Sawa bana nyie fanyeni kazi kwa umakini,najua kwasasa hakuta kuwa na wanoko maana wale wajinga tushamalizana!".
Sasa wakati nikiwa naendelea kukung'uta vyombo nilikuwa nawaza namna ya kuachana na ile biashara kichaa japo ilinipatia pesa ya kutosha lakini niliona inaweza kuniingiza kwenye matazizo makubwa!.Baada ya kupiga vyombo na kuona vimenitosha niliwaaga wao ili mimi nijikatae kwenda Sirari!.
Gabi "Unawahi wapi wewe,wewe kaa utatindike beer,kwako utaenda tu!"
Basi niliamua kukaa chini tena ili niendeleze makamuzi,baada ya kila mtu kuridhika siku hiyo tuliondoka,Gabi alinishawishi sana hatimae sikwenda Sirari nikaamua kwenda kulala kwake ili asubuhi anipatie fungu niondoke nalo kuelekea Sirari!.Baada ya kutufikisha pale nyumbani yule Bosi na dereva wake wao waliondoka.
Namshukuru Mungu asubuhi niliwahi kuamka na ndipo nikaelekea sebuleni kumsubiri Gabi aamke anikabidhi pesa haramu ili mimi nichafue zangu,sasa shemeji ndiye aliyetangulia kuamka na kuja pale sebuleni.
Mimi "Mambo vipi shemu"
Marieta "Safi,za tangu jana"
Mimi "poa kabisa"
Mimi "Jamaa bado amelala?"
Marieta "Ngoja nimuamshe"
Basi baada ya dakika 10 jamaa akawa amekuja pale sebuleni.
Mimi "Nataka kuondoka kaka,unaweza kunipatia mzigo?"
Gabi "We nenda tu nitakuletea huko,pia kuna jambo nikija tutazungumza"
Mimi "Poa,basi acha mi niwahi"
Gabi "Mida ya saa 10 jioni nitakupigia simu tuonane mahali"
Mimi "Poa kaka"
Baada ya mazungumzo yale mi nikamuaga jamaa nikaondoka zangu,sikujua ni kwanini jamaa alibadili maamuzi ile asubuhi kwasababu jana yake tulikuwa tumeongea akawa amesema asubuhi angenipatia hela lakini alibadilika.Yeye na huyo demu wake kiukweli baada ya hilo sekeseke inaonekana kabisa hawakuwa sawa na sikufahamu tatizo lilikuwa ni nin!.Sikutaka sana kuchimba na kuuliza uliza mambo ya ndani kwani ningeonekana mjuaji!,nilichoshukuru mimi ni kutoka nje na ile kesi iliisha!.
Baada ya kufika pale Sirari wanangu walitaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha hadi kujikuta nipo mikononi mwa mapongo.Sasa sikutaka kuwaeleza ukweli ikabidi nifanye siri kabisa,nilichowaambia ni kwamba kuna mtu alikuwa akinidai na hivyo aliamua kunipeleka polisi,wao wakaamini hivyo kumbe haikuwa hivyo!.
Sasa ilipofika mida hiyo ya saa 10 alasiri,Gabi akawa amepigia simu na kweli akawa yupo pale Sirari na akaniambia tuonane kwenye ile bar tuliyokutana ile siku ya kwanza.
Hapa sasa Mkuu ulipaswa msitue Monica afanye rescue.Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 6.
Maisha kwa upande wangu yalikuwa mazuri na hata yale majuto ya mzee wangu kunitimua nyumbani hayakuwepo tena,zaidi ni mimi ndiye niliyetamani nifanikiwe ili nikamringishie ajute kunifukuza nyumbani kwa kunidharirisha!.Nilikuwa nafanya kazi mbili kwa wakati mmoja,kazi yangu ya upiga debe ilikuwa ikinipatia pesa ya kula kila siku,kuhusu kula kwakweli nilikuwa siwazi kabisa!,ile pesa ya kubadili fedha haramu yenyewe ilifanya nikavaa vizuri,nikanunua samani za ndani na kupiga starehe!.
Marafiki na wadau wangu wa pale Sirari wao waliamini mimi ni mjanja mjanja na uenda nilikuwa najiongeza kutokana na elimu yangu kumbe pasipo kufahamu kijana mwenzao nilikuwa nafanya dili haramu.
Niliendelea kumsubiri bwana Gabi(Gabriel) ili atakapo rudi basi tuendelee na kazi yetu ambayo tayari ishanitia uchizi!.Sasa ndani ya mwezi mmoja baada ya kusubiri jamaa alirudi na alipofika tu alikuwa amenipigia simu akinitaka niende nikachukue hela niziingize mtaani ili kila mtu afe na chake!.Kiukweli pesa zilikuwa nyingi sana na sikuwahi kufahamu yeye alikuwa akizitoa wapi!. Kitu cha kumshukuru Mungu kwa upande wangu tangu nianze kujihusisha na ile biashara haramu,sikuwahi kushitukiwa na mtu yeyote na nilikuwa nimesema endapo siku nikashitukiwa basi mimi ningekufa na mtu yeyote kwa kumsingizia uongo ili nichomoke!.
Sasa nikiwa naifanya kazi ile kwa umakini mkubwa huku nikiendelea kuzuga kwenye kazi yangu ya upiga debe,mpaka muda huo nadhani mtaani nilikuwa nishaingiza si chini ya milioni 10.kuna siku mida ya saa 5 asubuhi mke wa jamaa akawa amenipigia simu huku akihitaji kufahamu niko maeneo gani.Sikuwahi kabisa kuwasiliana na yule mwanamke ijapokuwa namba yangu yeye alikuwa nayo na mimi pia ya kwake nilikuwa nayo,sasa kitendo cha kuniuliza niko wapi sikujua lengo lake ni lipi maana hata mumewe hakuwahi kuniuliza kwamba niko wapi!,nakumbuka ilikuwa ni ile siku ya kwanza tu ndiyo jamaa aliniuliza nipo maeneo gani ili aje tuzungumze!,sasa huyu mkewe lile swali lake la "Uko wapi" na namna alivyouliza ni kama Jamii yetu ya kikurya mwanaume kuambiwa na mkewe kwamba "Nitakupiga".Ikifika hatua hiyo basi unaweza kumkung'uta mwanamke na ukamuua kabisa!.Sasa kitendo cha kuniuliza uko wapi tena bila hata salamu kilinikera na kuniudhi sana lakini niliamua kukausha tu!.
Yeye "Marieta hapa naongea"
Aliendelea "Uko wapi?"
Mimi "Kuna shida?"
Yeye "Wewe niambie uko wapi?"
Mimi "Kwani siku zote huwa napatikana wapi shemu!?"
Basi baada ya kumwambia vile akakata simu,nilifahamu kama kungekuwa na tatizo angenipigia simu yeye,mimi niliendelea na kazi yangu bila presha!.Sasa baada ya kama dakika 10 kupita akawa amenipigia simu.
Yeye "Njoo nyumbani Gabi anakuita"
Mimi "Ok sawa,mwambie nitakuja jioni"
Yeye "Njoo muda huu kama unaweza ni ishu ya haraka!".
Mimi "Shemu kuna shida?"
Yeye "Hapana ni kawaida tu!".
Basi baada ya mazungumzo akawa amekata tena ile simu,sasa yule mwanamke alikuwaga anaongea kwa kisirani sana na kwa mkato,sikufahamu uenda ndivyo walivyokuwa wanawake kutoka huko Arusha au ilikuwa ni tabia yake tu!,kiukweli mimi alikuwa akiniudhi sana kama kijana wa kikurya niliyekuwa sipendi dharau na ndiyo maana hata nilikuwa sipandishi nae stori!.
Niliamua kumpigia simu bwana Gabriel mimi mwenyewe kama ni kweli alikuwa akinihitaji wakati ule pale nyumbani ama la!,sasa niliipiga sana ile simu ya jamaa ikawa inaita tu bila kupokelewa,nikaendelea kupiga lakini nikaona holaa!.Sasa akilini mwangu nikaanza kuwaza mambo ya kijinga,nikawa nasema uenda mtoto wa kike anahitaji kupelekewa moto na ile ilikuwa ni Zuga tu kujisemesha naitwa na jamaa ili niende pale nyumbani kwao!,lakini pia kilichonipa ujasiri ni kwamba kama jamaa angekuwa ananihitaji angenipigia simu mwenyewe!,sasa mawazo yakanipeleka mbali sana nikaingia tamaa ya moyo ghafla yule mwanamke akajaa usoni nikaanza kumvutia picha namna alivyo na namna nitakavyo mkung'uta shipa lenye ladha ya kikurya!.Basi nikaamua kumpigia simu ili kujiridhisha tena!.
Yeye "Umefika wapi?"
Mimi "Ndo nadandia usafiri nakuja"
Mimi "Nampigia jamaa simu naona hapokei"
Yeye "Mi sijui bana we njoo"
Basi mwanaume nikadandia mchomoko iliyokuwa ikielekea Tarime mjini nikaondoka!.Baada ya kufika pale Tarime niliingia stendi kule ambako kulikuwa na wanangu wenye magari ya kuelekea Musoma,nikadandia Hiace ikanishusha maeneo ya Buhemba yalipokuwa makazi ya Gabriel na huyo mkewe!.
Basi nilipofika getini nilikuta geti liko wazi nami nikalifungua na kuingia ndani,nilibisha hodi na hatimaye yule mwanamke alikuja kunifungulia mlango,sasa wakati anafungua mlango alionekana ni kama hana amani kabisa tofauti na siku zote!.
Mimi "Shwari?"
Yeye "Shwari,vipi!"
Sasa ile natia tu mguu ndani,kumbe kuna jamaa alikuwa amejificha nyuma ya mlango akawa amenivuta kwa ndani kisha akaufunga ule mlango na funguo akachomoa! .Basi yule jamaa akaniambia kwa ishara niongozane na yule mwanamke kuelekea sebuleni!.
Baada ya kufika sebuleni nikawakuta jamaa 3 na yule aliyefunga mlango walikuwa jumla 4,pia nikamkuta Gabriel amekaa kwenye kochi akiwa hana raha kabisa!.Basi miongoni mwa wale jamaa akaniongelesha kwa ukarimu kabisa!.
Jamaa "Umughaka mambo vipi kaka"
Mimi "Shwari kaka"
Jamaa "Vipi lakini mambo yako!"
Mimi "Mimi niko poa kabisa kaka"
Jamaa "Ooh sawa,sirari wanasemaje kaka"
Mimi "Tupo tu tunapambana"
Jamaa "Hivi pale Sirari huwa unaishi maeneo gani?"
Sasa kabla hata sijajibu,yule jamaa ambaye yeye kwa wakati huo akiwa amekaa na wenzie wamesimama kama milingoti,akaniambia nisimame nimsogelee alipokuwa amekaa!.
Jamaa "Hebu tuangalie humu mfukoni umeweka nini bwana Umughaka"
Jamaa moja kwa moja baada ya kumsogelea alizama mfukoni mwangu akatoa simu na hela nilizokuwa nazo!.
Jamaa "Hii simu ya nani?"
Mimi "Ya kwangu"
Jamaa "Na hii hela!"
Mimi "Ni yangu kaka"
Jamaa "Kumbe unaweza kufanya tu kazi zako vizuri na bado ukapata hela nzuri tu bwana Umughaka"
Sasa ile hela niliyokuwa nayo mfukoni muda huo ilikuwa ni elfu 16 na vichenji kadhaa!.
Jamaa "Huyu bwana unamfahamu?"
Mimi "Ndiyo,ni brother angu"
Jamaa "Mtu wa Arusha na mkurya ni ndugu wapi na wapi Umughaka wewe acha hizo bwana!"
Kiukweli yule jamaa alikuwa anaongea kama mtu fulani mnyenyekevu sana lakini kiuhalisia alionekana asiyekuwa na huruma hata chembe!,sasa mpaka wakati huo nilifahamu kabisa mambo yameshaharibika na sikupata tabu kuamini wale walikuwa ni mapongo (Askari).
Jamaa "Mbona jamaa anasema yeye hakujui!"
Sasa wakati jamaa anaongea na mimi alikuwa akiendelea kukipekua kiswanswadu changu.
Jamaa "Wewe unasema jamaa ni brother wako lakini jamaa nimemuuliza anasema hakujui"
Basi nilimtazama Gabriel nikadhani uenda ataniangalia ili anipatie ishara yeyote lakini jamaa akawa ameangalia chini tu huku akichezea vidole!.Baada ya kuona jamaa aniangalii mimi ikabidi nikomae kwamba jamaa ni brother angu!.
Jamaa "Sawa bwana umughaka naona mnateteana Mkurya na muarusha!"
Aliendelea "Jamaa mpaka sasa ameshakupatia shilingi ngapi bwana Umughaka!"
Lile swali kiukweli lilifanya nikakosa pozi nikaanza kujiuma uma hata kujibu nikashindwa!,na kibaya zaidi jamaa alikuwa anauliza kama utani lakini alionyesha yuko serious sana!.
Jamaa "Huna haja ya kuficha kaka wewe kuwa mkweli tu ili ukaendelee na shughuli zako".
Mimi "Kiukweli nikihesabu haraka haraka inaweza kufika milioni 1"
Jamaa "Hebu kuwa serious kidogo kaka uache utani,yaani miezi takribani mitano mnafanya kazi awe amekupa milioni 1 tu!"
Aliendelea "Acha hizo mambo bhana,wewe eleza ukweli ili uondoke ukafanye shughuli zako"
Mimi "Kaka hiyo ndiyo nayo ikumbuka"
Jamaa "Haya bhana!"
Aliendelea "Marco hebu nendeni na jamaa mpaka kwake huko nadhani atawaeleza vizuri,pengine hapa anaona aibu"
Basi baada ya jamaa kusema vile,kuna jamaa kati ya wale waliokuwa wamesimama akanishika shingoni akaniambia nisimame tuondoke!,kiukweli nilichanganyikiwa sana siku hiyo na nilifahamu kabisa mambo si mambo,nilijua tu kuna namna Gabriel na mkewe watakuwa waliharibu mahali na mimi sasa ndiyo kujikuta nimo kwenye msafara!.
Tulipotoka nje wale jamaa waliniambia nitembee pasipo kuwa na hofu yeyote na wala nisije kujaribu kukimbia maana wangenipiga mpaka waniue!.Basi tukaanza kutembea kuelekea barabarani kutafuta Hiace ili twende mpaka mjini tukapande mchomoko kuelekea sirari.
Sasa wakati tunatembea,jamaa wao walikaa kushoto na kulia,mimi nikawa katikati yao!.Muda huo tulikuwa tunapiga stori za kwaida kabisa kana kwamba hakuna tatizo huku mimi nikionyesha Kicheko feki kilichojaa majuto ndani yake! .
Kumbe mzazi wako alikuwa mwalimu sasa kipi kilitokea ukawa mwehu?Hongera sana kaka yangu wa Rebu unasimulia kama series yanii unatamani episode zitiririke.... napakumbuka rebu aisee wazazi walifanya kazi mkoa wa Mara na mama yangu alifundisha shule ya msingi Rebu enzi hizooooo UMUGHAKA
KhaaaaaKumbe mzazi wako alikuwa mwalimu sasa kipi kilitokea ukawa mwehu?