Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 13.

Mimi "Mama nyakuru Mwita"

Mama "Tata sabhoke"

Ilikuwa ni heshima na salamu ambayo nilimpatia mama yangu baada ya kuwa nimefika hapo sokoni kwenye meza aliyokuwa akifanyia biashara!.

Mama "Ulienda wapi baba?"

Mimi "Nilikuwepo tu mama!"

Mama "Mbona umenenepa hivyo,au umepata kibarua huko baba!?"

Mimi "Nabangaiza tu hivyo hivyo!"

Mama "Nilimpigia mama yako mkubwa lakini akaniambia uliondoka na akajua labda ulirudi nyumbani"

Mimi "Mama nilienda kupambana na maisha yangu!".

Mama "Sasa baba utaendelea kuhangaika hivi hadi lini,rudi nyumbani mimi niliongea na baba yako na akasema hayo yameisha"

Mimi "Mama kwa umri huu siwezi kukaa tena pale nyumbani"

Mimi "Nilipita tu kuwasalimia"

Mama "Ulipita nyumbani?"

Mimi "Nimeanzia huko ndiyo nikaja hapa"

Mama "Dada yako alikuja na amemaliza kuondoka wiki iliyopita!"

Aliendelea "Chukua namba yake utawasiliana nae alisema ukirudi nikwambie umtafute"

Basi baada ya mazungumzo na mama nilichukua ile namba ya dada yangu mkubwa(Sarah)kisha nikaondoka zangu!.Mama yangu mara zote alikuwaga rafiki yangu kipenzi,pamoja na lile seke seke la mzee lakini bado alitaka nirudi pale nyumbani kitu ambacho kisingewezekana kwa wakati huo!.Sasa wakati naondoka nilimpigia dada yangu simu ili kumjulia hali maana tangu nilivyokuwa nimemaliza shule sikuwahi kuongea nae kwasababu yeye alikuwa ameolewa huko Mwanza!.

Baada ya kuongea na dada kwa dakika kadhaa alishangaa sana kwa kile kitendo ambacho mzee alinifanyia na alilaumu sana kwanini nilishindwa kumshirikisha kwa muda wote huo nikawa kimya!.

Da'Sarah "Sasa sikuhizi unafanya kazi gani hapo Tarime?"

Sikutaka kabisa kumficha kitu dada nilimwambia niliamua kuwa mpiga debe angalau maisha yaendeleee,alinishangaa sana ya kwamba nawezaje kuwa na elimu halafu niende kupiga debe!.

Da'sarah "Nilimwambia baba ukweli na kama ni kuchukia ngoja achukie,haiwezekani pesa anamalizia kwa mama yake Robina halafu sisi tunahangaika!"

Aliendelea "Kwahiyo sasa ulikuwa unakaa wapi?"

Mimi "Niliamua kupanga hapo Sirari!"

Da'Sarah "Ngoja nimwambie shemeji yako aje akutumie nauli uje huku"

Aliendelea "Na huyo mzee wala usimwambie chochote,muacheni na hela zake,yeye si anaona mama yetu hana maana!"

Mimi "Mimi nishamsahau na wala sihitaji hata kumi yake!"

Mimi " Halafu dada kama huko kuna sehemu ya kufikia hilo suala la nauli kwangu alinisumbui,we hata usimsumbue shem we kama inawezekana hata leo nianze safari"

Da'Sarah " Sasa hivi kweli kuna gari za kutoka hapo kuja Mwanza?"

Mimi "Hilo suala wewe niachie mimi,mimi nikifika nitakwambia"

Da'Sarah " Sawa wewe panda gari uje kama una nauli na ngoja nimpigie shemeji yako simu muda huo!"

Ile kauli ya Dada kunitaka niende Mwanza nikama ilinisaidia maana mpaka wakati huo nilikuwa sielewi hatma yangu!.Basi nilielekea mpaka stendi ambako nilikuwa nikitembea kwa umakini na tahadhari kubwa ili nisije kujikuta naangukia mkoni mwa mapongo,wakati huo begi langu lilikuwa na hela lipo mgongoni sikutaka kabisa kuliachia!.Basi nilipofika pale stendi nilidandia Hiace za Musoma ambako nilipanga nikifika pale Zero zero( Makutano) nisubiri gari zinazoenda Mwanza kutokea Musoma mjini!.Nilifika pale Makutano mida ya saa 9 alasiri na nikatelemka kusubiri gari za Mwanza.

Sikutaka kupandia gari za Mwanza pale Tarime mjini maana kulikuwa na wajuaji wengi hivyo nikawa naogopa kukamatishwa!.Basi haukupita muda nikawa nimepanda gari za Mwanza na nikawasiliana na dada nikawa nimemjulisha nishapanda gari!.,Kiukweli akili yangu mpaka wakati huo ilikuwa inawaza mambo mengi sana,sikujali ya kwamba Sirari nimeacha vitu vyangu wala nini,mimi nilichojali ni usalama wangu na kama ni vitu niliona ningevifata hali ambapo ingetulia!.

Wakati nikiwa kwenye gari nilimtafuta mshikaji wangu Mtatiro ambaye niliamini yupo Mwanza na nilipanga nikifika Mwanza tuonane!.


Mimi "Mwanangu vipi?"

Mtatiro "Mwanangu umekuwa adimu sana kama mate ya nyoka!"

Mimi "Ahahahaa ahahaaa,nambie mwanangu"

Mtatiro "Nimekutafuta juzi kati ulikuwa hupatikani!"

Mimi "Kuna mahali nilikuwepo mtandao ulikuwa haushiki kaka"

Mimi "Nipo njiani mwanangu nakuja M-Z-A"

Mtatiro "Unakuja lini,leo!?"

Mimi "Yeah nipo njiani"

Mtatiro "Umefika wapi?"

Mimi "Tunakaribia Kiabakari"

Mtatiro "Mimi sipo Mwanza mwanangu"

Mimi "Ulirudi Tarime?"

Mtatiro "Hapana,nipo hapa Bunda kuna ki mgodi kimetema ndiyo tupo na brother"

Mimi "Duuu!"

Mtatiro "Mwanza unaenda kwa nani?"

Mimi "Naenda kwa sista Sarah!"

Mtatiro "Mwanangu achana na habari za Mwanza kwanza,we kama vipi telemkia hapo Bunda mimi nitakufata uje tuone kama tutapata chochote"


Mtatiro alinishawishi hadi nikajikuta tena safari ya Mwanza kama imetoweka moyoni mwangu,nilichokuwa namshukuru Mshikaji wangu Mtatiro alikuwaga kila fursa haachi kunishirikisha kama rafiki yake,iwe haramu au iwe halali,kiukweli kwenye hilo sitamsahau jamaa yangu(Kwasasa anaishi Uganda).

Mtatiro "We mwambie Konda akushushe kituo kinaitwa Nyasura"

Aliendelea "Akikushusha hapo Nyasura ndiyo itakuwa jirani na huku nilipo!"

Mimi "Sawa"

Basi safari ikawa inaishia Bunda ingawa nilishalipa nauli ya Mwanza moja kwa moja,sikuona taabu kwasababu bado fungu nilikuwa nalo la kutosha.Ingawaje pesa niliyokuwa nayo ilikuwa haramu lakini ilikuwa inanipa kujiamini kwingi sana!.

Baada ya safari ya dakika kadhaa tukawa tumefika pale Bunda na mimi kushushwa hapo Nyasura kama Mtatiro alivyokuwa amenielekeza!.Basi nilimpigia simu Mtatiro nikamueleza ya kwamba nishafika hapo Nyasura,jamaa akawa amenitaka nipumzike sehemu aje kunifuata maana alipokuwepo yeye kulikuwa na umbali mrefu kidogo!.
Bado fuko la pesa huliachi tu, una phd ya ubishi
 
Umeamua ukabadili hizo pesa kwa wachimbaji.
Unachokitafuta utakipata😂
 
Nilichojifunza!
1. Usifanye dili haramu na mwanamke hususani mpenzi
2. Rafiki anamuchango mkubwa kukutengeneza au kukuharibu tabia
3. Hakuna aliyemkamirifu ( mapongo walimwibia OMUGHAKA Pesa zake) na Bosi zao mapongo WALIWAACHIA kwa Kupokea RUSHWA ...
4. Kumfukuza mtoto nyumbani nikutaka kumpoteza! Omghaka ni mwanaume vipi kwa dadazetu si angekuwa KAHABA!
5. Elimu ya secondary kwa mtoto ni chimbuko la kuinuka au kuanguka kimaadili
6. Tamaa mbele mauti nyuma
7. Maisha ni vita
8. Pesa nyingi zinatokana na dili haramu, Rushwa, TOZO, magendo na sadaka feki Zilizo pambwa majina mazuri kuhalalisha! Lakini msingi wake mkubwa ni HARAMU
 
Mkuu Hoaxer huo utaratibu kwa mipakani ni kitu cha kawaida kabisa,labda kama hujawahi kukaa mipakani,uliza wenyeji wa Sirari wakuambie
Mkuu huyu hajui sirari kule njia za kuingia Kenya ni nyingi Sana Tena vichochoroni
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 14.



Baada ya kumsubiri Mtatiro hapo Nyasura kwa muda hatimaye nae akawa amekuja akiwa anaendesha baiskeli,kiukweli kama kawaida nilipokuwa nikionana na jamaa yangu huyo utani wa hapa na pale pia furaha kwa kiasi fulani ilichukua nafasi.


Mtatiro "Mwanangu unazidi kung'aa tu,naona Tarime imekukubali"

Mimi "Aah wapi mwanangu ni kuridhika tu!"

Mtatiro "Vipi lakini kina Monche na washikaji wengine wazima?"

Mimi "Mwanao Monche sijamcheki muda mrefu,siunajua tena mimi zangu muda mwingi huwa ni Sirari tu!"

Mimi "Nadhani atakuwepo!"

Mtatiro "Jamaa huwa nampigiaga simu hadi leo haipatikani"

Mimi "Uenda atakuwa alibadili simu"

(Monche alikuwa ni yule dereva wa ile Hiace ambayo Mtatiro alikuwa akifanyia kazi kabla hajaondoka kwenda Mwanza,hivyo walikuwa washikaji).

Wakati tunaondoka hapo Nyasura kuelekea huko walipokuwa kina Mtatiro,tuliamua kutembea ili kuendelea kupiga stori maana ilikuwa ni muda umepita sijaonana na jamaa,ile baiskeli japo ilikuwa na Carier(sehemu ya kukalia)lakini tuliona ni vema tutembee huku mastori yakiendelea.Tukiwa njiani niliamua kumwambia ukweli Mtatiro mambo yaliyokuwa yamenitokea kwasababu ukizangatia ni yeye ndiye aliyekuwa ameniunganisha na Gabriel.

Mtatiro "Jamaa sijaongea nae muda sana"

Aliendelea "Kwahiyo mlichomokaje?"

Mimi "We acha mwanangu!"

Mimi "Kuna jamaa anaitwa Eric ndiye aliyetuchomoa"

Mtatiro "Aah Eric nammanya mwanangu"

Aliendelea "Yule jamaa ndiye mwenye ile michongo na hata Gabriel ni mpambe tu!"

Mimi "Jamaa watakuwa wamemdaka maana baada ya kutoka Migori nilimtafuta lakini hapatikani!"

Mtatiro "Zile mishe zina njuruku(pesa) lakini ni hatari sana mwanangu,kila muda unakuwa macho kodo kama popo!"


Mimi "Mwanangu ninao mzigo kwenye begi!"

Mtatiro "Acha utani wewe!"

Mimi "Kwanini nikutanie!"

Mtatiro "Hebu tuone mwanangu!"

Nilishusha kile kibegi toka mgongoni nikawa nimempatia Mtatiro akawa amefungua na kutazama zile pesa ili ahakikishe nilichokuwa nakisema kama kina ukweli!.

Mimi "Hizo nilikimbia nazo kuingia Kenya ndo zimebaki!"

Mtatiro "Mwanangu hizi mbona zitatoka,we subiri uone!"

Basi baada ya mwendo mrefu huku tukiendelea kupiga mastori,Mtatiro akanitaka nipande kwenye baiskeli ili apige pedo(aendeshe) kwasababu bado kulikuwa kuna umbali tulipokuwa tukienda!.Baada ya muda tukawa tumefika hapo Kijijini ambako aliniambia kulikuwa na mgodi umetema,kiukweli palikuwa ni kijijini ambako hakukuwa pabaya sana maana karibia huduma zile muhimu zilipatikana hapo!.
Tulifika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na nyumba mbili za nyasi,Mtatiro akawa ameingiza baiskeli ndani akanitaka niweke lile begi ndani,akafunga ule mlango na kufuli akawa ameniambia tuelekee hapo kwenye hicho kimgodi!.Baada ya kufika pale mgodini tulikuta raia wanapambana kuchimba mashimo,kuna wengine walikuwa wamechimba mashimo marefu kiasi kwamba walikuwa hawaonekani,kuna ambao bado nilikuta waking'ang'ana kuchimba huku mashimo yakiwafika magotini!.Kiukweli kulikuwa na watu wengi sana huku kina mama wakiwa wanahangaika kubeba vifusi kwenye makarai na ndoo wakirundika mchanga kila mtu kwenye eneo aliloona kwake litakuwa salama kabisa.

Mtatiro alinipeleka mpaka kwenye shimo alimokuwa kaka yake na jamaa mmoja wakiendelea kuchimba,ile kazi ya uchimbaji haikuwa ya kitoto maana kulikuwa na vikokoto mshenzi kama vyote.

Sasa kwakuwa nilikuwa hapo ili kujaribu bahati yangu kwa upande huo wa madini,baada ya kumpa Hi brother ake Mtatiro nilikamata ndoo nikawa nasogeza ule mchanga pembezoni ya lile shimo!.Ile kazi tuliifanya hadi mida ya saa 3 usiku ndipo yule brother akasema tuondoke tukapumzike halafu kesho yake tungedamka mapema kuendelea!.Kiukweli familia ya kina Mtatiro haikuwaga na mambo mengi,nilichokuja kugundua ilikuwa ni familia yenye upendo sana,sema ndiyo hivyo tu hawakujaliwa kuwa na pesa!.


Ukweli ni kwamba,jamii yangu ya kikurya ni jamii ambayo huwa ina upendo na kuwajali watu wengine pia,ukiachilia tu yale madhaifu madogo madogo kama wanadamu wengine lakini wakurya ni kabila bora sana miongoni mwa makabila bora kwenye hii nchi!,yale madhaifu madogo madogo ya kupiga mwanamke,kukeketa na kuchinjana ovyo yalikuwaga ni kwasababu ya ukosefu wa elimu tu,sikuhizi hayo mambo kwa Tarime yamepungua na kama siyo kuisha kabisa baada ya watu kuelimika!.Tarime ni njema sana na atakaye na aende akajionee!.(Nilikuwa nachomekea tu ndugu zangu).

Tulipofika hapo nyumbani kwakuwa tulikuwa wanaume tupu,tulikoka moto tukaanza kupika ugali ambao tulikula na dagaa zilizokuwa zimepikwa mchana!.Namshukuru Mungu kulipokucha asubuhi Mtatiro alinipatia nguo zake ambazo zilikuwa zimechoka ili nivae twende tukapige kazi!.Kiukweli nilipofika hapo mgodini hiyo asubuhi tulikuta nyomi la watu kila mtu akiwa anapambana kwa upande wake!.Kama kawaida na sisi tukaanza kazi iliyotupeleka hapo,nikiwa nimekaa nasubiri udongo ili niupeleke maeneo husika,simu yangu ilianza kuita,ile nimeitoa mfukoni na kutazama nikakuta ni Da'Sarah alikuwa akinipigia!.


Da'Sarah "Mdogo wangu uko wapi?"

Mimi "Nisamehe Dada jana sikuwa na Vocha nikashindwa kukwambia niliteremkia hapa Bunda!"

Da'Sarah "Bunda tena umeenda kufanya nini!?"

Mimi "Hivi wale watoto wa mzee Marwa bado unawakumbuka?"

Da'Sarah "Marwa yupi?,yule jirani?"

Mimi "Eeh"

Da'Sarah "Mi namkumbuka yule mwanajeshi tu Ryoba"

Mimi "Sasa yupo mdogo wao ambae ni rika langu na ni rafiki yangu anaitwa Mtatiro,nilipita kumsalimia kaka yake anaumwa,alinipigia simu jana nikiwa kwenye gari nakuja hivyo nikaona niteremke kuja kumjulia hali!"


Niliamua kumdanganya dada yangu sababu ya mimi kuteremka pale Bunda ni kwenda kumuona kaka yake Mtatiro ambaye alikuwa mgonjwa ili asiendelee kunifikiria vibaya!.


Da'Sarah "Kwahiyo unakuja lini Mwanza!"

Mimi "Najitahidi dada nitawahi"

Da'Sarah "Uwahi kuja maana niliongea na shemeji yako akaniambia kuna muhindi alikuwa anatafuta mtu wa kusimamia boti zake za uvuvi"

Aliendelea "Siyo tumpange mtu kumbe na wewe huko una mambo yako!"

Mimi "Sawa dada nakuja"

Shemeji yangu alikuwaga akifanya kazi za uvuvi na yeye pia alikuwaga na mitumbwi yake kadhaa kwa ajili ya shughuli yake hiyo.Baada ya yale mazungumzo kazi zikaendelea kama kawaida,sasa lile eneo lilikuwa maarufu sana kama Nyasana Mgodini,kiumweli ni eneo lililokuwa limechanganya sana lakini jambo la ajabu hakukuwa na madini wala nini,maana Mtatiro alikuwa ananiambia wao wapo pale ndani ya mwezi na hakuna walichoambulia zaidi ya kupoteza hela tu!.


Mtatiro "Mwanangu hapa napo ni hasara tu,kila siku mara utasikia kuna kimkanda kimepita hapa,watu wakichimba kwenye hicho kimkanda hawaambulii kitu!"

Mimi "Kwani mlianza kuchimba lini?"

Mtatiro "Mimi nimekuja mwezi uliopita,lakini kina braza hapa wana miezi miwili,ndani ya miezi yote hiyo hawajawi hata kupata punje ya dhahabu!"

Mimi "Duuu!,mbona ni hatari"

Mtatiro "Kuna jamaa wao ndiyo walidai kuna mkanda umepita chini kutokea Geita,sasa watu wote hawa unao waona wanapambana kuutafuta mkanda!"

Mimi "Hakuna watu waliopata dhahabu hata mara moja?"

Mtatiro "Watu wanadai wanapata pata kimtindo lakini ukijaribu kuuliza waonyeshe walizopata hata huonyeshwi"

Aliendelea "Nishamshauri braza tuachane na hii biashara kichaa lakini hasikii,yeye bado anaamini kuna madini"


Kama kuna sehemu watanzania huwa wanapoteza muda na kulishana matango pori ni kwenye vimigodi uchwara,yaani unakuta wanaamini eneo husika kuna madini huku wakiendelea kupambana kwa nguvu na kupoteza pesa lakini mwisho wa siku wanaambulia patupu,na ndivyo ilivyokuwa hapo Nyasana,kuna muda unawaangalia ndugu zetu watanzania wanavyohangaika hadi huruma kwakweli,lile eneo ilikuwa inasemekana dhahabu ililipuka tu na watu wakaanza kujaa kwa wingi na kuanza kuchimba,sasa sikujua kama kuna wataalamu waliwahi kupima uwingi wa dhahabu ulioko pale ama la!.(Sijui kama hadi leo huo mgodi unafanya kazi).

Kuna muda tulikuwa tunatoka na mtatiro tunaingia mtaani kule kijijini tunabadili zile hela,tulipoona chenji kijijini hapo imekuwa ngumu tulikuwa tunaelekea pale senta ya Nyasura kupambana na ubadilishaji wa kununua bidhaa halisi na kurudishiwa chenji halali!.Kiukweli ile hela ikabaki chache sana!.

Kuna siku tukiwa tumetoka na Mtatiro tukiwa maeneo ya Bunda mjini kwenye mishe mishe hizo,simu yangu ikapigwa ikiwa ni namba ngeni!.

Mimi "Halloo"

Yeye "Mambo Umughaka"

Mimi "Poa,nani!"

Yeye "Hebu acha utani,kwahiyo namba yangu ushafuta!"
Mkuu mwaka 2008 nilikuwa hapo mgodini nyasana
 
Nilichojifunza!

8. Pesa nyingi zinatokana na dili haramu, Rushwa, TOZO, magendo na sadaka feki Zilizo pambwa majina mazuri kuhalalisha! Lakini msingi wake mkubwa ni HARAMU
Dili haramu zinalipa sana,unakuta kwa siku unatengeneza faida ya mpaka laki 5 tena kwa mtaji mdogo tu
 
Endelea endelea pls! Hivi pale tarime Nk bado ipo? iliyopo karibu na crdb bank? Kwa wenyeji wa Tarime
 
Back
Top Bottom