Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Hapa watu unawaandaa kwenda waibia. Na pia kuna watu wanatafutwa wajichanganye.... Wewe lete story humu hamna haja ya kuonana. Unataka uwateke na kuwaibia watu?hizi mbinu tunazijua. Usione tumo humu ukadhani wajinga.... Lete story weka episode nyingine leo haraka. Acha ujinga wa kutaka pesa kibwege. Lete story nasubiri.
mkuu punguza makasiriko, tafuta pesa, hujalazimishwa na mtu kuchanga, anaeamua ni mwenyepesa, sio wewe utupangie tusichange, no.
 
UMUGHAKA umekwenda kumchukua umukungu wako huko Kibumayi ache kukusaitia kutengeneza tengeneza ubusara na kukupikia kirerema & kitinya hapo Bhunju eti tatah mutimbaru
Tatoo vocab ya ndani ndani sana tatamura🤩🤓 kirerema&kitinya noma sana kikiwa mixed na steki/kemoro pembeni mtindi fresh kabisa amang'ana amachomu tata mtimbaruuu sokoro UMUGHAKA
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 9.


Nilifunguliwa lile geti nikawa nimetoka mle ndani.Yule askari aliyenifungulia alinichukia mpaka kwenye kile chumba ambacho jana tulifikishiwa baada ya kufika hapo kituoni!.Sasa nilipofika hapo nilimkuta jamaa mmoja aliyekuwa amevaa suti nyeusi,pembeni yake alikuwa amekaa Gabriel ila shemeji ambaye ni mke wa Gabi sikumuona!.

Afande "Kaa chini bhana hapa huwa hatusimami!"

Afande aliyeniambia nikae chini ndiye yuleyule aliyekuwa akituhoji ile jana na ndiye niliyemkuta kule nyumbani kwa Gabriel!.Basi mle ndani kulikuwa na ukimya wa muda fulani ambapo yule askari yeye alikuwa akiendelea kuandika huku kila mmoja akiwa kimya akimtazama.

Afande "Mkuu nadhani sasa tutawasiliana"

Jamaa "Sawa,haina tatizo!"

Basi baada ya hapo nikaambiwa na yule afande niende pale mapokezi nikachukue vitu vyangu nilivyokuwa nimekabidhi kabla ya kuingizwa Selo!.Baada ya kukabidhiwa vitu vyangu nakutoka nje,ndipo Gabriel akanitaka nipande gari iliyokuwa imepaki kando ya hilo jengo la kituo cha polisi na ilikuwa ni Toyota Prado nyeupe!.Basi nilipoingia ndani ya ile gari nikamkuta na demu wa Gabriel.

Yule jamaa aliyekuwa amevaa suti yeye alikaa mbele kando ya dereva halafu na sisi watatu tukakaa nyuma!.Gari ile iliondoka na tukaelekea nyumbani kwa Gabriel maeneo ya Buhemba!.Tulipofika tulishuka na kuingia ndani ambapo kila mmoja aliingia bafuni kuoga na kubadili nguo,sasa kwakuwa mimi nguo zangu zilikuwa Sirari,Gabriel aliniazima nguo zake nikavaa ingawa aliniambia nisimrudishie amenipatia kama ndugu yake!.

Baada ya hapo yule Bosi wa Gabriel alisema tutoke tutafute sehemu iliyotulia ili tupumzishe akili,sasa wakati tunatoka Gabriel akasema mkewe abaki pale nyumbani,sasa yule bosi wake akasema inabidi twende wote lakini Gabriel akakataa akasema yeye abaki na kama ni chakula angeletewa!.Basi tukawa tumeondoka kuelekea mjini!.

Basi baada ya kufika hotelini ile gari ikapaki na sisi tukashuka kuingia ndani!,baada ya kupata msosi wa nguvu ndipo kila mmoja akaanza kushushia vitu vyake,baada ya kupiga vitu niliona sasa Gabriel akaanza kuchamngamka!.

Gabi "Unajua yule mwanamke ni mpumbavu sana Bosi!"

Bosi "Nani!,Mkeo?"

Gabi "Aah! yule si mke wangu hata hivyo mi napita tu!"

Bosi "Kwanini unasema hivyo!"

Gabi "Kila siku naongea lakini yanapitia huku yanatokea kule"

Aliendelea "Ukiachana na hii ishu lakini nadhani unakumbuka kipindi kile Babati ilivyokuwa kaka!"

Bosi "Yeah!,sasa inabidi uwe makini maana serikali sasa hivi wako makini sana,sema ndiyo hivyo tunabanana na hawa askari,lakini kama sivyo ni hatari sana!"

Sasa mimi sikutaka kabisa kuingilia yale mazungumzo lakini nilichokuja kugundua ni kwamba,yule demu wa Gabi ndiye yawezekana alisababisha yale majanga kwasababu Gabi alikuwa amechukia sana na sikujua alisababishaje maana mimi hakutaka kabisa kuniambia na inaonekana si mara moja,yeye na huyo bosi wake ndiyo walikuwa wakifahamu,mimi kazi yangu niliifanya kwa uaminifu kabisa na sikuwa na longo longo!.

Sasa mpaka tunatoka pale polisi aliyesababisha sisi kutoka ni huyo jamaa ambaye Gabi alikuwa akimuita bosi,sikujua amefanya fanyaje hadi sisi kutoka lakini niliamini ilikuwa ni fedha inaongea maana jamaa alionekana alikuwa na hela hatari,na kitu kingine nilichokuja kukigundua baadae ni kwamba yule jamaa ndiye alikuwa akimpatia Gabi zile fedha!.Hii nchi kuna dili haramu nyingi sana lakini huwezi kukuta watu wanaohusika wanawekwa ndani,siye vinyangarakata tusio na mbele wala nyuma ukizingua kidogo tu,utafia gerezani!.

Bosi "Hivi uliniambia huyu jamaa anaitwa nani!?"

Gabi "Huyu anaitwa umughaka"

Bosi "Ooh sawa!"

Aliendelea "Sawa bana nyie fanyeni kazi kwa umakini,najua kwasasa hakuta kuwa na wanoko maana wale wajinga tushamalizana!".

Sasa wakati nikiwa naendelea kukung'uta vyombo nilikuwa nawaza namna ya kuachana na ile biashara kichaa japo ilinipatia pesa ya kutosha lakini niliona inaweza kuniingiza kwenye matazizo makubwa!.Baada ya kupiga vyombo na kuona vimenitosha niliwaaga wao ili mimi nijikatae kwenda Sirari!.

Gabi "Unawahi wapi wewe,wewe kaa utatindike beer,kwako utaenda tu!"

Basi niliamua kukaa chini tena ili niendeleze makamuzi,baada ya kila mtu kuridhika siku hiyo tuliondoka,Gabi alinishawishi sana hatimae sikwenda Sirari nikaamua kwenda kulala kwake ili asubuhi anipatie fungu niondoke nalo kuelekea Sirari!.Baada ya kutufikisha pale nyumbani yule Bosi na dereva wake wao waliondoka.

Namshukuru Mungu asubuhi niliwahi kuamka na ndipo nikaelekea sebuleni kumsubiri Gabi aamke anikabidhi pesa haramu ili mimi nichafue zangu,sasa shemeji ndiye aliyetangulia kuamka na kuja pale sebuleni.

Mimi "Mambo vipi shemu"

Marieta "Safi,za tangu jana"

Mimi "poa kabisa"

Mimi "Jamaa bado amelala?"

Marieta "Ngoja nimuamshe"

Basi baada ya dakika 10 jamaa akawa amekuja pale sebuleni.

Mimi "Nataka kuondoka kaka,unaweza kunipatia mzigo?"

Gabi "We nenda tu nitakuletea huko,pia kuna jambo nikija tutazungumza"

Mimi "Poa,basi acha mi niwahi"

Gabi "Mida ya saa 10 jioni nitakupigia simu tuonane mahali"

Mimi "Poa kaka"

Baada ya mazungumzo yale mi nikamuaga jamaa nikaondoka zangu,sikujua ni kwanini jamaa alibadili maamuzi ile asubuhi kwasababu jana yake tulikuwa tumeongea akawa amesema asubuhi angenipatia hela lakini alibadilika.Yeye na huyo demu wake kiukweli baada ya hilo sekeseke inaonekana kabisa hawakuwa sawa na sikufahamu tatizo lilikuwa ni nin!.Sikutaka sana kuchimba na kuuliza uliza mambo ya ndani kwani ningeonekana mjuaji!,nilichoshukuru mimi ni kutoka nje na ile kesi iliisha!.


Baada ya kufika pale Sirari wanangu walitaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha hadi kujikuta nipo mikononi mwa mapongo.Sasa sikutaka kuwaeleza ukweli ikabidi nifanye siri kabisa,nilichowaambia ni kwamba kuna mtu alikuwa akinidai na hivyo aliamua kunipeleka polisi,wao wakaamini hivyo kumbe haikuwa hivyo!.

Sasa ilipofika mida hiyo ya saa 10 alasiri,Gabi akawa amepigia simu na kweli akawa yupo pale Sirari na akaniambia tuonane kwenye ile bar tuliyokutana ile siku ya kwanza.


Muendelezo > Sehemu ya 10
Maisha ni mapambano.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hapa watu unawaandaa kwenda waibia. Na pia kuna watu wanatafutwa wajichanganye.... Wewe lete story humu hamna haja ya kuonana. Unataka uwateke na kuwaibia watu?hizi mbinu tunazijua. Usione tumo humu ukadhani wajinga.... Lete story weka episode nyingine leo haraka. Acha ujinga wa kutaka pesa kibwege. Lete story nasubiri.
Tanzania kila mtu anajiona great thinker kisa ana account jf! Eti lete story nasubiri! Yani alete kwa amri yako? Ushamuona mwizi sasa unamfatilia wa nini? What do you see in yourself?
 
Nyie ndio wabishi kwa kuona bodaboda ni kazi ya chini wakati kuna watu wanalea familia, wamejenga sababu ya bodaboda. Kweli siku haziwezi kufanana lakini bodaboda ina hela sana kama mtu yupo serious na kazi yake. Kinachowaponza bodaboda na bajaji ni ulevi, bangi, umalaya na kamali ndio zinaishia hela zao na madeni juu. Sibishi mimi kazi yangu ilikuwa pembeni kijiwe cha bodaboda nilijifunza mengi sana kuwahusu.

Bodaboda yupo radhi atoe 20000 ya guest kula mzigo na akampeleka mtu huyo bure ruti ndefu labda mbezi hadi gmboto hapo kashapoteza kiasi gani. Bado hajalewa na kucheza kamali. Na wala hawajali kuhusu kesho as wanajua kesho ikifika nitapata tena.

Sikushauri kununua bodaboda kuwapa madereva wao wanachojali ni kula, kulewa na kamali yupo radhi asipeleke hela ya bosi ila akacheze dubwi amalize hata 40000 huko. Pamoja na urafiki nao kindakindaki siwezi kurisk kununua bodaboda kumpa dereva anajua hata asipokupa hela yako utachukua chuma yako leo kesho anapata nyingine maisha yanasonga.

Kwa mtu anayejielewa na kujua nini anafanya kutoboa kwa bodaboda ni rahisi sana sometimes biashara inakuwa ngumu kwao ila nina ushahidi usio wa stori kuwahusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
"Wamejenga kwa sababu ya bodaboda" huu msemo wa hovyo sana.
 
Bodaboda "Wamejenga kwa sababu ya bodaboda" huu msemo wa hovyo sana.
Msemo wa hovyo ila ndio ukweli huo. Bodaboda ni kazi kama ilivyo uhasibu, na kazi nyingine na inawapa ridhiki kama wenye kazi zingine pia. Sema tuu watu wachache wanaipa sifa mbaya kazi.

Mimi baada ya kuwa nao karibu nikabadili kabisa fikra zangu kuhusu bodaboda mwanzo nilikuwa nawaweka kwenye kundi fulani ambalo lipo chini ila kuna watu wanaheshimika na wana familia zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi sifungui tena mpaka wiki 2 zipite najua nao utakua umeisha, hii arosto inatesa sana
 
Leo nipo na ninyi vilaza. Hasa wewe mtunga hadithi halafu unatumia ID zako nyingine kutaka waibia watu. Sisi wengine tuna akili. Lete episodes nyingine hapa tupoteze muda tupo mapumzikoni. Ila kuomba omba pesa ukome. Hatukuomba utunge hizi stories. Ni kukosa kwako kitu cha kufanya ukaona utuburudishe. Sasa leta burudani hapa.[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Hajawah omba popote pesa
 
Sio vizuri kuwaita watu majobless sababu kazi ni majaaliwa. Hata wewe ulienakazi leo unaweza kuipoteza kesho na ukala msoto heavy. Ambao tulishakuaga in,out,in,out,in kwenye kazi tunaelewa
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 12.

Niliendelea kumtazama dogo kwa makini asije kuwa anakuja na watu ili ikiwezekana nichukue hatua katika mbio!.Baada ya kujiridhisha ya kwamba alikuwa akija yeye mwenyewe nilikaa kwa kutulia nikiendelea kumsubiria!.

Dogo "Bro jamaa kasema akupatie ngapi!"

Mimi "Sijakuelewa!"

Dogo "Jamaa ameniambia waweza taka pesa ngapi kwa ile exchange!?"

Mimi "Kwani jamaa huwa anabadili kiasi gani kwa kila Tsh 10,000!"

Dogo "Sikia bro kwanini nisikupeleke kwa huyo mjamaa ukaelewane nae!"

Mimi "Jamaa anafanyia kazi zake wapi?"

Dogo "Yuko tu hapo ng'ambo na hata siyo mbali!"

Mimi "Hakuna wanoko?"

Dogo "Ati unasema aje!?"

Mimi "Hakuna tatizo nikienda kwake?"

Dogo "Wala hakuna problem yeyote,jamaa yuko fiti tu!"


Sasa baada ya mazungumzo na yule dogo kumbe alimuachia huyo jamaa ile hela na jamaa akawa amemwambia aje aniulize ili kujua kwenye ile laki mimi angenipatia kiasi gani, basi kiukweli niliogopa sana na nikaona uenda ulikuwa ni mchongo wa mimi kudakishwa!

Lakini nilipompeleleza yule dogo sana akaniambia jamaa anauza vifaa vya magari, hivyo pia huwa anabadilishaga na hela!.Basi ili kuonekana sikuwa na wasiwasi nikamwambia dogo tuelekee kwa yule jamaa!.Tulitembea kwa takribani dakika 4 tukawa tumefika kwa yule jamaa ambaye alikuwa na duka la spare za magari!.

Kiukweli niliamua kujiamini na niliamua kuiweka hofu kando,sasa yule jamaa alikuwa ni mkenya ambaye alionekana kiswahili kukifahamu vizuri japo kuna muda pia alikuwa akichapia!.

Jamaa "Mambo vipi bro"

Mimi "Poa kabisa"

Jamaa "Ni wewe ndiye umemwagiza Mkamilifu?"

Mimi "Yes ni mimi!"

Jamaa "Oooh hapo iko poa,maana hata sikumuelewa"

Aliendelea "Ulitaka sasa bro nikupee pesa ngapi?"

Mimi "Wewe huwa unabadili kiasi gani kwa kila Tsh 10,000?"

Jamaa "Mimi bro nitakupea Ksh 3500!"

Mimi "Ok sawa haina tatizo"

Basi kimoyo moyo nilikuwa namshukuru Mungu sana kukutana na yule jamaa maana kiukweli kama angekuwa mjuaji pale nisingechomoka!.Jamaa aliingia dukani akawa amenipa Ksh 3500 ambapo na mimi nilimpatia yule dogo Ksh 500.Sasa jamaa akaniambia kama nilikuwa ninapesa nyingine nimpelekee maana baada ya siku mbili alikuwa anatoka! sasa yeye alichoamini ni kwamba kupitia hela ile angejipatia faida mara dufu,kuna muda nilikuwa naona kabisa natenda dhambi lakini sikuwa na namna kwasababu mimi nilichotaka ni pesa tu!.

Jamaa "Bro kama uko na pesa ingine waweza tu niletea nikubadilishie!"

Kimoyo moyo nikasema "wewe humjui umughaka vizuri,ngoja nikuonyeshe mimi ni nani".Basi nilimwambia ningerudi jioni kuleta hela kiasi fulani anichenjie.Basi tuliondoka na dogo huku tukiendelea kupiga stori za hapa na pale,nilimwambia dogo anionyeshe maduka ya nguo ili ninunue sweta nivae maana kwa kipindi kile kulikuwa na baridi ya kiaina hapo Migori!.Baada ya kununua sweta mimi nilirudi lodge na dogo akaelekea kuendelea na mishe zake!.

Sasa ilipofika mida ya saa 12 jioni sikumuoma dogo nikajua uenda atakuwa ametingwa na majukumu,basi nikachomoa tena mle kwenye begi shilingi laki moja nikaelekea kwa yule jamaa.Nilipofika jamaa alinipatia Ksh 3500 kama kawaida na kiukweli alikuwa akinishangaa sana na alitaka kufahamu kwa Tanzania nilikuwa natokea maeneo gani,mimi nilimdanganya ni mwenyeji wa Mwanza!.

Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba, baada ya kujishughulisha na hiyo shughuli haramu hata muonekano wangu ulibadilika sana na ulikuwa ukiniangalia huwezi amini kama mimi ni mpiga debe pale Sirari!

Sasa baada ya jamaa kunipatia ile hela nililipa pale lodge pesa ya siku mbili nikawa nimebaki na pesa kadhaa!.Nilitaka nikae pale Migori ndani ya siku 3 halafu nigeuke zangu Sirari ili nikaone kama mambo yalikuwa yamepoa!. Niliamini ya kwamba kama jamaa angetoka akaenda kubadili zile hela halafu wakamshitukia basi najua angemtafuta dogo Joe akawaleta pale Lodge nikapata kashikashi, hivyo nilipanga nichomoke mapema kabisa!.

Sasa kabla ya kuondoka nilinunua begi dogo la mgongoni kisha nikanunua na suruali ya jeans moja nikawa nimebadilisha,zile hela niliziweka kwenye lile begi la mgongoni pamoja na ile shati niliyokuwa nimevaa siku naingia hapo Migori,ile sweta na jeans nikavaa nikawa sasa na muonekano mpya!

Sasa siku naondoka nilienda kuonana na yule dogo Joe pale stendi nikamkabidhi lile begi nikampatia na hela kiasi cha elfu 50 ya Tanzania,sasa ilikuwa ni juu yake kuzibadili ili aionjoi maisha,kama walidamka basi ni yeye na mungu wake!.

Nilipanda zangu shuttle za Isebania nikageuka zangu.Nilipofika pale Isebania nilishuka nikaingia zangu kitaani kupita njia isiyokuwa rasmi kuingia Sirari,ile njia walikuwa wakiipita watembea kwa miguu hivyo hakukuwa na bugudha toka kwa mamlaka zote mbili!.Ilijulikana ya kwamba watu wa Kenya wanapita kuingia Tanzania na watanzania walikuwa wanaingia Kenya kununua bidhaa na mahitaji.Sasa nilipofika hapo Sirari,sikutaka kabisa kwenda moja kwa moja nyumbani,nilianzia kwanza kijiweni!

Nilipofika pale niliwakuta wadau wangu wakiwa wanaendelea na kazi huku wengine wakishangaa na kuniuliza ndani ya siku mbili tatu hizo nilikuwa wapi!.Mshikaji wangu Nyamori sikumuona hapo kijiweni hivyo nikaelekea dukani kwa yule mama kununua vocha ili nimpigie simu.

Nilimpigia simu yake ikawa inaita tu bila kupokelewa,basi nilipoona haipokelewi nikaamua kuachana nae,sasa ikabidi nimpigie Gabriel,nilipoipiga namba yake ikawa haipatikani!,nikarudia tena lakini haikupatikana!.Sasa sikutaka kumtafuta kabisa yule mwanamke wake kwasababu nilikuwa nakifahamu kichwa chake kilivyokuwa kibovu!

Nia ya mimi kumtafuta Gabriel nilitaka kujiridhisha kama yuko hewani ili anieleze kilitokea nini siku ile,sasa nilipomkosa niliamua kupiga kimya!. Sasa wakati nikiwa naendelea kutafakari, kuna mshikaji alikuwa mdau hapo kijiweni nae alikuwa mpiga debe, huyu alikuwa akiitwa Magesa! Sasa jamaa akawa ananiambia kuna jamaa toka juzi alikuwa akinitafuta hapo kijiweni na hata asubuhi ametoka hapo kuniulizia!.

Mimi "Jamaa yukoje?"

Magesa "Ni jamaa mmoja hivi tolu halafu blaki!"

Mimi "Alikuwa anasemaje?"

Magesa "Aisee hata sijui maana juzi ameshinda hapa na hata leo pia amekuja lakini hakukaa!"

Mimi "Alikuwa na gari?'

Magesa " Sijajua kama ana gari maana hapa hakuja na gari"

Baada ya Magesa kuniambia vile kiukweli moyo wangu ulilipuka tena kwa hofu,kwa namna alivyozitaja sifa chache za huyo mtu nilijiridhisha kabisa ya kwamba hakuwa Gabriel.Sasa baada ya muda kidogo nikiwa pale kijiweni simu yangu ikawa inaita,kuangalia nikakuta ni Nyamori alikuwa akinipigia.

Nyamori "Mwanangu ulikuwa wapi?,mbona simu yako ilikuwa haipatikani!"

Mimi "Mwanangu nilienda hapo Migori mara moja"

Mimi " Nipo hapa kijiweni lakini sikuoni!"
Nyamori "Mi nilitoka niko Nyamongo tangu jana,kuna mzee tumemletea ng'ombe hivyo nitarudi jioni au kesho asubuhi"

Aliendelea "Sasa sikia,kuna jamaa mmoja ni askari namjua,toka juzi anakusarandia hapo kijiweni Mwanangu"

Basi baada ya jamaa kuniambia vile sikutaka kabisa kupoteza muda pale kijiweni nikawa nimeondoka,sasa ndipo nikaunganisha na yale maelezo ya magesa nikaona kumbe bado kulikuwa na msako unaoendelea kimya kimya!..

Nyamori " Mwanangu kwani kuna ishu gani?

Mimi "Mwanangu bado ni ile ishu ya deni!".

Nyamori "Kwanini usimwambie mshikaji uwe unamlipa kidogo kidogo mpaka umalize ili aache kukusumbua!"

Mimi "Nitajua cha kufanya Mwanangu!"

Yeye hakufahamu kwamba ni lile dili haramu ndilo lilikuwa likiniangaisha,alichofahamu na nilichomwambia ni kwamba nilikuwa ninadaiwa!.

Basi nikaondoka zangu nikawa natembea haraka uelekeo wa Tarime ili nikapande gari nielekee Tarime mjini,sasa sikutaka kunyooka na lami,nilipita pembezoni mwa barabara ili nikifika mbele nidandie gari mpaka Tarime!.Wazo la kurudi tena pale geto kwangu sikuwa nalo kabisa na niliamua kama ni vitu ngoja viozee ndani lakini si kwenda kujikamatisha!.

Sasa namshukuru Mungu nilifika Tarime na niliamua kupita njia nilizokuwa nazifahamu kuelekea nyumbani kwetu ambako Mzee miezi michache iliyopita alikuwa amenitimua!

Nilipofika hapo nyumbani nilimkuta binti ambaye nilikuwa simfahamu na nilipomuuliza wenyeji wameenda wapi akawa ameniambia Mzee hajui alipo kwenda ila mama yangu alikuwa ameenda sokoni na dogo Amos yeye alikuwa shule! sasa niliondoka mdogo mdogo kuelekea sokoni ambako mama yangu alikuwa akifanyia biashara zake!


Muendelezo > Sehemu ya 13
Ulivyokuwa mzembe mpaka mida huu wazo la kuchoma pesa feki (ushahidi hata ukikamatwa) moto huna.😂😂😂
 
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 15.



Mimi "Sidhani kama ningekuuliza kama ningekuwa nayo!"

Yeye "Jamani!,ila wanaume nyie hamuaminikagi kabisa!"


Aliendelea "Yaani umughaka leo nakupigia simu unaniuliza mi nani!"


Mimi "Hii line nime renew ile ya kwanza ilipotea!"

Yeye "Haya bhana,mi Leah"

Kiukweli ile sauti ya huyo mwanamke ilikuwa ni sauti mpya kabisa katika masikio yangu,mimi sikutaka mambo mengi nikawa nimeamua tu kumdanganya ya kwamba line ilipotea nika renew hivyo majina nayo yakaenda na maji,sasa aliponitajia jina la Leah ndipo akazidi kunichanganya kabisa kwasababu hakuna mwanamke niliyekuwa nikifahamiana nae akiitwa Leah.Nilikuwa nikijaribu kuvuta picha alikuwa ni Leah wa wapi lakini picha inakataa!,sasa nilifahamu uenda wakati nikiwa pale Sirari na washikaji wakati tunapiga mtungi kuna demu nimewahi kuchukua namba yake lakini kwasababu ya pombe nikashindwa kuisevu,niliamua kubaki na hiyo tafakari moja tu ya kwamba uenda tulikutana kwenye mabar huko!.

Sikutaka kumkatisha ili asijisikie vibaya,mimi nikaungana nae na kumpokea kwa kauli iliyoonyesha kumfahamu!.


Mimi "Oooh! za siku!?"

Yeye "Nzuri tu,uko wapi!"

Mimi "Nipo kijiweni"

Yeye "Mmh unanidanganya!"

Mimi "Kweli!,nipo kijiweni"

Yeye "Nimepita nikusalimie lakini sijakuona"

Mimi "Kwani we unajua mi nafanyia wapi kazi?"

Yeye " Tuachane na maswali mengi bhana,tuonane basi"

Mimi "Lini?"

Yeye "Leo kama itawezekana"

Aliendelea "Lakini leo sitaki kwenda Guest nataka kuja kwako"


Kiukweli nilijaribu kuvuta picha alikuwa ni mwanamke gani huyo lakini bado sikupata majibu yanayoeleweka!,lakini pia katika maisha yangu pale Sirari kwa wakati ule sikumbuki kama niliwahi kulala na mwanamke Guest,mimi nilikuwaga napenda kampani na washikaji tu na kunywa bia mbili tatu lakini sikuwahi kabisa kuwa addicted na masuala ya wanawake mpaka ifike steji ya kulala nao kwenye magesti,mademu wengi tuliokuwa nao wakati huo walikuwa ni mademu wa washikaji zangu na ndiyo wengi nilikuwaga na namba zao kama mashemeji zangu!.

Ile nyumba ambayo nilikuwaga nimepanga pia sikuwahi kabisa kumpeleka mwanamke wa aina yeyote,sasa ilikuwa ajabu kuongea na huyo mwanamke na kuniambia eti " Lakini leo sitaki kwenda Guest" kana kwamba hata hiyo gesti yenyewe nishalala na mwanamke!.Fedha yangu kubwa iliishia kwenye Misosi na Kupiga pamba,kiukweli hadi leo ndivyo vitu vinanilia hela na wala si wanawake!,sina hobby kabisa na mademu ingawaje ninaye demu mzuri tu wa kiwango cha kimataifa!.

Niliamua kumpigia mshikaji wangu Nyamori ili pengine anieleze uenda angekuwa anamfahamu yule demu lakini pia akasema yeye alikuwa amfahamu,pia nikampigia mwanangu Magesa nikamuuliza kuhusu jina la huyo demu nae akasema hamjui,nilijaribu kumpepeleza Magesa ili anifahamishe uenda kuna demu amewahi kuja kunitafuta pale kijiweni kwa siku za karibuni lakini jamaa akasema hakuna!.Sasa niliamua kumshirikisha Mtatiro lile suala ndipo akaniambia inapaswa niwe makini uenda mapongo walikuwa wakiandaa mtego wa panya ili wanidake kupitia mwanamke.

Mtatiro "Hebu nipe hiyo namba tuone"

Nikampatia Mtatiro ile namba akajaribu kuipiga,alipoipiga bahati nzuri ikapokelewa na mwanaume lakini mtu aliyepokea ilionekana alikuwa kwenye kelele kama za watu wengi hivyo hawakuweza kusikilizana!.

Mtatiro "Hii namba inabidi uachane nayo maana wajinga watakuwa bado wanakusaka"

Aliendelea "Tena huyo demu akipiga we usipokee mkatie kabisa"

Sikuwa na shaka na maelezo ya jamaa yangu Mtatiro maana ni mtu ambaye mara zote alikuwaga akinishauri sana!.

Nilichokifanya nilikopi majina yote muhimu kwenye ile simu na kisha nikatoa ile line ya simu nikaitupa,kesho yake nikaenda kusajili line mpya ya Airtel. Baada ya kuona hapo Nyasana mambo hayanilipi niliamua kumwambia Mtatiro ya kwamba mi inabidi nieleke Mwanza kwa sista.Mtatiro nae ni kama alikuwa keshakata tamaa ila braza ake ndiye alionekana kikwazo kwake!.

Mtatiro "Mwanangu mi namuaga kama akikataa kuondoka namuacha yeye apambane,atajua mwenyewe!".

Mtatiro alitaka arudi na yeye Mwanza akaangalie ishu nyingine maana pale kijijini ni kama alikuwa akipoteza muda,sasa aliniambia hapo Mwanza kuna nyumba ilikuwa imejengwa na kaka yao mkubwa ambaye alikuwa mwanajeshi na ndipo alipofikia,na huyo braza ake aliyekuwa hapo Nyasana mgodini pia alikuwa akiishi pale na familia yake kwakuwa hiyo nyumba haikuwa na mtu!.

Baada ya Mtatiro kumwambia huyo braza ake waondoke maana hapo ni kama alikuwa akipoteza muda lakini jamaa alikuwa haelewi kabisa,yeye alikuwa akisema lile eneo kuna madini na atabaki kukomaa,sisi kama tunaondoka basi tuondoke na yeye tumuache!.Hatukuwa na namna ilibidi sisi tuondoke kuitafuta Mwanza.Sasa mpaka wakati huo zile hela feki zilikuwa zimebaki Tsh milioni 1.8,na ambazo tulikuwa tumechenji na nyingine kutumia zikabaki halali laki 4.Hivyo zote halali na feki zilikuwa Tsh milion 2.2.

Tulipokuwa hapo Bunda tulinunua nguo na viatu pia mara kibao tulikuwa tukienda hapo mjini kupata beer na kula vizuri,hivyo kujikuta hela zinazidi kupukutika!.

Nilipofika Mwanza niliamua kutengana na Mtatiro,mimi nilielekea kwa sista aliyekuwa akiishi Meko na Mtatiro yeye akaelekea huko Usagara!.Nilimpatia jamaa yangu hela kama laki 6,feki nilimpa laki 4 na halali nikampatia laki 2 ili angalau zimsaidie atakapokuwa huko!. Baada ya kufika hapo kwa sista kiukweli sikutaka kabisa kukaa,sasa shemeji alikuwaga akitoka kuna alikuwa akimaliza hata wiki ndipo anageuka nyumbani!.Nilimwambia sista aongee na shemeji ili amwambie yule muhindi kama bado ile kazi ipo nikaifanye lakini kwa bahati mbaya jamaa akasema ishapata mtu muda mrefu tu!.

Kuna siku shemeji akawa ameniambia niende nae akanifundishe kazi ya kusimamia wavuvi wake kwenye ile mitumbwi yake ili nitakapokuwa na ujuzi wa kutosha awe ananiachia usimamizi na yeye kuendelea na shughuli nyingine,nikawa nimekubali maana sikutaka kukaa tu hapo kwa shemeji nionekane mzigo!.

Tuliondoka na shemeji tukawa kama tunaelekea Musoma,sasa tulipofika Magu tulishuka,kuna gari ilikuja kumchukua pale tukawa tumeondoka hadi kisiwani huko ndani ndani, kile kisiwa kilikuwa kinaitwa kisiwa cha Ijinga,Aisee nilipofika hapo nilikuta kuna mitumbwi kama uchafu,kuna ambayo ilikuwa imefungwa injini za Yamahama na Honda,pia ipo mitumbwi ambayo ilikuwa ya kawaida tu!.

Baada ya kufika hapo shemeji akawa amemuita jamaa mmoja wakaanza kuongea!.

Shemeji "Aisee nimewaongezea mvuvi"

Jamaa "Aaah ndo huyu bwana eeh!"

Shemeji "Eeeh bhana mfundisheni kazi ni shemeji yangu"

Jamaa "Sawa bosi wangu"

Nilibaki kuduwaa na kushangaa maana niliambiwa naenda kusimamia mitumbwi lakini baada ya kufika kibao kimebadilika na kuitwa mvuvi!


Muendelezo> Sehemu ya 16
Duu mvuvi tena ?
 
Leo nipo na ninyi vilaza. Hasa wewe mtunga hadithi halafu unatumia ID zako nyingine kutaka waibia watu. Sisi wengine tuna akili. Lete episodes nyingine hapa tupoteze muda tupo mapumzikoni. Ila kuomba omba pesa ukome. Hatukuomba utunge hizi stories. Ni kukosa kwako kitu cha kufanya ukaona utuburudishe. Sasa leta burudani hapa.[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Daaah,[emoji17][emoji17][emoji17]
 
Back
Top Bottom